Wednesday, July 8, 2015

NCHINI ZANZIBAR PEMBA POLISI WOTE WAMETAKIWA KUHESHIMU NA KUZITII AMRI NA SHERIA ZA HAKI ZA BINADAMU

  
WAPIGANAJI wa jeshi la Polisi kisiwani Pemba, wametakiwa kuwa mfano mzuri wa kuziheshimu na kuzitii haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kuwachapa makofi na mateke, watuhumiwa wanapowakamata.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Kusini Pemba, Shawal Abdalla Ali, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya haki za binadamu, yaliowashirikisha askari wa usalama barabarani 40, kutoka mikoa wili ya Pemba. Alisema pindi askari akiwa anaziheshimu na kuzitii kwa kina haki za binadamu kuanzia tokea ukamataji, inaweza kujenga misingi imara na endelevu kwa jamii juu ya haki hizo.

Mkuu huyo wa usalama barabarani alieleza kuwa, wapo baadhi ya askari wamekuwa na mikono mepesi kuwatwanga makofi, mateke na kuwanyima haki nyengine mtuhumiwa, jambo ambalo kisheria halikubaliki. “Sisi askari lazima tuwe mfano mzuri wa kuigwa kwenye eneo hili la kuheshima haki za binadamu, na ndio jamii itajenga nidhamu miongoni mwao katika hilo na kutuamini’’,alifafanua.

Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa usalama barabarani, alisema askari asiefuata maadili ya kazi zake na sheria za nchi, huwa ni mbabaishaji na hupelekea kulivuruga jeshi zima kwenye utendaji.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment