Tuesday, April 23, 2013

KHALEED NGWIJI ANA HAYA YA KUSEMA KUHUSU ZANZIBAR YETU KUWA NA MAMLAKA KAMILI

Photo: Gwiji-wazanzibar tuungane kulinda maslahi ya Nchi yetu.

Mwenyekiti wa vijana Zanzibar (VUK)Khaleed Gwiji asema kuwa Katiba ndani ya Nchi ni Kinga madhubuti baina ya Wananchi wenyewe na Watawala wao.

Gwiji ameyasema hayo wakati alipokuwa akichangia katika mjadala maalumu ulioandaliwa na taasisi ya wanasheria Zanzibar (law Sociey  ZLS )  hapo katika ukumbi wa taasisi mjini Unguja.

Mjadala huo ambao uliongozwa na Mwanasheria mkuu wa Serilali Bwana Othman Masoud pia uliwashirikisha wanafunzi mbali mbali wa vyuo vikuu pamoja na watu kutoka taasisi nyengine za kijamii.

Mdahalo pia uliokuwa na lengo la kujadili  nchi ya Zanzibar na mustakbali wake kupitia uundwaji wa katiba mpya.

Wakati akichangia Gwiji amesema kuwa anashangazwa na Serikali  kuwa bado haijawa na utamaduni wa kuheshimu Katiba na ndio maana hadi leo viongozi wa Uamsho wananyimwa dhamana jambo ambalo ni haki yao ya Kikatiba.

Pia amekiri kuwa ni kweli ndani ya jamii ya watu wa Zanzibar wapo watu tafauti ambao wanatafautiana maoni yao  katika muono wao wa uundwaji wa katiba mpya lakini busara iliobora ni kuheshimiwa mawazo yaliowengi ambayo wametoa kwa kutaka Zanzibar yenye mamlaka kamili.

‘’Ikiwa wananchi waliowengi ndani ya visiwa hivi vya Unguja na Pemba wametoa maoni yao ambayo simengin bali nikudai Zanzibar yenye mamlaka kamili basi ipo haja ya Serikali kuhakikisha kuwa Tume ya mabadiliko ya katiba inaheshimu mawazo hayo na kuyafanyia kazi”alieleza Gwiji.

Aidha amefahamisha kuwa kwa sasa wakati umefika kwa Serikali yetu ya Zanzibar kuwa na agenda ya Zanzibar kwanza ili tupate hatma njema pamoja na  mustakbal mzuri wetu sote pamoja na vizazi vyetu vya sasa na baadae.

''Lazima viongozi wetu wabebe agenda ya uzalendo na utaifa badala ya maslahi ya vyama vyao binafsi, Zanzibar ni zaidi ya vyama''aliseama gwiji.

Nao kwa upande wa baadhi ya wananchi wengine ambao walipata nafasi ya kuchangia kwa kutoa maoni yao wamesema kuwa bado hatujachelewa kuidai Zanzibar huru isipokuwa jamii ya kizanzibar inapaswa kubadilika kwa sasa kutokana na wakaazi wengi kujawa na jazba jambo ambalo haliwezi kutufikisha tunapotaka.

Mwenyekiti wa vijana Zanzibar (VUK)Khaleed Gwiji asema kuwa Katiba ndani ya Nchi ni Kinga madhubuti baina ya Wananchi wenyewe na Watawala wao.

Gwiji ameyasema hayo wakati alipokuwa akichangia katika mjadala maalumu ulioandaliwa na taasisi ya wanasheria Zanzibar (law Sociey ZLS ) hapo katika ukumbi wa taasisi mjini Unguja.
Mjadala huo ambao uliongozwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali Bwana Othman Masoud pia uliwashirikisha wanafunzi mbali mbali wa vyuo vikuu pamoja na watu kutoka taasisi nyengine za kijamii.
Mdahalo pia uliokuwa na lengo la kujadili nchi ya Zanzibar na mustakbali wake kupitia uundwaji wa katiba mpya.
Wakati akichangia Gwiji amesema kuwa anashangazwa na Serikali kuwa bado haijawa na utamaduni wa kuheshimu Katiba na ndio maana hadi leo viongozi wa Uamsho wananyimwa dhamana jambo ambalo ni haki yao ya Kikatiba.
Pia amekiri kuwa ni kweli ndani ya jamii ya watu wa Zanzibar wapo watu tafauti ambao wanatafautiana maoni yao katika muono wao wa uundwaji wa katiba mpya lakini busara iliobora ni kuheshimiwa mawazo yaliowengi ambayo wametoa kwa kutaka Zanzibar yenye mamlaka kamili.
‘’Ikiwa wananchi waliowengi ndani ya visiwa hivi vya Unguja na Pemba wametoa maoni yao ambayo simengine bali nikudai Zanzibar yenye mamlaka kamili basi ipo haja ya Serikali kuhakikisha kuwa Tume ya mabadiliko ya katiba inaheshimu mawazo hayo na kuyafanyia kazi”alieleza Gwiji.
Aidha amefahamisha kuwa kwa sasa wakati umefika kwa Serikali yetu ya Zanzibar kuwa na agenda ya Zanzibar kwanza ili tupate hatma njema pamoja na mustakbal mzuri wetu sote pamoja na vizazi vyetu vya sasa na baadae.
”Lazima viongozi wetu wabebe agenda ya uzalendo na utaifa badala ya maslahi ya vyama vyao binafsi, Zanzibar ni zaidi ya vyama”aliseama gwiji.
Nao kwa upande wa baadhi ya wananchi wengine ambao walipata nafasi ya kuchangia kwa kutoa maoni yao wamesema kuwa bado hatujachelewa kuidai Zanzibar huru isipokuwa jamii ya kizanzibar inapaswa kubadilika kwa sasa kutokana na wakaazi wengi kujawa na jazba jambo ambalo haliwezi kutufikisha tunapotaka.

No comments:

Post a Comment