WAKATI watanganyika bado wanatafakari hotuba ya Rais wao Jakaya Kikwete aliyoitoa siku tatu zilizopita akiwa sihi watanganyika pamoja na viongozi wa dini mbili kubwa nchini Ukiristo na Uslamu leo vita kubwa baina ya dini hizo imezuka Tunduma Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya.
Vita hiyo iloyodumu takriban masaa matano imelazimu Askari wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo ya Tanganyika kikosi maalum cha kutuliza Ghasia (FFU) kuingilia kati na kwenda mitaani humo na kupiga mabomu ya machozi kila mahali huku ikitoa amri yakuwataka wananchi kuingia ndani na kulala mchana.
Chanzo cha virugu hizo kubwa zilizodaiwa kuwa zimesababisha msikiti mmoja kuchomwa moto na mengine miwili kunusirika kuchomwa moto maeneo ya Mwaka na Kisimani zinadaiwa kuwa inatokana na mzozo wa uchinjaji nyama ambao Rais Kikwete alilitolea ufafanuzi na kusema kwamba busara itumike katika kutatua mzozo huo.
Akizungumza na mwandishi wetu wa free zanzibar people from mkoloni mweusi wa siri mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema kwamba mbali na mabomu ya machozi kupigwa ovyoa ovyo na polisi pia barabara zimefungwa, maduka yamefungwa huku matairi yakiendelea kuchomwa moto mabarabarani.
No comments:
Post a Comment