Tuesday, May 29, 2012

KUMBE NI BINU YAKUTAKA KUZIMA WAZANZIBAR WASIDAI NCHI YAO


Harakati za wazanzibari zikiongozwa na taasisi na makundi mbali mbali ya kijamii juu ya kuhoji, kuujadili na kutaka kuitishwe kura ya maoni juu ya muungano lilikuwa jambo lililowakosesha usingizi baadhi ya viongozi wa Serkali kwa wale wenye kufikiria mitumbo yao na baadhi yataasisi za kijamii zinazo faidika kutokana na muungano huu feki na bati unaendelea kuwadidimiza wananchi na nchi yao ya zanzibar.
Kuna uwezekano kuwa, mipango ilikuwa imesukwa muda mrefu juu ya namna ya kukabiliana na vugu vugu la kudai Zanzibar huru, labda muda muwafaka ulikuwa haujafika tu. Hivi sasa tumeshuhudia namna ambavyo nguvu kubwa iliyopita mipaka na ukosefu wa busara na maadili mema ya kazi inayotumiwa na vyombo vya dola na vile vya habari vya ndani na nje ya nchi yatu ya Zanzibar.
Kuchoma makanisa na mabaa imekuwa ndio kichwa cha habari na ajenda kuu sasa hivi, suali ni nani yuko nyuma ya matukio haya na kwa nini? wala hatuoni ktk vichwa vya habari msikiti wapingwa mabomu na askari wa kikuria wala hatuoni askari wanavyo wapiga na kuwanyanyasa vijana wa kizanzibar. Zanzibar kuna mamia ya makanisa, kabla na baada ya muungano, iweje sasa kuchomwa makanisa isiwe miaka yote hio iliopita, jee hii ni bahati mbaya!au ndio mbinu mpya ya kutaka kuuzima moto wa kudai nchi huru ya zanzibar..?
si bure, lengo ni kuziviza harakati za wazanzibari juu ya dai lao halali lakutaka kuitishwe kura ya maoni kuhusu muungano na kuwatwisha lawama viongozi wa UAMSHO juu ya fujo ambazo huenda zinachochewa na watu maalum na wenye ajenda maalum.ya kutaka kuibakisha zanzibar ktk ukolo mwisusi wa kitanganyika.
Hivyo basi, bidii yoyote au nguvu yoyote inayotumika kuzizima harakati hizi ni batili, ni kinyume na katiba zote mbili za Zanzibar na Muungano na nikinyume na tamko la haki za binadamu ikiwa kweli nyinyi munafuata sheria za katiba mulizo tunga wenyewe la kama ni serekali tu ya ubabe ubabe na uhuni na unyanyasaji wa rai basi sawa endeleni na uhuni wenu wakutuletea wakuria kuja kuwapiga rai wanyonge wa kizanzibar. Wananchi wapewe nafasi ya kujadili lolote linalo husu nchi yao ya zanzibar na mustaqbala wao kwa ujumla, nguvu za kijeshi na propaganda za vyombo vya habari hazitazaa matunda. Bali busara, hekma na mazungumzo ndio sulhu muwafaka.
Ewe Mola wetu mlezi ibariki Zanzibar na watu wake, tuhifadhi dhidi ya maadui zetu, tujaalia salama, amani na utulivu, tuepushe na kila balaa, njama ovu dhidi yetu na nchi yetu na utufanikishie muradi wetu na mustaqbala mwema kwetu na nchi yetu tuipendayo. Aamin.

1 comment:

  1. I do not leave a leave a response, but after looking at through some of the comments on "KUMBE NI BINU YAKUTAKA KUZIMA WAZANZIBAR WASIDAI NCHI YAO".

    I do have 2 questions for you if you do not mind. Is it just me or do a few of these comments
    appear like they are written by brain dead folks?
    :-P And, if you are writing on other online social sites, I would like to follow anything fresh you
    have to post. Could you post a list of the complete urls of your
    social networking pages like your Facebook page,
    twitter feed, or linkedin profile?

    my web site Joyce Banda

    ReplyDelete