Tuesday, April 30, 2013

MIAKA 49 YAMUUNGANO: MASWALI SITA NA MAJIBU YA KIPUMBAVU


Makala hii nimeinakili kutoka blog ya Zanzibar ni kwetu. Toa maoni yako
¤Kwenye kuingia mkataba wa Muungano, kwa nini Nyerere alimshirikisha mwanasheria wake Roland Brown wakati Karume alimpa mwanasheria wake Wolfgang Dourado likizo ya muda kwenda nchini Uganda wakati Karume hakuwa msomi ukiachia uzoefu wa kazi ya ubaharia pamoja na umaarufu wa kucheza mpira?
Nyerere alimshirikisha mwanasheria wake huyu kwa sababu andiye aliyekuwa mwanasheria wake. Tanganyika haikuwa na wanasheria wa kabila ile wakati ule. Karume alikuwa Rais aliyemteua Dourado kuwa mwanasheria mkuu na alikuwa na mamlaka ya kumtoa cheo hicho au kumpeleka likizo. Aidha, kwa kuwa mwanasheria ni mtumishi wa mteja wake, hana maamuzi yoyote nje ya yale anayotaka mteja wake; hivyo kama Dourado hakukidhi mahitaji/matakwa ya Karume, alipaswa kuwekwa kando kwa mtindo wowote ule. Wanasheria ni matarishi tu wa wateja wao katika ufundi wa sharia.
¤Hati ya Muungano ilikuwa na mambo 11. Hivi sasa yamefikia 23 kutokana na kuongezwa na Nyerere taratibu kwa kupitia decree. Je, Karume alijua kuhusu uwepo wa decree kwenye katiba?
Ni kweli mambo ya Muungano yamefikia 23 kutoka 11 ya awali. Kuna sababu zake, mojawapo ikiwa kwamba hakukuwa na makubaliano ya kubakia na yale yale 11 bali kulikuwa na makubaliano ya kuuboresha Muungano. Pili, si kweli kwamba ni Nyerere pekee aliyeyaongeza, au tuseme kwamba yaliongezeka wakati wa Nyerere tu. Soma historia ya Muungano ujielimishe. Aidha, Karume alikuwa shuhuda wa kuongezwa mambo ya awali, mfano baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa sarafu ya Afrika Mashariki na kisha kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania. Mambo haya yameongezeka kutokana na ulazima wake, umuhimu wake, na yalifuatwa utaratibu kila yalipoongezwa. Kumbuka, mambo ya Muungano yanasimamiwa na serikali ya Muungano, Rais wa Muungano na Bunge la Muungano, si nje ya hapo. Ili kufahamu sababu za kila jambo liliongezwa, anzia na tovuti ya Makamu wa Rais, kisha ukikwama, uliza.
¤Mkataba wa Muungano uliridhiwa na Bunge la Tanganyika (tena weekend). Kwa nini Bunge la Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikuwahi kukutana kuridhia? Je, Muungano ni halali?
Bunge lilikuwa na uwezo wa kukaa siku yoyote. Lingekaa Jumatatu ingebadili nini? Zanzibar haikuwa na Bunge halali. Hata hivyo, Baraza la Mapinduzi lilipitisha muswada wa Muungano ila kusichokuwepo ni rekodi. Muungano ni halali na nakala yake iko Umoja wa Mataifa, New York ambapo hawapokei mikataba magumashi.
¤Karume hakutaka muungano wa serikali mbili. Ilikuwaje Nyerere akakomaa?
Ukweli ni kwamba Karume alitaka serikali MOJA tu akisema, “Nyerere wewe kuwa rais, mimi Makamo”. Walizungumza na wakakubaliana kuunda serikali mbili na Karume akawa Makamu na miaka yote ya uhai wake hakupinga uwepo wa serikali mbili. Kudai hivyo ulivyosema ni mzaha.
¤Kama lengo la Muungano ni regional integration (as opposed to Kwame Nkurumah’s notion), kwa nini Muungano wetu haukuongezeka tena tokea 1964 (e.g. Kwa ku-include nchi za jirani e.g. Mozambique au Zambia? Je, ni kwa sababu waliona matatizo makubwa kwenye muungano wetu (kama Ethiopia/Eritrea, Sudan/South Sudan, Gambia/Senegal).
Lengo la Muungano halikuwa regional integration na wala haukufanyika ili kupingana na wazo la kidikteta la Nkrumah. Ili Muungano wa kikanda utokee ilipaswa kutimia ile ndoto ya Afrika Mashariki. Baada ya hoja hii swali linafia hapo hapo. Nenda kawaulize hao wengine sababu zao.
¤Kwa mazingira ya hivi sasa ambayo uwezekano wa kupata rais mzanzibar kuzidi kuwa mdogo, je, muungano unaweza kudumu miaka mingi mingine?
Rais wa Muungano kutoka Zanzibar ni jambo linalowezekana; si kweli kwamba haiwezekani. Mfano, kama Dkt. Salim Ahmed Salim asingepingwa na Wazanzibari kila anapojaribu, angekuwa Rais wa tatu (kama asingegoma kuweka jina lake) ama wa nne wa Muungano (kama angepata kura za kutosha). Aidha, muungano haupaswi kulindwa na zamu za urais. Urais ni taasisi nyeti, hatuwezi kupekezana kama njugu. Hii siyo kwenye Muungano tu, bali hata kwenye masuala mengine kama udini, ukabila, jinsia, umri, n.k.

MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ALIVYO ANZA KUIYUWA NA KUIMEZA NCHI YA ZANZIBAR


MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA
mkoloni mweusi  12 Januari 1964 alipinduwa serekali halali ya watu wa Zanzibar
April 1964 Mkoloni mweusi alianza hila za kumghilibu Sh Abeid Aman Karume, na pia kutimiza lile lengo lake la siku nyingi, kuua Taifa la Zanzibar.
22/04/1964 Mkoloni mweusi alifanya vitu vyake baada ya kulitia mikononi dola ya Zanzibar kwa gharama ya chee.
 [KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamuhuri ya Tanganyika na Abeid Karume, Rais wa Jamuhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia sahihi nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar, siku ya tarehe ishirini na mbili ya mwezi wa Aprili, 1964.]
Mkoloni mweusi Katika mkataba huu, Mkoloni mweusi alichukua nguvu zetu za utaifa na udola, Wakachukua uwezo wetu wa kiuchumi nakadhalika, kwa mambo yafuatayo:
(a) mkoloni mweusi  Ulinzi.
(b) mkoloni mweusi.   Polisi.
(c) mkoloni mweusi.   Mamlaka ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
(d) mkoloni mweusi.   Uraia
(e) mkoloni mweusi.  Uhamiaji
(f) mkoloni mweusi.   Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.
(g) mkoloni mweusi.  Utumishi katika Jamuhuri ya Muungano.
(h) mkoloni mweusi  Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha.
(i) mkoloni mweusi     Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu.
 25/04/1964 mkoloni mweusi alianza ubadhirifu wa hila, ujanja na udanganyifu wa kutumia kalamu kabla Muungano kuanza, juu ya yale waliyokubaliana na mwenzake Rais wa Zanzibar.  Tarehe hii kulikua hakuna Bunge la Muungano, kwani lililazimika liundwe baada ya sheria kupitishwa pia wawemo wabunge wasiopunga 32 kutoka Zanzibar (wajumbe wa Baraza la Mapinduzi).
(i) mkoloni mweusi        Bunge la Tanganyika lililokaa kupitisha sheria ya kukubali Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa makusudi, lilikubali kuifuta katiba ya Tanganyika na hivyo kuifuta Serikali yenyewe. Hivyo kuifanya katiba hiyo ya Tanganyika iwe katiba ya muungano.
“On the commencement of the Interim constitution of the United Republic, the Constitution of Tanganyika shall cease to have effect for the Government of Tanganyika as a separate part of the United Republic”
“Mara tu itapoanza kutumika katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katiba ya Tanganyika itasita kutumika kwa ajili ya Serikali ya Tanganyika kama ni sehemu nje ya katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar”
(ii)  mkoloni mweusi.              Siku hii wafanyakazi wote wa Serikali ya Tanganyika wakawa wafanyakazi wa Muungano.
(iii)  mkoloni mweusi            Mahakama ya Tanganyika ikawa ndiyo ya Muungano, na Majaji wake wakawa ndio majaji wa Muungano .
(iv) mkoloni mweusi             Muhuri wa Tanganyika nao ukawa ndio Muhuri wa Muungano (Public Seal).
(v) mkoloni mweusi               Rais wa Tanganyika akajipa madaraka ya kutunga kanuni zilizompa uwezo wa kutoa maagizo yanayohusu mambo ya Muungano kwa kutumia kanuni (Decrees) za sheria ya Tanganyika. Pamoja na kupewa madaraka hayo na makubaliano ya Muungano, lakini kanuni hizo zilikua zitungwe na Bunge la Muungano siyo Bunge la Tanganyika.
11/12/1964 Mkoloni Mweusi alijibadilisha jina na kuanza kutumia usanii wake kwa kuunda jina la TANZANIA kinyume cha makubaliano na mwenzake.
 “Prior to the enactment of the Interim constitution of 1965, another constitutional problem appears to have been created by the change of name of the United Republic from the United Republic of Tanganyika and Zanzibar to the United Republic of Tanzania, with effect from 11th December 1964 (declaration of Name Act 1964 (section 3).
18 Juni 1965 Mkoloni mweusi dhahiri shahiri aliziiba fedha na hazina za Zanzibar kwa kuanzisha Benki kuu ya Tanzania iliyoundwa kwa sheria ya benki Kuu ya Tanzania ya 1965. Kazi ya kwanza ya Tanganyika ikawa kuingiza shughuli za matumizi ya sarafu ya Tanganyika na utawala wa mabenki ya Tanganyika kuwa ni shughuli za Muungano. Mkoloni alipeleka Bungeni marekebisho ya Katiba hiyo na kuongeza kifungu cha orodha ya Makubaliano ya Muungano kinachohusu masuala ya fedha, mabenki, sarafu, fedha za kigeni na udhibiti wa fedha za kigeni kuwa katika orodha ya mambo ya Muungano kama inavyosemeka.
“The following matters are hereby reserved to the Parliament and Executive of the United Republic and declared Union matters:   currency, coinage and legal tender (including paper money; banks (including saving banks) and banking; foreign exchange and exchange control; and subsection (1) of the section 68 of the Interim constitution is hereby amended by adding the said matters as a new item (xii) to the definition of “Union matters” therein.”
(Interim Constitution 1965)
22 Machi 1966 Mkoloni mweusi alizikumbiza haki na amana zote (assets) za Zanzibar zilizokuwemo katika Bodi hiyo zipelekwe katika Benki Kuu chini ya Serikali ya Muungano na kwamba kuanzia pale ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania pekee ndiye tu ataeiwakilisha Tanzania katika Bodi hiyo.
Baadhi ya maelezo ya barua ya Mhe. Amir  H. Jamal yanasomeka hivi:
“ On behalf of  the Government of  United Republic of Tanzania (hereinafter referred to as “the Government”) I have to say that in view of sub-clause xi and sub-clause xii of the definition of  “Union matters” in section 85 of the Interim Constitution of Tanzania 1965 (No. 43 of  1965) barua inaendelea  —— (a) —-,
 (b) all distributions of capital or profits made by the Board in respect of Tanzania including any share which but for the provisions of  the Interim Constitution, referred to above, would be payable direct to the  Executive for Zanzibar, are due and payable only to the Government
Mwaka 1969 mkoloni mweusi Wameyaweka mafuta na gas asilia kuwa ni mambo ya muungano. Lakushangaza sheria zinazotumika ni za mwaka 1980.
[Petroleum exploration and development in Tanzania is governed by the Petroleum (Exploration and Production) Act 1980.]
5/2/1977 Mkoloni mweusi akahakikisha kwamba hatuna chama cha watu cha kutetea maslahi ya Zanzibar. Aliviunganisha vyama vya ASP na kile cha TANU. Mwishowe wameingia hata katika utamaduni wetu.
Mwaka 1977 Mkoloni mweusi alijifananiza na kinyonga, akaanza kujibadilisha tena jina la nchi yake ili apate kuibadilisha na nchi ya Zanzibar. Baada ya kutungwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara ya 94(1) ya Katiba hiyo inaweka majina ya Tanzania Bara ikimaanisha iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Tanganyika na Tanzania Visiwani ikiwa ni ile iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Mwaka 1984 mkoloni mweusi alifanya mabadiliko mengine ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mabadiliko hayo (The 5th Constitutional Amendment) yalifanywa ili kubadilisha maneno Tanzania Visiwani “Kuwa Tanzania Zanzibar” kwa kumaanisha ile iliokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Mwaka 1992 Mkoloni mweusi alijitengenezea mfumo wa vyama vingi chini ya himaya yake. Hali iliyoibana Zanzibar kutokuwa na vyama vya kutetea maslahi yake pekee bila ya idhini ya mkoloni.
Mwaka 1993 Mkoloni mweusi alikataa katakata na kuilazimisha Zanzibar iliyokwisha jiunga na jumuiya ya OIC, kujitoa.
Mwaka 1995 Mkoloni mweusi alikiondosha cheo cha Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Hali iliyopelekea kushuka hadhi ya Rais wa Zanzibar pamoja na kupoteza itifaki yake.
Mwaka 2003 Mkoloni Mweusi ulijikumbuzia mapato yatokanayo na uchumi wa Zanzibar pale walipoanzisha Tanzania Revenue Aothority (TRA).
Mwaka Mkoloni mweusi amejichukulia maliasili ya Zanzibar kwa kuifanya Bahari kuu (Deep sea) kuwa suala la muungano. Hata hivyo serikali ya Zanzibar bado haijaridhia uamuzi huu, tayari wameshaanza kuchukua mapato yapatikanayo kutoka bahari kuu
When the British Protectorate over Zanzibar was enforced in 1890, due to the death of Khalifa bin Said (ruler of Zanzibar), the island was in tatters. The new sultan was ‘allowed’ to continue in a ceremonial capacity but the British really called all the shots. By the end of World War I, the British were handed control of Tanganyika (to become Tanzania) but kept the two areas separate as Zanzibar still had a sultan.

MZINDAKAYA ANAJUWA KUWA MUUNGANO UKIVUNJIKA WAZANZIBARI WAKAJITENGA TU WATANGANYIKA WATAPIGANA NA KUBAGUWANA WENYEWE KWA WENYEWE KIMAKABILA


MZINDAKAYA AMEKUWA MBUNGE KWA MIAKA 40 KWENYE NCHI YA TANGANYIKA NINI KAFANYA KWA WANANCHI WA TANGANYIKA..?? ZAIDI YA KUJAZA TUMBO LAKE NA FAMILIA YAKE.

MBUNGE mstaafu wa Kwela,Sumbawanga mkoani Ruvuma, Chrisant Mzindakaya ameitaka katiba ilinde Muungano, kwa madai kuwa ukivunjika madhara yake kwa usalama wa nchi ni makubwa kuliko bomu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam baada ya kuwasilisha maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mzindakaya alisema kuwa hasara ya kuvunjika kwa Muungano ni kubwa kwani ni uhai wa taifa.

“Muungano ukivunjika tutatafutana hapa, kutakuwa na ugomvi na hasara itakayopatikana ni kubwa na nchi za Magharibi watafurahi maana watatugawa na hapo uvamizi wa rasilimali utazuka,” alisema.((nchi za magharibi miaka 40 ya ubunge wako nchi za magharibi zimekushika wapi mbona hujaijenga Tanganyika..??))

Mzindakaya ambaye ameshika wadhifa wa ubunge kwa miaka 40, alisema kuwa amependekeza katiba mpya iandaliwe kwa maslahi ya nchi na kuitaka tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, kutokubali maoni ya viongozi wanaotamani vyeo.

Alisema katiba hiyo iifanye nchi izaliwe upya ikiwemo rasilimali za nchi kuwa za Tanganyika ((Watanzania)) na mmiliki awe serikali.

“Ardhi, madini, gesi na maliasili zote zinaweza kuwekezwa, lakini wananchi wakamiliki asilimia 46, na lazima katiba ilinde wazalendo ili watu wasiwe watumwa katika nchi yao.

“Nimependekeza katiba ikatae biashara ya chumvi, maua eti mwekezaji katoka nje ya nchi, sasa sisi tufanye kazi gani? Nimetaka wawekezaji wasajiliwe,” alisema.

Alisema kuwa amependekeza rais asipewe nafasi ya kuchagua wabunge kumi wakiwemo wa viti maalumu, badala yake wapigiwe kura na si kuchaguana kama wafanyavyo sasa.

Naye Mbunge wa zamani wa Moshi Vijijini, Thomas Ngawaiya, amependekeza katiba mpya itamke wazi rasilimali za nchi ni mali ya wananchi na itamke mrabaha utakaotolewa kwa eneo husika lenye rasilimali hiyo, ili kuondoa migogoro kama ya gesi ya Mtwara na mafuta ya Pemba.((mafuta ya pemba!! ndio maana hamutaki kuvunja muungano sio kwa kuwa pemba kuna mafuta..???))

Ngawaiya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo (Cegodeta), alipendekeza kuondolewa kwa viti maalumu kwa sababu vinadumaza wanawake na kuchochea rushwa ya ngono ndani ya vyama vya siasa.

SHEIN ASEMA SIMUOGOPI MTU((HUYU KAEKWA ILI AWASHUGHULIKIE WAZANZIBARI WANAO DAI ZANZIBAR HURU


Waziri asiye na wizara maalum wa Zanzibar, Dk.Kumbi Ali Mohamed Shein amesema Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMIKI) hawana ubavu wa kuwaamsha Wazanzibari kwa kuwa wananchi wake wamekwisha amshwa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.
Dk. Kumbi Shein alitoa tamko hilo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika tawi la CCM Kinuni na kuwahutubia wananchi katika ziara yake ya kukagua uhai wa chama chake visiwani  nchini Zanzibar, juzi.
Dk Kumbi Shein alisema kuzinduka kwa wananchi na kupigania haki zao kasi yake iliongezeka kuanzia mwaka 1957 pale jumuiya mbili za Waafrika na Washiraz zilipoungana na kuzaliwa kwa chama cha Afro Shiraz Party (ASP).
“Uamsho unamuamsha nani, ni nani aliyelala wakati Wazanzibari waliamka kitambo na ilipofika mwaka 1964 wazee wakafanya Mapinduzi ya umma yaliyoongozwa na Mzee Abeid Karume,((karume hakuongoza alikuwa Tanganyika alikimbia ni john okello kama hujuwi historia kasome tena))”alisema Dk Kumbi Shein.
Alisema watu wanaofanya vitendo vya vurugu ikiwamo uharibifu wa mali na kuchomwa moto kwa matawi na maskani za CCM serikali yake haitawavumilia kwani mikono ya sheria itawakamata.((kwa kuwa mwanao ni jaji utafanya utakavyo))
Alisema nchi nyingi duniani zimesifia((tutajie majina ya hizo nchi))  muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ((Tanzania)) ikiendelea kupata sifa kutokana na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kuwapo kwa misingi ya demokrasia na kufuata utawala bora wa sheria.((wakuwaweka masheikh jela bila ya thamana na kuipiga kesi yao dana dana ndio utawala bora na sheria huwo kumbi shein..??))
Dk Kumbi Shein aliyasema hayo baada ya wananchi kulalamika mbele yake kuwa tawi moja la chama hicho katika eneo la Kununi kuchomwa moto na watu wasiojulikana zikiwamo na maskani kuu za Kisonge na Kachorora mjini Zanzibar.
“Siogopi mtu ila mimi hufanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria,((katiba ipi ya zanzibar au ya bwana wako Tanganyika mkoloni mweusi aliyekuweka madarakani..??)) sitomchelea kiongozi yeyote anayevunja sheria za nchi, Zanzibar ni yetu sote, ili tuishi kwa amani ni wajibu wetu kutii sheria zilizopo,”alisema.
Alisema watalii na wageni mbalimbali mashuhuri duniani huitembelea Zanzibar na kuingiza asilimia 80 ya fedha za kigeni kupitia sekta ya utalii na kwamba vitendo vya fujo na vurugu ni sawa na kuwafukuza watalii wakati ndiyo nguzo ya uchumi wa Zanzibar.
Alisema Zanzibar kwa asili yake haina historia ya matukio ya uchomaji moto kwa mali za serikali au watu binafsi na kuwaonya wanaofanya vitendo hivyo watafute kazi za kufanya kwa vile serikali yake imeshaamua kupambana nao kwa gharama yoyote.
Alisema vitendo vya vurugu na ghasia vilivyojitokeza mwaka jana haviwezi kukubalika katika nchi inayoongozwa kwa misingi ya utawala wa sheria na kuwaasa vijana wakatae kutumiwa na wanasiasa waliopoteza mwelekeo kwa kutafuta mafanikio ya kisiasa kwa njia za mkato.                        

((WEWE MWENYEWE HUKUSHINDA UCHANGUZI WA RAISI KILA MOJA ANAJUWA UKATUMIA NJIA YA MKATO YA MAJESHI YA KITANGANYIKA SASA UNAJIAMBIA MWENYEWE 

Sunday, April 28, 2013

SHEIN HABU KUBALI YAISHE KAMA WEWE SIO RAISI HEBU KUBALI DAAAAAAAAAH


MARAISI WATANO WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI WAKUTANA JIJINI ARUSHA NCHINI TANGANYIKA ZOMBI SHEIN UKO WAPI..?? AHAA NIMEKUMBUKA WEWE SI RAISI NI WAZIRI USIYE NA WIZARA UMEWEKWA HAPO UWATESE WAZANZIBARI WANAO TAKA NCHI YAO YA ZANZIBAR KUTOKA KATIKA MAKUCHA YA TANGANYIKA NDIO KAZI YAKO.
Arusha. Marais watano wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, wanakutana jijini hapa Arusha nchini Tanganyika katika mkutano wa dharura, ambapo pamoja na mambo mengine watajadili itifaki ya umoja wa fedha katika nchi za Afrika ya Mashariki, kabla ya kutiwa saini Novemba mwaka huu.
Marais hao ni Yoweri Kaguta Museveni Rais wa Uganda, ambaye ndiye Mwenyekiti, Jakaya Kikwete wa Tanganyika, Pierre Nkuruzinza wa Burundi, Paul Kagame wa Rwanda ambaye hayuko pichani na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta,je ((Dr Kumbi Shein Zombi..??)) wote walitarajiwa kuanza kuwasili jana Arusha.
Kenyatta anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa leo, kwani atakuwa anahudhuria kwa mara ya kwanza katika vikao vya EAC jijini Arusha nchini Tanganyika kama Rais wa Kenya.
Katika kikao cha marais hao, ambacho kitafanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto, pia anatarajiwa kuapishwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki anayetokea Kenya, Charles Njoroge na pia kuapishwa majaji wawili wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki, Dk Faustin Ntezilyayo kutoka Rwanda na Liboire Nkuruzinza kutoka Burundi.
Kikao cha marais hao, kilitanguliwa ni kikao cha makatibu wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na pia Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari ya Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Richard Sezibera, alisema mawaziri wa jumuiya hiyo, pia walijadili itifakiwa umoja wa fedha kwa nchi hizo na taarifa yao itapelekwa kwa marais leo.
Pia mawaziri hao, walijadili bajeti ya jumuiya hiyo ya mwaka 2013/14 ya Dola 117,238,966, walijadili pendekezo la kuongezea wigo na mamlaka Mahakama ya Afrika ya Mashariki na pia undaaji wa itifaki ya haki na kinga kwa watumishi wa jumuiya ya Afrika ya mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Afrika ya Mashariki wa Tanganyika, Samweli Sitta alisema tayari baraza la mawaziri, limepitisha bajeti ya jumuiya hiyo na taasisi zake zote.
Sitta alisema kuhusiana nauuamuzi wa masuala mbalimbali ambayo yalijadiliwa na mawaziri hao, taarifa rasmi itatolewa leo na marais baada ya kuyapitia .
Hata hivyo, alisema katika kikao cha mawaziri, Kenya iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Kenya kwa kuwa bado Waziri wa Kenya hajathibitishwa na bunge.((je mwanasheria mkuu wa Zanzibar anaejikuna kama anaupele wa ukurutu mbona hajatuwakilisha Wazanzibari..??))

KILA ANAYE HOJI MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR HUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA,HUULIWAA,HUNYANGANYWA MADARAKA KAMA NI KIONGOZI, AU HUWEKWA JELA KWA NINI..??


Zanzibar na Tanganyika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yakulazimishana kwa mabavu na nguvu za kijeshi na polisi nchi ya Tanganyika thaidi ya nchi ya Zanzibar ni zao la kuungana kwa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, ambazo ziliungana Aprili 26, 1964 bila ya kuuliza rai wao kama wanautaka au hawautaki.
Lakini miaka 49 tangu kuwapo kwa Muungano huo, suala linaloulizwa na Watanganyika, na Wazanzibari ni je, Muungano umeimarika au unadhoofika.? Yapo mawazo tofauti kutegemea na mtazamo wa mtu na vigezo anavyotumia kukiona kitu kimeimarika au kimedhoofika.
Kwa mtazamo wa wengi hapa nchini Zanzibar, Muungano unachechemea, yaani unakwenda ule mwendo unaoitwa ‘ kiguru cheche cheche’.
Kilicho wazi ni kuwa Watanganyika hawaelewi Muungano unatoka wapi na nini maana ya Muungano wao wanaona kama ni kula makongoro tu.ukija Zanzibar wanaelewa Muungano unakotoka hapa ulipo, lakini hawana hamu tena wala uhakika ni wapi hasa unakoelekea na wengi wao wanaona bora uishia hapa hapa kabla haujawamaliza.
Kila baada ya siku chache unasikia malalamiko mengi kutoka kwa watu wa pande zote mbili,nchini Tanagnyika na nchini Zanzibar pia, juu ya muundo na namna Muungano unavyoendeshwa. Haya yote yamepewa jina la kero za muungano.
Malalamiko ya muungano
Hivi karibuni tumesikia bungeni mjini Dodoma malalamiko mapya. Nayo ni kuwa majimbo madogo ya Zanzibar yanapewa mafungu mawili ya mfuko wa jimbo wakati ya Tanganyika yakibakiwa na fungu moja.

Kinachosahauliwa ni kwamba hata wakati wa kuungana hakuna aliyekuwa hafahamu kwamba Tanganyika ni kubwa na Zanzibar ni ndogo, lakini pande zote mbili zilikubaliana kuwa washirika sawa wa Muungano baina ya Nyerere na Mzee Karume.tafauti na sasa kumekuwa na kaka mkubwa na mdogo wake. Madai mengine ni madai kuwa Watanganyika wananyimwa haki ya kumiliki ardhi visiwani na kwamba Wazanzibari wamejazana kwenye Bunge la Muungano wakati Watanganyika hawaruhusiwi kuingia kwenye Baraza la Wawakilishi.
Lawama au kasoro hizi zinakwenda sambamba na malalamiko ya Wazanzibari kwamba Watanganyika wamejazana katika taaasisi za Muungano zilizopo visiwani, kama vile, Benki Kuu (BOT), Mamlaka ya Mapato Tanganyika  ((Tanzania)) (TRA)Ubalozi nje ya nchi zote ni Watanganyika n.k.
Katika hili zimetoka kauli zilizojaa hasira hata ndani ya Baraza la Wawakilishi za kutaka ((TRA)) ifunge virago vyake na kuondoka Zanzibar kwa kile kinachodaiwa kuwapo ajenda ya kuua uchumi wa nchi ya  Zanzibar, hasa katika sekta ya biashara.
Kwa bahati mbaya yote haya yanaonekana kama yanapuuzwa na viongozi na unachokisikia ni kuwa viongozi wa pande mbili za Muungano huu feki wanalishughulikia suala hili kwa misingi ya utashi wa kisiasa na sio kwa faida ya wananchi wa nchi hizi mbili.
Taarifa kuhusu kuungana
Siku ile ya tarehe 26 Aprili, 1964, saa 10 jioni watu wengi walikuwa wamekaa kwenye vijiwe vyao na kupumzika kijiwe kimoja maarufu cha Mtaa wa Baraste Kipande, mjini Unguja,watu wakizungumza na kungojea zamu zao ifike ili waweze kucheza dhumna na karata na bao.

Alikuja mwalimu mmoja wa skuli,na kueleza kuwa nchi yetu ya  Zanzibar na nchi ya Tanganyika zimeungana na mkataba wa muungano umetiwa saini mjini Dar es Salaam kati ya marais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Sheikh Abeid Amani Karume (Zanzibar).
Wazee na vijana waliacha mazungumzo waliyokuwa nayo na michezo yote … bao, dhumna na karata ilisimama. Mjadala ulianza na wengi walishangazwa na habari zile.
Mtu mmoja aliyepigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kushiriki kujenga daraja la Mto wa Kwai (angalia filamu ya sinema ya Bridge over the River Kwai) kule Mynamar, wakati ule Burma, Mzee Maulidi aliyejulikana kwa jina la ‘Kade Vondik’ alisema: “Tumekwisha.” Nini alichokusudia kulitegemea mtazamo wa mtu na tafsiri ya neno hilo.
Siku iliyofuata watu wengi walitumia muda mrefu kusikiliza redio na kusoma magazeti kujua habari za Muungano. Hapakuwa na sherehe zozote zile kuadhimisha kuungana kwa nchi hizi mbili unaweza kujiuliza kwa nini...?? Siku chache baadaye palifanyika mkutano wa hadhara ambao kila pembe ya uwanja wa mkutano walikuwapo askari waliobeba silaha wakitokea nchi ya Tanganyika ambao inasemakana waliletwa kuilanda Zanzibar ati isivamiwe.unaweza kujiuliza tena ivamiwe na nani..?? na ilikuwa ishavamiwa tayari na Watanganyika wakati huo.
Hapo Mzee Karume aliwauliza waliohudhuria kama walifurahia hatua ya kuungana au vipi. Sauti zilipaa kwa kusema, “Tunautakaaa!”
Hofu
Watu wengi waliiona hatua ya Mzee Karume ya kuwauliza wananchi kwa namna ile kama walikuwa wanautaka Muungano au vinginevyo kwenye mkutano ule ilikuwa na kasoro.

Kwanza, ilikuwapo dhana kuwa watu wangeulizwa kwanza kabla ya kuundwa kwa huo Muungano na siyo kuunganisha nchi na baadaye kuwauliza watu.
Pili, suala kama lile walihisi lilihitaji kupigiwa kura ya maoni. Tatu, ni kwamba mazingira yaliyokuwapo pale ya kila pembe kuwapo askari wa Kitanganyika yalikuwa ya kutisha na kwa hivyo hayakumfanya mtu kujisikia kuwa huru kutoa hisia zake zozote zaida ya tunautaka.
Zaidi ya hapo ni kwamba wakati huo watu wengi waliokuwa na mawazo tofauti na Serikali juu ya masuala mbalimbali walikuwa wakipotea kimyakimya na mpaka leo hawajulikani wako wapi watu hao wala makaburi yao yako wapi watu hao, hivyo hakuna hata mtu mmoja ambaye angethubutu kupinga hadharani. Muungano ulipo undwa ulionekana zaidi kuwa wa kisiasa kuliko wa kiuchumi.
Siku ya pili au ya tatu baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi, baadhi yao sasa marehemu, waliambiana vipi mambo haya na wengi wameshtukizwa tu na kuundwa kwa Muungano huu feki.Wapo watu waliofurahia kwa kueleza huo ulikuwa mwisho wa kamata kamata ya watu na kupotea kwa watu na kuuliwa watu kisiri siri bila ya kujulikana makaburi yao yaliyokuwa yakiendelea nchi Zanzibar, lakini wapo walioona haikuwa jambo la busara bali na kupelekwa pelekwa tu.
Mengi yalizungumzwa na mjadala uliendelea kwa siku nyingi, lakini kwa sauti ya chini huku watu wakiendelea kupotea wala muungano haikuwa ni sababu ya kuzuwia watu kupotea na kuliwa kisiri siri.
Nyerere siku moja alipokuja nchini Zanzibar aliwaambia viongozi kwamba wakiwamaliza hao wanaowaita siyo wanamapinduzi kuwauwa watauana wenyewe kwa wenyewe.
Ukweli ni kwamba palikuwa hapana fununu ya Zanzibar na Tanganyika kuungana. Hata aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Wolfango Dourado, aliyekuwa Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi (Baraza la Mawaziri) na mawaziri wa Serikali ya Rais Karume wamenukuliwa wakisema hawakushauriwa juu ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika na kuanzia hapo pia kila aliyepinga muungano huwa alifukuzwa kazi na kuishia jela au pia aliuliwa katika mazingira ya kutatanisha.
Dourado aliwekwa kizuizini wakati wa utawala wa Nyerere kwa kusema hakushauriwa Muungano ulipoundwa na kudai haukuwa halali na wengine wengi wamepotea hawajulikani walipo raisi mstafu Jumbe kavuliwa madaraka Maalim Seif alivuliwa madaraka na akasundwa jela weee na sasa uamsho hao hapo ushahidi kwa watu wanauthani kuwa kuhoji muungano si lolote ukihoji utapotea tu au utaka jela au kuuliwa katika mazingira ya utatanishi.
Watanganyika wanastahili kuamka na Wazanzibari wanastahili pongezi
Sasa, Muungano huu feki uliopitia kila aina ya mikiki na dhoruba umetimiza miaka 49 ya muungano wa lazima, wakati nchi nyingi za Kiafrika, Kiarabu na Asia zilizochukua hatua kama hii miaka ya nyuma zimeshindwa kuendelea kuungana kutokana na sababu za kisiasa na kiuchumi.

Watanganyika na Wazanzibari tumekuwa tofauti, kwani pamoja na matatizo yote tuliyonayo ya kisiasa na kiuchumi bado tumeishikilia kamba inayo tunyonga.
Kwa Watanganyika wengi,Wazanzibari wengi, suala la kuungana siyo tatizo. Kinachozusha mabishano na mivutano ni masuala gani ni ya Muungano na mambo gani yapo chini ya mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia serekali ya Zanzibar ipo ya Tanganyika imejificha wapi pia nchi moja kujifanya kaka mkubwa na nyengine kufanywa kama mkoa wa pwani.
Malalamiko juu ya mfumo wa Muungano yamesikika mara nyingi na yanaendelea kusikika. Katika mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya ya Tanganyika, suala la Muungano lilitawala mjadala.
Zanzibar wapo wanaotaka muundo wa sasa wa Serikali mbili uendelee, wapo wanaosema uwe wa Serikali moja wengi wao ni wahafidhina watumwa wa mkoloni mweusi Tanganyika na wapo wanaopendelea mfumo wa shirikisho wa Serikali tatu.
Lakini, pia lipo kundi linalotaka Muungano wa mkataba na lipo kundi wanaosema hawana haja ya Muungano hata kuusikia. Hii ni kudhihirisha kuwa wananchi wengi bado hawakupenda na hawatapenda kuendelea na Muungano huu feki,wakati umefika wa kuvunja au kama viongozi wanaogopa basi wawaulize wananchi katika kura ya maoni.
Wakati huu Watanganyika wanapoandika Katiba yao  Mpya,Wazanzibari wana katiba yao viongozi wasilififishe suala la Muungano huu feki, kama mjadala kuhusu je muungano wananchi  wanaoutaka au hawautaki wawaulize wala wasione haya kuwauliza.ila ikiwa viongozi watalazimisha na kuendele na udikteta wao wakuwalazimisha watu kuwa na muungano huu kwa kuwa Tanganyika inanufika na Wahafidhina wa Zanzibar wananufaika basi mutakuja kulia mdomo juu kama mbwa koko Gaddafi,Ben Ali,Saleh,Hussein Mubarouk na sasa Assad wangalieni kama hamjasoma basi wananchi watawasomesha.

Friday, April 26, 2013

SPIKA WA BARAZA LA WAWAKISHI NCHINI ZANZIBAR APANGUWA KAMATI ZA KUDUMU.((ILI WAGAWANE MAMILLIONI YA MAPESA BILA YA MAJUKUMU YOYOTE))


Omar Ali Shehe, Mtando wabakishwa PAC.
• Hamza kuendelea Ofisi za Viongozi wakuu, Mshimba, Subeit Waongezwa..
• Jussa aenda Mawasiliano na Ujenzi.
• Wenyeviti kuchaguliwa mwezi uajo

Na Himid Choko, BLW
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho amepanguwa Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Baraza hilo na kuwapanga upya .

Katibu wa Baraza hilo Yahya Khamis Hamad amesema, Spika amefikia uwamuzi huo kwa kutekeleza mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni ya 107(2) ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi (Toleo la 2012) inayohusiana na Uwezo wa Spika kuunda Kamati za Kudumu za Baraza.
“ Kanuni ya 107 inaelezea Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Kudumu ambapo Kanuni hii pia inakataza Makamo Wa Pili wa Rais, Waziri, Naibu Waziri au Mwanasheria Mkuu kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Kamahti hizo. Aidha kanuni hii ya 107 (2) inampa uwezo Mheshimiwa Spika Kuwateuwa Wajumbe wa Kamati hizo ” Alisema Katibu Yahya.
Amesema wajumbe hao wapya watazitumikia Kamati hizo kuazia Mwezi Mei 2013 mpaka kuvunywa kwa Baraza hapo mwaka 2015.
Katibu huyo wa Baraza la Wawakilishi amesema Katika uteuzi huo Mpya , aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Hamza Hassan Juma (Kwamtipura) amebakishwa kuitumikia tena Kamati hiyo.
Amesema Wajumbe wengine walioteuliwa kuitumikia Kamati hiyo ni Subeit Khamis Faki (Micheweni), Ali Mzee Ali ( Kuteuliwa) , Shadya Mohammed Suleiman ( Viti Maalum), Makame Msimba Mbarouk (Kitope) ambae hapo awali alikuwa akiongoza Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi . Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Kamati hiyo ni Saleh Nassor Juma (Wawi) na Ashura Sharif Ali (Viti Maalum).
Katika Kamati ya Katiba , Sheria na Utawala , walioteuliwa ni Mansour Yussuf Himid ( Kiembe Samaki), Wanu Khafidh Ameir (viti Maalum) , na Suleiman Hemed Khamis (Konde). Wengine ni Abdullah Juma Abdullah (Chonga) , Bikame Yusuf Hamad (Viti Maalum) na Nassor Salin Ali (Rahaleo).
Aidha katika uteuzi huo Mwakilishi machahari wa Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu amehamishwa kutoka Kamati yake ya awali ya Katiba, Sheria na utawala na sasa atatumikia Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi . Wengine walioteuliwa kuunda Kamati ya Mawasilino na Ujenzi ni Marina Joel Thomas ( Kuteuliwa), Mohamed Haji Khalid (Mtambile) , Hussein Ibrahim Makungu (Bububu), Mahamoud Moh,d Mussa (Kikwajuni) , Salma Mohammed Ali (Viti Maalum) na Mheshimiwa Panya Ali Abdullah ( Viti Maalum).
Walioteuliwa kuunda Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii ni pamoja na Mgeni Hassan Juma ( Viti Maalum), Mwanaidi Kassim Mussa (Viti Maalum), Hassan Hamad Omar (Kojani), Farida Amour Mohammed ( Viti Maalum), Addi Mossi Kombo (Matemwe), Ali Salum Haji (Kwahani) na Mohammed Mbwana Hamad (Chambani).
Aidha katika uteuzi huo Mheshimiwa Spika amewabakisha Omar Ali Sheikh (Chake Chake), Mbarouk Wadi Mtando (Mkwajuni), Shamsi Vuai Nahodha (Mwanakwerekwe), Fatma Mbarouk Said (Amani) kuwa Wajumbe wa Kamati ya Kuchunguza na Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (PAC). Wengine walioteuliwa katika Kamati hiyo ni Rafai Said Rufai (Tumbe), Mwajuma Faki Mdachi (Viti Maalum) na Salma Mussa Bilal (Viti Maalum) na Jaku Hashim Ayoub (Muyuni).
Katika uteuzi huo mpya wanaounda Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ni pamoja na Salmin Awadh Salmin (Magomeni), Salim Abdullah Hamad (Mtambwe), Hamad Masoud hamad (Ole ), Viwe Khamis Abdullah (Viti Maalum), Asha Abdu Haji (Viti Maalum), Hija Hassan Hija (Kiwani) na Raya Suleiman Hamad ( Viti Maalum).
Katika Kamati ya Mifugo, Utalii na Uwezeshaji na Habari walioteuliwa ni Asha Bakari Makame (Viti Maalum), Mlinde Mabrouk Juma (Bumbwini) na Kazija Khamis Kona ( Viti Maalum). Wengine ni Asaa Othman Said (Wete), Abdullah Mohammed Ali (Mkoani), Amina Iddi Mabrouk (Viti Maalum), Mussa Ali Hassan ( Viti Maalum) na Mohammedraza Hasanali Dharamsi (Uzini).
Kamati hizi mpya za Baraza la Wawakilishi zitafanyakazi zake kuazia sasa mpaka kumalizika muda wa Baraza la Nane la Wawakilishi kwa mujibu wa Maamrisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Kifungu cha 85 (1) Cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 kinasema kua “ Kutakuwa na Kamati za Kudumu za Baraza la Wawakilishi zitakazoundwa kwa mujibu wa wa Kanuni za Baraza la wawakilishi”.
Aidha Kanuni ya 109 (4) ya Baraza la wawakilishi toleo la 2012 inasema kwamba Wajumbe walioteuliwa Katika Kamati Fulani ya Kudumu wataendelea kuwa Wajumbe wa Kamati hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na miezi sita kuazia siku ya uteuzi wa kwenye kamati hiyo.
Hata hivyo katibu Yahya amesema Kamati hizo zinategemewa kukutana ili kuwachagua Wenyeviti na Mawakamo Wenyeviti kabla ya kuanza kazi za Kamati Mapema mwezi ujao.
.((ILI WAGAWANE MAMILLIONI YA MAPESA BILA YA MAJUKUMU YOYOTE MAANA NCHI IKO VILE VILE INANUKA))

SAMIA SULUHU ASEMA WATU WENGI HAWAUJUWI MUUNGANO VIJIJINI ZANZIBAR!!!


SAMIA SULUHU KUMBE NI MGOGO ASILI YAKE NDIO MAANA KAZI KUOMBA OMBA APATE KUMALIZA MJENGO WAKE ANAO UJENGA ANAJIDAI ATI ANATAKA ASAIDIWE ILI AWAFIKIYE WATU WA VIJIJINI AWAELIMISHE NINI MAANA YA MUUNGANO WEWE MAMA WATU WA ZANZIBAR WANAUJUWA MUUNGANO KULIKO WEWE MTAPIA MLO MWENYE NJAA USIYE SHIBA UNATAKA KUIYUWA ZANZIBAR KWA MADARAKA MUTAKUFA NYINYI KISHA TUTAWAOMBEA SAADA ZA KUWAZIKA MAANAMUMEZOWEA KUOMBA SIO ZANZIBAR MUTAIWACHA HAPA HAPA.
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu amesema miongoni mwa changamoto anazokabiliana nazo ni kukosa rasilimali za kumwezesha kuwafikia watu hasa wa vijijini na kuwaelewesha dhana nzima ya Muungano.
Waziri Sululu alitoa kauli hiyo mjini hapa alipotembelewa ofisini kwake na Balozi wa Uingereza nchini, Diana Melrose, ambaye alitaka kujua changamoto anazokutana nazo katika nafasi aliyonayo.
Waziri huyo alisema kuwa watu wa vijijini wengi hawaelewi Muungano, hivyo kumuomba balozi huyo kuzungumza na wafadhili wengine, ili wawapatie rasilimali za kufanikisha lengo hilo.
Aidha, Balozi Melrose alipenda kufahamu zaidi kuhusu maoni ya waziri juu ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar na pia changamoto zitokanazo na muungano huo.
Waziri Suluhu alisema kwa upande wake anaona ni bora kuendelea na Muungano kuliko kuuvunja na kushauri mabadiliko yafanyike ili kuuboresha.
Pia alisema yapo makundi yenye ushawishi mkubwa katika jamii hivyo hutumia nafasi waliyonayo kuwashawishi wananchi kuwa Muungano uvunjike sababu hauna maana.

Alitoa mfano wa baadhi ya makundi hayo ni wanasiasa na viongozi wa dini akisema sababu wao wanao ushawishi mkubwa katika jamii.
Akijibu swali la Balozi Melrose ambaye alitaka kujua kwamba inasemekana watu wa Zanzibar hawana furaha sababu ya Muungano hivyo ndiyo maana wanashauri uvunjwe, alikiri kuwapo kwa watu hao na kusema hali hiyo anafikiri inatokana na ubinafsi

KILA ATAKAE JARIBU KUZUNGUMZA MUUNGANO ATAKIONA CHA MTEMA KUNI


LULA ANAONA KUWA WAZANZIBARI WANA UHURU ZAIDI NA KUFANYA WANANVYOTAKA KATIKA MUUNGANO HUU KULIKO WATANGANYIKA ANA HAYA YA KUSEMA
Lula wa Ndali Mwananzela
GARIMOSHI la Katiba mpya linaendelea kwenda kasi na hakuna dalili ya kukoma mpaka Katiba “mpya” itakapopatikana. Msisitizo hadi sasa umekuwa juu ya ujio wa “Katiba mpya” hata kama upya wake utakuwa bado na mambo ya zamani. Mchakato huu ambao ulikosewa toka mwanzo una kila dalili ya kufanya zoezi la Katiba mpya kutofanikiwa na kutokukidhi mahitaji ya Watanganyika.(Watanzania).

Sheria inayosimamia mchakato huu na ambayo iliweka uwezekano wa tume ya Katiba kuundwa imeweka wazi mambo kadhaa ambayo wananchi (yaani wenye nchi) hawapaswi kuyazungumzia na kuyabadilisha isipokuwa tu kujadili kwa namna ya kuboresha. Yaani, wananchi (wenye nchi) wakitaka kuondoa jambo fulani kati ya haya, sheria inakataza.
Kifungu cha 9 cha Sheria hiyo ya 2011 kifungu kidogo cha 2 kimeweka orodha ya mambo ambayo ni lazima yadumishwe kwenye Katiba mpya na la kwanza kati ya hayo ni “kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano”.
Jambo hili kwa haraka laweza kuonekana kuwa ni jema, lakini tukiangalia kwa karibu tutaona kuwa kwa maamuzi ya watu walioko madarakani mojawapo ya matatizo makubwa kabisa ya kisiasa ambalo Taifa linahangaika nalo ni hili – uwepo wa Jamhuri ya Muungano.
Ikumbukwe kuwa tulipoungana na kuunda taifa la ((Tanzania)) tulikuwa nchi mbili kila moja ikiwa na hakimiya kamili. Kulikuwa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kulikuwa na Jamhuri ya Tanganyika. Nchi hizi mbili ziliungana na kuunda nchi hii ya ((Tanzania)). Tangu wakati huo hadi sasa hata hivyo Muungano wetu umekuwa sababu ya fahari lakini pia sababu ya maswali.
Miaka ya karibuni maswali haya yameanza kugeuka na kuwa shari baina ya watu wa pande zetu mbili. Kuna mgogoro ambao tayari umehusisha viongozi wa kitaifa. Wapo wananchi wa Zanzibar ambao wanaamini kuwa pamoja na kuingia katika Muungano, Zanzibar ilibakia kuwa nchi na imeendelea kuwa nchi. Hawa wanachodai ni kuwa kilichopotea baada ya Muungano ni serikali ya Tanganyika lakini Zanzibar imeendelea kuwapo.
Matokeo yake ni kuwa Wazanzibari wameendelea kushikilia Zanzibar lakini wakati huo huo wanadai ((Tanzania)) ((hapa nitakujibu hakuna mzanzibari anae shikila Tanzania na ikiwa yupo basi anasili ya Tanganyika)). Wazanzibar wana haki zote kama Wazanzibari na wana haki zote kama Watanzania.((huwo ni uwongo kabisa wazanzibari hawana haki hata ndani ya nchi yao zanzibar kwa kutawaliwa na nyinyi wakoloni weusi)) Wazanzibar wanaweza kuteuliwa katika ajira Zanzibar na wanaweza kuteuliwa katika ajira Bara;((huu pia ni uwongo)) wanaweza kuomba kazi Zanzibar wanaweza kuomba kazi Bara;((uwongo)) wanaweza kumiliki ardhi Zanzibar na wanaweza kumiliki ardhi Bara. Wazanzibar wakija Bara kwamba wanatoka Zanzibar haichukuliwi kwa namna yoyote tofauti((wanachukuliwa na kubaguliwa na kuitwa wapemba nyie wapemba rudini kwenu labda wewe hujuwi)).
Hivyo, Mzanzibari anaweza kwenda Bukoba, Iringa, Mwanza au Tanga na kufanya shughuli zake akijua yuko ndani ya nchi yake((hapana wanajuwa wapo ugenini kama walivyo ugenini katika nchi nyengine ulimwenguni)). Lakini pamoja na hayo bado ana haki ya kipekee Zanzibar((ndio maanake ndio nchi yao wewe ukienda india muhindi anahaki sio wewe ukienda canada mcanada ana haki sio wewe chaajabu kipi hapa au kwakuwa ni zanzibar..??))
Mtu wa Bara (Mtanzania anayetoka Bara) ((sema mtanganyika akitoka tanganyika hakuna mtanzania)) akienda Zanzibar hana haki zile zile isipokuwa kama vile ni mgeni (alien). Hana haki ya ajira au kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali.((huwo ni uwongo sepetu ni mtu wa wapi kama sio mbara..? ofisi nzima ya TRA ni wabara watupu na majaji ni wabara polisi wabara majeshi wabara ajira ngani unayozungumzia wewe..?? ya uchukuzi na kubeba mizigo na kuuza vibuwa ndio labda wanayofanya ni wazanzibari)) Rais wa Zanzibar hawezi kumteua mtu wa Bara kufanya kazi za Zanzibar bila kuonekana ameenda ‘nje’ ya Zanzibar kutafuta ajira japo Mzanzibari naye ni Mtanzania na mtu wa Bara naye ni Mtanzania.((usiseme mtu wa bara sema kweli mtu wa tanganyika)) Mtu wa Bara ni Mtanzania akiwa Tanzania lakini akiwa Zanzibar yeye ni Mbara kwani Zanzibar ni ya Wazanzibari lakini Tanzania ni yetu sote.((hapana zanzibar ni ya wazanzibari na tanganyika ni yawatanganyika na tanzania ni ngozi tu ya kondo ambayo tanganyika imeiva wasijulikane kama wao ni fisi bali ni kondo huku wakilaa zanzibar taratibu.))
Mtu wa Bara kwa Zanzibar yeye ni mgeni. Na tumeshuhudia baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakijaribu kutunga sheria zenye kuwashughulikia watu wa Bara kama wageni Zanzibar ndani ya Muungano huu huu.((wewe kweli kipofu baraza la wawakilishi ni watumwa wenu nyinyi wakoloni weusi kama sio wao leo hii hakuna muungano ila wao ndio wanaowarudisha na kuwafunga wazanzibari wanaotaka zanzibar huru))
Inaonekana walioungana ni watu wa Bara lakini watu wa Zanzibar wao bado hawajaungana.((hapa umepatia kabisa wazanzibari hawajaungana na wala hawataungana na watanganyika)) Wanataka chetu kiwe cha wote lakini cha kwao kiwe cha kwao.((hata mtanganyika ndio anataka cha wazanzibari kiwe chao na chawatanganyika kiwa cha watanganyika,ushahidi ni madini mbona mukipata pesa hatugawani nusu nusu..? gasi..? ubalozi nchi za nje..? lakini toka musikie zanzibar kuna mafuta sasa haraka haraka munataka kunda katiba mpya ili muifanye kuwa ni nchi moja muimeze zanzibar na kuipoteza katika ramani ya dunia asiyejuwa ni nani..?? Kisingizio (haiwezi kuwa sababu) ni kuwa ati “Zanzibar ni ndogo”.((ni dongo kweli sio uwongo wala kisingizio nyinyi mkoa moja tu unawatu millioni ngapi..?? na zanzibar nzima ina watu millioni ngapi..? nusu mkoa ukiwa utakuja zanzibar na kila ajae anapewa shamba au kiwanja kutakuwa hakuna tena zanzibar wewe vipi.))
Hivyo, kutokana na udogo wake basi ni lazima kuwe na nafasi za kuwalinda Wazanzibari.((ndio kabisa ))Hivyo ardhi ni kwa ajili ya Wazanzibar na ajira mbalimmbali ni kwa ajili ya Wazanzibari.((ndio kabisa ndio wenye nchi ati)) Ni sawa sawa na kule Marekani ati mtu wa California akienda Michigan aonekane ni mgeni na asiwe na haki hizo japo na yeye ni Mmarekani.((ile ni marekani hii ni zanzibar na tanganyika unajuwa ni nchi ngapi zile za marekani au wewe unathani ni nchi moja tu..?))
Katika mfumo huu ambao tunaambiwa una kero nyingi mara nyingi kinachoitwa “kero” ni kile ambacho Muungano unaathiri Zanzibar.((ndio kabisa muungano umeimaliza zanzibar sio kuiathiri tu bali imeuwa kabisa zanzibar)) Lakini maoni yangu ni kuwa kama kuna kero kubwa ya kimfumo ni ile ambayo inawabagua watu wa Bara wanapoenda Zanzibar au wanapotaka kuishi na wao kunufaika na Zanzibar kama sehemu ya nchi yao.((kwa nini iwe lazima zanzibar na sio Kenya,Uganda,Burundi,Rwanda ambazo mumepakana mipaka huku mpaka muvuke bahari kwa nini..??)) Wakati Bara mtu anaweza kutoka Kigoma na kwenda Arusha au kutoka Mwanza kwenda Tabora kujaribu maisha na asipate shida yoyote ya kuonekana mgeni alimradi yeye ni Mtanzania((sio mtanzania mtanganyika na yote hiyo ni mikoa ya tanganyika sasa tabu iko wapi na nyinyi nyote ni watanganyika ni nyinyi kwa nyinyi tabora arusha mwanza kigoma mumeungana mulikuwa na nchi zenu kwanza..??)) mtu huyo huyo akienda Zanzibar ataonekana mgeni na hatopewa ule ulinzi wa kisheria ambao yeye kama Mtanzania anao katika nchi yake.
Mtu wa Bara anapoenda Zanzibar ni kana kwamba anakwenda nchi nyingine((ndio ni nchi nyengine ushasahau kama tuliungana..??)) lakini Mzanzibari akija Bara anaenda sehemu ya nchi yake.((hata siku moja tunajuwa tukija bara ni wageni tena ndio mukatuita wapemba au wewe hujuwi..??)) Hivyo, swali ambalo huwa watu wanauliza kwanini Wazanzibari wanapewa ajira kwenye wizara zisizo za Muungano lina makosa kwa kiasi chake. Lina makosa kwa sababu Mzanzibari ana haki zote kama Mtanzania lakini si kila Mtanzania ana haki sawa Zanzibar – japo nayo ni Tanzania.((nikuwa hakuna tanzania ni ngozi tu))
Mzanzibari anapo omba nafasi kwenye chuo kikuu chochote Bara anafanya hivyo kama Mtanzania na nina uhakika Bodi ya Mikopo inatoa mikopo kwa Wazanzibari vilevile – kwa sababu na wao ni Watanzania.((huwo ni uwongo wazanzibari kibao wemenyimwa mikopo ili waendele kuwa wajinga na watanganyika waerevuke ili muendele kututawala.))  Mzanzibari anaweza kuomba kazi kwenye idara au vitengo vya Bara ambavyo si vya Muungano na akapewa ajira hiyo((hata siku moja unaota wewe)) – si kama mgeni (kwa mfano Mkenya au Mganda) bali akapewa nafasi kama Mtanzania kwani hiyo ni haki yake.
Lakini mtu wa Bara hawezi kuomba ajira kwenye idara au kitengo Zanzibar akachukuliwa kama Mtanzania tu; itapaswa ajibu swali kama yeye ni Mzanzibari. Kwani Wazanzibari wana urithi Zanzibar na wana urithi Bara.((hapa wazanzibari wanaurithi wa zanzibar yao tu na urithi ulikuwepo tanganyika wazanzibari hata mukitupa hatutaki chukueni nyinyi ndio maana hatutaki tena tuna taka kila moja awe na nchi yake kama tulivyokuwa awali))
Ni katika hili tunaweza kuona kuwa kutozungumzia uwepo wa Jamhuri ya Muungano ni kosa kubwa. Kama Wazanzibari wanataka kuendelea kuwa na nchi yao na ambayo watoto wao watairithi basi wapewe nafasi hiyo.((habu muambiye raisi wenu wa tanganyika kikwete afanye hivyo)) Watu wa Bara nao wapewe nafasi ya kufurahia urithi wao bila watu “wengine” kupewa urithi wasioutaka.((haswana tutaendele kuishi kwa amani na kama majirani))  Kosa hili la kutokuzungumzia “uwepo wa Muungano” ni kosa ambalo bado litaendelea kutuandama kama jinamizi.
Watu wa Bara nao wataanza kuchoka kuona nafasi “zao” zinachukuliwa na Wazanzibari wakati wao hawawezi kuchukua nafasi kule Zanzibar((hata tatizo wabara hawataka kutupa uhuru maana wao ni wakoloni weusi mumetupinduwa mwaka 1964 na mpaka leo zanzibar ni koloni la tanganyika ndio ukaona watanganyika wamengangania kuizuwia zanzibar maana wanajuwa ikipata uhuru tu basi)) bila ya kuonekana wanachukua nafasi za “Wazanzibari”. Hivyo, japo ni kweli wanaweza kutuletea Katiba mpya, ((sisi wazanzibari hatuwaletei nyinyi katiba mutajiletea wenyewe maana katiba yenu imeja viraka zanzibar inakatiba yake haina wasi wasi))hali halisi ni kuwa bado tutakuwa na tatizo lile lile la zamani; Muungano. Hata tukiwa na serikali tatu bado matatizo yatakuwa yale yale.
Je, Wazanzibari watakuwa na haki zozote Tanganyika..? Je, Watanganyika watakuwa na haki zozote Zanzibar..? Kosa hili litakuja kutugeuka mbele ya safari na kutuumiza kama Taifa.((litawaumiza nyinyi watanganyika wazanzibari tushaumia tushakufa tushafufuka na sasa tunataka nchi yetu nyinyi hata kuamka bado na kuuliza viongozi wenu nchi yenu ya tanganyika iko wapi hamuwezi je atakae umia nani..??)) Tufikirie

Tuesday, April 23, 2013

SHEIN NA KIKWETE WAKO HAMUNA UWEZO WAKUWATESA MASHEIKH ILA MUNAJIPALIA MKAA WENYEWE WAKWENDA KUWACHOMA VIZURI SIKU YA KIYAMAA.


makame silima
Wazanzibar wengi wanashindwa kufahamu matatizo ya Muungano hasa yapo wapi..???
Wengi husema ni Tanganyika yani (Watanganyika) mimi sikubaliani na hili moja kwa mmoja, Chanzo hasa cha Muungano ni Wazanzibar wenywe .
Nasema hivi kwa ushahidi kamili na kama kuna wakunipinga alete hoja zake hapa zifanyiwe kazi.
Wazanzibar tumejigawa ndio maana Watanganyika wakautumia mwanya huu na vivuli hivi kufanya watakavyo,Kama isingelekuwa hivyo basi tungekuwa na Zanzibar yenye heshima nje na ndani na Tanganyika yenyewe ingeliheshimu Zanzibar kama nchi na sehemu Moja kuu kubwa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Lakini wapi..?? tumeyatupa wenyewe yani wahafidhina walitupeleka ovyo na wanazidi kutupeleka ovyo kwa kukumbatia  CCM na kuuwacha Uzalendo na Mapenzi ya nchi yao Zanzibar, hili limewapa Mwanya hata Watanganyika na wenye asili ya Tanganyika kujiona wao ni Bora zaidi kuliko Wazanzibar ndio mzanzibar yoyote mwenye asili ya Tanganyika huwa yuko Tayari kuisaliti Zanzibar kwa kuipigania Tanganyika Ijitayo ((Tanzania)) kuendelea kuibinya Zanzibar.
Ikiwa Wazanzibar wenyewe wana wapa priort ya hali ya juu na kuwapa hata nafasi kubwa wageni na kuwapa kipau mbele huku wakiwanyima Wazanzibar asili tutegemee nini mbeleni..?? nikutoka katika Bad kuingia katika Warst.
Kilicho tawala Zanzibar ni ubaguzi,Chuki , Husda na Choyo , hizi ndio kero kubwa za Muungano na tutashindwa kufanya lolote kama tutaendelea nazo hizi , nyiyi hamuoni kila heri ikija na ikichanua hufuia kwa mambo haya.
Ndani ya nafsi za Wananchi wa Zanzibar mambo haya ndio yenye kututeketeza na kuiteketeza Zanzibar , Zanzibar imekuwa kama mtoto yatima asie na walezi.
Chuki zinapaliliwa hasa na hao wajitao Wahafidhina wengi wao wana nundu za Sijda lakini nafsi zao ni wabaguzi wakubwa na chuki na fitna ndani ya nyoyo zao huyu nani huyu nani.
Katika Serekali ya SMZ-GNU  na baraza lake la Wawakilishi takribani % 100 ni Waslima lakini % 100 hio hio ni Wanafiki na wasio juwa hata uislamu ni nini na jambo hili ni aibu kwa hulka ya Wazanzibar kuwa asilimia ya Viongozi wake ni Wanafiki tena Unafiki wao hivi sasa umeshika kasi na Ubaguzi.
Leo mtu anasthamini Sera za Chama na itikadi za Chama kuliko Dini ya Mwenyewe M/mungu.?? na mtu huyo ana chukuwa chuki za kisiasa kwa kuwahilikicha Mashekh wetu na maulamaa wetu kwa misimamo tu ya chuki za kisiasa..?? ama kweli Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ).
Tuangalie mifano hai hapa hapa Zanzibar ya viongozi wetu walivyo mbali na Dini ya Allah na wafuasi wake na wajumbe wake.!!!  Wanapokufa Mashekh kiongozi unae muona ni mmjo huyo huyo siki zote lakini Wakifa Mapadri hata Mikowani Tanganyika basi viongozi nusu ya SMZ-GNU huenda akiwemo Shein.
Padri akifa hapa Zanzibar tena ndio usiseme Serekali yote huenda kuzika kisha wakaja kukaa matanga, Lakini wakifa Mashekh hata habari hawana ,kafa Sheikh Nassor Bachu zaidi ya Ummati wa Wananchi viongozi wa Serekali ni Maalim Seif huyo huyo na Waheshimia wa-CUF .
Lakini Kafa Bi Kidude angalia Serekali ya Muungano yote ilikuweko Mazikoni na Matangani Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ).
Huu ndio ubaguzi na Jambo jengine wananchi angalia Mashekh wetu wanavyo teseka Magerezani huu hivi sasa ni mwenzi wa 5 kama sikosei wanakosa kutowa dawa ,wanakosa kusomesha ,wanakosa hata sala za ijumaa kusali na kutowa dawa hizo sala na kusoma masahafu naskia mwanzo walinyimwa humo ndani walivyo fanywa ni sistem ile ile ya Wantanamo Cuba.
Jee kweli Huyu Shein ni Muislamu kweli huyu na anaongoza jamii ya waislamu wa Zanzibar au anafuata itikadi za kitahuti na ubaguzi wakidini.??
Maana ikiwa anafuata sera na itikadi za Chama chake basi hata hizo sera za chama chake hazifuati!!! Wao viongozi wanafiki si wanasema Serekali haina dini yani Zanzibar na Tanganyika ((Tanzania)) haina dini..?? Sasa tuangalie kweli Serekali haina dini au inayo dini ina ikingia kifua Serekali.
Rais wa Muungano wa ((Tanzania)) Mrisho Jakanya Kikwete Jee huyu si Muislamu.?? Rais wa Zanzibar aliye wekwa na mkoloni mweusi Tanganyika  Dr Kumbi Ali Mohammed Shein , Jee huyu si Muislamu..??
Sasa marais wote hawa hawajuwi kuwa kusema Na Bii Issa Nabii Issa (Alayhis salaam) kuwa ni Muungu ni kosa kubwa kwa uislamu na Waislamu na nisawa na kuibua hasira mbele ya Waislamu mbona Maskofu na Mpadri na wanao wachunga makanisani na mitani huhubiri na kusema Hazarani kuwa Nabii Issa ni Mungu.!!! jee hawa mbona hawachukuliwi hatuwa zozote za uchochezi..??
Bali kuna Kijana Yule alofungwa Miezi 6 eti kakashifu dini ya watu na kuleta uchochezi wa kidini kusema Nabii Issa( Yesu sio Mungu ni Nabii wa M/mungu.)
Jee Ali Mohammed Shein kuna Padri yoyote uliomchukulia hatua hapa Zanzibar kwa uchochozi wa kukacshifu dini ya waislamu ambayo pia ni dini yako na Wazanzibar kusema Nabii Issa ni Mungu..?? au ndio chama kwanza na itikadi zake..??
Leo wewe na viongozi wenzako muujitao waislamu munakaa raha mustarehe huku Mashekh wako magerezani kwa ushauri na chuki za kisiasa tu ama kweli wewe Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ).
Wewe kwa mawazo yako unaona unawakomowa wale na kuwatesa lakini maskini hujuwi kuwa unajikomowa wewe na kujitesa wewe mbele ya Allah, kumbuka kuwa roho ya mumini haifi na hio imetokea mifano sehemu nyingi tu za dunia ikiwepo Saudia.
Kuna watu wa litaka kujenga wakanunua eneo na bada ya kuchimba eneo kwa kujenga wakogonga kaburi na kuona damu na kitambaa cheupe kiko vile vile na katika ufuatiliaji nikuwa hapakuwa na mava pale kipindi cha karne nyingi baada ya kuona mkasa huo ukaingiliwa na watafiti kujuwa vipi kaburi lile na kuwa bado maiti mbichi na sanda yake..??
Kuangalia kumbukumbu za karne za nyuma nikuwa eneo lile lilipiganwa Jihadi na wapiganaji Jihadi wengi walizikwa pale kwa hio Shein Roho ya Mumini haifi hua iko hai siku zote na aya zipo za M/mungu kusibiticha hayo.
Kwa hio na hawa Masheikh wetu ni watu waliojitolea kupigania haki na maonevu wanayofanyiwa waislamu wa Zanzibar kwa hio Shein na Kikwete wako mujuwe tu kuwa maisha ya dunia niyakupita tu na yana muda mfupi mbele ya Allah.
Kuna watu wakiishi miaka mirefu na kuwa majabari lakini baada ya kukaribiwa na mauti walijihisi maisha waloishi ni kupwesa na kupwesua tu na wakajuta na wakaomba waongezewe angalau siku ili waitumiliye kwa kutubu na kufanya ibada wapi..??yalaitani.
Wewe Shein huna mateso yakuwatesa wachamungu uwezo wako wakuwatesa ni mdogo na huna, Wachamungu ni watu waliozichukuwa nafsi zao na kumkabidhi Allah kwa hio utawatesa na wakishakufa huwezi kuwatesa tena huo ndio uwezo wako tu.
Lakini kumbuka na wewe jee baada ya kufa wao wewe una muda gani wakuishi.?? na jee ukionana na Mola wako na Uliowatesa tena wajumbe wake Allah utamwambiaje Dr Kumbi Shein Mollah wako..???
M/mungu walinde masheikh zetu na wakorofi hawa.

KHALEED NGWIJI ANA HAYA YA KUSEMA KUHUSU ZANZIBAR YETU KUWA NA MAMLAKA KAMILI

Photo: Gwiji-wazanzibar tuungane kulinda maslahi ya Nchi yetu.</p>
<p>Mwenyekiti wa vijana Zanzibar (VUK)Khaleed Gwiji asema kuwa Katiba ndani ya Nchi ni Kinga madhubuti baina ya Wananchi wenyewe na Watawala wao.</p>
<p>Gwiji ameyasema hayo wakati alipokuwa akichangia katika mjadala maalumu ulioandaliwa na taasisi ya wanasheria Zanzibar (law Sociey  ZLS )  hapo katika ukumbi wa taasisi mjini Unguja.</p>
<p> Mjadala huo ambao uliongozwa na Mwanasheria mkuu wa Serilali Bwana Othman Masoud pia uliwashirikisha wanafunzi mbali mbali wa vyuo vikuu pamoja na watu kutoka taasisi nyengine za kijamii.</p>
<p>Mdahalo pia uliokuwa na lengo la kujadili  nchi ya Zanzibar na mustakbali wake kupitia uundwaji wa katiba mpya.</p>
<p>Wakati akichangia Gwiji amesema kuwa anashangazwa na Serikali  kuwa bado haijawa na utamaduni wa kuheshimu Katiba na ndio maana hadi leo viongozi wa Uamsho wananyimwa dhamana jambo ambalo ni haki yao ya Kikatiba. </p>
<p>Pia amekiri kuwa ni kweli ndani ya jamii ya watu wa Zanzibar wapo watu tafauti ambao wanatafautiana maoni yao  katika muono wao wa uundwaji wa katiba mpya lakini busara iliobora ni kuheshimiwa mawazo yaliowengi ambayo wametoa kwa kutaka Zanzibar yenye mamlaka kamili.</p>
<p>‘’Ikiwa wananchi waliowengi ndani ya visiwa hivi vya Unguja na Pemba wametoa maoni yao ambayo simengin bali nikudai Zanzibar yenye mamlaka kamili basi ipo haja ya Serikali kuhakikisha kuwa Tume ya mabadiliko ya katiba inaheshimu mawazo hayo na kuyafanyia kazi”alieleza Gwiji.</p>
<p>Aidha amefahamisha kuwa kwa sasa wakati umefika kwa Serikali yetu ya Zanzibar kuwa na agenda ya Zanzibar kwanza ili tupate hatma njema pamoja na  mustakbal mzuri wetu sote pamoja na vizazi vyetu vya sasa na baadae.</p>
<p>''Lazima viongozi wetu wabebe agenda ya uzalendo na utaifa badala ya maslahi ya vyama vyao binafsi, Zanzibar ni zaidi ya vyama''aliseama gwiji. </p>
<p>Nao kwa upande wa baadhi ya wananchi wengine ambao walipata nafasi ya kuchangia kwa kutoa maoni yao wamesema kuwa bado hatujachelewa kuidai Zanzibar huru isipokuwa jamii ya kizanzibar inapaswa kubadilika kwa sasa kutokana na wakaazi wengi kujawa na jazba jambo ambalo haliwezi kutufikisha tunapotaka.


Mwenyekiti wa vijana Zanzibar (VUK)Khaleed Gwiji asema kuwa Katiba ndani ya Nchi ni Kinga madhubuti baina ya Wananchi wenyewe na Watawala wao.

Gwiji ameyasema hayo wakati alipokuwa akichangia katika mjadala maalumu ulioandaliwa na taasisi ya wanasheria Zanzibar (law Sociey ZLS ) hapo katika ukumbi wa taasisi mjini Unguja.
Mjadala huo ambao uliongozwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali Bwana Othman Masoud pia uliwashirikisha wanafunzi mbali mbali wa vyuo vikuu pamoja na watu kutoka taasisi nyengine za kijamii.
Mdahalo pia uliokuwa na lengo la kujadili nchi ya Zanzibar na mustakbali wake kupitia uundwaji wa katiba mpya.
Wakati akichangia Gwiji amesema kuwa anashangazwa na Serikali kuwa bado haijawa na utamaduni wa kuheshimu Katiba na ndio maana hadi leo viongozi wa Uamsho wananyimwa dhamana jambo ambalo ni haki yao ya Kikatiba.
Pia amekiri kuwa ni kweli ndani ya jamii ya watu wa Zanzibar wapo watu tafauti ambao wanatafautiana maoni yao katika muono wao wa uundwaji wa katiba mpya lakini busara iliobora ni kuheshimiwa mawazo yaliowengi ambayo wametoa kwa kutaka Zanzibar yenye mamlaka kamili.
‘’Ikiwa wananchi waliowengi ndani ya visiwa hivi vya Unguja na Pemba wametoa maoni yao ambayo simengine bali nikudai Zanzibar yenye mamlaka kamili basi ipo haja ya Serikali kuhakikisha kuwa Tume ya mabadiliko ya katiba inaheshimu mawazo hayo na kuyafanyia kazi”alieleza Gwiji.
Aidha amefahamisha kuwa kwa sasa wakati umefika kwa Serikali yetu ya Zanzibar kuwa na agenda ya Zanzibar kwanza ili tupate hatma njema pamoja na mustakbal mzuri wetu sote pamoja na vizazi vyetu vya sasa na baadae.
”Lazima viongozi wetu wabebe agenda ya uzalendo na utaifa badala ya maslahi ya vyama vyao binafsi, Zanzibar ni zaidi ya vyama”aliseama gwiji.
Nao kwa upande wa baadhi ya wananchi wengine ambao walipata nafasi ya kuchangia kwa kutoa maoni yao wamesema kuwa bado hatujachelewa kuidai Zanzibar huru isipokuwa jamii ya kizanzibar inapaswa kubadilika kwa sasa kutokana na wakaazi wengi kujawa na jazba jambo ambalo haliwezi kutufikisha tunapotaka.

Sunday, April 21, 2013

AMANI INAYOLILIWA NA SEREKALI YA SMZ-GNU-INA FAIDA GANI KWA WAZANZIBARI WENYE MAISHA YA UMASIKINI NA ITHLALI..???


makame silima 
Amani ikitoweka, masikini watapoteza nini..??
MJADALA juu ya tishio la kutoweka kwa amani nchini umeshika kasi. Wanasiasa wanawalaumu viongozi wa dini; viongozi wa dini wanawalaumu wanasiasa na serikali; serikali inawalaumu viongozi wa dini pamoja watu “wasiojulikana”. Kila upande unalaumu na hakuna upande unaokubali hadharani kuwa ni nani haswa amesababisha tishio hili.
Rais Jakaya Kikwete raisi wa nchi ya Tanganyika mara kadhaa amesikika akisema kuwa katika vita ya kidini hakuna mshindi. Kaulimbiu hii na kibwagizo hiki kitamu kimedakwa kwa ustadi na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari wanaoshindilia kuwa amani ikitoweka kila mtu ataathirika. Wote hapo juu hakuna anayetumia akili wala marifa wala muda kujiuliza nini chanzo cha kutoweka kwa amani nchini ni nini haswa chanzo cha kutoweka amani hawajiulizi.
Wasomi mbali mbali walifafanua kuwa amani ni tunda la haki. wakachambua kuwa bila haki amani itatoweka. Kisha wakasema, Zanzibar kuna amani lakini siyo kwamba kuna haki bali kuna tumaini kuwa siku moja haki itatendekea.
Tumaini la kutendewa haki ndilo limeshikilia mstakabali wa kuwa na amani nchini. Kinachoelekea kutokea kwa sasa, ni kukata tamaa. Watu wengi hasa masikini wamekata tamaa kuwa haki haiwezi kutendeka tena na ukali wa maisha unaongezeka kila kukicha Wazanzibari wana safa na maisha wala hawana mtetezi wala hawana wakuwahurumia.
Kukata tamaa kwa wananchi walio wengi kumeambatana na serikali ya majambazi SMZ kukosa uwezo wa kuongoza na kutawala. Ni rahisi kuwaambia watoto wenye njaa watulie kidogo na wavumilie kama wanaona wazazi wanashughulika kupika hata kama chungu kinachotokota kimejaa mawe tu. Jitihada za wazazi zinaweza kuwafanya watoto wenye njaa wapitiwe na usingizi na siku hiyo ipite.
Serikali ya majambazi ya SMZ  imeshindwa kabisa kushughulikia viashiria vya kutoweka kwa amani na hasa kuhakikisha haki inatendeka na masikini wanashughulikiwa kero zao. Kinachoonekana kutokea ni serikali kutumia ubabe wa nguvu za jeshi na polisi kila masikini wakinuwa sauti zao kudai haki. serekali kutumia baadhi ya taasisi ili zicheleweshe masikini kudai haki zao kwa njia yoyote watakayoona inawasaidia kwa sababu amani iwepo isiwepo hali ya masikini haibadiliki.
Mwanzo wa wiki hii wamiliki wa vyombo vya habari wamekutana jijini DSM huko nchini Tanganyika na kujadili suala hili wakitofautiana waziwazi juu ya nani anasababisha hali hii na pia ikiwa wana habari pia wana mchango katika hali hii tete. Wapo wana habari wanaolalamika kuwa wana habari wamenunuliwa na wanasiasa na kujikuta wanachochea mgogoro wa kidini nchini. Hawa wanalalamika kuwa wana habari watasababisha umwagaji damu kama ilivyotokea kule Rwanda.
Kundi jingine linakataa mtizamo huu. Linasema kule Rwanda si wana habari waliosababisha mauaji ya kimbali, bali ni wanasiasa na Vigogo. Wana habari walikuwa wanatangaza kile kinachosemwa na wanasiasa. Kwa ajili hiyo, mkutano wa wana habari pamoja na kukutana, hawakuleta jambo jipya katika mjadala huu na waliishia kulialia sawa na mtindo wa wanasiasa wetu pamoja na serikali. Hakuna aliye tayari kusema ukweli, na hakuna anayekubali kuwa anatumiwa.wala hakuna aliyejiuliza ni nini chenzo na hao wanao athirika wamesaidiwa vipi hakuna kabisa.
Kwa hali ilivyo nchini, mimi nasita kukubali kuwa amani ikitoweka watu wote watapata hasara. Hii ni kwa sababu lipo kundi kubwa hapa nchini ambalo halijafurahia uwepo wa amani inayoliliwa kuwa inaelekea kutoweka. Kundi hilo ni watu masikini wa kipato na masikini wa hali zote lakini matajiri na viongozi wao wataililia amani hii iwepo maana yao yanawaendea vizuri kabisa.
Mathalani, masikini anayekwenda katika hospitali zetu zisizo na dawa lakini akaishia kutozwa rushwa kila hatua anayopitia ndani ya hospitali. Tangu anapofika mapokezi mpaka anapata huduma anaombwa au kulazimishwa kutoa rushwa bila kujali anacho au hana. Huyu masikini ana manufaa gani na amani inayoliliwa na Serekali ya SMZ..??
Masikini anayebambikiziwa kesi na polisi japokuwa hajafanya jambo hilo ila anabambikiwa tu ili alipe mapesa ndio achiwe huyu ana manufa gani na amani  inayoliliwa na serekali ya SMZ..?? au masiki kupeleka malalamiko yake polisi akaishia kuombwa rushwa kwanza ndio asaidiwe katika malalamiko yake huyu ana manufa gani na amani inayoliliwa na serekali ya SMZ..?? Masikini wengi ndio wanakaa rumande muda mrefu; kesi zao huchukua miaka mingi, na ndio wanalazimika kuuza utu wao ili kuwahonga polisi waweze kuachiwa. Nyumba zinauzwa na mashamba yanauzwa ili kuwahonga polisi wafutiwe kesi zao.
Siku hizi matajiri nao wanaweza kuwanunua polisi ili wawatese masikini waliokosana nao kwa mambo binafsi. Hivi sasa vituo vya polisi kote nchini vimegeuka kuwa vituo vya kukusanya rushwa za watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya kweli na ya kubambikizwa. Masikini anayefanyiwa haya Amani inayo hubiriwa ina thamani gani mbele ya polisi wala rushwa na waonevu wa tashi wa kisiasa..?? Tukubaliane amani haitikuja katu mbele ya maonevu na ubambikizaji wa kesi za uongo. Ikiwa wao vyombo vya Usalama Jeshi la polisi kazi yao kubwa nikulinda usalama wa raia na mali zao ,leo wao ndio wavunjaji sheria na wala rushwa na wakadamizaji wa wanyonge,jee amani kweli itakuwepo na kwa faida ya nani amani hiyo..??
Barabara zetu kuu na za mitaani zimejaa polisi wa usalama barabarani ambao kazi yao kubwa ni kukusanya rushwa tangu asubuhi mpaka jioni rushwa mtu. Polisi hawa wanakusanya rushwa kutoka kwa waendesha pikipiki na madereva wa magari , polisi hao hao wamekuwa wakitumia vyeo vyao ili kuthalilisha raia na kuwabambikizia makesi yasio kichwa wala miigui rai wema wasio na hatia.
Hivi sasa makesi ya kubambikiziwa wananchi yamejazana mahakamani na huku washukiwa wakiteseka ndani ya magereza ,Jee bado tunaita Amani..?? au tunaita uvunjwaji wa Amani..?? maana hio amani iliopo mwananchi wa kawada hafaidiki nayo zaidi ya mateso mathilaa na masundogo na kujikuta kuwa hana uhuru wala hana mtetezi wala hana wa kumlilia toka anapo amkaa mpaka anrudi kulala yeye ni mateso na hofu iliyo mja kuwa labda hatarudi nyumbani na ataishia mikononi mwa polisi wala rushwa na kujihisi kama yatima aliyesahauliwa.
Amani hii ina maana gani kwa mkulima masikini anayenyang’anywa ardhi yake na wafugaji wanaowanunua watendaji wa serikali.?? Wakulima wamebaki yatima katika nchi yao ili kupisha mifugo ya watawala amani hii ina maana gani kwa mkulima masikini aliye nyang;anywa shamba lake na kiongozi wa serekali au natajiri mwenye mapesa ya kuwahonga wakuu wa serekali wanao shughulikia mambo ya ardhi amani hii ina maaana gani..??
Amani hii ina faida gani kwa wakina Mama zetu na Dada zetu waja wazito masikini wanao kufa na mtoto wake kwa kukosa huduma za hospitali ina faida gani kwa masikini amani inayoliliwa na serekali ya SMZ..?? Mama huyu kabla hajafaa anadaiwa rushwa na wauguzi ukiacha lundo la matusi na kejeli anazopata na hata kupingwa makofi saa nyengine mbele ya waajiriwa hawa wa serikali. Amani hii ina faida gani kwa wafanya biashara wadogo wadogo kunyanyaswa na askari wa baraza la manispa watowe rushwa au kuchukuliwa biashara zao na kupingwa vibaya ina faida gani amani hii inayoliliwa na serekali ya SMZ..??
Watoto wa masikini wanaohitimu katika vyuo mbalimbali hawana ajira wakati watoto wa Waheshimiwa na wanasiasa wanaletewa ajira zao vyuoni kabla hata hawajahitimu. Tofauti ya tabaka hizi mbili ndilo chimbuko la kukosekana kwa amani katika Serekali hii ya majambazi ya SMZ.
Viongozi Kama hawa Seif Iddi wanapohubiri Amani nikuwazuga tu wananchi ili tu wapate utulivu wakufanya uharamia wao bila kero maana wanajuwa bila ya amani yao hayatakuwa na nafasi kufanikiwa ndio akawa muhubiri mkubwa wa amani, Mzanzibar wa kawaida hafaidiki chochote na hio Amani ihubiriwayo kila siku.
Ikiwa ni mateso Wazanzibar wanateseka ,ikiwa ni kubambikiziana makesi Wazanzibari wanabambikiwa toka serekali hii ishike madaraka mwaka 1964 mpaka sasa mchezo ndio huwo huwo kubambikiwa kesi.ikiwa ni kuteseka Wazanzibari wanateseka ikiwa ni ukali wa maisha Wazanzibar wa kawaida wamepata depreshni kwa mgorogano wa mawazo, kwa hio kuna faida gani ya Aman iloko na ni kwa nani..??