Friday, August 10, 2012

SHEIKH FARID WAZANZIBARI WAMENYIMWA UHURU WAO WA KWELI.

Baadhi ya viongozi hao wachache wa Chama Cha Mapinduzi wanaendeleza ajenda ya Tanganyika dhidi ya Wazanzibari na kuendelea kuitawala Zanzibar chini ya sera batili.Kwa miaka 48 (takriban nusu karne) sasa, Wazanzibari wamenyimwa uhuru wa
kweli wa kuamua hatma ya Muungano kwa vitisho vya sera hizo. Sasa viongozi hao wachache wa CCM wanaendeleza kiini macho
dhidi ya Wazanzibari na Watanzania kwa kuwaekea mipaka kwa hiyo tunawaomba w a n a c h a m a w a C C M Zanzibar kuweka uzalendo mbele na kutumia haki yao ya maamuzi na kuirejeshea
Zanzibar heshima yake mbele ya jamii za kimataifa na jumuiya za madola na ndani ya muungano wa mkataba watakaouridhia wananchi wa Zanzibar kwa umoja wao.J u m u i y a n a Ta a s i s i
z a  Kislamu  Z a n z i b a r  haikubaliani hata kidogo na Azimio la baadhi ya viongozi wachache wa Chama Cha Mapinduzi kwa wanachama wake wanaotoka Zanzibar ambalo linawashurutisha
kusema ati serikali mbili bila ya mamlaka kamili ya kitaifa na kimataifa ya Zanzibar ndio msimamo wao.Kitendo hiki ni hatari kwa Zanzibar yenye hadhi ya kitaifa na ya kimataifa kwani nchi yoyote huru haiwezi kupata uhalali wa katiba yake ikiwa sehemu ya jamii imeshurutishwa na kunyimwa haki za msingi za kufikiri na
kuamua bila ya shinikizo na kitendo hiki kinakua hatari zaidi kwani CCM ndicho chama kinachotawala sehemu zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ikiwa viongozi hao wachache wa CCM wanawashurutisha wanachamawenziwao ,sisi wengine tunaamini tutanyimwa haki zetu juu ya aina ya mfumo wa utawala
tuutakao sisi wananchi wa Zanzibar.Hata huko Tanganyika kuna tetesi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi( C U F ) a m e f u a t w a  n a kuambiwa kuwa sera ya chama chake ni serikali tatu.
Waliomuendea wanahoji mbona CUF Zanzibar inaunga mkono hoja ya Wazanzibari ya kuitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili na kufuatiwa na mkataba? Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar
zitapinga kwa msimamo mmoja chama chochote cha kisiasa kitakachoonesha dhamira/nia ya kuisaliti Zanzibar na Wazanzibari
katika kupata mamlaka yake kamili ya ndani na nje.Baada ya kusema hayo tunapenda kuwashukuru Wazanzibari wote na nchi
nzima ya Zanzibar na visiwa vyake kwa mshikamano mlioonyesha na kwa kutuunga mkono toka mwanzo hadi hapa ambapo kwa kushirikiana k w a p a m o j a t u m e w e z a kuufikisha umma katika mustakbal mzuri. Ndugu Wazanzibari tunakuombeni tusimame pamoja na kwa sauti moja tuwaunge mkono Wawakilishi wetu wote waliosimama ndani ya Baraz la Wawakilishi kuitetea ardhi na nchi yetu ya Zanzibar.Tunapenda kutoa shukurani za dhati na maalum kwa Mzee Mheshimiwa Hassan Nassor Moyo kwa kuendeleza msimamo wake usiotetereka katika kuitetea Zanzibar na maslahi ya Wazanzibari bila ya kujali itikadi ya chama chake.
Tunahitimisha tamko hili kwa kuwahakikishia viongozi wetu wa ngazi za juu na Wawakilishi wote katika Baraza la Wawakilishi na
kila anaesimamia maslahi ya Zanzibar wakae wakijua kuwa umma wa Kizanzibari pamoja na ofisi zote na viongozi wote watakuwa pamoja nao katika kuipigania nchi yetu.Iwapo Wawakilishi wetu wataendelea kutishwa na kufedheheshwa, basi tuko tayari kuitisha mkusanyiko wa amani (sit-in) nchi nzima utakaomalizikia Baraza la
Wawakilishi kwa lengo la kuwaunga mkono na kuwalinda Wawakilishi wetu wenye kuitetea Nchi ya Zanzibar yenye hadhi zake zote za Kitaifa na Kimataifa.
Tunatamka wazi kuwa tuko tayari kuwatetea Wawakilishi
wetu na kulilinda Baraza letu la Wawakilishi ambalo ni
chombo cha kisheria chenye kusimamia matakwa na matilaba
ya wananchi wa Zanzibar bila ya kujali vyama vya kisiasa.
Na tunauthibitishia ulimwengu kuwa tutalinda amani na
utulivu wa nchi yetu na hatutowapa mwanya maadui wa nchi
ya Zanzibar kututia ndani ya mtego wa kuvuruga neema na
amani na mfungamano baada ya Allah Subhana wa Taala
kuiokoa Zanzibar baada ya nusu karne ya fitina baina ya
ndugu wa nchi moja.
Wabillaahi Tawfiq.
……………………………………….
AMIR: Farid Hadi Ahmed
Msemaji Mkuu wa Umoja wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislam Zanzibar.
NAKALA:
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Spika na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar.
Waziri wa Katiba na Sheria
Kamishna wa Polisi.
Viongozi wa Dini na Jamii.
Vijana wa Umoja wa Kitaifa (Wanafunzi wa Vyuo
Vikuu).
Mabalozi na Wawakilishi wa Nchi za Nje.
Waandishi na Vyombo vya Habari.
Viongozi wa Vyama vya Siasa.

No comments:

Post a Comment