Sunday, July 19, 2015

ZEC ZANZIBAR NI KIGARAGOSI, KITUMWA, KITWANA, CHA KUWAHUNDUMIA MASULTANI WEUSI TANGANYIKA

Afbeeldingsresultaat voor zec zanzibar
Nchini Zanzibar Leo ni skukuu ya pili, mambo yanaanza kuchemka. Tulikuwa na mzee wetu Abdi Salim kipindi sasa hatujamsikia. Pengine ni uzee umemzidi au kafa kihoro. Alaaa kulli hali, mamlaka kamili ya Zanzibar yanahitji kuendelea kupiganiwa. Nirudi kwenye lengo la leo ni mchanganyiko wa ukatwaji wa majimbo. Wananchi wengi hawafahamu jee hapa nchini petu Zanzibar kuna majimbo mangapi ya uchaguzi....?? Au Zanzibar itatowa wabunge wangapi uchaguzi wa 2015...??
Hili limetokana na Tume ya Uchaguzi ya nchi yetu ya Zanzibar ZEC kibaraka cha Mkoloni Mweusi Tanganyika kuongeza majimbo 4 kwa upande wa Unguja na kufikisha idadi ya majimbo 54 kwa nchi ya Zanzibar nzima. Haina mushkeli kwa vile ZEC kigaragosi ndio chombo chenye mamlaka ya kuongeza amma kupunguza majimbo ndani ya nchi yetu ya Zanzibar. Kwa upande wa pili wa sakata nikusikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi nayo ikiongeza majimbo 26 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015 bila ya kuyajumuisha na haya 4 yaliyoengezwa hapa nchini Zanzibar. Huku kukiwa na fununu kwamba NEC haitambui ongezeko hili la majimbo 4 ya hapa nchini Zanzibar wala sio kwamba tunawaomba wayatambue ila kwa sasa nchi ya Zanzibar haina mamlaka kamili kwa hiyo tunajaribu kufuata utaratibu ili wasije kusema aha oha maha baada ya uchaguzi.
Hapo ndio mchanganyiko wenyewe ulivyo. Bahati mbaya suala hili halijazungumzwa kwa kina na wananchi wakafahmishwa hali ya kuwa linawaathiri hasa watia nia ya kugombea nafasi ya ubunge kwa majimbo yaliyoongezwa. Hapo itakuja suala kwani ni jimbo lipi limeongezwa......?? Jawabu halijulikanwi. Kwani mengi yamebadilishwa majina na mipaka. Tukisema jimbo la Malindi ni jipya ndio limeongezwa, hivyo Mbunge wake hatambulikanwi na NEC itakuwaje...?? Kwa utata huu ndio ninapoona ZEC inakuwa kikarogosi kinachotumikia bwana wake Mkoloni Mweusi Tanganyika ambaye ni NEC. Muda mrefu ZEC ilikuwa na mchakato wa uhakiki wa majimbo, ikiwakusanya wadau na kuwashirikisha wanachi watoe maoni yao. NEC ILIKUWEPO WAPI.....??? Hata ije sasa na ikatae ongezeko hili. Wakati umefika wa kadhia kuzungumzwa kwa kina na tupewe jawabu sasa kabla ya hatujaingia kwenye kampeni.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment