Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa SULUHISHO wa kisiasa wa nchi ya Zanzibar, yameendelea tena jana Ikulu mjini hapa nchini Zanzibar.Mazungumzo hayo yaliyowajumuisha viongozi watano wa kitaifa akiwamo Shein na Maalim Seif Sharif Hamad, yalichukuwa takriban saa sita.Mazungumzo hayo yalianza saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni huku kukiwa hakuna taarifa zozote zilizopatikana kilichofikiwa katika mazungumzo hayo.
Bado vikao hivyo vya mazungumzo vimekuwa na usiri mkubwa licha ya kuenea kwa taarifa zisizo rasmi na mitaani zimepewa jina la “Dripu”.Viongozi wengine walihudhuria mazungumzo hayo jana ni Marais wastaafu Amani Abeid Karume, Ali Hassan Mwinyi na Balozi Mkazi wa nchi ya Tanganyika.Vikao hivyo vimekuwa na usiri mkubwa ambapo hata viongozi wa vyama vikuu vya siasa vinavyohusika na mgogoro wa uchaguzi Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF), vimeeleza havielewi kilichozungumzwa ndani ya vikao hivyo huku mahasidi wa nchi ya Zanzibar na CCM viburi maiuti wakiendelea kujazana :DRIPU;.
No comments:
Post a Comment