Friday, March 22, 2013

WAISLAMU 52 NCHI TANGANYIKA WATUPWA JELA NA MAHAKAMA YA NCHI YAO YA KINAFIKI.



WAKOMBOZI 52 wa Watanganyika na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kusingiziwa kufanya maandamano ya haramu, wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya wanafiki na maduwi wa uislamu nchini Tanganyika juu ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, baada ya wafuasi hao kukutwa na hatia kwa makosa matatu kati ya manne yaliyokuwa yakiwakabili. Hata hivyo watakaa jela kwa mwaka mmoja kutokana na adhabu zote kwenda kwa pamoja.

Hata hivyo aliyekuwa mshtakiwa wa 48, Waziri Omar Toy, aliachiwa huru baada ya Mahakama kuridhika kwamba hana hatia kutokana upande wa mashtaka kushindwa kuthitibisha madai dhidi yake!!!

Baada ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo kusoma hukumu hiyo, ilizuka tafranwi miongoni mwa ndugu wa washtakiwa hao ambapo wengine waliangua vilio na wengine kuanguka chini.Mwanamke ambaye ni ndugu wa washtakiwa hao, alionekana kama mtu mwenye hasira sana na kutaka kumvamia askari wa kike.

Hakimu Fimbo mnafiki mkubwa katika hukumu hiyo alisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za pande zote pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka matatu dhidi ya washtakiwa hao.

Hata hivyo, Hakimu Fimbo alisema kuwa katika shtaka la uchochezi lililokuwa likiwakabili washtakiwa wanne, upande wa mashtaka umeshindwa kulithibitisha!!!!

“Mahakama imeridhika na ushahidi uliwasilishwa na upande wa mashtaka kuwa umethibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa wa 48,” alisema Hakimu Fimbo na kuongeza:

“Hivyo Mahakama imewatia hatiani washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa wa 48, katika shtaka la kwanza, la pili na la tatu na katika shtaka la nne, Mahakama imeona kuwa washtakiwa hawana hatia.!!!!

Washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama za kutenda makosa, kufanya maandamano yaliyozuiwa na Polisi na kwa pamoja kufanya mikusanyiko haramu na kusababisha uvunjifu wa amani.

Akitoa adhabu kwa washtakiwa hao baada ya kuwatia hatiani, Hakimu Fimbo alisema: “Nimezingatia kuwa karibu kila mshtakiwa ana majukumu ya kifamilia na kwa kuzingatia `nature’ (asili) ya mashtaka.!!!

Aliongeza: “Katika kosa la kwanza ninawahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela na kosa la pili pia mwaka mmoja jela na tatu mwaka mmoja jela. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.”Kauli za Mawakili
Kabla ya adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya aliyekuwa akisaidiana na Wakili Joseph Maugo, aliieleza Mahakama kuwa hawana kumbukumbu za makosa ya jinai kwa washtakiwa hao na akaiomba Mahakama iwape adhabu kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Wakili wa washtakiwa hao, Mohamed Tibanyendela aliiomba Mahakama iwaonee huruma kwa kuwaachia huru washtakiwa hao au kwa kuwapa adhabu ndogo sana.
Wakili Tibanyendelea alidai kuwa washtakiwa hao ni mara yao ya kwanza kutenda makosa hayo na kwamba wana familia ambazo zinahitaji huduma kutoka kwao huku akidai kuwa wengine tangu walipokamatwa, familia zao hazijui waliko.

Pia Wakili Tibanyendelea alidai kuwa washtakiwa wengine wanaumwa kisukari na shinikizo la damu, huku akitoa mfano wa mshtakiwa wa 21, Kassim Mohamed Chogo, aliyefutiwa mashtaka kuwa alikuwa mgonjwa na ameshafariki dunia.

No comments:

Post a Comment