Tuesday, June 18, 2013

NCHINI TANGANYIKA-MTOTO ASEMA NIMEPINGWA RISASI NA POLISI-ARUSHA-CCM OYEEEEEEE


Arusha/Dodoma. Wakati watu waliofariki kwenye tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa Chadema ukizidi kuongezeka baada ya jana kufariki kwa mtoto Amir Ally (7), mtoto mwingine wa miaka kumi na moja aliyejeruhiwa vibay, amesema kwamba alipigwa risasi na polisi kwenye tukio hilo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye ametoa tamko kuwa chama chake kina ushahidi wa kutosha wa watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa kampeni wa chama hicho.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Arusha Medical Lutheran Center (ALMC), Dk Paul Kisanga alisema jana kuwa, Amir alifariki jana asubuhi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani yaliyodhuru ubongo wake.

Dk Kisanga alisema huyo ni mmoja wa watoto watano, waliojeruhiwa wakati wakitoka madrasa huko Kaloleni, jirani na Uwanja wa Soweto kulipokuwa na mkutano na alifariki jana asubuhi hospitalini hapo.

Alisema watoto wengine wawili ambao ni ndugu; Fatuma na Sharifa Jumanne wamepelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma. Dk Kisanga aliwataja watoto wengine waliojeruhiwa kuwa ni Fahad Jamal (7) ambaye yupo ICU akisubiri timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kutoruhusu kusafirishwa. Pia yupo Abubakar Adam (11) ambaye amejeruhiwa mguuni na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru.
 

Mtoto aeleza kupigwa risasi

Adam alisema jana kuwa alipigwa risasi na mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu yake, Fahdi katika eneo la Soweto.

Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini.

“Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi huku akitokwa machozi.

Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Mount Meru, Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto huyo ana vyuma viwili katika mguu wake.

“Tunasubiri afanyiwe upasuaji kwani tayari mashine ya X-ray inaonyesha vyuma kuwepo katika mguu wa Adam siwezi kusema ni risasi au la,” alisema Semdeli.

No comments:

Post a Comment