KAMA KWELI MUNATAKA KUJENGA NCHI VIONGOZI NYOTE RUDISHENI NYUMBA ZA WATU NA MASHAMBA YAWATU MULIYO WANYANGANYA WATU 1964 MAPINDUZI MAANA ZOTE HIZO NI MALI ZA THULMA NA KAMA HAMUKURUDISHA MUTAKWENDA WALIPA WATU SIKU YA KIYAMA MZEE KARUMA ASHATANGULIYA NA WENZAKE WANATAMANI WARUDI DUNIANI WAJE WAEKE MAMBO SAWA LAKINI WAPI MDA UMEKWISHA BASI NA NYINYI CHUGENI KWELI KWELI AU MWISHO WENU NI MBAYA SANA.
Mansour Yussuf Himid Machano Othman Said ni miongoni mwa mawaziri waliotajwa katika kamati teule ya baraza la wawakilishi ya kuchunguza ubadhirifu uliofanyika katika sekta mbali mbali na kutumia madaraka yao vibaya wakiwemo maafisa wa Ikulu Zanzibar
Kamati imebaini kwamba, Mikataba yote ya mauziano iliyofungwa baina ya Serikali na Ndg. Juma Ali Kidawa na baina yake na Ndg. Amina Aman Abeid Karume ni batili na ya udanganyifu. Aidha, Hati ya Matumizi ya Ardhi aliyopewa Ndg. Amina Aman Abeid Karume na Mhe. Mansour Yussuf Himid, kama tulivyoitolea ufafanuzi wake katika ukurasa wa 182-183, imekiuka taratibu za kisheria na kiutawala.Mhe. Spika: Pia tumegundua kuwa: Mzee Juma Ali Kidawa sio Mmiliki halali kisheria wa Nyumba. iliyokuwa imefuatiliwa na wala hakuhusika na Uuzaji wa Nyumba hiyo kwa mtu yoyote na hakuwahi kufuatilia Utengenezaji wa Warka wa Nyumba hiyo.Mhe. Spika:Hata hivyo, kwa mujibu wa nia njema na mazingira halisi yalivyojitokeza yanaonesha Mzee Juma Ali Kidawa alihusika na kufanya kazi kwa Mhindi aliyeimiliki nyumba hiyo kabla ya kutaifishwa na Serikali.Mhe. Spika:Kamati imejiridhisha kwamba:Ndg. Ramadhan Abdalla Songa na Mama Fatma Karume walishiriki katika Udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano uliofungwa baina ya Serikali (Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati) na Ndg. Juma Ali Kidawa. Mhe. Spika:Maelezo haya yanafafanuliwa katika ukurasa wa 178 hadi wa 180 wa ripoti yetu.Mhe. Spika: Mbali na taarifa hizo, lakini pia Kamati imebaini kwamba:Ndg. Mwalimu Ali Mwalimu kama Katibu Mkuu, amechangia kufanyika kwa udanganyifu wa Mkataba wa Mauziano baina ya Wizara yake na Ndg. Juma Ali Kidawa.
No comments:
Post a Comment