Friday, June 21, 2013

PINDA ASEMA SASA PIGA TU-AVUNJA KATIBA BILA YEYE MWENYEWE KUJUWA

 Katika swali la nyongeza, Mangungu alisema kutokana na hali iliyokuwapo, sasa wananchi wengi wamekuwa na hofu, lakini pia hata shughuli za uzalishaji mali zimeingia kwenye shaka na kuumiza uchumi wa nchi.
 “Serikali ipo tayari kiasi gani kuweza kubainisha na kuchukua hatua stahiki badala ya kusakama makundi fulani. Tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani, ambavyo vyombo vya dola vinashughulikia..??” alihoji na kuongeza:
“Maana yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara, wananchi wanapigwa na vyombo vya dola. Sasa serikali ipo tayari kutoa kauli ni kiasi gani wamefanya uchunguzi na kupata suluhisho la kudumu la matatizo hayo..??”
Akijibu swali hilo, Pinda alionekana kukerwa na swali la nyongeza, hasa pale mbunge huyo aliposema kuwa wakazi wa Mtwara wanapigwa na vyombo vya dola.
“Hapa unaona anasema (Mangungu) vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo wakati umeambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria,” alisema na kuongeza:
“Kama wewe umekaidi hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi,  wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu na mimi nasema muwapige tu alisema pinda. Kwa sababu hakuna namna nyingine. Maana tumechoka sasa.”
Akiendelea kusema juzi alimsikiliza mbunge mmoja, ambaye anadhani anatoka Mtwara, naye alijaribu kugusia gusia kwamba, vyombo vya dola vinakamata watu vinapiga watu.
“Mara ya mwisho nilisema tunataka turejeshe hali ya amani katika maeneo hayo ya Mtwara…tukawaambia Watanganyika tunawaombeni radhi sana katika jambo hili tutakapoanza kufuatilia mtu mmoja mmoja. Tunajua kuna watu watajitokeza kuanza kuvisema vyombo vya dola.
“Nikawaomba msamaha. Tuacheni tufanye hiyo kazi Mtwara. Pale tuna orodha sasa ya watu, ambao wanasemekana ndio vyanzo vya matatizo na vurumai mnataka tusiwakamate..??? Lazima tuwakamate na katika kuwakamata wakifanya jeuri jeuri watapigwa tuuuu kabla ya kuwapeleka wanapotakiwa kupelekwa.”
Alisema hawawezi kuendelea na hali hiyo na wakadhani kwamba, watafika wanakokwenda.
Alisema ni lazima serikali ijitahidi na kwamba, vyombo vya dola vijipange imara ili kuhakikisha wanadhibiti hali  hiyo na kuirejesha hali ya utulivu maana hakuna namna nyingine.
Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji, alihoji kauli ya awali aliyoitoa Pinda kuwa watu wapigwe tu.
“Katiba ya Jamuhuri ya Muungano katika Ibara ya 13 kifungu kidogo cha pili inasema ni marufuku kwa mtu yeyote aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo hadi hapo atakapothibitika kutenda kosa hilo,” alinukuu.
Alisema pia Katiba hiyo Ibara 12 inasema ni marufuku kwa mtu yeyote kuteswa ama kuadhibiwa kinyama na kumpa adhabu, ambazo zinamtesa mtu na kumdhalilisha.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kauli yako nzito hiyo uliyoitoa huoni kwamba, umevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanganyika ((Tanzania))..????” alihoji Haji.
Akijibu, Pinda alimtaka kuweka tofauti ya mtu aliyekamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kwamba, hapo ndipo Katiba inamwelekeza kuwa asifanye jambo lolote katika eneo hilo.
“Mimi nazungumza ni pale mtu ameamua kufanya vitendo hajakamatwa. Ndiyo maana nilisema nikikwambia usiandamane, hapa hutakiwi kwenda. Wewe ukaamua kutumia mabavu kwa sababu mpo wengi ukaenda,” alisema na kuongeza:
“Ndiyo maana nikasema hawa watu tutashughulika nao hivyo hivyo. Sizungumzi mtu ameshakwenda mahakamani na kukamatwa hata kidogo. Mtanganyika awe mwepesi wa kutii sheria bila shuruti.”

No comments:

Post a Comment