Friday, March 15, 2013

DPP WA NCHI YA ZANZIBAR SI DPP NI MASHUZI MATUPUUUU


Ilipoanza tu kesi ya inayowakabili viongozi wa Uamsho, nilisema kuwa ofisi ya DPP ina mkono mkubwa katika kesi, na dhima kubwa sana.
Wengine kama kawaida yao, waliniona mimi ‘chizi’ au hamnazo. Kama ilivyo nchi yetu ya  Zanzibar na Wazanzibari, mpaka ‘ugonge ukuta’ ndio unajua kuwa umefika.
Wengine walimsifu sana DPP, Ibrahim Mzee, just kwa sababu anakwenda pale Baraza la Wawakilishi na kupiga kelele eti anatetea ‘Uzanzibari’ na huku watu wakipiga kofi. Inasikitisha sana kuona majority ya Wazanzibari tumekuwa hivi, yaani tumekuwa wavivu wa kufikiri hata mtu kumuuliza jina lake, anataka mtu mwengine amsemee.
Ofisi ya DPP sasa, mumeiona, imejitokeza rasmi hadharani — kesi ya juzi ya Uamsho. imekuja, katika lugha ya kigeni ‘true colour’ yake.
Na bado. DPP ofisi haifai, na nilisema pale uajiri wote ni mazonge mazonge tu, ujamaa na kujitegemea, mtoto wa nani, na umezaliwa wapi, na wa nani huyu mtoto wa halo yake na chachi yake ndio upate kazi, vyeti vyao ….., hao walimu wao wanaowasomesha nao…….; hivi kweli usomee sheria kisawa sawa, usijue kesi hii inasikilizwa court ipi (regional, district, high court n.k); hivi kweli hatujui nani anastahiki kutoa ombi la dhamana na nani hahusiki..? Hao nasikia ni watu wenye viwango vya BA Law au MA law (LLB na LLM), it’s a mockery of justice! (hili neno labda watakuwa wanalijua zaidi nikisema hivi ‘mockery of justice’.
Unajua kuwa so long kama hujazaliwa Zanzibar, na huna nasaba na hapa, huwezi hata siku moja kuwa na huruma na zanzibar na watu wake. Ofisi zetu zimejaa wageni, bara wanatutawala nje na ndani ya muungano. Watanganyika wamejaa ofisi zetu, na juu yao, wapo maofisa wanaojiita ni Muungano, ndio hao akina Kikwete, Kinana, Nchimbi, Chiligati, n.k
Sitaki kusema sana, maana mwisho mtasema mimi ni……mwisho mtasema mimi ni……..jamani wazanzibar hebu amkeni. Ina maana nyie wazanzibari wenzangu, mnakubali kila jambo, anakuja mtu anauza ‘dawa ya panya,viroboto, mende, kunguni, na eti dawa za asili’ mnanunua tu.
Anakuja mtu anasema yeye ni DPP kwa sababu anasema sana, na anasema kile mnachotaka kukisikia, mnakuwa sawa tu. Anautaja Uzanzibari, au kero za muungano, huku anakuumizieni watu wenu, mnaitikia tu – hewala bwana tu.mpaka lini..? huyu DPP anatakiwa pia ashtakiwe maana kisheria yeye pia amejipa madaraka yasio muhusu je atashtakiwa je atajiuzulu au ndio mapinduzi daima...?

No comments:

Post a Comment