Sunday, December 7, 2014

SHEIN AKEMEA UDHALILISHWAJI WA WANAWAKE YEYE MWENYEWE ANAWATHALILISHA WANAUME UMEWAPELEKA WAZANZIBARI NCHINI TANGANYIKA WAMELAWITIWA,WAMETIWA CHUPA NA MAJITI HUO SHEIN UNAUTAJE....???????


HUYU ALIYE SIMAMA KATIKATI NDIE YULE ALIYESEMA HAITAMBUWI KAMATI YA MARIDHIANO HAPA KWENYE PIC ANAFANYA NINI NA YEYE HAWATAMBUI...?

UMEWASAFIRISHA KUTOKA ZANZIBAR MPAKA NCHI YA TANGANYIKA WAMETHALILISHWA NA WAKE NA WATOTO WAO WAKO HAPA ZANZIBAR HAWAJUWI WAUME ZAO,BABA ZAO,AMI ZAO,KAKA ZAO,SHEMEJI ZAO VIPI JE HUWO SIO UTHALILISHAJI SHEIN....?? 

Rais wa Maskani ya Kisonge nchini Zanzibar,Shein, amesema ni aibu kubwa Zanzibar kukithiri vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto kutokana na asilimia kubwa ya wananchi wake kuwa waumini wa dini. Alisema dini zote zinapingana na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto na asilimia ya wananchi wake ni waumini wa dini ya Kiislamu. Alisema hayo alipokuwa akizindua kampeni ya kupambana na ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto. Alisema ni lazima jamii ikubali kuwa na mahusiano mema katika kurejesha mapenzi ndani ya familia zao kwa kuzingatia mafunzo na maamrisho ya dini. Alisema imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya binadamu kuwaachia ulezi akinamama pekee jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji.Shein alisema akinamama wasaidiwe katika suala hilo na itambulike kwamba ulezi ni wa mama na baba. Alisema kuwa utafiti wa mwaka 2013 uliofanywa na Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, umebaini kuwa kiwango cha ndoa kuvunjika kimefikia asilimia 31. Alisema hali hiyo inaleta matokeo mabaya katika familia na ndiyo chanzo kinachochangia udhalilishaji. Waziri wa Uwezeshaji, Zainab Omar Mohammed, alisema kuwa wanawake, watoto wa kike na wakiume wameendelea kuathirika na vitendo vya udhalilishaji hali inayosababisha kuishi kwa hofu.Aliongeza kuwa ni imani yake kwamba kampeni hiyo ya miaka miwili ya kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto itasaidia kulinda haki zao.Akisoma risala katika uzinduzi huo, Hadiya Makame, kutoka Mkoa wa Kaskazini alimuomba Shein kuwekwe mikakati madhubuti ya kumuondolea vikwazo mtoto mwenye ulemavu hasa wa akili, uoni na usikivu, yatakayowawezesha kupata haki zao.Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la kesi za udhalilishaji wa kijinsia hasa kwa watu wa makundi hayo ambao watu hutumia udhoefu wa ulemavu wao katika kuficha ushahidi.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment