TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuhu
Baada ya kumshukuru Mwenye ezi Mungu na Kumtakia rehma na amani kiongozi wetu Bwana Mtume Muhammad S.A.W.
Tunapenda kuwafahamisha ya kwamba baada ya siku chache tutakuwa tumeingia katika Mwezi wa mfungo sita.Na huu ndio Mwezi aliozaliwa Bwana Mtume S.A.W. kwa mujibu wa kalenda ya kiislamu.Waislamu wote ulimwenguni unapofika mwezi wa mfungo sita husherehekea juu ya mazazi ya Bwana Mtume S.A.W.
Baraza kuu la Waislamu wa Tanganyika linapenda kuwafahamisha juu ya utaratibu wa matukio tuliyoyapanga katika kipindi hiki cha mwezi wa kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W.Katika wiki ya kwanza ya mwezi huu wa mfungo sita kutakuwa na wiki ya misikiti ndani ya wiki hii waislamu watatakiwa kuongeza nguvu zaidi katika majukumu yao ya kila siku ya kuhakikisha kuwa mazingira yao yote yanakuwa katika usafi wa hali ya juu kama ilivyo kawaida.Vilevile katika mwezi mzima kutakuwa na mihadhara mbalimbali misikitini, kwenye redio, magazetini pamoja na televisheni masheikh mbali mbali watashiriki katika mihadhara hii.
Aidha, natoa wito kwa Masheikh na Maimamu nchi nzima kutumia kipindi hiki cha Shahru Milaad (Mwezi wa Mazazi ya Mtume S.AW), kumuelezea Mtume (S.a.w) kwa kina katika Nyanja mbalimbali kama vile elimu, siasa, uchumi, uongozi, utawala bora na kadhalika.Pia napenda kuwafahamisha ya kuwa nimeunda timu maalum ambayo nimeipa majukumu ya kufanya maboresho ndani ya BAKWATA.Timu hii nimeipa pia majukumu ya kupitia mikataba yote ya BAKWATA ili kuweza kuangalia ile mikataba mibovu na kuona namna ya kufanya ili BAKWATA iweze kuwa na mikataba yenye maslahi na Bakwata kwa niaba ya Waislamu.
Aidha timu hii nimeipa majukumu ya kukagua hesabu za BAKWATA kuanzia ngazi ya Makao Makuu na nchi nzima.Mwisho, kwa mamlaka niliyonayo, nimemsimamisha kazi Karim Majaliwa - Mkurugenzi wa Utawala wa BAKWATA Makao Makuu, kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya kadhia ya magari 82, pamoja na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.
Wabillahi Tawfiiq.
Sheikh Abu bakari Zuberi
Mufti wa Tanganyika
05/12/2015
Sheikh Abu bakari Zuberi
Mufti wa Tanganyika
05/12/2015
No comments:
Post a Comment