Sunday, April 7, 2013

WARIOBA ALITHANI YEYE NI NYERERE WA PILI MAALIM SEIF AMUWEKA SAWA KUHUSU KATIBA


KATIBU mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad ambae pia ni makamo wa raisi nchini Zanzibar amemshangaa Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu Katiba mpya nchini Tanganyika ((Tanzania)), Jaji Joseph Warioba kichwa cha korosho kuhusu aina ya mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba mpya ya warioba sio ya Watanganyika na Wazanzibari kama alivyo kuwa akisema.
Maalim amesema anamshangaa Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa kuja na mapendekezo yake, na anawaona Wazanzibari kuwa na akili za kitoto, jambo ambalo wameshang’amua.
Maalim Seif alisema: “Tunamshangaa sana Jaji Warioba kwa kutugeuza Wazanzibari ‘danganya toto’ anatufanya sisi tuna-akili za kitoto…hizo serikali tatu ni nani hao waliyozitaka,” alihoji Maalim Seif.
Alisema maoni ya wananchi na viongozi wa Zanzibar, waliyoko madarakani na waliyostaafu (aliwataja kwa majina) yanatosha kuzingatiwa na Tume kuhusu aina gani ya mfumo wa Muungano wanaouhitaji Wazanzibari.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar, alisema asilimia kubwa ya Wazanzibari, pamoja na viongozi wanaoitakia kheri Zanzibar, walitoa maoni ya kutaka Zanzibar, iwe na MAMLAKA yake kamili ya ndani na kimataifa.
Akionekana kuzumza kwa kukereka katika mkutano wa hadhara uliyofanyika leo jioni Mkwajuni, Kaskazini Unguja. Maalim Seif, alimueleza Warioba kuwa Zanzibar serikali tatu wala nne hawazitaki na kinachotakiwa ni kuzingatia maoni ya kweli yalitolewa na Wazanzibari na sio ‘danganya-toto’:
“Mhe Jaji Warioba…tunakwambia bila Zanzibar yenye MAMLAKA yake kamili ndani na kimataifa hatutakubali…kwa hivyo rudia maoni ya Wazanzibari,” alisisitiza Maalim Seif..

No comments:

Post a Comment