Friday, October 19, 2012

SHEIKH FARID HADI AHMED ATEKWA NYARA


Kutoweka kwa Farid
Akizungumzia tukio la kutoweka kwa kiongozi wa Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed,mtetezi wa wazanzibari na mkombozi wa nchi ya zanzibar. Kamishna alisema: “Ilikuwa saa 6:30 mchana wa juzi tulipokea taarifa kutoka kwa Sheikh Msellem Ally kwamba kiongozi mwenzao wa Jumuiya ya Uamsho ametekwa na haonekani tangu jioni ya Oktoba 16.
“Baada ya taarifa hii, uchunguzi ulianza na mmoja wa watu waliohojiwa ni Said Omar Said ambaye ni ndugu wa Sheikh Farid ambaye ni dereva na ndiye aliyekuwa naye walipokwenda katika eneo la Mazizini kununua umeme kutokana na maelezo ya dereva huyo.”
Kamishna Mussa alisema kwa mujibu wa Said, Sheikh Farid alimwamuru dereva huyo kwenda nyumbani kupeleka umeme wakati yeye akizungumza na watu walikuwamo ndani ya gari aina ya Noah. sisi wazanzibari tunauliza hivi kipindi cha nyumaa alipochukuliwa sheikh musa pia alichukuliwa na gari aina ya Noah.na walikuwa ni polisi wakampeleka madema je sio Noah hihi ndio labda imemteka sheikh wetu farid..? kamshna anaendelea kusema gari ambalo hata hivyo nambari zake za usajili hazikufahamika. Alisema ilipotimu saa 6:30 mchana juzi wakati taarifa hizo zinapelekwa kituoni, wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho walikuwa wanaendelea kujikusanya katika msikiti wa Mbuyuni na kuanza kulizana nini kimemtokea sheikh wetu pasi na jibu kupatikana.
“Baadaye vijana wakagunduwa ni mchezo ule ule walio ufanya kwa sheikh musa sasa wanaufanya tena kwa sheikh farid ndipo fujo hizo zikaanza muda sio mrefu zilisambaa katika maeneo mengine ya mjini kwa kufanyika vitu ambavyo Serikali, Chama Cha Mapinduzi vitawafanya wamke na mkutafuta sheikh maana walikuwa hata hawajali kabisa kama sheikh kapote kiolele vijana wakaingia kazini mpaka sasa wako kazini kuhakikisha sheikh anapatikana.
Alisema katika vurugu hizo watu hao walichoma moto magari kadhaa, ambapo gari la Serikali lilivunjwa kioo kidogo cha pembeni, gari la Zimamoto kuvunjwa kioo cha mbele pamoja kuvunja maduka ya pombe. Kamishna Mussa alisema, mpaka sasa, watu 10 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika katika vurugu.

No comments:

Post a Comment