MZEE Hassan Nassoro Moyo amemtengenezea njia ya kupita Rais Jakaya Mrisho Kikwete juu ya hatma ya muungano.
“ Aw a u l i z e ‘ Wa n a u m e ’wanataka nini kama Mzee Karume alivyomwambia Nyerere mwaka 1970.”Hayo ni maoni ya baadhi ya wananchi waliosikiliza maelezo ya Mzee Hassan Nassoro Moyo wiki iliyopita.Katika maelezo yake Mzee Moyo alisema kuwa mwaka 1970 Mzee Karume akiongozana na wajumbe wa Baraza la Mapinduzi waliitwa Ikulu Dar es Salaam ambapo Mzee Karume aliwasilisha mambo manne waliyokuwa wakitaka Wazanzibari. Mambo hayo ni Zanzibar kuwa na Sarafu yake, Jeshi lake la Polisi, Rais wa Zanzibar kuwa na mamlaka ya kuulizwa inapotaka kutangazwa hali ya hatari. Kwa
maana kuwa Mamlaka ya Uamiri Jeshi Mkuu isibakie pekee kwa Rais wa Tanzania.Na la nne likiwa ni kuwa na uwezo na uamuzi juu ya mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa.Kwamba katika masuala ya kuingia mikataba na mashirikiano na nchi nyingine, Zanzibar isingoje ruhusa ya Bara kama ilivyo hivi sasa.Mzee Moyo anasema kuwa,baada ya Mzee Aboud Jumbe kuwasilisha madai na msimamo huo wa Wazanzibari, Nyerere alimuuliza Karume, je huo ndio msimamo wa Wazanzibari? Karume akamjibu: “Waulize wanaume hao.” Na alipouliza,Wajumbe wote wa Baraza la M a p i n d u z i w a l i o k u w e p o wakasema ndio.
Na Mwandishi Wetu Ni kwa maelezo hayo, baadhi ya wananchi wanasema kuwa mjadala wa hali na mfumo wa muungano utakuwa mwepesi kama viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar watamwambia Rais Kikwete “awaulize wanaume” wanataka mfumo gani.Ni kwa muktadha huo, Mzee Moyo anasema kuwa haya wanayodai vijana, hawakuanza wao bali kama ni fujo walianza wazee wao wakiongozwa na Mzee Karume ambaye mwaka
1970 aliwarudisha vijana wa Kizanzibari waliokuwa wakipelekwa vitani Msumbiji.Mwaka huo, bila kumwambia Karume, Rais Julius Kambarage Nyerere alitoa amri wachukuliwe vijana wa Kizanzibari kwenda vitani Msumbiji.Mzee Moyo anasema, meli iliyowachukua vijana hao ilipofika Chumbe, Mzee Karume akaamuru warudi.Anasema Nyerere alipouliza
k u l i k o n i , M z e e K a r u m e alimrushia maswali ambayo hakuweza kuyatolea majibu.Akaomba radhi.Ufupi wa maneno anasema Moyo kuwa Mzee Karume alimwambia Nyerere kuwa Rais wa Zanzibar ndiye dhamana ya vijana wa Wazanzibari na lolote litakalotokea huko vitani ndiye atakayeulizwa na wazazi wao.Kwa hiyo hawezi kuruhusu vijana hao kwenda vitani bila yeye kujua au kuridhia tena wakati ni Makamo wa Rais.Ilikuwa baada ya mkasa huo,anasema Mzee Moyo kuwa ndio
serikali ya Zanzibar ilitaka kuwa na sarafu yake, Polisi na kuwa na maamuzi katika kupeleka jeshi vitani, halikadhalika mambo ya nje.Kwa hiyo, anasema kama ni fujo wameanza wazee, vijana hivi sasa wanaendeleza tu na akawataka viongozi wa serikali kuwa wakweli na kuacha woga.Amesema, hivi sasa Rais wa Zanzibar hana mamlaka yoyote katika siasa na mahusiano ya kimataifa baada ya suala la Ushirikiano wa Kimataifa kufanywa ni la muungano.“Mfano ushirikiano wa
kimataifa, halikuwa ni jambo la Muungano katika hapa wakaliongeza la Ushirikiano wa kimataiafa, hilo limeingia kinyemela tu, kwa sababu hiyo hata Rais wetu akienda Nairobi hapo hawezi kutia hata saini kununua unga wa ngano, hawezi mpaka ruhusa ipatikane Bara.”Akasema Mzee Moyo na kuongeza kuwa hata hili suala la kujadili Katiba hivi sasa limekuja kinyumenyume.Akataka jambo la mwanzo lifanywe mwanzo kwanza,kwamba watu wajadili kwanza m u u n g a n o w a k u b a l i a n e unatakiwa uwe wa namna gani na ndio huo uwekewe vipengele katika katiba.“ K a t i b a unamtengezea
nani? Madogori? Tuzungumze muungano kwanza.”Amesema Mzee Moyo na kusisitiza kuwa yeye anataka muungano wa kimkataba.
Mzee Moyo akiongea na waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment