Wednesday, March 13, 2013

DR KUMBI SHEIN WAACHA KUICHEZEA QURAAN NA HADITHI ZA MTUME MOHAMMED S.A.W. KWA FAIDA YAKO


Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema hatavumilia kuona baadhi ya watu wanafanya vitendo vya chokochoko za kidini kwa nia ya kutaka kugawanya Watanzania.(KAMA UNATAKA KUSEMA KWELI USITAJE TANZANIA SEMA WAISLAMU)
Akizungumza kwenye Maulidi ya kuzaliwa Mtume Mohamad (SAW) katika Msikiti wa Majumuiyat wa Temeke jijini Dar es Salaam juzi, Dk Shein alisema mgawanyiko kati ya Watanzania ni kitu kisichokubalika daima.(MWENYEZI MUNGU ANATAKA KUBAINISHA MUMIN WA KWELI NA MNAFIKI NA HARAMU NA HALALI WEWE HUTAWEZA KUEPUKA MAANA THULMA ZENU ZIMEKITHIRI SASA ALLAH ANAWANGAMIZA KIDOGO KIDOGO NA MNAJUWA HILO NDIO MAANA SASA MUNAWAFUNGA JELA WAUMINI WAKWELI NA NYINYI WANAFIKI MNAPITA MUKIENEZA KASUMBA KAMA KWELI MNAIJUWA DINI KUMBE MBUMBUMBU)
Kwenye sherehe hiyo iliyoandaliwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum, ilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na viongozi mbalimbali.
Dk. Shein alisema msingi wa dini ya kiislamu ni usawa wa binadamu kwa kila mmoja kumpenda mwenzake,(JE WEWE UNAWAPENDA WAZANZIBARI..? MBONA UMEWAPINGA MABOMU KWENYE MSIKITI..?MBONA UMERUHUSU POLISI KUINGIA NDANI YA MISIKITI NA MAJIBWA NA VIATU..?MBONA UMEUWA MTOTO PALE BUBUBU WAKATI WA UCHANGUZI MDOGO..?MBONA MUMEMUWA KIJANA WA WATU POLISI KISHA MUKAMUAMBIA BABA YAKE AJE KUMCHUKUWA MWANAWE MAITI..?MBONA SHEIKH KAULIWA KITOPE HUKUSEMA KITU..? MASHEIKH MPAKA LEO UMEWAWEKA JELA NA UNAJUWA FIKA KUWA HAWAJAFANYA KOSA JE NDIO KUWAPENDA HIVYO..? UNASEMA USAWA JE UNAKULA NINI WEWE NA WATOTO WAKO NA MKEO..? JE WAZANZIBARI WANAKULA KAMA UNAVYOKULA WEWE..? JE WAZANZIBARI WANALALA KWENYE KITANDA KAMA UNACHO LALA WEWE..? JE WATOTO WA WAZANZIBARI WANASOMA NA KUTUNZWA NA KULINDWA KAMA WANAVYOKULA NA KULINDWA WATOTO WAKO WEWE..? HUO NI USAWA JE UNAUTIMIZA MBONA ZANZIBAR INANUKA MPAKA LEO..? ni kosa kubwa kutumia dini kwa kudhulumu maisha ya mtu au mali zake.JE NI HALALI KUTUMIA CCM KWA KUTHULUMU MALI ZA WATU NA KUUWA WATU..?
Aliwasisitizia waumini hao warudi kwenye dini na kuangalia misingi yake pamoja na hadithi za Mtume (SAW).HEBU RUDI WEWE KWANZA UTAONA KUWA HATA URAISI UNAO JITAMBIA SIO WA HALALI MAANA HUKUSHINDA UCHANGUZI NA UNAJUWA JE WEWE HUHITAJI KURUDI KWENYE DINI NA MISINGI YA HADITHI ZA MTUME MOHAMMED S.A.W..?
Alisema Zanzibar ina historia kubwa ya watu wa dini zote kuishi kwa pamoja kama ndugu na yaliyotokea kwa viongozi wa dini kuuawa ni matukio mageni yanayotakiwa kuondolewa haraka.VIPI UTASAFISHA UCHAFU WAKATI WEWE MWENYEWE SHEIN NI MCHAFU..?
Awali mlezi wa msikiti huo, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alisema lazima Watanzania walinde amani yao iliyodumu kwa miaka mingi.
Alitahadharisha endapo waumini wa kiislamu wakitaka kuwadhuru wakristo kwa namna yoyote, na wakristo nao wakawa na nia kama hiyo, nchi haitakuwa salama na hakuna atakayefurahia maisha.
“Tanzania ni ya sisi sote, ndani tupo wa dini na makabila mbalimbali, hivyo inatulazimu tupendane na kuishi kwa pamoja kulinda utamaduni wetu wa upendo,” alisisitiza mzee Mwinyi.
Kwa upande wa Sheikh Majid Salehe, alisema wanasiasa waepuke kuwajaza watu maneno ya uongo na kusababisha maandamano na kuchukia serikali yao.
Sheikh huyo aliongeza kwamba endapo wanasiasa wakitumia njia hiyo watakuwa wanakwenda kinyume na matakwa ya dini na itasababisha nchi kukosa amani.
Alipongeza hatua ya Sheikh ya mkoa kutetea kwa nguvu zote suala zima la amani, kitendo hicho ni kufuata kwa vitendo mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Hata hivyo, Alhaji Salum ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, aliwatunuku watu mbalimbali vyeti vya kutambua mchango wao wa kulinda amani nchini.
Waliotunukiwa vyeti hivyo ni Dk. Mengi, Lowassa, Waziri Nahodha, Waziri wa Viwanda, Dk. Abdallah Kigoda na Mkuu wa Mkoa wa Said Meck Sadick.

No comments:

Post a Comment