Saturday, August 11, 2012

MOHAMMED SEIF KHATIB AKIWA DODOMA ANAVA NEPI NA ANAKUWA NA HAYA YA KUSEMA

Hayo yakitokea Zanzibar, wabunge wa CCM kutoka Zanzibar wamewajia juu na kuutaka uongozi wa chama hicho kuwachukulia hatua ya kinidhamu baadhi ya viongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaotaka kuuvunja Muungano.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa wabunge kutoka Zanzibar,Dk. Mohammed Seif Khatib akiwa amefuatana na wabunge wapato 30 kutoka visiwani, alisema wao kama wabunge wanashangaa kusikia viongozi hao wakitamka maneno makali ya kuvunjwa Muungano huku wakitazamwa.
Alisema wao kama wabunge waliopata ushindi kutokana na Ilani ya CCM inayotamka wazi kuunga mkono wa serikali mbili, wataendelea kutetea msimamo huo kwa sababu wanachoamini kama yatafanyika mabadiliko mbalimbali kwenye Katiba, hatimaye kila upande utapata haki yake ya msingi.
“Kuna baadhi ya viongozi wanashabikia kuvunjwa kwa Muungano, hilo sisi wabunge tunawaachia viongozi wa ngazi za juu kuhakikisha wanachukua hatua za kinidhamu ili kukomesha tabia hiyo,” alisema Dk. Khatib.
Dk. Khatib alisema wanaamini mfumo wa serikali mbili una faida kubwa kwa Zanzibar na watu wake ikiwa utawekewa mfumo wa kikatiba wa utekelezaji katika kuondoa kabisa kero hizo zilizoko katika Muungano.
Alisema kuwa ilani ya uchaguzi ya CCM waliotumia kuombea ridhaa kwenye majimbo yao, inaweka wazi kuhusiana na mfumo wa serikali mbili, hivyo kulingana na ilani hiyo wote kwa pamoja wanaunga mkono msimamo huo.
Hata hivyo, aliwataka wananchi wa Zanzibar kuaacha kujikita katika suala moja la Muungano wakati wanapotoa maoni yao juu ya Katiba mpya, kwani kuna maeneo mengine muhimu ambayo wanayaacha bila kuchangia.
Tamko hilo limekuja kufuatia baadhi ya wanasiasa, wakiwemo makada wakongwe wa CCM Zanzibar kutoa maoni yanayokwenda tofauti na msimamni wa chama hicho kuhusiana na mfumo wa Muungano.
Wiki iliyopita, mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibae,mzee Ali Nassoro Moyo na Waziri Asiye na Wizara Maalum, Mansour Yusuf Himid, walisema kuwa Muungano wa sasa unakabiliwa na kasoro nyingi na kupendekeza uanzishwe Muungano wa mkataba.
Mbali na Moyo na Mansour, viongozi wengi wa Chama cha Wananchi (CUF) wamekuwa wakitetea Muungano wa mkataba ambao wanasema utasadia Zanzibar kuwa na bendera na kiti chake katika Umoja wa Mataifa (UN).
Kadhalika, Jumiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu (Jumiki) imekuwa pamoja na wananchi na masikini na wanyonge wote wa zanzibar waliothalilishwa kwa miaka 48 ambayo inakaribia nusu karne ya tharuba na kuthulimiwa na Tanganyi Uamsho imesimama kidete kuitetea zanzibar na kuhakikisha anarudi katika hadhi yake kama ilivyokuwa hapo awali zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa pia Zanzibar kujitenga na Muungano huu wa kidhulma na muungano huu unaotumiliwa kuwauwa wazanzibar kila siku za changuzi na kuibiwa mali zao muungano huu unaolete madawa ya kulevya (drugs)muungano huu ulitujazia mabaar kila kona muungano huu uliotulete wanawake wa kitanganyika kuja kujiuza tupu zao kwa pesa na kutupa ukwimi muungano huu huu huu.......
Hata hivyo, tamko la Balozi Seif linakwenda kinyume cha maelekezo yaliyotolewa na Tume Warioba ambayo inakusanya maoni ya Katiba mpya, ambayo iliwatoa wasiwasi Watanganyika na wazanzibar wote na kuwataka watoe maoni yao kuhusu katiba bila woga.
Jaji warioba alisema kuwa tume yake itawasikiliza watu wote, wakiwemo wanaoupinga Muungano.sasa mbona DUULI Balozi anaendele kuropoka kama aliye kunywa maji ya choo wakati ni ramadhani...?au nchi hii ni babu yake kamuandikia..?

No comments:

Post a Comment