Amani ikitoweka, masikini watapoteza nini..??
MJADALA juu ya tishio la kutoweka kwa amani nchini umeshika kasi. Wanasiasa wanawalaumu viongozi wa dini; viongozi wa dini wanawalaumu wanasiasa na serikali; serikali inawalaumu viongozi wa dini pamoja watu “wasiojulikana”. Kila upande unalaumu na hakuna upande unaokubali hadharani kuwa ni nani haswa amesababisha tishio hili.
Rais Jakaya Kikwete raisi wa nchi ya Tanganyika mara kadhaa amesikika akisema kuwa katika vita ya kidini hakuna mshindi. Kaulimbiu hii na kibwagizo hiki kitamu kimedakwa kwa ustadi na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari wanaoshindilia kuwa amani ikitoweka kila mtu ataathirika. Wote hapo juu hakuna anayetumia akili wala marifa wala muda kujiuliza nini chanzo cha kutoweka kwa amani nchini ni nini haswa chanzo cha kutoweka amani hawajiulizi.
Wasomi mbali mbali walifafanua kuwa amani ni tunda la haki. wakachambua kuwa bila haki amani itatoweka. Kisha wakasema, Zanzibar kuna amani lakini siyo kwamba kuna haki bali kuna tumaini kuwa siku moja haki itatendekea.
Tumaini la kutendewa haki ndilo limeshikilia mstakabali wa kuwa na amani nchini. Kinachoelekea kutokea kwa sasa, ni kukata tamaa. Watu wengi hasa masikini wamekata tamaa kuwa haki haiwezi kutendeka tena na ukali wa maisha unaongezeka kila kukicha Wazanzibari wana safa na maisha wala hawana mtetezi wala hawana wakuwahurumia.
Kukata tamaa kwa wananchi walio wengi kumeambatana na serikali ya majambazi SMZ kukosa uwezo wa kuongoza na kutawala. Ni rahisi kuwaambia watoto wenye njaa watulie kidogo na wavumilie kama wanaona wazazi wanashughulika kupika hata kama chungu kinachotokota kimejaa mawe tu. Jitihada za wazazi zinaweza kuwafanya watoto wenye njaa wapitiwe na usingizi na siku hiyo ipite.
Serikali ya majambazi ya SMZ imeshindwa kabisa kushughulikia viashiria vya kutoweka kwa amani na hasa kuhakikisha haki inatendeka na masikini wanashughulikiwa kero zao. Kinachoonekana kutokea ni serikali kutumia ubabe wa nguvu za jeshi na polisi kila masikini wakinuwa sauti zao kudai haki. serekali kutumia baadhi ya taasisi ili zicheleweshe masikini kudai haki zao kwa njia yoyote watakayoona inawasaidia kwa sababu amani iwepo isiwepo hali ya masikini haibadiliki.
Mwanzo wa wiki hii wamiliki wa vyombo vya habari wamekutana jijini DSM huko nchini Tanganyika na kujadili suala hili wakitofautiana waziwazi juu ya nani anasababisha hali hii na pia ikiwa wana habari pia wana mchango katika hali hii tete. Wapo wana habari wanaolalamika kuwa wana habari wamenunuliwa na wanasiasa na kujikuta wanachochea mgogoro wa kidini nchini. Hawa wanalalamika kuwa wana habari watasababisha umwagaji damu kama ilivyotokea kule Rwanda.
Kundi jingine linakataa mtizamo huu. Linasema kule Rwanda si wana habari waliosababisha mauaji ya kimbali, bali ni wanasiasa na Vigogo. Wana habari walikuwa wanatangaza kile kinachosemwa na wanasiasa. Kwa ajili hiyo, mkutano wa wana habari pamoja na kukutana, hawakuleta jambo jipya katika mjadala huu na waliishia kulialia sawa na mtindo wa wanasiasa wetu pamoja na serikali. Hakuna aliye tayari kusema ukweli, na hakuna anayekubali kuwa anatumiwa.wala hakuna aliyejiuliza ni nini chenzo na hao wanao athirika wamesaidiwa vipi hakuna kabisa.
Kwa hali ilivyo nchini, mimi nasita kukubali kuwa amani ikitoweka watu wote watapata hasara. Hii ni kwa sababu lipo kundi kubwa hapa nchini ambalo halijafurahia uwepo wa amani inayoliliwa kuwa inaelekea kutoweka. Kundi hilo ni watu masikini wa kipato na masikini wa hali zote lakini matajiri na viongozi wao wataililia amani hii iwepo maana yao yanawaendea vizuri kabisa.
Mathalani, masikini anayekwenda katika hospitali zetu zisizo na dawa lakini akaishia kutozwa rushwa kila hatua anayopitia ndani ya hospitali. Tangu anapofika mapokezi mpaka anapata huduma anaombwa au kulazimishwa kutoa rushwa bila kujali anacho au hana. Huyu masikini ana manufaa gani na amani inayoliliwa na Serekali ya SMZ..??
Masikini anayebambikiziwa kesi na polisi japokuwa hajafanya jambo hilo ila anabambikiwa tu ili alipe mapesa ndio achiwe huyu ana manufa gani na amani inayoliliwa na serekali ya SMZ..?? au masiki kupeleka malalamiko yake polisi akaishia kuombwa rushwa kwanza ndio asaidiwe katika malalamiko yake huyu ana manufa gani na amani inayoliliwa na serekali ya SMZ..?? Masikini wengi ndio wanakaa rumande muda mrefu; kesi zao huchukua miaka mingi, na ndio wanalazimika kuuza utu wao ili kuwahonga polisi waweze kuachiwa. Nyumba zinauzwa na mashamba yanauzwa ili kuwahonga polisi wafutiwe kesi zao.
Siku hizi matajiri nao wanaweza kuwanunua polisi ili wawatese masikini waliokosana nao kwa mambo binafsi. Hivi sasa vituo vya polisi kote nchini vimegeuka kuwa vituo vya kukusanya rushwa za watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya kweli na ya kubambikizwa. Masikini anayefanyiwa haya Amani inayo hubiriwa ina thamani gani mbele ya polisi wala rushwa na waonevu wa tashi wa kisiasa..?? Tukubaliane amani haitikuja katu mbele ya maonevu na ubambikizaji wa kesi za uongo. Ikiwa wao vyombo vya Usalama Jeshi la polisi kazi yao kubwa nikulinda usalama wa raia na mali zao ,leo wao ndio wavunjaji sheria na wala rushwa na wakadamizaji wa wanyonge,jee amani kweli itakuwepo na kwa faida ya nani amani hiyo..??
Barabara zetu kuu na za mitaani zimejaa polisi wa usalama barabarani ambao kazi yao kubwa ni kukusanya rushwa tangu asubuhi mpaka jioni rushwa mtu. Polisi hawa wanakusanya rushwa kutoka kwa waendesha pikipiki na madereva wa magari , polisi hao hao wamekuwa wakitumia vyeo vyao ili kuthalilisha raia na kuwabambikizia makesi yasio kichwa wala miigui rai wema wasio na hatia.
Hivi sasa makesi ya kubambikiziwa wananchi yamejazana mahakamani na huku washukiwa wakiteseka ndani ya magereza ,Jee bado tunaita Amani..?? au tunaita uvunjwaji wa Amani..?? maana hio amani iliopo mwananchi wa kawada hafaidiki nayo zaidi ya mateso mathilaa na masundogo na kujikuta kuwa hana uhuru wala hana mtetezi wala hana wa kumlilia toka anapo amkaa mpaka anrudi kulala yeye ni mateso na hofu iliyo mja kuwa labda hatarudi nyumbani na ataishia mikononi mwa polisi wala rushwa na kujihisi kama yatima aliyesahauliwa.
Amani hii ina maana gani kwa mkulima masikini anayenyang’anywa ardhi yake na wafugaji wanaowanunua watendaji wa serikali.?? Wakulima wamebaki yatima katika nchi yao ili kupisha mifugo ya watawala amani hii ina maana gani kwa mkulima masikini aliye nyang;anywa shamba lake na kiongozi wa serekali au natajiri mwenye mapesa ya kuwahonga wakuu wa serekali wanao shughulikia mambo ya ardhi amani hii ina maaana gani..??
Amani hii ina faida gani kwa wakina Mama zetu na Dada zetu waja wazito masikini wanao kufa na mtoto wake kwa kukosa huduma za hospitali ina faida gani kwa masikini amani inayoliliwa na serekali ya SMZ..?? Mama huyu kabla hajafaa anadaiwa rushwa na wauguzi ukiacha lundo la matusi na kejeli anazopata na hata kupingwa makofi saa nyengine mbele ya waajiriwa hawa wa serikali. Amani hii ina faida gani kwa wafanya biashara wadogo wadogo kunyanyaswa na askari wa baraza la manispa watowe rushwa au kuchukuliwa biashara zao na kupingwa vibaya ina faida gani amani hii inayoliliwa na serekali ya SMZ..??
Watoto wa masikini wanaohitimu katika vyuo mbalimbali hawana ajira wakati watoto wa Waheshimiwa na wanasiasa wanaletewa ajira zao vyuoni kabla hata hawajahitimu. Tofauti ya tabaka hizi mbili ndilo chimbuko la kukosekana kwa amani katika Serekali hii ya majambazi ya SMZ.
Viongozi Kama hawa Seif Iddi wanapohubiri Amani nikuwazuga tu wananchi ili tu wapate utulivu wakufanya uharamia wao bila kero maana wanajuwa bila ya amani yao hayatakuwa na nafasi kufanikiwa ndio akawa muhubiri mkubwa wa amani, Mzanzibar wa kawaida hafaidiki chochote na hio Amani ihubiriwayo kila siku.
Ikiwa ni mateso Wazanzibar wanateseka ,ikiwa ni kubambikiziana makesi Wazanzibari wanabambikiwa toka serekali hii ishike madaraka mwaka 1964 mpaka sasa mchezo ndio huwo huwo kubambikiwa kesi.ikiwa ni kuteseka Wazanzibari wanateseka ikiwa ni ukali wa maisha Wazanzibar wa kawaida wamepata depreshni kwa mgorogano wa mawazo, kwa hio kuna faida gani ya Aman iloko na ni kwa nani..??
No comments:
Post a Comment