Friday, December 19, 2014

VIONGOZI MAJAMBAZI,WALEVI,WEZI,WAUWAJI,WANAOPENDA STAREHE,WASIO JALI UTU WALA WATU ZAIDI YA MATUMBO YAO,WAKE ZAO,MAHAWARA WAO NA WATOTO WAO N.K. UKIWAPA NCHI KUONGOZA UNATARAJIA NINI...????


WALEVI UKIWAPA NCHI KUONGOZA UNATARAJIA NINI...........?????

MASULTANI WEEE WARABU WEEEE MR ZANZIBAR SI NCHI AKIWA OMAN KAKIMBIA HUKO HUKO NCHI ZA KIARABU KWENDA KUJIFICHA MPAKA BALAA LA ESCROW LIPOWE AKIRUDI UTASIKIA CHUKI ZAKE MASULTANI WALE WABAYA WALE YAGUJUUU

Inastajabisha na kushangaza kusikia kiongozi mkuu wa serikali ya Tanganyika, kama Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Nchi ya TANGANYIKA kuwa amesafiri ziara nje ya nchi kwa muda wa zaidi siku 15, wakati nchi iko katika hali tete sana kisiasa, na isitoshe yeye mwenyewe Pinda ni moja wa watu wanaotuhumiwa kila upande – kuanzia kasi ya ESCROW, hadi huu uvurugaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika nchi ya Tanganyika. Katika hali kama hii, sisi tuliopata mafunzo zamani ya kiutawala, na labda ulinzi/wa nchi basi ilikuwa hata katibu mkuu haruhusiwi kuondoka kutoka kituo kimoja cha kazi hadi chengine; yaani hata kama uko Dar, basi huwezi kwenda hata Tanga mpaka kijulikane (au kwa lugha yenu ya siku hizi vijana, mpaka kieleleweke).
Mimi nimeitafsiri ziara ya Pinda nje ya nhci ni moja ya jeuri zake na kibri alichonacho anachokiendeleza na pia kutokuwa na umakini wa Rais mwenyewe, Kikwete. Vipi hali kama hii anamruhusu Waziri Mkuu wake aondoke nchini (je, akibadilisha kibao huko, na kuamua kumpinga akiwa nje ya nchi, ok hili si tatizo lakini kwa nini amruhusu jambazi hili....??); au kwa maelelezo tuliyosoma jana, ni kuwa kama vile Rais hajui! Daaah! Hivi kweli Rais hajui kuwa Waziri Mkuu wake hayupo nchini, mpaka kuagizishia arudi.....? Hivi kweli inaingia akilini hii......? wewe basi Raisi au shaghala balaaa hujuwi Waziri Mkuu wako kuwa hayupo Nchini utajuwa shida za wananchi wako kweli.......? situnadanganyana tu. Kama ni hivyo, ni aina gani ya uongozi au uendeshaji wa serikali...???? Kama ni hivyo,basi raha sana kuongoza nchi ya  Tanganyika — kuwa hata Katibu Mkuu, au Mkurugenzi anaweza kuondoka nchini bila kujulikana…..tunajua amekwenda kufanya nini huko.....??
Pinda anasema eti amekwenda kutafuta vitega uchumi na wawekezaji. Huu ni uwongo usiokuwa na macho wala miguu, wiki mbili basi....?? Hee jama limeiba kisha limeona kashfaa inakuja limesepa nchi za uwarabuni kwenda kupoza kwanza na kusikiliza upepo ili watu wasahau kisha akirudi kama kawaida wapi tuibe weee……Obama alikuja nchini Tanganyika siku moja na nusu, na alifanya deal ya billions of dollars, Putin yupo India na kwengineko, kila pahala siku moja…..na anavuna trilions of dollars…kama vitega uchumi, na kukuza biashara….yule tapeli number moja siku duniani, Mchina…..rais wake hupita tu pahala wala halali au kukaa….anavuna billions na kuiba rasilmali zote zilizopo kwa kila nchi, na akipata wajinga kama hivi nyie Watanganyika au Wazanzibari basi ndio huokota kama anavyo-okota embe dodo (kwa sisi watu wa shama). Jamani nchi lazima iwe na nidhamu — kisheria na taratibu hata Rais wa nchi anatakiwa ajulikane ziara zake ni siku ngapi; lakini sio mwezi au miezi miwili kama anavyofanya Raisi wenu mwenyewe JK eti anatafuta vitega uchumi na kuvutia wawekezaji yaguuujuuuuu.
Sasa jeuri kama hizi za akina Pinda na wenzake, ndio inaifanya nchi ya Tanganyika kuwa mpaka leo haina maji, ndoo kichwani….haina umeme Miaka 50 na ushiyaa Viongozi wa CCM majambazi wameshindwa kuwa wananchi maji na umeme tu ndio kweli wataweza kuleta maendeleo......???  (sasa mgao umerudi Tanyangika kutokana na upuuzi kama huu wa akina Pinda au Tibaijuka na hayo majambazi yalio jaa bungeni kazi kuiba tuuu. Jana nimesoma kuwa Tibaijuka anasema kuwa yeye hajiuzulu maana hajaiba wala kuhusika na sakata la EScrow. Heeee….mama weee unayejisifu kuwa ni mstaaf wa UN. OK, hujaiba wala hujachukua cha mtu unamdanganya nani......??? Hii kufanyiwa trasation ya 1.6 bilion ni halali, kwa nchi gani......????? financial regulations zinasemaje hapa Tanganyika, sikwambii huko UN unakojisifu kuwa wewe ni mstaafu wake. Je, UN inaruhusu kitita kama hichi cha pesa kusafirishwa au kuwa wired trasfer kama hivi. Mimi siku zote nina shaka sana na taasisi kama UN maana watendaji wake ndio kama hawa Tibaijuka, au Asha Rose Migiro na wengine kama hao, watu ambao credibility zao ni mashaka mashaka. Watu wenye mashaka mashaka kama hawa Tibaijuka, ndio waliofanya na kuandika rasimu mpya ya katiba…ile wanayoitaka wao, sio wanayoitaka wananchi, ili wapate kuiba zaidi na zaidi…….hiyo ndio nchi ya Tanganyika/wezi mtupu na ndio wanaowafundisha Viongozi wa nchi ya Zanzibar kuwa majizi namba 1

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment