Wednesday, April 17, 2013

MAMILLIONI KWA MAMILLIONI YANAINGIA NCHINI TANGANYIKA NA ZANZIBAR LAKINI YOTE YANAISHIA KWENYE MATUMBO YA VIONGOZI.



Mbunge ahoji matumizi ya fedha za wahisani
JIBU LA SWALI LA MBUNGE VITI MAALUM
na Mwandishi wetu wa siri afichuwa mamillioni yanayo liwa na viongozi wa nchi mbili hizi ya Tanganyika na Zanzibar, Dodoma.                                                                                                                                                                                        MBUNGE wa Viti Maalumu, Thuwayba Idris Muhamed (CUF), ameibana serikali ya Tanganyika na kuitaka ieleze itawasaidiaje Watanganyika na Wazanzibari ili apate kuelewa fedha iliyokopwa kutoka kwa wahisani imetumika katika mazingira gani maana mamillioni ya pesa yanakuja kutoka kwa wahisani lakini nchi hizi mbili ziko vile vile kama zilizo tapikwa na paka baada ya kula vumba la samaki.
Mbunge huyo pia alitaka kujua serikali ya Tanganyika na Zanzibar ina uhakika gani kwamba fedha hiyo imefanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo. Akijibu swali la msingi la mbunge huyo, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema fedha zinazokopwa zimekuwa zikitumika kugharamia miradi ya maendeleo hususan miundombinu ya nishati barabara, maji, afya na elimu.
Alisema kuwa fedha zilizokopwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 na 2011/2012 zilielekezwa katika miradi ya ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawati 60 jijini Mwanza na ni euro milioni 61 kutoka HSBC.                Aidha, alisema ujenzi wa kufua umeme wa megawati 100 Ubungo, Dar es Salaam kiasi cha dola za Marekani milioni 103.728 kutoka HSBC zimetumika.
Alisema fedha nyingine zilizokopwa katika kuelekezwa katika miradi mbalimbali ya barabara nchini dola milioni 350 ni kutoka Benki ya Credit Suisse. Mkuya pia alieleza kuwa serikali ilikopa dola za Marekani milioni 178.125 kutoka Exim Bank ya India kugharamia miradi mbalimbali ya maji, pia zilikopwa dola za Marekani bilioni 1.2 kutoka Exim Benki ya India ya China kugharamia ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na dola za Marekani milioni 230 kutoka Standard Bank kwa lengo la kugharimia miradi mbalimbali ambayo ilikuwa imeainishwa katika bajeti ya maendeleo kwa mwaka husika (Kitabu Vol. 1V), upande wa nchi ya Tanganyika.
Kwa upande wa nchi ya  Zanzibar, Mkuya alisema kuwa Serikali ya Zanzibar ilikopa dola milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kutoka Serikali ya Korea Kusini na dola milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Zanzibar kutoka Serikali ya Watu wa China.
Pia alisema kuwa dola milioni 42 zilikopwa kwa ajili ya uimarishaji wa sekta ya elimu kutoka Benki ya Dunia, dola milioni 21 zilikopwa kwa ajili ya mradi wa serikali mtandaoni na miradi mingine mingi ambayo ilitekelezwa kwa utaratibu huo.
je dolla milioni 50 na dolla milioni 70 na dolla milioni 42 na dolla milioni 21 walizo kopa nchi yatu ya Zanzibar au ndio tusema baada mkoloni mweusi kuchukuwa anazo taka kisha akaturushi na sisi hizo zilizo baki swali hapa ni je hizo pesa ziko wapi maana Zanzibar iko vile vile je mushagawana tayari..???

No comments:

Post a Comment