Viongozi wote watatu: Dr.Shein, Maalim Seif, na Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika Seif iddi wanapenda kuimba nyimbo ‘uhifadhi wa mazingira’; na wakati mwengine waajivuna ‘zanzibar ya kale’ – zanzibar ilivyokuwa.
Inasikitisha sana kuona kuwa ujenzi umeanza pale Botanical Garden pale Kilimani/Migombani. Inashangaza kuwa Dr.Shein hajauona ujenzi huu wala Seif Ali Iddi au maalim Seif ilhali kuwa wanapita kila siku hapo zaidi ya mara tatu kwa siku. Ujenzi unafanywa mbele ya macho yao.
Hivi kweli hawajaona au hawataki kuona au mushakula furushi lenu ndio maana muko kimya..? Hivi kweli Dr.Shein, ziara yako ya juzi ya Mkoa Mjini Magharib, hujaona ujenzi huu – ambao, by any definition, hauruhusiwi kwa kuzingatia kuwa hilo ni eneo ‘ama tuliite reserved area au preserved area’, tena ni eneo nyeti sana (kituo cha polisi ndio mpaka wa ukuta).
Kihistoria eneno hili lilikuwa na miti mingi sana ya akila aina, kutoka kila kona ya dunia, na ni eneo pekee kwa Afrika Mashariki (la kwanza kuwa na botanical garden).
Leo yote imefyekwa fyekwa kama nyasi za uwanja wa mpira, na sasa inamegwa kidogo kidogo na kuanza kujengwa. Alianza Naushad, halafu kituo cha Polisi, sasa nani sijui amepewa.
Itakavyokuwa huyu anayejenga hapa ama ni CCM au mtu mkubwa serikalini, au ni mtu wa biashara anayeiunga mkono CCM 100%.
Hivi kweli Dr.Shein tukuamini vipi, akifanya Farid, Azan, Msellem n.k. tunawaweka ndani mpaka watu wanasahau kama wako ndani, wakifanya wengine na kuhujumu mali ya umma, unawabeba kichwani na kuwaimbiya taarabu kwa raha zako huwo uwaminifu mulio apishiwa wakati mukiwa vingozi uko wapi..? au uwamanifuu wenu ni kwa masheikh tu lakini wengine wachee waicheze serekali na mali za serekali kama hawana akili vizuri sio..?
Hivi kweli wakubwa wote serikalini mnataka kusema hamjaona hapo kuwa panajengwa ilhali haparuhusiwi kujengwa.? Hii ni njia kuu, wakubwa wote takriban 95% wanapita njia hii go-and-back. Basi hakuna hata mmoja aliyeweza kusema kitu..? nyote mekuwa mabubu...? au mazezeta..?
Iko wapi Idara ya Ardhi, au ile Mipango Miji..? Juzi juzi tu, Idara hizi mbili walikwenda kuvunja nyumba za masikini kule Kwarara/au sijui kunaitwa wapi eti “wamevamia” ardhi just kwa sababu “hamkuelewana vizuri kimaslahi sio..? Huyu hapa mnamuacha kama alivyo, kwa sababu……..???
Dr.Muhammed Juma – Mkurugenzi wa Mipango Miji, na January Fussi – kweli hamuoni haya, yanayofanyika hapa Kilimani/Migombani botanical garden?? Mnawavunjia nyumba maskini ya Mungu, hawa mnawawacha. Dr.Muhammed, ujue wewe kuwa unatoka mbali,umehangaika sana mpaka umefika hapo (Habari za Paris balahau…..est que tu….?)
Pale Mambomsiige, na ile open space, mmempa mtu anajenga hoteli, pamoja ya kuwa wakaazi wa mji mkongwe wamekataa tena kwa petition, mwisho Dr.shein anasema kuwa serikali haihojiwi kwa kuuza chake. Sasa, na wengine watauza ardhi, gari, na nyumba za serikali and don’t question please. Mimi nahisi kuuza mali za serikali ndio inahitaji kuhijiwa zaidi kuliko kuuza mali ya mtu binafsi au sio..?
Tunaomba tuone hatua imechukuliwa. Kinyume chake,wengine tutaomba viwanja pale Mnazi Mmoja vya club za mpira ili tujenge vyoo na bafuu za kuogea wakija rai wa nchi ya Tanganyika,Kenya,Uganda,Burundi,Rwanda na wakongo wataoga na kutulipa pesa au sio hakuna kuhojiwa kila moja afanye anavyotaka maana sio nchi hii ni tambara kila moja anajifutia anavyotaka deki twende,kamasi twende,matapishi twende, na wala musituhoji.
No comments:
Post a Comment