Sunday, August 19, 2012

TANGANYIKA HAITA PIGANA NA MALAWI LAKINI WAZANZIBARI WATASHIKA ADABU ZAO KWA JESHI LETU NA NCHI YAO SIWAPI HAHAHAH.


JK awaumbua Lowassa, Membe,
RAIS Jakaya Kikwete amesema hajaliagiza Jeshi la Wananchi wa  Tanganyika
(Tanzania) (JWT) kupigana vita na Malawi kwa sababu za mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya nchi hizo mbili.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama imekuja siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuitaka Serikali ya Malawi kusitisha utafiti wa gesi na mafuta unaofanywa kwa ndege juu ya ziwa hilo.
Baada ya Membe kutoa onyo hilo, aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Kikwete, Edward Lowassa alisema wakati Bunge la Bajeti lilipokuwa likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma kwamba, jeshi lipo tayari kuingia vitani na Malawi, endapo nchi hiyo itakaidi agizo la kuziondoa ndege zinazofanya utafiti kwenye anga la Ziwa Nyasa.
Kikwete awakata maini
Katika kile kinachotafsiriwa na wachambuzi wa musuala ya siasa kuzikana kauli za Membe na Lowassa, Rais Kikwete alimhakikisha Rais Joyce Banda wa Malawi, kwamba Tanganyika(Tanzania) haina mpango wa kuingia vitani dhidi yao, na kusisitiza kuwa hizo ni chokochoko za wanasiasa na waandishi wa habari.
Rais Kikwete aliyekuwa kwenye mazungumzo na Rais Banda wakati wa kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana jioni nchini Msumbiji, aliwataka Wamalawi kuondokana na hofu ya vita.
“Nanakuhakikishia dada yangu na watu wote wa Malawi, kwamba hatuna nia wala mpango wa kuingia vitani… hatuna matayarisho ya jeshi wala jeshi halijasogea popote kwani hakuna sababu.
“Mimi ndiye kamanda mkuu wa majeshi, na sijapanga wala kutoa maelekezo ya vita, tuviachie vyombo vyetu vifanye kazi. Hebu tuvipe nafasi. Wanasiasa na waandishi wa habari wajiepushe na maneno yanayosababisha taharuki na chokochoko, hayana maana… waachie diplomasia ifanye kazi yake,” alisisitiza.
Rais Kikwete alisema kumekuwa na sintofahamu ya muda mrefu kuhusu mpaka huo, huku akibainisha kwamba maofisa wa Malawi na Tanganyika(Tanzania) wameanza kulizungumzia suala hilo kwa nia ya kulitatua kwa amani.
Naye Rais Banda alisema amefarijika baada ya kusikia kauli ya Rais Kikwete iliyomhakikishia kwamba hakuna vita, huku akieleza kuwa tishio la vita liliwasumbua wananchi wake na kuwaongezea mshikamano.
“Nimefarijika sana, suala hili limetusumbua mpaka Wamalawi wote wakaungana bila kujali tofauti zao… navishukuru vyombo vya habari vya Malawi kwa kuonesha uzalendo na ukomavu katika suala hili,” alisema Rais Banda.
Rais Kikwete na Banda walikutana jijini Maputo nchini Msumbiji kwenye kikao cha viongozi SADC ambapo Tanganyika(Tanzania) ilichukua Uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Awali nafasi iliyochukuliwa na Tanganyika (Tanzania) ilikuwa inashikwa na Afrika Kusini huku Uenyekiti wa SADC ukichukuliwa na Msumbiji kutoka kwa Angola nafasi watakazokuwa nazo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premi Kibanga, Rais Kikwete alirejea nyumbani jana akitokea Msumbiji.

No comments:

Post a Comment