Wednesday, December 16, 2015

MAHAKAMA YA RUFAA NCHINI TANGANYIKA M (TCM) IMETUPILIA MBALI OMBI LA RUFAA ILIYOKATWA NA MKURUGENZI WA MASHITAKA DPP

MAHAKAMA ya Rufaa ya nchi ya Tanganyika M (TCA), imetupilia mbali ombi la rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) la kupinga kupatiwa dhamana viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiisilamu (JUMIKI), kutokana na kukosa vigezo vya kisheria Lakini hata hivyo, pamoja na uamuzi huo mahakama hiyo imetoa nafasi maalumu kwa DPP kuwasilisha tena rufaa hiyo mahakamani hapo ndani ya siku 14.Uamuzi huo umetolewa na jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa, baada ya kusikiliza pingamizi za awali zilitolewa na wapinga rufaa hiyo kwa madai rufaa ya DPP juu yao imekiuka taratibu za kisheria.Katika maamuzi yake, Mahakama ya Rufaa ya M (TCA), ikiongozwa na Jaji Othman, Jaji Kimaro pamoja na Jaji Mussa imeungana na upande wa wapinga rufaa kwamba rufaa iliyowasilishwa na DPP imekiuka taratibu za kisheria kwa kukatwa nje ya wakati uliowekwa.Kutokana na kasoro hizo za kisheria zilizojitokeza katika ukataji huo wa rufaa, mahakama hiyo imeungana na upande wa wapinga rufaa na kuitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na DPP mahakamani na kumtaka kuiwalisha tena ndani ya siku 14, endapo atashindwa sheria itachukua mkondo wake.Katika kikao kilichopita, wapinga rufaa hiyo kupitia Mawakili wao wa kujitegemea Abdalla Juma na Rajab Abdalla waliiomba mahakama itupilie mbali rufaa ya DPP dhidi ya wateja wake kwa madai imekatwa nje ya wakati.Mawakili hao walitoa hoja hizo wakati walipotoa pingamizi za awali ambapo Mawakili wa serikali kutoka ofisi ya DPP Raya Issa Mselem na Suleiman Haji, walidai rufaa hiyo ilikuwa ndani ya wakati na ilifuata vigezo vyote vya kisheria.Wakitetea hoja zao katika kikao hicho, Mawakili hao walidai Jaji wa Mahakama Kuu Fatma Hamid Mahmoud, hakulazimika kuwapatia dhamana wapinga rufaa hiyo kwa madai tayari walikuwa wameshatoa indhari (notice) mapema ya kutaka kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi huo.Walidai, kutokana na hali hiyo Jaji Fatma alitakiwa kuchukua uamuzi huo baada ya rufaa yao kusikilizwa pamoja na kutolewa uamuzi na Mahakama ya Rufaa na kuiomba mahakama ikubaliane na rufaa yao na kutupilia mbali pingamizi za awali za wapinga rufaa kwa madai hazina msingi wowote.Viongozi hao wa Jumuiya hiyo ya uamsho pamoja na wafuasi wao, walikatiwa rufaa na DPP kupinga uamuzi wa kupatiwa dhamana na Jaji Fatma Hamid ,Mahmoud kutokana ni haki yao ya kisheria na Kikatiba na kuzingatia kesi hiyo imekaa muda mrefu mahakamani bila ya kusikilizwa.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment