Saturday, April 9, 2016

VIDEO-SHEIN ATANGAZA BARAZA LAKE LA HARAMU LA MAWAZIRI CCM MAPINDUZI DAIMA MAPINDUZI DAIMA MAPINDUZI DAIMA




Anae jita na kulazimisha watu waite kuwa yeye ni Rais wa nchi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi jipya lililo wapinduwa Wazanzibari kwa kutumia jeshi la Mkoloni Mweusi Tanganyika, Shein na Balozi Mkazi wakiendelea na wazimu wao japo kuwa na wanava suti lakini sote tushawajuwa ni wandawazimu.
‘Anayejifanya’ Rais wa nchi ya Zanzibar, Shein ametangaza Baraza la Mawaziri lenye mawaziri 13 na naibu mawaziri saba. Kwenye baraza hilo kuna waziri mmoja ameingizwa kwa kigezo kutoka upande wa upinzani. Hadi sasa hakuna majina ya Naibu Mawaziri yaliyopatikana. Baraza jipya la Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jipy lililo wapinduwa wazanzibari lina mfumo wa chama kimoja cha siasa (CCM), halikidhi mahitaji ya katiba ya Zanzibar, toleo la mwaka 2010, inayoelekeza uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), kulingana na ukubwa wa upinzani wa Vyama vya Siasa.
Baraza la Mawaziri la Shein, kama lilivyo hapa chini:-
1). Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu (CCM).
2). Wizara ya Katiba, Sheria na Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman (CCM).
3). Wizara ya Tawala za Mikoa na Idara Maalum – Haji Omari Kheir (CCM).
4). Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar – Mohamed Aboud (CCM).
5). Wizara ya Fedha na Mipango – Dk Khalid Salum Mohamed (CCM).
6). Wizara ya Afya – Mahmoud Thabit Kombo (CCM).
7). Wizara ya Elimu – Riziki Pembe Juma (CCM).
8). Wizara ya Viwanda na Masoko – Amina Salum Ali (CCM).
9). Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Abeid Karume (CCM).
10). Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma (CCM).
11). Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohd (ADC/CCM).
12). Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko (CCM, mzaliwa wa nchini Zambia).
13). Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib (CCM).
Serikali mpya ya Shein, imekuja baada ya mbinu na hila za kisiasa kutokana na kuvurugwa kwa makusudi Uchaguzi Mkuu wa nchi ya Zanzibar wa tarehe 25/10/2015 kwa madai kuwa ati ulikuwa umegubikwa na kasoro nyingi wkati kila moja anajuwa kuwa CCM ilikuwa imekwisha kabisa haina lake jambo tena ndio wakafanya mapinduzi yao ya kuwapinduwa wananchi wao wakitumia mtutu na jeshi la Wakoloni Weusi Tanganyika. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jesha Firauni Jecha alitangaza Oktoba 28, mwaka jana kufuta matokeo ya uchaguzi huo, huku akidai kuwa ulitawaliwa na kasoro nyingi, ikiwa ni pamoja na wingi wa kura zilizopigwa hasa kwa upande wa Pemba pia sote tunajuwa kuwa hana mamlaka yoyote ya kufutu uchaguzi si kisheria wala si kikataba lakini hawana lakufanya washashindwa na wananchi kikura ndio wakamuwa kuwapinduwa wananchi kwa kutumia mtutu na jeshi la wakuriya la kutoka mrima kwa Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Hata hivyo, madai hayo yalionekana kuwa ni njia ya kuibeba CCM baada ya uchaguzi huo kutoa mwelekeo kuwa Chama cha Wananchi (CUF), kimeshinda na CCM, kilikuwa tayari kimepoteza ushindi. Taasisi nyingi za ndani na nje zilizokuwa zikifatilia uchaguzi huo zilithibitisha kuwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana haukuwa na mapungufu yoyote kupelekea Mwenyekiti wa Tume kuufuta. Waangalizi wote walithibitisha kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment