Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika limefanya mabadiliko ya kurusha matangazo yake ambayo yanaviwezesha vyombo vya habari (redio na tv) kupata matangazo hayo moja kwa moja bila kufunga mitambo yao katika eneo la bunge.
Katika taarifa ambayo imetolewa na kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha bungeni imeeleza kuwa mfumo huo utakuwa ukirusha mtangazo kupitia satellite ambapo vituo vya redio na runinga vitakuwa vikitumia satellite kupokea matangazo hayo na kuyarusha katika vituo vyao.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa redio na vituo vya runinga vitakuwa vikiyapata matangazo kupitia satellite Intelsat 17, nyuzi 66 upande wa Mashariki.
SATELLITE: Intelsat 17 @ 66 East
FREQUENCY: 11024.2500MHZ
SYMBOLRATE: 3071.8 Mbps
POLARIZATION: Horizontal
FEC: 1/2
MODULATION: 4PHASE-QPSK
AUDIO: CH. 1…noneI, CH.2…none, CH.3…TV Audio na CH. 4…Radio
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mfumo huo ndiyo unaotumika na mabunge mengi duniani na kutumika kwa mfumo huo hakuwazuii waandishi wa habari kwenda bungeni kuchukua habari.
No comments:
Post a Comment