Sunday, April 28, 2013

KILA ANAYE HOJI MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR HUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA,HUULIWAA,HUNYANGANYWA MADARAKA KAMA NI KIONGOZI, AU HUWEKWA JELA KWA NINI..??


Zanzibar na Tanganyika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yakulazimishana kwa mabavu na nguvu za kijeshi na polisi nchi ya Tanganyika thaidi ya nchi ya Zanzibar ni zao la kuungana kwa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, ambazo ziliungana Aprili 26, 1964 bila ya kuuliza rai wao kama wanautaka au hawautaki.
Lakini miaka 49 tangu kuwapo kwa Muungano huo, suala linaloulizwa na Watanganyika, na Wazanzibari ni je, Muungano umeimarika au unadhoofika.? Yapo mawazo tofauti kutegemea na mtazamo wa mtu na vigezo anavyotumia kukiona kitu kimeimarika au kimedhoofika.
Kwa mtazamo wa wengi hapa nchini Zanzibar, Muungano unachechemea, yaani unakwenda ule mwendo unaoitwa ‘ kiguru cheche cheche’.
Kilicho wazi ni kuwa Watanganyika hawaelewi Muungano unatoka wapi na nini maana ya Muungano wao wanaona kama ni kula makongoro tu.ukija Zanzibar wanaelewa Muungano unakotoka hapa ulipo, lakini hawana hamu tena wala uhakika ni wapi hasa unakoelekea na wengi wao wanaona bora uishia hapa hapa kabla haujawamaliza.
Kila baada ya siku chache unasikia malalamiko mengi kutoka kwa watu wa pande zote mbili,nchini Tanagnyika na nchini Zanzibar pia, juu ya muundo na namna Muungano unavyoendeshwa. Haya yote yamepewa jina la kero za muungano.
Malalamiko ya muungano
Hivi karibuni tumesikia bungeni mjini Dodoma malalamiko mapya. Nayo ni kuwa majimbo madogo ya Zanzibar yanapewa mafungu mawili ya mfuko wa jimbo wakati ya Tanganyika yakibakiwa na fungu moja.

Kinachosahauliwa ni kwamba hata wakati wa kuungana hakuna aliyekuwa hafahamu kwamba Tanganyika ni kubwa na Zanzibar ni ndogo, lakini pande zote mbili zilikubaliana kuwa washirika sawa wa Muungano baina ya Nyerere na Mzee Karume.tafauti na sasa kumekuwa na kaka mkubwa na mdogo wake. Madai mengine ni madai kuwa Watanganyika wananyimwa haki ya kumiliki ardhi visiwani na kwamba Wazanzibari wamejazana kwenye Bunge la Muungano wakati Watanganyika hawaruhusiwi kuingia kwenye Baraza la Wawakilishi.
Lawama au kasoro hizi zinakwenda sambamba na malalamiko ya Wazanzibari kwamba Watanganyika wamejazana katika taaasisi za Muungano zilizopo visiwani, kama vile, Benki Kuu (BOT), Mamlaka ya Mapato Tanganyika  ((Tanzania)) (TRA)Ubalozi nje ya nchi zote ni Watanganyika n.k.
Katika hili zimetoka kauli zilizojaa hasira hata ndani ya Baraza la Wawakilishi za kutaka ((TRA)) ifunge virago vyake na kuondoka Zanzibar kwa kile kinachodaiwa kuwapo ajenda ya kuua uchumi wa nchi ya  Zanzibar, hasa katika sekta ya biashara.
Kwa bahati mbaya yote haya yanaonekana kama yanapuuzwa na viongozi na unachokisikia ni kuwa viongozi wa pande mbili za Muungano huu feki wanalishughulikia suala hili kwa misingi ya utashi wa kisiasa na sio kwa faida ya wananchi wa nchi hizi mbili.
Taarifa kuhusu kuungana
Siku ile ya tarehe 26 Aprili, 1964, saa 10 jioni watu wengi walikuwa wamekaa kwenye vijiwe vyao na kupumzika kijiwe kimoja maarufu cha Mtaa wa Baraste Kipande, mjini Unguja,watu wakizungumza na kungojea zamu zao ifike ili waweze kucheza dhumna na karata na bao.

Alikuja mwalimu mmoja wa skuli,na kueleza kuwa nchi yetu ya  Zanzibar na nchi ya Tanganyika zimeungana na mkataba wa muungano umetiwa saini mjini Dar es Salaam kati ya marais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Sheikh Abeid Amani Karume (Zanzibar).
Wazee na vijana waliacha mazungumzo waliyokuwa nayo na michezo yote … bao, dhumna na karata ilisimama. Mjadala ulianza na wengi walishangazwa na habari zile.
Mtu mmoja aliyepigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kushiriki kujenga daraja la Mto wa Kwai (angalia filamu ya sinema ya Bridge over the River Kwai) kule Mynamar, wakati ule Burma, Mzee Maulidi aliyejulikana kwa jina la ‘Kade Vondik’ alisema: “Tumekwisha.” Nini alichokusudia kulitegemea mtazamo wa mtu na tafsiri ya neno hilo.
Siku iliyofuata watu wengi walitumia muda mrefu kusikiliza redio na kusoma magazeti kujua habari za Muungano. Hapakuwa na sherehe zozote zile kuadhimisha kuungana kwa nchi hizi mbili unaweza kujiuliza kwa nini...?? Siku chache baadaye palifanyika mkutano wa hadhara ambao kila pembe ya uwanja wa mkutano walikuwapo askari waliobeba silaha wakitokea nchi ya Tanganyika ambao inasemakana waliletwa kuilanda Zanzibar ati isivamiwe.unaweza kujiuliza tena ivamiwe na nani..?? na ilikuwa ishavamiwa tayari na Watanganyika wakati huo.
Hapo Mzee Karume aliwauliza waliohudhuria kama walifurahia hatua ya kuungana au vipi. Sauti zilipaa kwa kusema, “Tunautakaaa!”
Hofu
Watu wengi waliiona hatua ya Mzee Karume ya kuwauliza wananchi kwa namna ile kama walikuwa wanautaka Muungano au vinginevyo kwenye mkutano ule ilikuwa na kasoro.

Kwanza, ilikuwapo dhana kuwa watu wangeulizwa kwanza kabla ya kuundwa kwa huo Muungano na siyo kuunganisha nchi na baadaye kuwauliza watu.
Pili, suala kama lile walihisi lilihitaji kupigiwa kura ya maoni. Tatu, ni kwamba mazingira yaliyokuwapo pale ya kila pembe kuwapo askari wa Kitanganyika yalikuwa ya kutisha na kwa hivyo hayakumfanya mtu kujisikia kuwa huru kutoa hisia zake zozote zaida ya tunautaka.
Zaidi ya hapo ni kwamba wakati huo watu wengi waliokuwa na mawazo tofauti na Serikali juu ya masuala mbalimbali walikuwa wakipotea kimyakimya na mpaka leo hawajulikani wako wapi watu hao wala makaburi yao yako wapi watu hao, hivyo hakuna hata mtu mmoja ambaye angethubutu kupinga hadharani. Muungano ulipo undwa ulionekana zaidi kuwa wa kisiasa kuliko wa kiuchumi.
Siku ya pili au ya tatu baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi, baadhi yao sasa marehemu, waliambiana vipi mambo haya na wengi wameshtukizwa tu na kuundwa kwa Muungano huu feki.Wapo watu waliofurahia kwa kueleza huo ulikuwa mwisho wa kamata kamata ya watu na kupotea kwa watu na kuuliwa watu kisiri siri bila ya kujulikana makaburi yao yaliyokuwa yakiendelea nchi Zanzibar, lakini wapo walioona haikuwa jambo la busara bali na kupelekwa pelekwa tu.
Mengi yalizungumzwa na mjadala uliendelea kwa siku nyingi, lakini kwa sauti ya chini huku watu wakiendelea kupotea wala muungano haikuwa ni sababu ya kuzuwia watu kupotea na kuliwa kisiri siri.
Nyerere siku moja alipokuja nchini Zanzibar aliwaambia viongozi kwamba wakiwamaliza hao wanaowaita siyo wanamapinduzi kuwauwa watauana wenyewe kwa wenyewe.
Ukweli ni kwamba palikuwa hapana fununu ya Zanzibar na Tanganyika kuungana. Hata aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Wolfango Dourado, aliyekuwa Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi (Baraza la Mawaziri) na mawaziri wa Serikali ya Rais Karume wamenukuliwa wakisema hawakushauriwa juu ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika na kuanzia hapo pia kila aliyepinga muungano huwa alifukuzwa kazi na kuishia jela au pia aliuliwa katika mazingira ya kutatanisha.
Dourado aliwekwa kizuizini wakati wa utawala wa Nyerere kwa kusema hakushauriwa Muungano ulipoundwa na kudai haukuwa halali na wengine wengi wamepotea hawajulikani walipo raisi mstafu Jumbe kavuliwa madaraka Maalim Seif alivuliwa madaraka na akasundwa jela weee na sasa uamsho hao hapo ushahidi kwa watu wanauthani kuwa kuhoji muungano si lolote ukihoji utapotea tu au utaka jela au kuuliwa katika mazingira ya utatanishi.
Watanganyika wanastahili kuamka na Wazanzibari wanastahili pongezi
Sasa, Muungano huu feki uliopitia kila aina ya mikiki na dhoruba umetimiza miaka 49 ya muungano wa lazima, wakati nchi nyingi za Kiafrika, Kiarabu na Asia zilizochukua hatua kama hii miaka ya nyuma zimeshindwa kuendelea kuungana kutokana na sababu za kisiasa na kiuchumi.

Watanganyika na Wazanzibari tumekuwa tofauti, kwani pamoja na matatizo yote tuliyonayo ya kisiasa na kiuchumi bado tumeishikilia kamba inayo tunyonga.
Kwa Watanganyika wengi,Wazanzibari wengi, suala la kuungana siyo tatizo. Kinachozusha mabishano na mivutano ni masuala gani ni ya Muungano na mambo gani yapo chini ya mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia serekali ya Zanzibar ipo ya Tanganyika imejificha wapi pia nchi moja kujifanya kaka mkubwa na nyengine kufanywa kama mkoa wa pwani.
Malalamiko juu ya mfumo wa Muungano yamesikika mara nyingi na yanaendelea kusikika. Katika mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya ya Tanganyika, suala la Muungano lilitawala mjadala.
Zanzibar wapo wanaotaka muundo wa sasa wa Serikali mbili uendelee, wapo wanaosema uwe wa Serikali moja wengi wao ni wahafidhina watumwa wa mkoloni mweusi Tanganyika na wapo wanaopendelea mfumo wa shirikisho wa Serikali tatu.
Lakini, pia lipo kundi linalotaka Muungano wa mkataba na lipo kundi wanaosema hawana haja ya Muungano hata kuusikia. Hii ni kudhihirisha kuwa wananchi wengi bado hawakupenda na hawatapenda kuendelea na Muungano huu feki,wakati umefika wa kuvunja au kama viongozi wanaogopa basi wawaulize wananchi katika kura ya maoni.
Wakati huu Watanganyika wanapoandika Katiba yao  Mpya,Wazanzibari wana katiba yao viongozi wasilififishe suala la Muungano huu feki, kama mjadala kuhusu je muungano wananchi  wanaoutaka au hawautaki wawaulize wala wasione haya kuwauliza.ila ikiwa viongozi watalazimisha na kuendele na udikteta wao wakuwalazimisha watu kuwa na muungano huu kwa kuwa Tanganyika inanufika na Wahafidhina wa Zanzibar wananufaika basi mutakuja kulia mdomo juu kama mbwa koko Gaddafi,Ben Ali,Saleh,Hussein Mubarouk na sasa Assad wangalieni kama hamjasoma basi wananchi watawasomesha.

No comments:

Post a Comment