Thursday, May 3, 2012

UAMSHO-JUMIKI INAFUATA SHERIA NA KATIBA YA Z,BAR.JE MOHAMED ABOUD UNAFUATA..?



Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR.
KWA VYOMBO VYA HABARI BAADA YA KAULI YA MHE. MOHAMED ABOUD YENYE NIA YA KUVUNJA NA KUVURUGA AMANI YA NCHI ILIYOTOKA JANA TAREHE 2/5/2012 ZBC.
03/05/2012
NDUGU WAANDISHI WA HABARI
ASSALAMA ALAYKUM WARAHMATU -LLAH WABARAKATU
Awali nachukua fursa hii kumshukuru Allah subahana wataala muumba mbingu na ardhi mwenye kumpa Ufalme amtakae na kumnyima amtakae pia tunamtakia rehma kipenzi cha umma Mtume wetu Muhammada (S.A.W) baada ya shukurani hizo tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Rais wetu mpenzi Dr. Ali Mohammed Shein kwa uongozi wake imara uliojaa uadilifu, hekima pamoja na serikali yetu ya Kitaifa na usimamizi wake madhubuti wa kuhakikisha anatandika zulia la demokrasia na kuhubiri amani, umoja na mshikamano.
Ndugu waandishi wa habari.
Kwa kweli tumesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Mohammed Aboud aliyoitoa jana kwenye vyombo vya habari yenye lengo la kuzuia mihadhara inayoendeshwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa kusimamiwa na Jumuiya ya Uamsho JUMIKI kwa kisingizio cha sheria No. 8 ya mabadiliko ya Katiba kwa maana hiyo tunapenda tutoe ufafanuzi juu ya sheria hiyo katika ibara zake zinazohusu suala la utoaji elimu. Ibara ya 17:8 “Mtu au asasi yoyote itakayotaka kuendesha programu ya kutoa elimu juu ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, kabla ya kuanza kutoa elimu hiyo sharti, iwe imesajiliwa ……… na itawajibika kueleza kwa tume chanzo cha fedha ya kuendesha programu hiyo” ibara ya 21:2C “Mtu yeyote atakaeendesha programu ya elimu… kinyume na masharti ya sheria hii atakuwa ametenda kosa”
Ndugu waandishi wa habari
Napenda mzingatie kuwa:
1. programu ya elimu inayomtia mtu hatiani kwa mujibu wa sheria hiyo ni elimu inayohusu sheria ya mabadiliko ya Katiba.
2. Masharti yaliyoekwa ni kuwa Jumuiya imesajiliwa Serikalini.
3. Inalazimika kutoa taarifa tu na kueleza chanzo cha fedha sio kutaka ruhusa au kuomba kibali.
Kwa bahati nzuri Jumuiya za Kiislamu imeliona hilo mapema na tayari
programu za elimu juu ya mabadiliko ya Katiba zimemaliza kwa muda
mrefu kwa sasa hivi Jumuiya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuweza
kujua sheria za nchi na Katiba yao jambo ambalo kwa muda mrefu Serikali
haikuwa na utaratibu endelevu wa kuelimisha raia zake na hiyo ndio kazi
inayoifanya Jumuiya kuisaidia Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa sambamba
na kutoa elimu ya Kiislamu kufunza maadili mema, kudumisha amani,
umoja, utulivu na mshikamano kwa wazanzibari wote bila kujali tofauti zao
za kidini, kisiasa, rangi na ukabila pamoja na kusisitiza umuhimu wa kudai haki zao na uhuru wa maoni pamoja na kulinda mali ya umma na kutii Katiba ya Zanzibar na sheria za nchi. Ibara ya 23:1 ya Katiba ya Zanzíbar inasema “kila mtu anawajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Zanzíbar” 23:3 inasema “watu wote watatakiwa na sheria kulinda vizuri mali ya Zanzíbar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu… kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadea ya Taifa lao”.
Ndugu waandishi wa habari.
Jumuiya ya Uamsho inaendesha mihadhara kwa miaka mingi kuzingatia Katiba yake pamoja na kufuata Katiba ya Zanzíbar inayotoa uhuru wa maoni kutipia ibara ya 18 inayosema “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yupo huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”.
Pia Katiba ya Zanzíbar imetoa uhuru wa kuabudu kwa kusema katika ibara ya 19:2 “Bila ya kuathiri sheria zinazohusika kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru na jambo la hiari ya mtu binafsi” kwa maana hiyo basi Jumuiya za Kiislamu katu hazitosita kuendelea na uhuru huo unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar usio athiriwa na sheria ndogo ndogo zinazotungwa kwa malengo maalum pia zitaendeleza mihadhara yake ikizingatia kudumisha amani ambayo inaonesha wazi kuwa kwa wale madhalimu wasiowatakia mema Wazanzibar tayari wameanza kujichomoza kutaka kuvunja amani kwa visingizio visivyokuwa na hoja ya kisheria pia inaonesha dhamira yao mbaya ya kutaka kumpaka matope Mhe. Rais wetu wa Zanzíbar Dr. Mohamed Shein pamoja na Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa lakini hatushangazwi na watu hao kujitokeza kutaka kuhatarisha na kuvunja amani kwani hao ndio waliosimama kidete kupinga kuanzisha Serikali yetu ya umoja wa Kitaifa jambo ambalo linaonesha kuna ajenda ya siri ya kutaka kuwagawa Wazanzibar na kuhatarisha amani.
Jumuiya za Kiislamu zinawatahadharisha watu hao na kuwataka mara moja waache kuhubiri uchochezi na uvunjifu wa amani na kuwakumbusha kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria ibara ya 12 ya Katiba inasema “ Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote” vile vile wajue hizi ni zama za uwazi haki na sheria hivyo tunawasihi wasijisahau wakavitumia vyeo na ngazi za uongozi kwa maslahi ya wachache sana wasioitakia mema Zanzíbar watambue kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Zanzíbar na sheria za nchi rejea ibara ya 14,16,23 ya Katiba ya Zanzíbar.
Pia Jumuiya zinapenda kuchukua fursa hii kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 17:8 na 21:2C kwa kuzingatia uhuru wa kuabudu na uhuru wa maoni unaolindwa na Katiba ya Zanzíbar. Pia kutoa ufafanuzi juu ya kifungu cha 10 cha Sheria hiyo hiyo No.8 ya mabadiliko ya Katiba kinachoipa Tume uhuru na mamlaka kamili ambayo Mhe. Mohamed Aboud anaonekana kuvikiuka na kuingilia kazi za tume kwani Katibu Mkuu wa Tume hakuwa na taarifa yoyote wakati Jumuiya zinawasiliana nae akiwa bado ndio kwanza anataka kuisoma taarifa hiyo kwenye mtandao.
Imani yetu huu ndio Mwanzo wa uvunjifu wa sheria hiyo. Tunapenda kumkumbusha Mhe. Mohamed Aboud maneno ya Rais Dr. Shein aliwataka wananchi wa Zanzíbar wanaishi kwa umoja na mshikamano inapaswa hitilafu ziondolewe ili Wazanzibar waishi vizuri kwa amani na utulivu na kamwe asitokee mtu akiwa ana lengo la kuivunja amani iliyopo rejea gazeti la Zanzíbar leo lenye kichwa cha maneno TUSICHAFUE AMANI toleo No 3743.
Ndugu waandishi wa habari .
Tunapenda kumalizia taarifa hii kwa kutoa shukurani zetu za dhati kwa jeshi la polisi kusimama imara katika kudumisha amani ya nchi na kutokubali kuburuzwa na hao wachache wasioitakia mema nchi yetu ya Zanzíbar.
Ahsanteni sana.
Nakla:
Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Mwanasheria Mkuu wa Zanzíbar,
Waziri wa Katiba,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais,
Jeshi la Polisi,
Idara ya Mufti Zanzibar ,

No comments:

Post a Comment