Thursday, April 14, 2016

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AWATUMBUWA MAJIPU JAPO KUWA WAMEKATA KUMPA HAKI NA KUMUAPISHA, ATAKA AKAUNTI ZOTE ZA VIONGOZI WA SMZ NA SHEIN ZICHUNGUZWA



MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD.
WAKATI Shein, akijipanga na kujitutumuwa ati kuanza kupambana na vitendo vya ubadhirifu na ufisadi baada ya kukamilisha safu ya Baraza la Mapinduzi la maharamia wenzake mawaziri harama ambao hawakuchaguliwa na wananchi lakini wote wanalindwa na jeshi la Pombe Magufuli kuendeleza harama nchini Zanzibar na huku Pombe anajua kabisa kama wale wote ni mawaziri harama na Raisi haramu,
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, ameiomba jumuiya ya kimataifa na nchi za wahisani kuchunguza akaunti za fedha za viongozi wa SMZ zikiwamo za anajitamanisha na kujita mwenyewe kuwa ati yeye ni Rais huyo kuhifadhiwa benki za nje. Maalim Seif Sharrif Hamad alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini nchini Zanzibar na kutangaza mwelekeo wa chama chake baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu haramu wa marudio bila ya wao kushiriki, hivyo kupoteza viti vyote vya majimbo 54 vya uwakilishi, 111 vya udiwani na nafasi ya kiti cha urais wa nchi ya Zanzibar. “Natoa wito kwao kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya watawala hawa waovu, ikiwamo kuwawekea vikwazo vya kusafiri, kufuatilia akaunti zao za fedha nje ya nchi na hatua za kuchunguza matendo yao ya uhalifu dhidi ya binadamu na CCM, ni lazima wawajibishwe kwa matendo yao maovu,” alisema Maalim Seif.

Akiwa ameandamana na viongozi waandamizi wa ngazi za juu wa chama hicho, Maalim Seif alisema kuna viongozi ndani ya serikali ya CCM wanamiliki fedha za kutisha nje ya nchi, hivyo jumuiya za kimataifa kwa kutumia sheria ya utakatishaji wa fedha ianze kuchunguza akaunti za viongozi zilizoko ndani na nje ya nchi.“Halihitaji tochi, kuna viongozi wanamiliki fedha nje ya nchi na wengine wana vitega uchumi zikiwamo nyumba huko Dubai, bila ya kipato chao cha fedha kueleweka,” alisema Maalim Seif, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu wa nchi ya Zanzibar.Alisema wakati umefika kwa jumuiya za kimataifa na nchi wahisani kuwanyima nafasi ya kusafiri nje ya nchi viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa vile wamewekwa madarakani kinyume cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Maalim Seif alisema serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Dk. Shein si serikali halali kwa mujibu wa Katiba kwa kile alichosema imeundwa bila ya kuzingatia masharti ya ibara ya 9(1) inayolazimisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) pamoja na ibara ya 39, 39A na 42 za Katiba ya Zanzibar zinazoelezea namna ya uundwaji wa SUK, na kwamba masharti yake yanaendelea kuvunjwa na mtawala aliyeamua kuyapiga teke maamuzi ya Wazanzibari na kujiweka madarakani.“Kwa hivyo serikali yake haiwezi kuwa ni inayokwenda na Katiba, kwa ufupi si serikali halali kwa mujibu wa Katiba na marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar mwaka ya 2010,” alisema Maalim Seif.

MWELEKEO WA CUF
Akielezea mwelekeo wa CUF, alisema wanapanga mikakati madhubuti ya utekelezaji wa maazimio ya Baraza Kuu la uongozi ambayo itatekelezwa kwa kutumia njia za amani, za kidemokrasia na za kikatiba ili kufanikisha malengo ya chama kuona maamuzi ya watu wa Zanzibar waliyoyafanya kupitia uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana yanaheshimiwa. “Nina hakika kabisa kuwa mikakati tunayoipanga itazaa matunda, hatua ambazo zitaibana serikali haramu na hatimaye itasalimu amri, wananchi wa Zanzibar ambao kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ndio wenye mamlaka ya kuiweka madarakani serikali wanayoitaka, katika dunia ya leo hatuwezi kuongozwa na watawala ambao hawakupewa mamlaka na watu wenyewe,” alisema Maalim Seif. Hata hivyo, Maalim Seif alisema akiwa kiongozi anayewapenda wananchi na kujitolea kuwatumikia katika umri wake wote, hawezi kuwaongoza kuelekea kwenye fujo na ghasia au vitendo vitakavyosababisha kuiharibu nchi na kuathiri watu na kwamba ana imani kubwa njia wanazozifuata za kutafuta haki zitafanikiwa. Alisema kitendo cha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana, kimeirudisha nyuma Zanzibar katika siasa za utengano, chuki na uhasama pamoja na fujo na kuvuruga msingi mzima wa mafanikio ya maelewano waliyoyafikia na Rais mstaafu wa awamu ya sita, Dk. Amani Abeid Karume, kwa kuzaliwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

“Natoa wito kwa Wazanzibari wenzangu, tukatae kurudishwa katika siasa za ubaguzi, utengano, chuki, uhasama na fujo na kila mmoja afanye lile liliomo katika uwezo wake kuendeleza maelewano, upendo mshikamano na udugu katika jamii yetu,” alisema Maalim Seif. Alisema kama CUF wangekubali kurudi katika uchaguzi wa marudio, nchi ingetumbukia katika machafuko kwa sababu watawala walikuwa tayari yatokee machafuko kuliko kuridhia maamuzi halali ya wananchi ya kuleta mabadiliko ya utawala kwa njia ya kidemokrasia. “Uamuzi tuliochukua na kuusimamia umesimama juu ya misingi ya heshima na utu wa watu ambao ulikuwa ndio malengo sahihi ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Hayati Shaikh Abeid Amani Karume na malengo sahihi ya Chama cha Afro Shirazi(ASP) na malengo sahihi ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964,” alisema. Alisema CUF iliona ni heri kususia uchaguzi mkuu wa marudio badala ya kushiriki katika ubakaji wa demokrasia, matumizi ya nguvu za kijeshi ili kulazimisha watawala wasiokuwa na ridhaa ya wananchi ya kubakia madarakani kwa malengo ya kuepusha shari kutokea.

UADILIFU WAKE
Kuhusu uaminifu wake, Maalim Seif alisema CCM hawana fedha ya kumnunua na hanunuliki kwa kuwa analinda heshima yake kuliko fedha ambazo alisema akifa ataziacha duniani na hawezi kuuza utu wake, heshima na uaminifu aliojijengea kwa wananchi. Alisema katika maisha yake ya uongozi wa kisiasa, hakuna kiongozi wa CCM aliyewahi kujitokeza na kumshawishi abadili msimamo wake kwa masilahi binafsi na kwamba wanajua kuwa hanunuliki na hakuna mwanachama wa CUF mwenye hofu na uaminifu wake tangu kuasisiwa kwa chama hicho.

ABOUD AZUNGUMZA
Alipoulizwa na Mwandishi wetu kuhusiana na tuhuma za Maalim Seif kwa viongozi wa serikali ya Zanzibar, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, alisema atakuwa tayari kujibu zitakapofikishwa kwao rasmi na kwamba kwa sasa hawezi kuzungumza chochote. Viongozi wa CUF waliohudhuria Mkutano huo ni Naibu Katibu Mkuu wa cha hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, Mshauri wa Mikakati wa Katibu Mkuu na Waziri wa zamani wa SMZ, Mansour Yusuph Himid, Mkurugenzi wao wa Mambo ya Nje, Ismail Jussa, Mkurugenzi wa Fedha, Abdallah Juma, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Ali Shehe na mawaziri wa zamani wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Said Ali Mbarouk, Fatma Abdulhabib Ferej, Zahra Ali Hamad pamoja na msemaji wa chama hicho, Hamad Masoud Hamad.

No comments:

Post a Comment