Thursday, April 11, 2013

MGAO WA UMEME SASA BASI NCHINI ZANZIBAR-BAADA YA MUDA MCHACHE WAKATIKA TENA












Nchi Zanzibar. Huduma za umeme katika nchi ya Zanzibar, jana zilikatika kwa zaidi ya nusu saa baada ya kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa umeme kutoka nchi ya Tanganyika.
Uzinduzi wa mradi huo, ulifanywa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, katika Uwanja wa Amaan nchini hapa Zanzibar.
Sherehe za uzinduzi wa mradi huo, zilihudhuriwa pia na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Hata hivyo muda mfupi baada ya shughuli hizo, huduma za umeme katika Nchi hiyo ya Zanzibar, ulikatika kuanzia saa 9 mchana na kudumu kwa zaidi ya nusu saa.
Meneja wa Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco), Mbarouk Hassan, alithibitisha kuwa huduma zilikatika na kwamba tatizo lilikuwa ni kutoka nchi  Tanganyika ambako ndiko kunatowa umeme huo.
“Umeme ulikatika kabisa, lakini tatizo lilianzia Bara, hata hivyo limemalizika,” alisema Meneja huyo kwa njia ya simu.
Akizindua mradi huo uliogharimu Dola za Marekani 64.4 milioni Dk Shein aliwataka wananchi kulinda miondumbinu ya  umeme kwa kuzingatia kuwa inatengenezwa kwa gharama kubwa.
Dk Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, aliita Zeco kufuatilia madeni yake na kuwataka wananchi kulipia gharama za umeme.
Alisema kufanya hivyo kutatoa fursa nzuri kwa wawekezaji kuwekeza visiwani Zanzibar kwa sababu watakuwa na umeme wa uhakika.

Mradi huo unaotekelezwa kwa msaada wa Marekani, umeanzia Ras Kiromoni wilayani Bagamoyo hadi Mtoni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment