MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Saturday, December 6, 2014
WALIO FANYA KWELI MAPINDUZI YA ZANZIBAR WANAJUTA NA HAWATAKI HATA WAJULIKANE SHEIN,BALOZI,VUAI,ASHA BAKARI,SHAMSI,SAMIA,BORAFYA, NA KATHALIKA WA KUFYATA MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU
Victor Mkello Kama Alivyokuwa mwaka 2003
Untold Story,
Mimi nitakupa fikra zangu binafsi kuhusu jambo hili.
Ziko dalili nyingi sana kuwa wazee wetu waliokuwa katikati ya siasa
wakati ule walijua mpango wa kupindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte. Lile ambalo hawakulijua ni kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki Sakura na Kipumbwi iliyokuwa imetayarishwa pale ili kuvamia Zanzibar.Wazee wetu walikujapata na mshtuko pale iliowadhihirikia kuwa kuna mauaji mengi sana yametendeka bila sababu na mauaji hayo ni baada ya serikali ikiwa imeshaanguka. Ndiyo maana mtu kama Ali Mwinyi Tambwe katika maisha yake yote hakutaka kunasibishwa na mapinduzi ya Zanzibar ingawa yeye alikuwa katika ya mipango ile. Nimelitaja jina la Ali Mwinyi Tambwe kwa kuwa lilikuja kuwa dhahir katika kitabu cha Dk. Harith Ghassany na katika kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi kapewa nishani. Lakini wako wazee wetu wengine bado wahai na waliujua mpango wote wa mapinduzi na inajulikana kuwa walihusika lakini hadi leo wamepiga kimya.
Hivi juzi tu nimepokea nakala ya barua kutoka kwa sahib yangu aliyeko Northwestern University, Marekani barua inayotoka kwa Abdulwahid Sykes kwenda kwa Aboud Jumbe. Huyu sahib wangu tulifahamiana nilipokwenda kuzungumza Northwestern University na nilimpa nakala ya kitabu cha Sykes. Kwa kujua utafiti nilokwushafanya kuhusu maisha ya Abdul Sykes ndiyo akaniletea barua hii. Barua hii imeandikwa mwaka 1967. Ukisoma barua hii inaonyesha ule ukaribu waliokuwanao hawa watu wawili. Hii inaonyesha kuwa udugu wao una historia ndefu kwa hiyo wana
mengi. Issa bin Nasser Al-Ismaily alipata kumuuliza Abdul Sykes miaka mingi baada ya yale mauaji kutokea kuwa ilikuwaje ikawa vile. Jibu la Abdul Sykes ni kuwa alimsihi Sheikh Issa wasizungumze habari za Zanzibar kwani huenda zikavunja udugu wao. Kisa hiki Sheikh Issa kakieleza katika kitabu chake ''Zanzibar: Kinyan'ganyiro na Utumwa.''
Dk. Ghassany halikadhalika kutokana na umuhimu wake na yeye kakitaja katika kitabu chake.
Sasa swali la kujiuliza ni hili, kwa nini Abdul Sykes alijibu vile? Nini alikuwa anatakakuficha na hakupenda Sheikh Issa akijue? Alipokufa David Kimche magazeti mengi Ulaya yaliandika taazia
yake. Ukitaka kumjua Kimche ni nani ''google,'' sina uwezo wa kumueleza mtu huyu. Kwa ufupi huyu alikuwa Mossad na akifahamiana na mmoja wa wazee wetu kipindi kile cha kupanga mapinduzi ya Zanzibar. Hivi sasa si siri tena kuwa Waisraeli pia walihusika katika mapinduzi ya Zanzibar. Huyu mzee wangu inajulikana ingawa yeye mwenyewe anaficha kuwa alihusika katika mipango ya mapinduzi na alikuwa karibu sana na Wayahudi. Baada ya kusalimiana nikamwambia kuwa Kimche amefariki.
Jibu lake, ''Ala! sikuwa na habari.'' Alionyesha kushangaa lakini nadhani kwa kunijua akajua ''I was in
the know,'' kama wasemavyo Waingereza hakuniliza kitu zaidi.
Nyerere mwenyewe hakutaka ijulikane kuwa alihusika katika njama
zile.
Hii ndiyo hali ilivyo.
Kubwa la hawa wote nilioeleza habari zao ni kuwa hawakutaka wahusishwe na mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu ya yale mauaji yaliyotokea na inasadikiwa mauaji mengi yalifanywa na Wamakonde kutoka katika Mashamba yale ya mkonge ya Sakura. Ilimchukua Victor Mkello takriban miaka mitatu hadi siku moja alipoamua kutoa yake ya moyoni kuhusu mchango wake katika
mapinduzi ya Zanzibar na hapo ndipo alipomweleza Dk. Ghassany nini kilipitika.Dk. Ghassany akienda Muscat na kurudi Tanga kwa subira kubwa akisubiri siku Mkello atakapofunguka. Ingawa mmoja wa washirika wake Mzee Mohamed Omar Mkwawa tayari alikuwa keshaeleza mpango mzima lakini kauli ya Mkello kutoka
kinywani kwake mwenyewe ilikuwa muhimu kusadikisha lile tayari lililokuwa wazi.
Baada ya mapinduzi yale kufanikiwa si Nyerere wala Karume sasa walikuwa hata kwa chembe wanawahitajia hawa wazee wetu kwa hiyo Karume alifanya hayo yote aliyofanya bila ya kuwepo mtu hata mmoja wa kumzindua au kumshika mkono kumtanabaisha hata kwa mbali na kumwambia, ''Muogope Allah.'' Kwa kukhitimisha ni kuwa hili jambo la roho za watu waliodhulumiwa bure
halitakwisha na litakuwa linaturejea miaka nenda miaka rudi mpaka pale tutakapokubali ukweli kuwa limetokea na yalikuwa ni makosa, watu wakaa wakalizungumza wakataka msamaha kwa Allah na ikapigwa fatha.
Hanga kabla hajafa alijuta kwa yale yalotokea katika mapinduzi na akataka
msamaha kwa Allah na kaacha usia khasa kuhusu hatari ya ubaguzi.
Atakae kujua zaidi kuhusu habari hizi na akisome kitabu cha Dk. Ghassany
mimi nimepita mle mle alimopita yeye.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment