Wednesday, June 5, 2013

SIO SAMIA SULUHU TU KUMBE KUNA NA DAFTARI MAMA TUBIA ULICHO IBA USHAIBA KAMA HUJAIBA HUTAIBA TENA

 
MWENYEZI MUNGU AKUOKOWE NA URUDI KWAKE KABLA HUJAFA KWA TAMAA
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maua Daftari
Mapendekezo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuhusu muundo wa serikali tatu, umeibua kauli za kukinzana miongoni mwa wabunge.
Kundi moja linatoa kauli zinazobainisha kuwa sasa kila upande ubabe mzigo wake.
Hata hivyo, wananchi na makundi mengine ya jamii yameunga mkono mapendekezo mengi yaliyomo katika rasimu hiyo na kukosoa machache.

Miongoni mwa wabunge wanaotoka nchini Zanzibar, wameelezea wasiwasi kuhusu hatima ya kiuchumi na kiusalama kwa eneo hilo la Muungano, ikiwa litaachwa kuwa katika mamlaka yake kamili.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maua Daftari moja katika hao walionufaika na muungano na wako tayari nchi ya Zanzibar imezwe lakini yao yanawaendea, alisema Zanzibar haijaimarika kiasi cha kuwa na uwezo wa kuhudumiwa serikali yake na kuchangia katika serikali ya Muungano.(si vichekesho hivi)akiendelea kusema.
“Ni lazima tuwe wakweli, Zanzibar inasaidiwa kwa kiasi kikubwa na Muungano kwa kutegemea rasilimali za Bara!!!, sasa tukisema tujitenge, si rahisi (Wazanzibari) tukamudu kuiendesha serikali yetu na kuichangia ile ya Muungano,” alisema jana wakati wa kutoa maoni yake kuhusiana na tume kupendekeza kuwapo kwa serikali ya Zanzibar, Tanganyika na Shirikisho.
“Ingefaa zaidi kabla ya kuwasilisha mapendekezo hayo, Tume ingezitafakari faida na hasara za serikali tatu, na mimi binafsi naona hasara zake ni nyingi kuliko faida,” alisema Daftari ambaye kwa asili wanadai anatokea nchini Zanzibar inawezakuwa hivyo ila chembe chembe zake ni zakitanganyika ndio maana bado ananganganiya serekali mbili na muungano.
Daftari aliyewahi kushika nyadhifa tofauti serikalini ukiwamo naibu waziri, alisema ni vizuri kwa Zanzibar kujitafakari upya kuhusu kuingia katika mfumo wa serikali tatu, huku akikielekezea kidole Chama Cha Wananchi (CUF) kuwa watetezi wa mfumo huo.(kasahau kuwa sasa sio CUF tu hata hao CCM pia wanataka hayo isipokuwa wahafidhina kama yeye mwenyewe mama Daftari alivyo.
“CUF walihamasishwa sana kuhusu kuwapo kwa serikali tatu, kwa maana tangu awali Muungano unaonekana si sehemu ya hitaji lao,” alisema Daftari huyo.
Daftari alisema miongoni mwa hofu inayomkabili ni kuhusu hatima ya wafanyabiashara Wazanzibar waliowekeza na kuweka makazi ya kudumu upande wa Bara, ikiwa zitaundwa serikali za Zanzibar na Tanganyika (Bara).
“Wazanzibar wanafanya biashara sana Bara, wamejazana kila sehemu ya nchi, sasa tukifikia kila upande kuwa na serikali yake, maana yake itabidi warudi Zanzibar ili serikali ya Bara iwatambue na kuwahudumiwa raia wake,” alisema.(tunamulizwa swali huyu mama je wahindi wameungana na Tanganyika..? Wachina wameungana na Tanganyika..? wacha sera zenu bovu na kutapia mlo mama zere usioka ukatubia mamilioni uliyo iba bado.
Akiendelea kusema hali ilivyo sasa, wafanyabiashara hao wanaendesha shughuli zao pasipo kubughudhiwa, hali ambayo bila shaka itawaathiri ikiwa Bara itaunda serikali yake.
Daftari alisema jambo la msingi lililopaswa kufanyika ni kushughulikia kero za Muungano pasipo kuathiri muundo wa Muungano

No comments:

Post a Comment