Monday, June 20, 2016

WABUNGE WA UPINZANI WATOKA BUNGENI KWA MTINDO HUU






WABUNGE WA UPINZANI WATOKA BUNGENI KWA MTINDO MPYA, WAMEJIFUNIKA MDOMO KWA KARATASI NA GUNDI
Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo wametumia mtindo mpya kueleza hisia zao baada ya kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wamejifunika midomo kwa karatasi.
Hii ni wiki ya tatu mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.

No comments:

Post a Comment