Friday, April 26, 2013

SPIKA WA BARAZA LA WAWAKISHI NCHINI ZANZIBAR APANGUWA KAMATI ZA KUDUMU.((ILI WAGAWANE MAMILLIONI YA MAPESA BILA YA MAJUKUMU YOYOTE))


Omar Ali Shehe, Mtando wabakishwa PAC.
• Hamza kuendelea Ofisi za Viongozi wakuu, Mshimba, Subeit Waongezwa..
• Jussa aenda Mawasiliano na Ujenzi.
• Wenyeviti kuchaguliwa mwezi uajo

Na Himid Choko, BLW
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho amepanguwa Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Baraza hilo na kuwapanga upya .

Katibu wa Baraza hilo Yahya Khamis Hamad amesema, Spika amefikia uwamuzi huo kwa kutekeleza mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni ya 107(2) ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi (Toleo la 2012) inayohusiana na Uwezo wa Spika kuunda Kamati za Kudumu za Baraza.
“ Kanuni ya 107 inaelezea Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Kudumu ambapo Kanuni hii pia inakataza Makamo Wa Pili wa Rais, Waziri, Naibu Waziri au Mwanasheria Mkuu kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Kamahti hizo. Aidha kanuni hii ya 107 (2) inampa uwezo Mheshimiwa Spika Kuwateuwa Wajumbe wa Kamati hizo ” Alisema Katibu Yahya.
Amesema wajumbe hao wapya watazitumikia Kamati hizo kuazia Mwezi Mei 2013 mpaka kuvunywa kwa Baraza hapo mwaka 2015.
Katibu huyo wa Baraza la Wawakilishi amesema Katika uteuzi huo Mpya , aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Hamza Hassan Juma (Kwamtipura) amebakishwa kuitumikia tena Kamati hiyo.
Amesema Wajumbe wengine walioteuliwa kuitumikia Kamati hiyo ni Subeit Khamis Faki (Micheweni), Ali Mzee Ali ( Kuteuliwa) , Shadya Mohammed Suleiman ( Viti Maalum), Makame Msimba Mbarouk (Kitope) ambae hapo awali alikuwa akiongoza Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi . Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati hiyo ni Saleh Nassor Juma (Wawi) na Ashura Sharif Ali (Viti Maalum).
Katika Kamati ya Katiba , Sheria na Utawala , walioteuliwa ni Mansour Yussuf Himid ( Kiembe Samaki), Wanu Khafidh Ameir (viti Maalum) , na Suleiman Hemed Khamis (Konde). Wengine ni Abdullah Juma Abdullah (Chonga) , Bikame Yusuf Hamad (Viti Maalum) na Nassor Salin Ali (Rahaleo).
Aidha katika uteuzi huo Mwakilishi machahari wa Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu amehamishwa kutoka Kamati yake ya awali ya Katiba, Sheria na utawala na sasa atatumikia Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi . Wengine walioteuliwa kuunda Kamati ya Mawasilino na Ujenzi ni Marina Joel Thomas ( Kuteuliwa), Mohamed Haji Khalid (Mtambile) , Hussein Ibrahim Makungu (Bububu), Mahamoud Moh,d Mussa (Kikwajuni) , Salma Mohammed Ali (Viti Maalum) na Mheshimiwa Panya Ali Abdullah ( Viti Maalum).
Walioteuliwa kuunda Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii ni pamoja na Mgeni Hassan Juma ( Viti Maalum), Mwanaidi Kassim Mussa (Viti Maalum), Hassan Hamad Omar (Kojani), Farida Amour Mohammed ( Viti Maalum), Addi Mossi Kombo (Matemwe), Ali Salum Haji (Kwahani) na Mohammed Mbwana Hamad (Chambani).
Aidha katika uteuzi huo Mheshimiwa Spika amewabakisha Omar Ali Sheikh (Chake Chake), Mbarouk Wadi Mtando (Mkwajuni), Shamsi Vuai Nahodha (Mwanakwerekwe), Fatma Mbarouk Said (Amani) kuwa Wajumbe wa Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (PAC). Wengine walioteuliwa katika Kamati hiyo ni Rafai Said Rufai (Tumbe), Mwajuma Faki Mdachi (Viti Maalum) na Salma Mussa Bilal (Viti Maalum) na Jaku Hashim Ayoub (Muyuni).
Katika uteuzi huo mpya wanaounda Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ni pamoja na Salmin Awadh Salmin (Magomeni), Salim Abdullah Hamad (Mtambwe), Hamad Masoud hamad (Ole ), Viwe Khamis Abdullah (Viti Maalum), Asha Abdu Haji (Viti Maalum), Hija Hassan Hija (Kiwani) na Raya Suleiman Hamad ( Viti Maalum).
Katika Kamati ya Mifugo, Utalii na Uwezeshaji na Habari walioteuliwa ni Asha Bakari Makame (Viti Maalum), Mlinde Mabrouk Juma (Bumbwini) na Kazija Khamis Kona ( Viti Maalum). Wengine ni Asaa Othman Said (Wete), Abdullah Mohammed Ali (Mkoani), Amina Iddi Mabrouk (Viti Maalum), Mussa Ali Hassan ( Viti Maalum) na Mohammedraza Hasanali Dharamsi (Uzini).
Kamati hizi mpya za Baraza la Wawakilishi zitafanyakazi zake kuazia sasa mpaka kumalizika muda wa Baraza la Nane la Wawakilishi kwa mujibu wa Maamrisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Kifungu cha 85 (1) Cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 kinasema kua “ Kutakuwa na Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi zitakazoundwa kwa mujibu wa wa Kanuni za Baraza la wawakilishi”.
Aidha Kanuni ya 109 (4) ya Baraza la wawakilishi toleo la 2012 inasema kwamba Wajumbe walioteuliwa Katika Kamati Fulani ya Kudumu wataendelea kuwa Wajumbe wa Kamati hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na miezi sita kuazia siku ya uteuzi wa kwenye kamati hiyo.
Hata hivyo katibu Yahya amesema Kamati hizo zinategemewa kukutana ili kuwachagua Wenyeviti na Mawakamo Wenyeviti kabla ya kuanza kazi za Kamati Mapema mwezi ujao.
.((ILI WAGAWANE MAMILLIONI YA MAPESA BILA YA MAJUKUMU YOYOTE MAANA NCHI IKO VILE VILE INANUKA))

No comments:

Post a Comment