15th June 2012 Mbunge wa Chakechake, Pemba, Rajab Mbaruku Mohammed (CUF), amevishutumu vyombo vya habari kwa madai ya kuandika upande mmoja wa vurugu zilizotokea Zanzibar, akidai havikuripoti uchomaji wa misikiti na mali za watu na badala yake vilitangaza kuhusu uchamaji wa makanisa pekee.
Hata hivyo, wakati Mbunge huyo akitoa tuhuma hizo, kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa na Jeshi la Polisi Zanzibar kuhusiana na matukio hayo, hakukuwa na taarifa za misikiti kuchomwa moto.
Huku akirejea vurugu zilizotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wan chi hiyo ambapo mamia ya watu waliuawa na mali zao kuharibiwa, Mohammed alisema ripoti ya uchaunguzi ilionyesha kuwa, vurugu hizo zilichochewa pia na
vyombo vya habari.
Aliishauri Serikali ya Muungano na Zanzibar kuunda tume huru ya uchunguzi ili wahusika wavurugu za Zanzibar wachukuliwe hatua na kudhibiti hali hiyo isitokee tena.
“Katika vurugu zilizotokea Zanzibar Mei 26 na 27 mwaka huu, vyombo vya habari havikuripoti uchomaji wa baadhi ya misikiti na mali na badala yake viliripoti kuhusu uchomaji wa makanisa na mali zake…viliripoti habari za upande mmoja tu, sasa unasemaji kuhusu vyombo hivyo vilivyotoa taarifa za upande mmoja,” alihoji.
Akijibu Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema: “Rai ya kuunda tume huru ya uchunguzi ni nzuri lakini siwezi kulisemea moja kwa moja hapa, tutawasiliana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuona hatua walizofikia kumaliza tatizo hilo na kama kuna haja ya kuunda tume.
Kuhusu uandishi wa habari alisema ni lazima habari ziandikwe kwa ulinganifu. Hata hivyo, alisema jambo kubwa hapa ni kudhibiti chanzo. “Ni vizuri jambo hili likadhibitiwa, lisiendelee.” Alisema.
FREE ZANZIBRA PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI.
DR SHEIN,MAALIM SEIF,BALOZI IDDI mume bana kimya na munajuwa misikiti imepingwa mabomu na kuchomwa moto na nyinyi ati ndio maraisi wa nchi hii munabebe tu mambo mutakwenda kumueleza vizuri mwenyezi mungu nyinyi.kama walivyo juwa kumshika sheikh mussa na hao polisi walio choma moto msikiti na kuipinga mabomo walikuwa washtakiwe na wafungwe maana nyinyi ni viongozi mukisema tu ni nani aliyefanya hayo atajulikana ila mume bana kimya munawachiya watu waendele kuipaka matope uamsho ili izimwe ila kwa uwezo wa mola haitazimwa ile mpaka nchi yetu ya zanzibar iwe huru na nyinyi kaliyeni madaraka tu na kula raha za dunia kumbukeni kiyama hakiko mbali kaburi haliko mbali.
MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment