Ndugu waislamu,
Ilinukuliwa na Ibn Umar RAA kwamba,
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu SAAW alikuwa akifanya I’tikaaf katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani
صدق رسول الله صلى الله عليه وسلم Sadaqa RasuluLlah SAAW
Tujitahidini kwa kila mwenye kuwa na nafasi asiikose fursa hii.Mtume S.A.W alikuwa kila kumi la mwisho la Ramadhani akikaa Itikafu.
Maana ya Itikafu ni kuwa ni kikaoo cha msikitini kwa kufanya ibada bila kutoka kwenda kufanya shughuli na mahangaiko ya dunia ila kwa udhuru tu.Kukaa huku kunanzia kabla ya kuchwa jua siku ya tarehe 19 au ishiri yenyewe unakuwa tayari ndani ya msikiti hutoki humo mpaka mwandamo wa mwezi wa sikukuu.Unachua mahitajio yako yote muhimu ili usiwe na sababu za kukutoa nje.Inapendekezwa ukae kwenye msikiti ambao unasaliwa Ijumaa ili usiwe na sababu ya kutoka kwenda kufata Ijumaa msikiti mwengine.Kusudio la kikao hichi ni Ibada tu. Kusali, dhikri, mawaidha na Dua. Malipo yake ni makubwa sana.Na tusisahau pia uskiu wa Lailatu Qadri umo katika kumi hili la mwisho.
Tujitahidini kwa kila mwenye kuwa na nafasi ya kuweza kukaa Itikafu afanye hivyo na asisahau katika Dua zake kuiombea nusra,amani,utulivu,kheri na baraka na ukombozi nchi yetu ya Zanzibar.
TANBIHI
Unapokuwa na udhuru wa kufiwa au moja katika watoto au watu wako mgonjwa unaruhusiwa kwenda na kurudi kuendelea na kikao cha Itikafu.Pasipo dharura au ulazima wa kutoka hairuhusiwi kufanya hivyo.
Pia tujiepushe na kulala sana msikitini hata ibada za Kiamu cha usiku zinakupita.Na vile vile mazungumzo yasio kuwa ya dini hayatakiwi ndani ya msikiti.
Wabillahi at tawfiq.
No comments:
Post a Comment