Sunday, April 10, 2016

VIDEO-NI KWELI ZANZIBAR NI NCHI YA KIMAPINDUZI MOHAMED SHAMTE NA ALI MUHSIN WALIWEZA KUMUONDOWA MGEREZA KISHA WAO WAKAPINDULIWA NA JOHN OKELLO,KASSIM HANGA,ABDULRAHMANI BABU KISHA NA WAO WAKAPINDULIWA NA MZEE KARUME NA JESHI ALILO PEWA NA NYERERE LIMLINDE KISHA NA YEYE AKULIWA NA SASA SHEIN KASHAMPINDUWA MAALIM SEIF JESHI ALILO PEWA NA KIKWETE NA SASA LINAMLINDA KWA AMRI YA MAGUFULI

HII NDIO SERIKALI YA KWANZA YA MAPINDUZI KABLA YA WAO PIA KUPINDULIWA NA MZEE KARUME NA KUFUKUZWA NCHI WENGINE KUFUNGWA WENGINE KUULIWA KAMA WALIVYO FANYA WAO KWA WAZANZIBARI.
MWANAHARAKATI  John Gidion Okello, kama alivyokuwa mkombozi wa Cuba, Ernesto “Che Guevera”, ni mmoja wa wanamapinduzi nadra na mashuhuri duniani walioendesha mapambano kukomboa nchi zisizo zao, kisha wakafukuzwa kama watu wasiotakiwa.
Lakini tofauti na “Che Guevera”, raia wa Argentina aliyeongoza mapambano yaliyofaulu, kupindua Serikali dhalimu ya dikteta Fulgencio Batista nchini Cuba, wakishirikiana na wanaharakati wazalendo, akiwemo Fidel Castro na wengineo, baada ya hapo akawa Waziri nchini humo; John Okello, kwa upande wake, baada ya kufanikisha mapinduzi nchini Zanzibar, Januari 12, 1964, alifukuzwa, akapigwa teke bila huruma wala shukrani kama mtu asiyetakiwa ni wazi kuwa aliye mlete John Okello nchini Zanzibar alikuwa na mpango wake kamili kuwa John atafanya kisha atamtimuwa na ikiwa John Okello hata fanikiwa yeye huyo Mr X mikono yake itakuwa safi kwa nchi jirani kuwa sio yeye bali alikuwa ni John Okello mganda. “Mimi nilimfanya Sultani apoteze ufalme wake, lakini hali yangu ni mbaya zaidi kuliko yake.  Sultani alipokelewa vizuri Uingereza, lakini mimi ndugu zangu (Waafrika) wenyewe wamenifukuza”, alilalama miezi michache baada ya kufukuzwa nchini Zanzibar John Okelo. Na katika kuhakikisha kwamba historia ya ushiriki wake katika mapinduzi hayo ya kihistoria inatupwa na kufunikwa chini ya zulia isahaulike na kupotea, viongozi CCM nchini Zanzibar wamehodhi historia ya mapinduzi ili waweze kujikweza kwa kujipachika sifa kuwa wao ndio wakombozi wa Zanzibar kutoka utawala wa Sultani vichekesho. Ni kwa sababu hii, natofautiana na Mwandishi wa habari gwiji, mkongwe na wa kimataifa, katika mada yake:  “Siku Field Marshal John Okello alipotimuliwa Zanzibar”, kwenye gazeti la 22 – 29/2/2012 alipodai kwamba, mwanamapinduzi “Field Marshal” John Okello, raia wa Uganda, hakuwa muhimu na mwenye nafasi duni isiyohesabika katika mapinduzi ya nchi ya Zanzibar.
Mwanahabari anaeleza, pamoja na mambo mengine (na hapa ndipo utata ulipo), kwamba, makada 200 wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP), wakiongozwa na Yusuf Himid, ndio walioongoza mapinduzi hayo, na kwamba hawakukabiliwa na upinzani wowote.
Anasema, haijulikani ni nani hasa aliyepiga risasi ya mwanzo au ya mwisho katika mapinduzi hayo, ila kwamba, waliokuwa wakiongoza mambo tangu mapinduzi yaanze hadi siku ya pili, Januari 13, 1964, walikuwa Aboud Jumbe (ASP), Thabit Kombo (ASP) na Badawi Qullatein wa Umma Party [UP]. Anaeleza, hakuna uhakika mpaka sasa nani alimpeleka Okello kujichanganya na wanamapinduzi na pia kutangaza kwenye redio juu ya kufanikiwa kwa mapinduzi hayo, na kwamba, Aboud Jumbe alipomwona na mabastola yake alishtuka akauliza:  “Nani huyu...??  Katokea wapi...??” Kadri ninavyomfahamu mimi muandishi huyu, alivyo mdadisi wa mambo kabla ya kuandika, nalazimika kuamini kwamba, ameiandika simulizi hii kabla ya kufanya utafiti wa kina; na pia kwamba (kama anavyokiri mwenyewe) ameandika “baada ya kuzungumza na walioshiriki katika mapinduzi hayo” na ambao kusema kweli, wengi wao ndio wenye kupotosha historia ya mapinduzi. Mapinduzi ya Januari 12, 1964 yalitabirika. Vuguvugu la chini kwa chini lilianza pale Serikali ya Uingereza ilipokabidhi uhuru kwa Serikali ya mseto ya vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP), Desemba 10, 1963 kutokana na uchaguzi mkuu wa 1963, ambapo Mohamed Shamte wa ZPPP, aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa nchi ya Zanzibar. Wazanzibari wengi, hasa wanachama wa vyama vya ASP cha Mzee Abeid Karume na Umma Party (UP) cha Abdulrahman Mohamed Babu, waliona wameuzwa kwa kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki na hayo ndio yanaendelea mpaka leo CCM na CUF ila wakati ule alikuwa Mkoloni Mweupe sasa tuna Mkoloni Mweusi na chaguzi ndio hivyo hivyo sio za haki. Hiki ndicho kilikuwa kichocheo kikuu cha mapinduzi. Katika uchaguzi huo, Muungano wa ZNP/ZPPP ulipata viti vya Bunge 18 na ASP 13 kati ya viti 31 vilivyogombewa. Itakumbukwa kuwa, siku ya uhuru, Babu alipoombwa kutoa salaam za Uhuru kwa niaba ya chama chake mbele ya Waingereza, Sultani na wageni wa kimataifa, alitamka maneno yaliyomsisimua kila Mzanzibari na kuwakanganya watawala wapya.  Alisema:
“Salaam kwa Wazanzibari na wapenda haki wote.  Umma Party na Wazanzibari kwa ujumla, wanasubiri kunyakua utawala wa nchi na kuuweka mikononi mwao saa itakapowadia”.
Maneno haya yaliashiria kwamba, Babu na Chama chake, pamoja na wanamapinduzi wengine, walikuwa na fundo dhidi ya Serikali mpya; walipenda kuona ikipinduliwa nafasi ikitokea hapa tayari ni kiashiria kuwa Babu ni moja katika hao walio panga mapinduzi japo kuwa alipohojiwa yeye na Mzee Karume na John Okello Babu alikana na kusema hakujuwa kama kulikuwa na Mapinduzi na Mzee karume pia alikana kama kulikuwa na Mapinduzi ila misome kama hii inakuashiria kuwa lipo jambo linapangwa na ni lipi ikiwa sio Mapinduzi maana hakuna tena uchaguzi ushakwisha. Baada ya kuingia madarakani, Serikali ya ZNP/ZPPP ilianzisha programu ya kuwarejesha makwao Watanganyika walio zanga nchini Zanzibar na Askari Polisi wa waliotokea Kenya,Uganda na Tanganyika ambao walikuwa hapa nchini Zanzibar kwa kuwakwa na Mkoloni Mweupe Mgereza ambao walikuwa wakifanya kazi tafauti kama kulima,kuvunja mawe na kokoto,kuangusha nazi,kupalilia na kuchuma karafu msimu ukifika n.k. wengi wao wakiwa wa kabila la Makonde kutoka Tanganyika na Msumbiji na wengine kutoka Kenya,Waganda na nafasi zao kuchukuliwa na  Wazanzibari halisi ili wafanya kazi hizo wenyewe wasitegeme watu kutoka nchi za jirani kuwafanyia kazi zao ikiwa ni pamoja polisi na jeshi ambalo lilikuwa limejazwa Watanganyika kama ilivyo sasa, Waasia na Wazanzibari asilia waliochaguliwa kwa umakini mkubwa kwa hofu ya usaliti na tunaona mpaka leo wapo ndugu zetu wanatusaliti Wazanzibari na kuendelea kushirikiana na Mkoloni Mweusi. Kwa kufanya hivyo, Serikali ilijipunguzia nguvu ya usalama wa ndani kisiasa na kiulinzi, licha ya kuua morali ya jeshi la polisi kwa ujumla. Kwa sababu hii, ilianza kuajiri kwa njia ya dharura, walinzi wasio na mafunzo ambao ndio Wazanzibari wazawa. Hivyo ni dhahiri kwamba, kama Serikali mpya ingeshambuliwa kutoka nje wakati huo, isingeweza kuhimili kishindo kwa sababu ya kuwa na walinzi wasio na uzoefu wala mafunzo.Mbaya zaidi ni kwamba, Serikali mpya haikuwa na mkataba wa kijeshi wa ulinzi na Uingereza kuweza kusaidiwa, kama ilivyokuwa Serikali ya Sultani kuanzia miaka ya 1890 hadi Uhuru, Desemba 10, 1963 kwa hiyo hii ni pigo tosha kuwa nchi yoyote iliyukuwa hasimu au hasidi wa nchi ya Zanzibar ni rahisi sasa kuishambulia kwa sasababu ni nchi changa kijeshi,kipolisi.
HII NI PICHA KASSIM HANGA NA MZEE KARUMA KABLA YA KUGEUKIANA NA KUWA MADUWI NA MZEE KARUME KUWAPINDUWA HANGA NA KUNDI LAKE LA ASP,BABU NA VIJANA WAKE WALIO PEWA MAFUNZO CUBA W UMMA PARTY NA JOHN OKELLO NA KUNDI LAKE LA WATANGANYIKA,MZEE KARUME ALIWAGEUKA WOTE NA KUWA NA SERIKALI YAKE MPYA YA KIMAPINDUZI JESHI LAKE LA ASKARI 300 KUTOKA TANGANYIKA ALIYO PEWA NA NYERERE.
Vigogo hawakutaka mapinduzi
Licha ya kulalamikia matokeo ya uchaguzi yaliyoiweka Serikali ya Vyama vya ZNP/ZPPP madarakani kama ilivyo sasa CCM kuekwa madarakani na Mkoloni Mweusi, Viongozi wakuu wa ASP hawakupendelea kuiondoa madarakani Serikali mpya kwa njia ya mapinduzi na ndio yale yale yanaendelea mpaka leo kuwa viongozi wakuu wa CUF hawataki kuiondowa madarakani serikali mpya ya Mkoloni Mweusi kwa kuitumilia CCM. Si Karume, Kombo wala Aboud Jumbe aliyekuwa na wazo la mapinduzi hadi yalipotokea.Si Maalim SEif,Nassor Mazrui wala Jussa ambao wanawaza au kufikiri mapinduzi. Itakumbukwa baada ya uhuru, Karume alimwendea Waziri Mkuu Shamte, kumbembeleza akubali kuundwa kwa Serikali ya mseto wa Vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi vya ZNP, ZPPP na ASP;
Kushoto: Ibun Saleh, Juma Aley, Mohamed Shamte, Dr. Baalawy, Ali Muhsin
HAWA NDIO SERIKALI YA KWANZA BAADA YA KUPATA UHURU KUTOKA KWA MKOLONI
NA KUPINDULIWA NA JOHN OKELLO KUNDI LAKE LA WATANGANYIKA,BABU NA VIJANA WAKE WALIO PEWA MAFUNZO CUBA,NA VIJANA WA HANGA WA ASP
lakini Shamte akamkatalia katakata akisema: “Uhuru maana yake si kugawana mateka; hakuna mateka wa kugawana hapa”,  aling’aka na kumtaka avunje Chama  chake cha ASP.
Shamte alidai kuwa nafasi kama hiyo ilitolewa mara mbili kwa Karume, mwaka 1962 na 1963, wakati wa mazungumzo ya Lancaster House, pale viongozi wa ASP, ZNP, ZPP na Umma Party, walipokutana mjini London na Waziri wa Makoloni wa Uingereza kuzungumzia mchakato wa Katiba na Uhuru wa nchi ya Zanzibar, lakini (Karume) alikataa kwa matarajio kwamba ASP kingeshinda “kwa kishindo”. Moja ya makubaliano yaliyofikiwa na vyama vyote katika mikutano yote miwili, kuanzia na uliofanyika kati ya Machi 19 na Aprili 6, 1962, na wa Septemba 20 – 24, 1964 ni Zanzibar kupata uhuru Desemba 10, 1963 chini ya Waziri Mkuu, na Sultani kuwa Mkuu wa nchi, kama zilivyo sasa Canada, Australia na New Zealand ambazo pamoja na kwamba zilipata uhuru kutoka kwa Waingereza, lakini ziliendelea kubakia kuwa chini ya himaya (monarch) ya Malkia wa Uingereza. Ndiyo kusema, kwa makubaliano hayo, hata kama ASP kingeshinda, kisingeweza kubadili mfumo huo. Wakuu wa ASP wamedai mara nyingi kwamba walikubali mfumo huo kwa matarajio wangefanya mapinduzi baadaye. Lakini je, ingewezekanaje wakati wao wenyewe walikuwa watii kwa Serikali na waoga wa umwagaji damu...?? Katika hali ya kukata tamaa, Karume alisema, “Inshallah, Mungu yupo, siku moja nasi atatutunuku ushindi”; kisha akaendelea kuwataka vijana wa ASP wasifanye vurugu wala kuichokoza Serikali  isije ikapata kisingizio cha kutumia nguvu ya ziada kwao na Chama cha ASP. N hayo ndio anayo sema Maalim kila siku musichokozeke,tulieni,tunaendelea kupambana kwa amani.Kwa mawazo ya Karume na wenzake, ilikuwa bora kuendeleza mapambano hadi ushindi kwa njia ya sanduku la kura kwa kujizatiti zaidi katika uchaguzi unaofuata.Na ndio anavyo fanya Maalim seif mapambano yananedelea kwa njia ya sanduku la kura kwa kujizatiti zaidi katika uchaguzi unaofuata 2020.
KASSIM HANGA KIONGOZI WA ASP ABDULRAHMANI BABU KIONGOZI WA UMMA PARTY
Vijana hawakusikia la vigogo
Ule usemi wa wahenga kwamba “asiyesikia la mkuu huvunjika guu”, haukufua dafu kwa mori ya kimapinduzi iliyowapanda vijana baada ya uhuru, licha ya Mzee Karume kutopendelea fujo dhidi ya Serikali. Kulikuwa na makundi matatu yaliyopata ujasiri kulipiza kisasi. Kwanza, kulikuwa na kundi la vijana wa ASP lenye siasa za mrengo wa kikomunisti, likiongozwa na Kassim Hanga na wenzake. Hili lilitaka mabadiliko ya haraka nchini Zanzibar badala ya kusubiri uchaguzi unaofuata. Pili, kulikuwa na kundi la vijana wa Umma Party (UP) lenye sera za mrengo mkali wa kikomunisti, likiongozwa na Abdulrahman Mohamed Babu, kiongozi wa Umma Party aliyejiengua yeye na vijana wake kutoka ZNP miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu, baada ya kutofautiana sera na mitazamo ya kitaifa na kuunda Chama hicho. Wakati huo ndio kwanza baadhi ya vijana wake walikuwa wamerejea kutoka Cuba, walikopelekwa kwa mafunzo ya kijeshi na harakati za kimapinduzi tangu mwaka 1961. Kuonesha kwamba walikuwa wamepikwa wakapikika sawa sawa dhidi ya ubeberu wa kimataifa, kauli za kimapinduzi dhidi ya ubeberu zilitawala ndimi zao wakinena kwa lugha ya Kihispaniola: “Zanzibar si, yanqui no”, yaani, “Zanzibar juu, Marekani zii”. Hawa walikuwa tayari kuliko wakati wowote kuingia katika mapambano enzi hizo za vita baridi kati ya nchi za ubepari wa Magharibi, na nchi za kisoshalist za Mashariki. Kundi la tatu la vijana walalahoi na wakulima, ambao nao walikuwa tayari kupigana, liliongozwa na John Okello, aliyewapa mafunzo katika vikundi vidogo vidogo mafichoni porini na chini ya minazi pamoja na wale wamikonge walio kuwa wakifanya mazoezi ya Tanga nchini Tanganyika wakihudumiwa na Mr X. Hawakuwa na silaha za kisasa bali mapanga, marungu, pinde na mishale.
Kuwapata vijana hao,John Okello aliwatumia Waafrika wenye asili ya Tanganyika na Kenya na uganda pia alikotuka yeye au aliko zaliwa ambao wengi wao walikuwa wamefukuzwa kwenye Jeshi la Polisi na jeshi la kawaida na Serikali Mpya ya Shamte, kama nilivyoeleza mwanzo.  Ndiyo maana haishangazi kwamba, siku ya mapambano usiku wa mapinduzi, askari hao waliofukuzwa walishiriki kikamilifu, wakitumia silaha za kisasa, huku wakulima wakitumia silaha za jadi. Okello alianza kuwapa mafunzo hayo mwezi Julai 1963 kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwisho kuelekea uhuru, uliofanyika Julai 8 – 15, 1963.  Aliwafunza matumizi ya silaha zote katika mapambano – mapanga, pinde na mishale, marungu na bunduki kwa kutumia miti iliyochongwa badala ya bunduki halisi. Mwezi Septemba 1963,John Okello alionana na aliyekuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa ASP,Kanal Seif Bakari, na akamuunga mkono, lakini John Okello hakumwelezea programu ya mapinduzi. Kundi la vijana wa ASP na lile la vijana wa Umma Party walishabihiana kwa mtazamo na kwa programu ya mapinduzi; waliunganishwa na itikadi ya kikomunisti, wakati kundi la John Okello lilijitegemea. Aidha, vijana wa ASP walibaini mapema kuwa, Abeid Amani Karume hakutaka mapinduzi yafanyike; alikuwa mwoga wa umwagaji damu.  Kwa sababu hii, waliamua kutomsikiliza na kuungana na wenzao wa Umma Party kupanga mapinduzi kwa siri bila kuwashirikisha vigogo wote wa ASP wakisema, “Sasa ni zamu yetu”. Moja ya mbinu za kwanza zilizotumiwa na vijana hao, ilikuwa ni kuhujumu miundombinu ya Serikali – Ofisi, miradi na mitambo mbalimbali kufanya nchi isitawalike. Hali hiyo ya vurugu ilipokithiri, Desemba 26, 1963, Serikali ilikipiga marufuku Chama cha Umma (Umma Party) na Babu akasakwa akamatwe ili afunguliwe mashitaka ya uhaini, lakini alitorokea jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika hadi baada ya mapinduzi akarejea hapa utaelewa kuwa Babu na kundi lake la vijana alio wapeleka Cuba walikuw na nia ya Mapinduzi na Umma Party yao.Hanga na kundi lake la ASP bila ya Mzee Karume walikuwa na nia ya Mapinduzi na John Okello na kundi lake la walalahoi na watanganyika walio fukuzwa kazi na Serakali mpya ya Zanzibar pia walikuwa na nia ya Mapinduzi kwa hiyo haya makundi matatu yakiongozwa na na Babu,Hanga na John Okello ndio yalio kamilisha mapinduzi ya Zanzibar.
Ni nani huyu John Okello...??
John Gidion Okello alizaliwa Lang’o Uganda mwaka 1937.  Haifahamiki vyema kiwango chake cha elimu; lakini inasemekana alishiriki kwa muda katika vita ya “Mau Mau” nchini Kenya upande wa wazalendo dhidi ya utawala wa Waingereza, akapanda cheo kufikia ngazi (Kimau Mau) ya “Brigedia” kutokana na umahiri wake wa kuota na kutafsiri ndoto za matukio ya mapambano na ukakamavu wake na sauti yake ya kivitisho. Alihamia Pemba ambako aliajiriwa katika Jeshi la Polisi kwa kipindi kifupi, kati ya mwaka 1958 na 1959, kabla ya kujiunga na ASP ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tawi wa Chama hicho.Kwa maelezo yake baadaye,John Okello hakufurahishwa na matokeo ya uchaguzi wa hila,kama wenyewe wanavyo ita ati namna Waarabu wa Kimanga walivyowanyanyasa Waafrika:  “Niliyaanzisha mapinduzi kwa sababu nilijisikia vibaya jinsi Waarabu walivyokuwa wakiwachinja Waafrika masikini”, alisema John Okello. Alihamia Unguja baada ya Uchaguzi Mkuu, Julai 1963 kufanya maandalizi ya kupindua Serikali mpya iliyotarajiwa kuingia madarakani, huku akifanya kazi ya kujiajiri kama fundi mwashi kwa hiyo haiwezekeni kuwa Jumbe au mwengine yoyote katika ASP wakati huo walikuwa ati hawamjuwi John Okello wote walikuwa wakijuwa vizuri sana.
Nani aliongoza mapinduzi....??
Tumeona jinsi vijana wa ASP na Umma Party wenye fikra za mrengo wa kikomunisti walivyoteta kwa siri na kukubaliana kufanya mapinduzi ndani ya nchi yao katika serakali yao Mpya ambayo walikabidhiwa na Mkoloni Mweupe ila hawakufurahi kwa sababu sio viongozi wao walio pewa madaraka ya kuendesha nchi,hii pia inatuonyesha jinsi gani Wazanzibari walivyo shiriki kikamilifu katika Mapinduzi ya kuipinduwa nchi yao wenyewe basi tu kwa uchu wa madaraka na ndio maana hawakutaka kuwashirikisha viongozi wao kwa hofu kwamba wangeyazuia. Tumeona pia jinsi mwanachama mwingine wa ASP, John Okello alivyoendelea kutoa mafunzo porini kwa vikundi vidogo vidogo kama sehemu ya maandalizi ya mapinduzi.  Yote haya yanaonesha kwamba mapinduzi hayo yaliandaliwa na kundi zaidi ya moja na kwa mazingira yasiyofanana. Si kweli, asemavyo muandishi, kwamba Aboud Jumbe, Thabit Kombo na Badawi Qullatein ndio walioongoza mambo tangu mapinduzi yaanze  hadi siku ya pili, na tunao ushahidi wao pia walishiriki kivyao ila hawawezi kumkana John Okello kuwa sio moja katika wanamapinduzi halizi hilo kufutwa hata CCM wadanganye vipi umma bado John Okello ni moja katika watu wali shiriki kufanya mapinduzi katika nchi ya Zanzibar. Minael Hosanna O. Mdundo, katika kitabu chake “Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha”, amemnukuu mzee Thabit Kombo (uk. 132) akikana hilo:
“Usiniulize vijana wetu walioendesha mapinduzi walipata wapi mafunzo, au nani alivamia mahali gani, mimi sijui.  Nasikia hadithi tu kila mmoja anajinasibu baada ya kushinda, mengine ya kweli na mengine ya uongo mtupu”.
Kiongozi huyo wa ASP anaendelea: “Mimi sijui mazoezi waliyoyafanya huko mashambani, wala mipango yao, kujua (kundi)] gani lilikwenda wapi.  Lakini najua hawakuwa na silaha za kisasa”.
Hapa panazuka swali:  Ni kundi lipi kati ya haya matatu, liliongoza mashambulizi na hivyo, mapinduzi...??  Makundi haya matatu yalishiriki vipi..?? je ni Vijana wa Babu ambao ni wazanzibari walio pewa mafunzo Cuba, Vijana wa hanga wa ASP au walalahoi wa John Okello...?? au wote walishirikiana na kupinduwa serikali ya halali ya kwanza ya nchi ya zanzibar.....??
Field Marshal John Okello: Shujaa na muuwaji wa mapinduzi ya nchi ya  Zanzibar 
asiyekumbukwa.

  • Ujasiri wake uliwapatia Wanamapinduzi bunduki ya kwanza je ni kweli...??
  • Alimwita Abeid Karume kupitia redio ili kumpa urais wa Zanzibar ni nani aliye muamuru 
  • afanya hivyo...?
KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya, tuliona namna Mapinduzi ya nchi ya Zanzibar ya 
 Januari 12, 1964 yalivyoandaliwa na vikundi vitatu tofauti viongozi wawili wa 
vyama tafauti wote wazanzibari na kiongozi moja sio mzanzibari lakini akiwa katika 
chama cha wazanzibari katika vyama tafauti vya vyama vyenye lengo moja 
lakini kwa mazingira tofauti, bila kuhusisha viongozi wa vyama vyao.Vikundi hivyo vilikuwa ni 
kikundi cha vijana wa Chama cha Afro-Shirazi  (ASP) na kikundi cha vijana wa 
Chama cha Umma (UP) ambapo hivi viwili viliunganishwa na kushabihiana kwa 
itikadi ya kikomunisti.Pia kulikuwa na kundi la walalahoi, la wakulima na wakwezi 
na askari wastaafu/waliofukuzwa kazi na Serikali mpya ya ZNP/ZPPP baada ya uhuru ambao 
wote sio wazanzibari ni Watanganyika,Wakenya,Waganda na wazaramo kutoka msimbiji 
au kutoka nchi hiyo hiyo ya Mr X. Hili liliongozwa na John Gidion Okello likipewa pia baraka na Mr X. 
Tulihoji:  Nani au ni kundi lipi lililoongoza Mapinduzi ya nchi ya Zanzibar....?? 
Tuendelee na sehemu hii ya pili kupata jibu. Jumamosi ya Januari 11, 1964 asubuhi, 
Sultani Jamshid Abdullah bin Khalfa “aliumwa sikio” na mmoja wa marafiki zake kwamba 
yangetokea machafuko siku hiyo au kesho yake; na pia kwamba Wamakonde ndio 
waliofanya njama za machafuko hayo na wangetumia silaha zao za jadi – pinde na mishale, 
mapanga na mashoka. Jamshid alipuuza uvumi huo akiamini kwamba, jambo kama hilo 
kamwe lisingetokea kwenye utawala wake. Jamshid alikuwa mkuu wa nchi na 
Mohamed Shamte alikuwa mkuu (Waziri Mkuu) wa Serikali ya ZNP/ZPPP.
Jumamosi hiyo ilikuwa ndiyo siku ya mwisho ya mfungo wa Ramadhan na 
shamra shamra za Waislamu kufungua mwezi zilikuwa zimeanza kwa mbali.
Siku hiyo, mji wa Unguja ulianza kushuhudia nyuso zisizo za ‘kimjini’ na 
zisizo za kawaida; lakini kila mtu alichukulia ni vituko tu vya sikukuu iliyotarajiwa.
Mzee Thabit Kombo amenukuliwa katika kitabu cha “Masimulizi ya Sheikh Kombo Jecha” 
akisema:  “Vikosi vya Mapinduzi vilianza kuingia mjini toka saa kumi jioni na kuendelea 
mpaka usiku”.Bila shaka yoyote ile, hivyo vilikuwa ni vikosi vya vijana wa kizanzibari wa ASP 
na vikosi vya wakulima na wakwezi wa mashambani, waliopewa mafunzo na John Okello kwa 
kificho vijijini, kama nilivyoeleza mwanzo maana sio wote walio ijuwa vizuri unguja kwa hiyo 
kwa vyovyote vile vijana wa John Okello walihitaji vijana wa kizanzibari ili wajuwe wapi paa 
kujificha na wapi paa kusubiri taimu ifiki ili wanza kazi yao ya Mapinduzi.
Inaonekana, kufikia jioni ya siku hiyo, Sultani Jamshid alianza kuamini ule uvumi wa 
awali juu ya machafuko kutokea, kwani yapata saa moja hivi, askari wa kuzuia fujo wa 
Kituo cha Mtoni, walipewa amri kwenda mjini kuzuia fujo umbali wa kilomita nne hivi, na 
kuacha baadhi yao wachache kituoni.Baada ya usiku wa manane, yapata saa 7.00 hivi, 
Januari 12, 1964, kikosi cha John Gidion Okello chenye wapiganaji 400, kilivamia Kituo cha 
Polisi cha Ziwani, baada ya kukata waya na kuingia.Katika hali iliyoonyesha kwamba 
wapiganaji wengi kati ya hao 400 hawakuwa na mafunzo ya kutosha, wala ujasiri na 
mbinu za kimapambano, na pengine baada ya kuona hali ya usalama wao shakani, na 
magumu ambayo yangeweza kuwapata waliamuwa kubaki nyuma; wote, 
isipokuwa vijana wapatao 40 akiwamo John Okello wakamuwa wao waingie kwanza wengine 
walirudi nyuma kwa woga huku wakisubiri kuamriwa kuingia na kumwaacha Jonh Okello na 
wenzake 39 wakisonga mbele, na wao wakasubiri ishara.Kwa ujasiri mkubwa, John Okello 
akanyemelea mbele na kumpokonya bunduki askari mlinzi na kumuua kwa singe ya bunduki hiyo.  
Hapo,John Okello akawa amekipatia kikosi chake cha Wanamapinduzi silaha ya kwanza ya kisasa.  
Wakasonga mbele tena,John Okello akafyatua risasi ya kwanza, askari wa zamu wakasalimu 
amri na wachache kuuawa wakachinjwa vibaya sana na kuuliwa vibaya vibaya tukumbuke hawa
 askari walikuwa vijana wakizanzibari wapya walio chaguliwa na serekali mpya iliyo pata uhuru 
kutoka kwa mkoloni mweupe leo wanajichijwa kama kuku sio kama wanavyo danganyka watu 
kuwa atii walikuwa wamanga; kisha Wanamapinduzi hao, na wale wakasubiri, wakavamia 
ghala la silaha walipo fike katika ghala la silaha walilikuta lipo wazi halijafungwa ikiwa ni rahisi 
kabisa kupata silaha hizo za kisasa na kuteka silaha nyingi hii ni shara kuwa John Okello na 
kundi lake peke yao sio walio fanya mapinduzi bali kulikuwa na watu ndani ya jeshi wakishiriki 
kikamilifu kukamilisha mapinduzi ya nchi ya zanzibar ndio maana wakakuta ghali la silaha liko wazi
wakapata,bunduki na mabomu.  Hapo, Mapinduzi yakawa yameanza na kupamba moto. 
Kutoka Ziwani, wapiganaji hao na wengine walio tumwa kuishambulia Kambi ya Mtoni maana 
walio kwenda mtoni baadhi pia walikuwa wakisubiri silaha hizo za kutoka ziwani baada ya kupata 
tu silaha haraka wakawapelekea wa mtoni na wao wakanza kuishambulia kambi ya mtoni 
na kuteka silaha nyingi zaidi kuuwa zaidi, tena kwa urahisi kwa sababu askari wengi walitumwa 
mjini jioni ya jana yake.Vijana wa Babu (Umma Party) wengi wao walipata mafunzo ya kijeshi 
nchini Cuba waliambiwa waishambulie kituo cha Malindi kwani kilikuwa bado kinalindwa na 
mgereza, wakati Mtoni ikiwaka moto, na tayari John Okello washaimaliza Ziwani na 
kuiweka chini ya ulinzi. Hawa vijana wa Babu, pamoja na majukumu lukuki, walipewa jukumu 
pia la kuteka uwanja wa ndege wa Zanzibar.Taarifa za Kibalozi siku hiyo asubuhi zilisema: 
“Afro-Shiraz vijana wa Hanga na (kundi la John Okello) wanatoa askari tu, lakini Umma Part 
(kikundi cha Babu) ndio wanaoweka na kusimamia mipango, mikakati na mbinu zote za mapambano'".
Hii ina maana kuwa Babu alikuwa anajuwa kila kitu kinacho endelea nchini Zanzibar. 
Japo kuwa yeye alikuwa amejificha huko nchini Tanganyika, kuingia kwa vijana wa Umma Party
kuliongeza kasi ya mapambano na kwa ufanisi zaidi hivi kwamba, kufikia saa 11.00, saa nne 
tangu kuanza mapambano, vituo vikuu vya ulinzi vya Ziwani na Mtoni vilikuwa vimetekwa; na 
kufikia saa 12.00 asubuhi, upinzani pekee ulitoka Kituo cha Polisi, Malindi, karibu na Bandari ya Unguja. 
Ilipofika saa 2:30 asubuhi, Malindi nayo ikawa mikononi mwa vijana wa Babu maana wao ndio walio
juwa njia za kupigana kivita maana ndio walio pikwa kivita huko Cuba na sio kama wanavyo danganya
watu kuwa walikuwa wakwezi na wakulima na mikuki yaguju mkiki na mashingani unafanya masihara
wao ndio walio kiteka maana wao pia walikuwa na silaha nzito za kivita na wakijuwa kuzitumia wakakamilisha
kazi ndio hapo Wanamapinduzi wakajuwa wameshinda. Ndipo saa 3:00 asubuhi hiyo,
 
PICHA YAKE ALIPO WASILI UINGEREZA BAADA YA KUPINDULIWA NA JOHN OKELLO
askari wa Sultani Jamshid, walimgongea mlango na kumwambia kwa kifupi, “Vita tumeshindwa”; wakasema, 
hakuwa na budi ila kuondoka kwenye Kasri lake ndani ya dakika 10 vinginevyo angetekwa.
Kwa kutumia ulinzi wa kituo hicho cha Malindi, Jamshid na familia yake wakatorokea 
kwenye Meli iitwayo ‘SALAMA” ila ilikuwa ndogo iliyowafikisha kwenye meli kubwa ya Sultani
 iliyongojea Pwani, iitwayo SEYYID KHALFA na kung’oa nanga kwenda Mombasa 
ambako alikataliwa kutia nanga na Kinyatta aliyekuwa Raisi wa nchi ya Kenya wakati huo; 
kisha akageuza kwenda mpaka jijini Dar es Salaam kwa Nyerere ambaye ndie aliyekuwa 
raisi wa  nchini Tanganyika ambako alipokewa na kupewa hifadhi na Nyerere, hadi 
alipokamilisha mipango ya kwenda uhamishoni London nchini Uingereza, wiki kadhaa baadaye 
na humo pia kulikuwa na waingereza walio kuwa wakimtumikia Sultani Jamshid,na wale polisi 
wa kiengereza walio kuwa katika kituo cha Malindi pia walikuwa katika Meli hiyo hiyo,
hapa pia tunaona Mkono wa Muingereza jinsi alivyo mlaghai Sultani Jamshid kwa kumuambia
asikimbilie nchini Oman kwa  kuwa ati watu wangelifikiri kuwa anajianda tena huko Oman ili
arudi tena Zanzibar kwa hiyo bora akimbilie Uingereza kumbe ndio wanakwenda kumaliza maana
wao waingereza pia hakuwa na furaha kufukuzwa nchini Zanzibar na kumuacha Sultani Jamshid
akiwa bado ni Mfalme wa nchi ya Zanzibar kwa hiyo wao pia waingereza walitaka, mapinduzi yafanyike
ili iwe wao waingereza wamekosa na yeye pia Sultani Jamshid amekosa.
BABU AKIFURAHI NA VIJANA WAKE WA UMMA PARTY BAADA 
YA KUMPIDUWA SULTAN JUMSHID NA BABU KURUDI ZANZIBAR
Vijana wa Umma Party wateka Uwanja
Wakati huo mapambano ya kuteka uwanja wa ndege wa Zanzibar, yakiongozwa na vijana wa Umma Party, 
yalikuwa yakiendelea hadi saa 9:20 mchana, uwanja huo ulipotekwa.Mapema asubuhi, 
Shamte alikuwa ametuma ndege ndogo kwenda Pemba kuleta silaha, lakini njia ya kwenda uwanjani 
ilifungwa kabla ndege haijarejea, hivyo ikarejea Pemba na silaha hii hakuna ushahidi wowote.
Siku hiyo alasiri, Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje wa nchi ya Tanganyika, Oscar Kambona, 
alipiga simu mnara wa redio wa Kiwanja cha Ndege cha Zanzibar, kutaka kujua hali ya usalama, 
lakini akajibiwa kijeuri: “Mshenzi we! Tuliomba msaada wenu saa sita zilizopita (saa 12 asubuhi); 
askari wenu wako wapi...??”.  Hii inaonyesha kwamba, wakati Kituo cha Malindi kikikaribia kutekwa saa 12:00 asubuhi hiyo,
Serikali ya Shamte iliomba msaada wa Tanganyika bila mafanikio hakujuwa kama hiyo serikali ya Tanganyika inashiriki kikamilifu.
Hilo Shamte hakulijuwa na ndio maana hawakupata msaada wowote kutoka nchi ya Tanganyika,ndio maana Oscar Kambona
alikuwa akipiga na kutaka kujuwa vipi je vijana wa mapinduzi washafanikiwa kukiteka kiwanja cha ndege cha Zanzibar na sio kuisadia
Serikali ya Shamte Saa 8:10 alisikika tena mtu wa redio uwanjani Zanzibar akiongea na mwenzake 
wa uwanja wa ndege wa jiji la Dar es Salaam nchini Tanganyika:  “Mambo ni mabaya sana.  Lori lenye watu 30 limefika; 
na watu wenye silaha (Wanamapinduzi wa Umma Party) wapo chini. Sasa nakwenda kukutana nao”.
Naye mwenzake wa jiji la Dar es Salaam nchini Tanganyika, akihisi kwamba uwanja wa Zanzibar ungetekwa wakati wowote, 
alijibu kwa kifupi:  “Nakuombea dua”. Dakika kadhaa baadaye, uwanja huo uliangukia mikononi mwa Wanamapinduzi vijana wa Umma Part.
Kutekwa kwa uwanja wa ndege kulikamilisha mapambano makuu ya kimapinduzi nchini Zanzibar, 
lakini yaliendelea kwa kiwango kidogo hapa na pale vijijini, kati ya Waarabu wa Kimanga na walio kuwa wakijihami na familia. 
Wanamapinduzi hao waliunganishwa siku ya mapambano (bila mipango ya pamoja ya awali) 
na dhana (theory) ya mapambano ya Che Guevara, kwamba: 
“armed action on its own would create a momentum among the population”, 
yaani, mapambano ya silaha pekee yanatosha kutia nguvu na kusukuma umma kuingia kwenye mapambano. 
Na ndivyo ilivyokuwa.Lakini pamoja na hayo, ili kufanikiwa lazima pawe (na palikuwa) 
na kiongozi wa mapambano hayo; na kwa haya, Field Marshal John Okello, wengi wa CCM
wanamkana kuwa si chochote na kuzidi kudanganya Umma kua ati babu zao ndio walio pinduwa, 
lakini bila kutaja mtu mwingine tofauti aliyeongoza mapambano hayo.
Kwa namna Mapinduzi yalivyoendeshwa kwa ustadi na ufanisi mkubwa wa kijeshi, 
ni dhahiri yalitekelezwa na kuratibiwa na wajuzi waliopitia mafunzo ya vita ambao ndio vijana wa Umma part wa Babu, 
ambapo wakulina na wakwezi walisaidia tu kuongeza idadi na nguvu ya wapambanaji.
Wakati hakuna ubishi kwamba John Okello alikuwa kiongozi mkuu wa viongozi hao wakati wa kazi, 
ni dhahiri pia kwamba watekaji 40 wa mstari wa mbele wa Kambi ya Mtoni walikuwa ni pamoja na 
askari waliofukuzwa Jeshi la Sultani niliowaeleza mwanzo, na wale wa Umma Party waliofunzwa Cuba
hapa ndio unajuwa kuwa wazi vijana wa Umma part wa Babu kutoka Cuba ambao ni wzanzibari
na wale wakwezi na wakulima wa John Okello walishirikiana mkono kwa mkono sio kama wanavyo
jinata CCM babu zetu wee babu zetu wee ndio walio pinduwa na ukichunguza zaidi utakatu babu
zao walikuwa hata hawajulikana katika mapinduzi wala hawakuwepo kabisa.
Field Marshal atangaza Serikali
Jumapili, Januari 12, 1964 jioni, mtu mmoja aliyejitangaza kupitia redio kama “Field Marshal” 
bila kutaja jina lake, alitangaza kwa Kiswahili Baraza la Mawaziri la mseto wa vyama vya 
ASP na Umma Party, la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.Aliwataja Sheikh Abeid Amani Karume (ASP) kuwa Rais, 
Kassim Hanga (ASP), Makamu wa Rais, na Abdulrahman Babu (Umma Party), 
Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje, na yeye mwenyewe (Field Marshal) 
akajitangaza kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi. Nafasi zingine za Baraza hilo zilikwenda 
kwa makada wengine wa ASP na Umma Party.Licha ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Mapinduzi ya watu 14, 
John Okello pia alikuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.  Gazeti la Serikali ya Zanzibar 
la Januari 25, 1964, lilipotangaza majina 30 ya wajumbe wa Baraza hilo, 
lilianza na orodha ya mawaziri wa Serikali; kisha orodha ya Kamati ya Mapinduzi, 
ambapo jina la “Field Marshal John Okello lilikuwa la kwanza.
Wakati “Field Marshal” akitangaza Serikali yake, Januari 12, 1964 jioni, 
aliacha kitendawili kifuatacho:  alipomaliza kutaja jina la Mzee Karume kuwa Rais, 
alimwita na kuagiza kwa sauti ya mamlaka akisema,  “….Karume, popote ulipo, 
rudi haraka na kuchukua nafasi yako”.Swali ni je, Karume alikuwa wapi kipindi chote cha Mapinduzi..??
Naikiwa Mzee Karume ndio aliyepanga mapinduzi kwa nini alihitaji kuitwa popote alipo arudi...??  
Alitekelezaje majukumu yake kama Rais wa kuteuliwa na John Okello, kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, 
aliyedumu kwa miezi miwili madarakani..??  John Okello aliachaje madaraka hayo na kusahaulika 
haraka hivyo...??Kwa kuwa hakuna ubishi kwamba,John Okello alisimamia Serikali ya Mapinduzi 
(iliyotambuliwa na mataifa kama ya – Kenya, Uganda na nchi zingine) 
kwa miezi miwili mfululizo akitoa maagizo yaliyoheshimiwa na wote kipindi chote hicho, 
je, kuna nini kinachomfanya asiitwe au kutambuliwa kama kiongozi wa Serikali ya 
Awamu ya Kwanza Zanzibar hadi naye alipopinduliwa.....??  Alipinduliwaje......??
Field Marshal John Okello: Shujaa na muuwaji mapinduzi Zanzibar asiyekumbukwa;

  • Nyerere katikati ya mvutano kati ya Mzee Karume na John Okello
KATIKA sehemu ya pili ya makala haya, tuliona jinsi Wanamapinduzi ya Zanzibar ya 
Januari 12, 1964 walivyokamilisha kazi hiyo siku hiyo mchana, na jioni hiyo hiyo Kiongozi wa 
Mapinduzi hayo kutangaza Serikali yake.Niharakishe kutamka hapa mapema kuwa, 
katika Baraza la Mapinduzi lililotangazwa jioni hiyo, Karume, Thabit Kombo, 
Jumbe na Edington  Kisasi, Mwafrika pekee mwenye cheo cha juu kabisa katika Jeshi la Polisi 
wakati huo, hawakuwemo.Ukweli siku hiyo, Kisasi aliamshwa tu kutoka usingizini na Wanamapinduzi wakati tayari moto 
ukiwaka, na hatuelezwi kama alishiriki au alikata mbuga.Inafahamika kuwa, katika harakati hizo za Mapinduzi, 
Absalom Anwi, raia wa Kenya, alikuwa wa msaada mkubwa sana kwa John Okello, pengine kuliko wapiganaji wengi.
Wakati akitangaza Serikali yake, kwa nini John Okello aliita:  “Karume, popote ulipo, 
rudi haraka na kuchukua nafasi yako..”??  Karume alikuwa wapi..?? Kwa nini hakuita hivyo kwa Babu na Hanga..??
Tunajua, Babu alitoroka Zanzibar tangu Desemba 1963 wakati akitafutwa na Serikali mpya ya Wazanzibari ikiongozwa na shamte.
akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, kwa kutishia na kuhatarisha usalama wa 
Serikali ya ZNP/ZPPP. Kwa Hanga, tunaambiwa, na kama alivyosema yeye mwenyewe 
baadaye lakini bila uthibitisho, kwamba aliondoka Visiwani siku moja kabla ya Mapinduzi 
kwenda jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika kufanya mazoezi ya kutumia silaha za vita, na pia kumnong’oneza 
rafiki yake, Oscar Kambona juu ya mpango wa Mapinduzi.  Ukweli ni kwamba, 
aliondoka kwa mtumbwi usiku saa chache kabla ya, au wakati Mapinduzi yalipoanza.
Lakini kwa Karume kuna dhana moja inayokaribiana na ukweli; kwamba, 
alikimbia kutoka Visiwani usiku wa Jumamosi saa chache kabla ya, au wakati Mapinduzi 
yalipoanza kwa sababu ama hakujua habari za Mapinduzi hayo kabla na nani aliyaongoza; 
au hakutaka kuwa Kisiwani kama jaribio la Mapinduzi lingeshindwa.Tunachojua tu ni kwamba, 
Jumapili 12, 1964 usiku (saa chache baada ya John Okello kutangaza Serikali yake Zanzibar), 
Karume alikutana na Mwalimu Nyerere mjini Dar es Salaam nchini Tanganyika ambaye aliona kuwa Mzee Karume 
alihitajika zaidi (na John Okello) kutuliza mambo nchini Zanzibar Mzee Karume na hanga na 
ASP ndio wenye wafuasi wengi kwa hiyo ni rahisi watu kuwasikiliza,  akamwambia, kama alivyotaka John Okello 
“arudi nyumbani mara moja”, huku “Field Marshal” akiendelea kusisitiza kupitia redio 
“rudi haraka sana”.Na kwa kuwa uwanja wa Ndege wa Zanzibar ulikuwa bado umefungwa, 
Mzee Karume na Hanga walipata msaada wa boti kutoka kwa Mzungu mmoja mvuvi aitwaye 
Mishar Fainziber; wakaondoka  jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika eneo la Silver Sands, saa nane alfajiri, 
Jumatatu 13, ikiwa zimepita saa 28 baada ya Mapinduzi, wakafika Zanzibar asubuhi na 
kwenda moja kwa moja kwenye jengo la “Raha Leo” na kulakiwa na “Field Marshal” John Okello, 
kisha wote hao na wengineo, wakala chakula pamoja.Nimeelezea hili kwa 
kirefu kuwezesha wasomaji kujua Mzee Karume alikuwa wapi wakati wa Mapinduzi. 
Na yeye mwenyewe alikiri baadaye akisema:  “Nilikwenda Tanganyika kumweleza 
Julius Nyerere jinsi (Mapinduzi) yalivyofanyika”. Sababu zinazotolewa zina ‘usanii’ kidogo:  
Hanga anadai alikwenda jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika Jumapili 12, kumnong’oneza Kambona juu ya 
Mapinduzi; Karume naye alikwenda Dar es Salaam kumwambia Nyerere, juu ya jambo hilo hilo. 
Wadadisi wa mambo wanahoji, busara gani waliyotumia kuondoka kabla au wakati mapambano yakiendelea..??  
Kwa nini hawakupiga simu wakati zilikuwa zikifanya kazi siku hiyo..?? Je, si kweli kwamba walikimbia Mapinduzi..??  
Tuache hayo, turejee kwenye mchakato wa Serikali ya John Okello.
Nyerere hakumtambua Karume
Jumapili 12, 1964 asubuhi, Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje wa nchi ya Tanganyika, Oscar Kambona, 
alikwenda Nairobi nchini Kenya na Kampala nchini Uganda na akiwa huko, akafahamu kwamba,
Kenya na Uganda zilikuwa mbioni kuitambua Serikali mpya ya Mapinduzi ya John OKello.Kwa hiyo, 
alimpigia simu Mwalimu Nyerere kumwomba naye afanye hivyo alilokuwa halijuwi Oscar Kambona.
Ni kuwa Mwl Nyerere ndio mpangaji wa hayo mapinduzi yeye ndie aliyeweka vijana Tanga yeye ndie,
aliye agiza silaha kutoka algiria meli ilifunga poti ya Dar es Salaam na hii ndio style ya Nyerere
kujifanya kama hajuwi linalo endelea kumbe yeye ndio kashika rimote ana bonyeza tu
Kenya na Uganda ziliitambua Serikali ya John Okello, Jumatatu alasiri, Januari 13, 1964; 
wakati huo Mzee Karume ndiyo kwanza alikuwa anarejea Zanzibar kutoka (mafichoni?)
jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika.Kambona pia alimjulisha Mwalimu juu ya Sultani aliyepinduliwa kukataliwa 
kutia nanga Mombasa na Serikali ya Kenya, na kumwomba naye amkatalie vivyo hivyo. 
Nyerere aliyakataa kata kata maombi yote ya Kambona akidai kuwa, hakuwa na hakika 
kama kweli Mzee Karume na ASP walikuwa wameshika hatamu za uongozi nchini Zanzibar; 
badala yake akamruhusu Sultani Jamshid na kikundi chake kutia nanga na kukaa 
jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, kama nilivyoeleza mwanzo.Ingawa wengi wanaamini 
kwamba Mwalimu alimruhusu Sultani kuishi nchini kwa sababu ya ubinadamu tu, 
lakini inaonesha pia kwamba hakuwa na ugomvi mkubwa na Serikali iliyopinduliwa ila pia hakuitaka.
Nimeeleza haya kuthibitisha kwamba, si Serikali ya Tanganyika, 
wala jumuiya kubwa ya Kizanzibari, iliyoamini kwamba Mapinduzi hayo yalisimamiwa 
na viongozi wakuu wa ASP; bali kwamba, yalifanywa na vijana wa ASP na 
Umma Party bila matarajio wala viongozi wao kujua na John Okello na kundi lake la watanganyika.
Field Marshal ajitambulisha
Januari 13, 1964, Kiongozi wa Mapinduzi hayo, ambaye awali alijitambulisha kwa cheo tu cha 
“Field Marshal”, alijitambulisha kikamilifu redioni kwa jina la “Field Marshal” John Okello, 
kisha akasema: “Sultani amefukuzwa na hatakanyaga tena ardhi ya Zanzibar; jumba lake na 
mali yake imetaifishwa”.
Wakati huo, mapigano ya hapa na pale yalikuwa bado yakiendelea mashambani; 
John Okello akaomba kutoka Tanganyika shehena ya Ndege nzima ya dawa, 
na akatoa amri kwa wauguzi wote kurejea kazini jioni hiyo.
Katika kuhakikisha usalama wa mali za raia na juu ya vitendo vya usaliti,John Okello alionya: 
“Mtu yeyote atakayejaribu kuwa mnafiki, atapata adhabu ya kifungo cha miaka hamsini; 
atakayeiba, hata mche wa sabuni, ataadhibiwa kifungo cha miaka minane. 
Mimi naweza kutengeneza mabomu mia nane kwa saa moja”
Siku nyingine, katika kuonyesha kwamba alikuwa kiongozi mwenye mamlaka ya kijeshi alisema: 
“Mimi ni Field Marshal ninayezungumza. Mtaona jinsi tunavyowanyonga watu na kuwachoma 
kama kuku.  Wengine watakatwa vipande vipande na kutandazwa mitaani; wengine 
watatupwa baharini, na wengine watafungwa kwenye miti na kupigwa risasi”.
Kila siku alitoa hotuba za vitisho akisema:  “Nitachukua hatua kali, kali mara themanini na 
nane na zaidi.  Hakuna ruhusa mtu kuacha mkewe; atakayefanya hivyo, atachapwa viboko 
sitini na tano.  Sultani alikuwa Shetani; mabeberu na mabepari ni mashetani.
Mnayakataa mashetani haya...??”, aliwauliza wananchi kupitia redio ya Zanzibar.
Maneno haya yanaweza kuonekana ya kihayawani, lakini hayashangazi kwa kuwa yalikidhi 
lengo na madhumuni yake ya kutisha na kuwaogopesha masalia ya wafuasi wa ZNP na ZPPP, 
waliokuwa na kusudi la kujaribu kuyaondoa Mapinduzi hayo.
Ni maneno yasiyoshangaza pia kutamkwa na mtu wa kabila la Walang’o wa jamii ya kabila la 
Rais wa zamani wa Uganda, “Field Marshal” Idi Amin Dada.  Je, Idi Amin hakuwahi kusema 
mwenyewe kwamba alikuwa na uwezo wa kuliangamiza Jeshi la Makaburu wa Afrika Kusini 
kwa nusu saa na kuitawala nchi hiyo..?? Je, hakuwahi kuwapeleka viongozi wa nchi huru za 
Kiafrika (OAU) waliofanya mkutano wao mjini Kampala, kwenye kisiwa kimoja kidogo cha 
Ziwa Victoria, eti kushuhudia Ndege zake zikidondosha mabomu “kuchakaza” sehemu hiyo, 
kuthibitisha jinsi alivyokuwa na uwezo wa “kuichakaza” Afrika Kusini ya makaburu na kuikalia?.
Je,wakati wa vita ya Kagera, hakumtaka Mwalimu Nyerere wakutane kwenye ulingo wa masumbwi, 
wazichape huku yeye (Amin) amefungwa kamba mkono wa kulia na kupigana kwa mkono mmoja 
wa kushoto, na Nyerere apigane kwa mikono yote miwili; akajitapa kwamba, bado angeweza 
kumchakaza Mwalimu kwa mkono mmoja..??Je, Amin huyo huyo hakuagiza mabalozi wa kigeni (Wazungu) 
nchini Uganda, kumbeba juu ya machela na kumtembeza mitaani, nao wakafanya 
hivyo eti kuwathibitishia kwamba yeye (Amin) alikuwa “mshindi wa himaya ya Uingereza?”
Pamoja na yote hayo ya kihayawani, lakini hayakumfanya Amin asiwe kiongozi na mtawala wa 
Uganda. Vivyo hivyo, maneno haya ya kihayawani ya “Field Marshal” John Okello, 
hayakumfanya asiwe au asitambulike kama Kiongozi wa Serikali ya Awamu ya 
Kwanza ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Karume, Okello wateta na Mwalimu
Katika mfululizo wa matangazo yake redioni Jumanne, Januari 14, 1964,John Okello, 
kama Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi, alitamka kwamba, Mawaziri wa zamani wa Serikali 
ya ZNP/ZPPP wangenyongwa.  Jumatano,Mzee Karume 
(ambaye ni Rais wakuwekwa na John Okello wakti huwo), alikanusha na kumpinga vikali 
kwamba, hakuna mtu atakayenyongwa, wala kulipiza kisasi.  Huo ulikuwa mwanzo wa 
migongano kati ya viongozi hao wawili.Alhamis, Januari 16, 1964, Rais Mzee Karume, Babu na Hanga 
walikwenda jijiniDar es Salaam nchini Tanganyik kwa Ndege atii kumsihi Nyerere aitambue 
Serikali ya Mapinduzi, na pia asaidie kupeleka askari wachache kwenda kurejesha 
amani na utulivu.Lakini kulikuwa na mengi nyuma pazia na maombi hayo tunavyo fikiri sisi
nikuwa hawakupenda jinsi John Okello anavyo endesha nchi bila ya ustarabu wa Kizanzibari
kwa hiyo hawakuwa na lakufanya isipokuwa kwenda kumsemesha Nyerere ili amsemeshi mtu
wake ambaye ni John Okello na kundi zima la Watanganyika maana Babu katuliza vijana wake,
wa Umma Party na Hanga na Mzee Karume wametuliza vijana wao wa ASP lakini hili kundi la 
Watanganyika,Wakenya na Waganda likiongozwa na John Okello lilikuwa halisiki amri ya yoyote,
isipokuwa John Okello na Nyerere maana ndio walio kuwa wakuu wao wakiwaongoza.  
Mzee Karume alikuwa ameingia mgogoro na viongozi wenzake wa ASP wenye siasa za kikomunisti, 
wakiongozwa na Othman Sharrif, wakidai alikuwa ameshindwa kuongoza 
wakatishia kumpindua hapo Mzee Karume akaona madara hayoo yananza kumtoka hakuwa na budi.
ila sasa nikutafuta uwezo wake mwenyewe ambao akinena jambo watamsikia na kufuta amri zake.
Othman Sharrif waliungwa mkono sana na vijana wa ASP na Umma Party .
Ingawa John Okello alijitahidi kusuluhisha mgogoro huo ukaonekana kumalizika kwa juu juu tu, 
lakini azima ya “kumchuna ngozi” Mzee Karume ilibaki ikiibuka kwa  vipindi, na hivyo akaomba 
msaada wa ulinzi kutoka Tanganyika.Nyerere alikubali ombi hilo, kwamba baada ya siku mbili tu 
askari 300 walitumwa Zanzibar kurejesha amani na “kumlinda”Mzee  Karume hapa ikawa John Okello,
ameshapinduliwa kiaina na Mzee karume maana sasa Mzee karume ana jeshi pia alikuwa Mzee Karume,
ashawapinduwa Othman Sharrif,Hanga na kundi lao la ASP wenye siasa za kikomunisti.
Hatua ya Mzee Karume kupelekewa ulinzi ilimfunga jiwe shingoni kiasi kwamba maana kwa Zanzibar
hawakumpenda tena walimuona kuwa amewapinduwa na wao kuona mapinduzi yao walio fanya,
yamekwenda na maji bila ya faida yoyote sasa ikawa Mzee Karume kuwashughulikia wanamapinduzi,
ili yeye aweze kutawala kwa amani pia hakujuwa kama yeye mwenyewe kutaka msaada wa jeshi kwa
Nyerere ni kosa kubwa hakujuwa ila alipata habari yake kuwa lilikuwa ni kosa kubwa baada ya 
miezi mitatu baadaye, pale Nyerere aliposhinikiza Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar 
na Mzee Karume kuonyesha kutokuwa tayari kwa hilo, (Nyerere) alitishia kuwaondoa askari 
hao ili kumwacha (Mzee Karume) mtupu apinduliwe na vijana wa wanamapinduzi. 
 
Kwa sababu hiyo alisalimu amri na kukubali Muungano huo haraka haraka ili abaki madarakani.
Siku hiyo John Okello, pengine bila kujua safari ya Dar es Salaam nchini Tanganyika 
ya Mzee Karume na wenzake; na pengine kwa kuudhika na “ubishi” wa Mzee Karume uliokuwa 
umeanza kujitokeza, alibatilisha uteuzi wa Mzee Karume kuwa Rais, badala yake akampa 
cheo cha Makamu wa Rais kwa madai kwamba “hakushiriki hata kidogo katika mapambano ya Mapinduzi”.
Jioni hiyo, akajipa cheo cha Rais John Okello. Lakini, pengine baada ya kushauriwa, pamoja na maridhiano 
kati yake na Mzee Karume, alifuta mabadiliko hayo wakati tayari hatua hiyo ilikuwa imetia ufa wa 
kiuongozi kati yao.Kwamba, Aboud Jumbe alishangaa alipomwona John Okello 
na mabastola yake akauliza: “Na mtu huyu ni nani na katoka wapi..??”,ni maneno ya kupotosha 
historia ya Mapinduzi ya Zanzibar.Hiyo ilikuwa ni Alhamis, Januari 16, 1964 mchana.  
John Okello alifika Jumba la Makao Makuu yake “Raha Leo” akakuta mamia ya watu 
wamekusanyika wakimsubiri kwa shauku, wengi wamevaa vitambaa vya kijani na manjano 
mabegani kuonyesha kwamba walishiriki kwenye mapambano ya mapinduzi ya Zanzibar.
Mara alipotokea, huku amevalia mavazi meusi na bastola zikipishana kiunoni, 
wananchi wakalipuka kwa shangwe wakipaza sauti: “Jamhuri!  Jamhuri!”; 
kila mmoja akiwania kumshika mkono. Kama kweli Aboud Jumbe alikuwepo na kushuhudia ukweli huo, 
na kama kweli alitamka maneno hayo aandikavyo mwandishi, basi, atakuwa ni mmoja wa 
wasaliti wa Mapinduzi ya Zanzibar ya kweli kwa lengo la kujikweza.Jumapili Januari 19, 1964, “Field Marshal” John Okello 
alikwenda Dar es Salaam kwa mapumziko kidogo baada ya kazi kubwa; ambapo siku hiyo 
usiku, alikuwa na mazungumzo marefu na kiongozi mwenzake, Rais Julius Nyerere wa Tanganyika, 
ambaye alimshauri afanye kazi kwa imani pamoja na Rais Karume.Haifahamiki “Field Marshal” John Okello 
na Mwalimu walimaliza mazungumzo yao saa ngapi usiku huo, na kama John Okello 
alilala Ikulu ya Dar es Salaam nchini Tanganyika au aliondoka. Lakini inafahamia kuwa, 
saa chache baadaye,alfajiri ya Jumatatu, Januari 20, 1964, Jeshi la Tanganyika  - “Tanganyika Rifles” (TR), 
liliasi na Mwalimu akakimbilia mafichoni.
Field Marshal John Okello: Shujaa na muuwaji mapinduzi Zanzibar asiyekumbukwa.
Siku Jeshi lilipoasi serikali ilinywea 
KATIKA sehemu ya pili ya makala haya wiki iliyopita, tuliona namna Waziri wa Mambo ya Nje 
na Ulinzi wa Tanganyika, Oscar Kambona, alivyoweza kuwashawishi wanajeshi wa Tanganyika 
walioasi Januari 20, 1964, kurejea kambini kwa ahadi ya malalamiko yao kushughulikiwa.
Hadi waasi hao wakirejea kambini, hapakuwa bado na taarifa yoyote ya alikokimbilia 
Rais wa nchi yao Tanganyika Julius Nyerere isipokuwa, “Field Marshal” John Gidion Okello, 
aliyekuwa na mazungumzo naye Ikulu saa chache kabla ya maasi hayo kutokea, 
aliibukia Nairobi nchini Kenya siku hiyo, akazungumza na waandishi wa habari 
akilaani mabeberu na mabepari barani Afrika, akiwaita “mashetani”. 
Endelea na sehemu hii ya tatu na ya mwisho kujua kilichotokea.
KITENDO cha Oscar Kambona cha kutokutaja alikokuwa Mwalimu Julius Nyerere, 
wala kwamba alikuwa bado anatawala, kilitafsiriwa na maadui wake kwamba alikuwa na 
njama za kunyakua madaraka.Wahenga walisema, “akutukanaye hakuchagulii tusi”; 
ndivyo walivyomtuhumu.Kama kweli Oscar Kambona alikuwa na mpango wa kumpindua Nyerere, 
angeshindwaje wakati askari walioasi walimsikiliza na kumtii hata wakarejea kambini...?? 
Uvumi huo dhaifu uliishiwa nguvu na kufa haraka.Januari 22, siku moja baada ya waasi kurejea kambini, 
hali ilikuwa haijawa shwari mitaani kufuatia kuibuka kwa uvunjifu wa amani kwa watu 
kuvunjiwa maduka na hata kudhuriwa.Oscar Kambona alilazimika kutumia wanajeshi kutuliza 
hali kutokana na upungufu wa askari polisi baada ya askari 300 kupelekwa nchini Zanzibar 
kuimarisha Serikali ya Abeid Karume ya kuwapinduwa wanamapinduzi ambao ni makundi matatu,
John Okello na kundi lake la watanganyika,Hanga na Othman Sharrif na kundi lake la ASP,
Babu na vijana wake kutoka Cuba.Katika Mtaa wa Magomeni,jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, 
Mwarabu mmoja mwenye duka aliwaua askari wawili na raia wawili Waafrika ambao 
mmoja wao alivunja duka na kuiba.  Hasira ya wanajeshi ilitua kwa Mwarabu huyo kwa 
kuipiga nyumba yake mabomu ikawaka moto; na alipochomoka kutoroka asiungue yeye 
na binti yake wa miaka sita, wote wawili waliuawa kwa risasi, huku watu watano wengine 
wa familia yake wakiteketea kwa moto ndani ya nyumba yake.
Hali yazidi kuwa tete
Januari 23, kwenye mazishi ya wanajeshi waliouawa na Mwarabu, 
Sajini Ilogi alijitahidi kukwepa kuzungumza na Kambona pia kumtazama usoni, 
tabia iliyoashiria shari na kumlazimu Kambona kuelekeza watu wa Usalama 
wafuatilie nyendo zake.Haukupita muda siku hiyo hiyo, taarifa ikafika kwamba Kikosi cha Pili cha Jeshi, 
Tabora nacho kilikuwa kimeasi na kuwakamata baadhi ya maafisa wa Jeshi. Mmoja wa 
maafisa hao waliokamatwa Tabora alikuwa ni Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya.
Uingereza yaandaa jeshi kupambana
Siku hiyo pia, Mwalimu Nyerere, kwa njia ya hotuba iliyorekodiwa kutoka mahali alikojificha, 
alizungumza na Taifa, akasema:  “Jana (22/1/1964), ilikuwa siku ya aibu sana.  
Watu wengine walipitapita wakieneza uzushi kwamba mimi sipo tena, na kwamba 
Serikali yangu imepinduliwa. Huo ni upuuzi mtupu….  Matumaini yangu na Serikali ni kwamba tangu leo, 
hatutashuhudia tena aibu kama tuliyoipata, kurudiwa nchi yetu ya Tanganyika”.
Licha ya hotuba ya Mwalimu, maswali mengi yalizidi kuibuka, wengine wakihoji 
“yuko wapi?”, wengine wakisema ametekwa; na wengine wakikana kuwa hiyo 
haikuwa sauti ya Mwalimu, ilikuwa ya kuigiza kuuhadaa umma.
Kama hatua ya tahadhari, Serikali ya Uingereza iliyokuwa na vikosi kadhaa vya Jeshi 
Afrika Mashariki kwa kile kilichoitwa “kufuatilia mikakati ya Ukomunisti baada ya Mapinduzi ya 
Wakomunisti nchini Zanzibar”, ilianza maandalizi ya kupeleka askari 2,000 zaidi eneo hilo kwa 
tukio la nchi ya Tanganyika la Januari 20 na maasi mapya huko Tabora, kwa hofu kwamba huenda 
maasi hayo yalikuwa na mkono wa Wakomunisti.Manowari iitwayo Rhyl ilitia nanga nje ya 
Pwani ya jiji la Dar es Salaam, na nyingine, Centaur, iliyobeba ndege, ilikuwa njiani kutoka 
Aden ikiwa na vifaa na askari 600.
Mwalimu ajitokeza hadharani
Ghafla, Januari 24, asubuhi, Mwalimu akajitokeza hadharani katika gari ambalo alikuwemo 
pia Mama Maria Nyerere na Waziri wa Mambo ya Ndani, John Malecela Lusinde. 
Wakatembelea mitaa iliyoathirika kwa maasi, hasa eneo la Magomeni na kuwapa pole wananchi,
pia kuwatoa hofu kwamba jambo kama hilo halitatokea tena.
Januari 25, Mwalimu alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kuwa madai ya 
wanajeshi yalikuwa yanafikiriwa.  Kuhusu kwa nini Uingereza ilikuwa ikisogeza vikosi vyake
Pwani ya nchi ya Tanganyika, Mwalimu alisema hawakutarajia kuita majeshi ya Uingereza; 
“Tunao uwezo wa kuyakabili matatizo yetu sisi wenyewe”, alisema.Na kuhusu kama angewaadhibu 
askari walioasi, Mwalimu alikaa kimya kwa sekunde tano, na ghafla akasema, 
“Aksanteni sana, Waheshimiwa”, akafunga mazungumzo.Huku kikosi cha Tabora kikiendelea na maasi, 
Oscar Kambona akatuma simu ya maandishi huko kueleza kuwa alikuwa 
amemteua Kapteni Sarakikya kuwa Mkuu wa Kikosi. Sarakikya akatolewa mahabusu; 
akaamuru simu isomwe kwa sauti; kisha akatoa amri askari wasimame “mguu sawa”,
wafungue magazini na kutoa risasi,  wakamtii.  Usiku huo, alifanya mipango ya kuwasafirisha 
maafisa wote Wazungu kwenda jijini Dar es Salaam na hatimaye makwao.
Jeshi lamgomea Nyerere, laasi tena
Siku hiyo, Mwalimu alitoa amri askari wote wavae sare maalumu kuwapima utii.  
Walikataa kutii amri hiyo hii ni ushahidi kuwa hata watanganyika hawakupenda utawala wa Nyerere.
Wakati huo huo, mazungumzo kati ya Serikali na wanajeshi 
yalionekana kuvunjika na askari walianza kuasi tena.  Tofauti na maasi ya Januari 20, 
ambayo hayakuhusisha wanasiasa au kubeba hisia za kisiasa, safari hii viongozi wa vyama 
vya wafanyakazi kupitia TFL, walikuwa wakikutana na askari kwa siri kambini Colito, na 
kwamba TFL lilikuwa limeandaa ngomo nchi nzima mwisho wa wiki kuungana na askari waasi.
Maasi ya pili yaliambukiza majeshi ya Kenya na Uganda kuasi vivyo hivyo, siku hiyo hiyo, 
saa na wakati huo huo.  Kenyatta na Obote wakasoma maandiko ukutani, wakaita majeshi 
ya Uingereza kuzima maasi; Nyerere hakutaka, hakuamini kwamba jeshi lake mwenyewe 
lingeweza kumhujumu na kumpinduwa, lakini baadaye aliyakubali ya Kenyatta na Obote, 
kama tutakavyoona hivi punde.
Nyerere alianza kuamini “lisemwalo lipo…..”, pale maafisa usalama walipomwonyesha orodha
ya mawaziri watarajiwa kama mapinduzi yangefanikiwa na zaidi kwamba, 
mmoja wa watu wake wa karibu ilithibitika alikuwa ameombwa na waasi akubali kuwa 
makamu wa rais.
Mitafaruku yashika kasi
Yapata saa 11.30 jioni siku hiyo, Mwalimu alimwita Ikulu, Naibu Balozi wa Uingereza, 
F. Stephen Mills, akamwomba msaada wa jeshi la nchi yake; naye bila kuchelewa, 
akapeleka taarifa London na kujibiwa kwamba ombi lilikubaliwa bila masharti. 
Kisha Oscar Kambona akaenda hima Ubalozi wa Uingereza kumtafuta Brigedia Douglas 
aliyejificha huko tangu mwanzo wa maasi, Januari 20; kumwomba msaada wa kuratibu 
mipango. Usiku huo, Brigedia Douglas na afisa mwingine, walinyatia hadi kwenye manowari 
ya kivita, Centaur, iliyokuwa imefichwa Pwani huu ni ushahidi tosha kuwa viongozi wote wa tatu,
wa nchi tatu Tanganyika Nyerere,Kenya Kinyatta na Uganda Obote wote walikuwa sio marais
walio pendwa na wananchi na hata majeshi ya nchi hayakuwapenda kwahiyo walikuwa tu vibarak
wa muingereza walio wekwa na kuendelea kukandamiza wananchi wao ili tu wao wabaki madarakani.
Waasi wanyukwa
Jumamosi, Januari 26, saa 12:20 asubuhi kazi ikaanza; helikopta sita kutoka Centaur 
zilichukua askari 60, akiwamo Brigedia Douglas, hadi eneo la Colito. Dakika 10 baadaye, 
saa 12:30, manowari hiyo na meli nyingine ya vita, Cambrian, zilianza mashambulizi kwa 
mizinga kuwatisha waasi. Na kutoka umbali wa mita 40 hivi, Douglas akatangaza kwa kipaza 
sauti kwamba alikuwa ameshika madaraka yake tena, akawaamuru watoke nje “silaha juu” na 
kukaa chini barabarani. Aliwapa dakika 10 za kujibu; akaanza kuhesabu kwa lugha ya Kiswahili:
“Kumi, tisa, nane ….. moja”.  Hakuna aliyetoka;  nyumba ya walinzi ikafumuliwa paa kwa roketi, 
Askari wakaanza kujisalimisha!.Dakika 10 zilizofuata wakatoka askari 150 “silaha juu”,
na wengine 150 baada ya saa moja; na kufikia saa 1.30, Askari wote walikuwa wamesalimu amri.
Ikabaki kazi ya kufuatilia kuwakamata baadhi yao waliokimbilia porini.  Maasi hayo, 
yaliyosababisha vifo vya raia 17 na askari wazalendo wawili, yakawa yamezimwa.
Hakuna askari wa Kiingereza aliyeuawa au kujeruhiwa.nchi ya Tanganyika haikumwaga damu wakati 
wa kudai uhuru, ilimwaga damu wakati wa uhuru kwa Serikali kutokuwa sikivu na hayo ndio wanayo
yafanya nchini Zanzibar leo hii kwa kufanya Shein kuto kuwa msikivu na kufanya atakavyo kwa kuwa,
anajiamini kuwa Wazanzibari hawawezi kufanya kitu chochote mbele ya jeshi lake la kukopesha,
kutoka nchini Tanganyika.Sajini Francis Nhingo Ilogi aliibukia mjini kwenye Ofisi za Kampuni ya 
Simu za Nje – East African External Telecommunications Company (Extelcoms) 
mwenye hofu, akipiga simu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), U Thant.
Simu yake ya maandishi ilisomeka: 
“MAJESHI YA NCHI YA TANGANYIKA YAMETEKWA NA ASKARI MAMLUKI WASIOJULIKANA 
SAIDIA HARAKA KULETA MAJESHI YA UN.  LUTENI KANALI ILOGI – MKUU WA JESHI”.  
Umoja wa Mataifa haukujibu.Wakati wanajeshi hao 60 wa Uingereza wakizima maasi 
Tanganyika asubuhi hiyo, majeshi ya Kiingereza yalikuwa yakifanya hivyo pia nchini Kenya na Uganda,
siku na muda huo huo.  Kwa Uganda, askari walisafiri alfajiri kwa gari kutoka Entebbe hadi 
Kambi ya Jinja iliyoasi na kuwapokonya silaha, kisha kuwachukua mateka.  Na huko Kenya, 
kikosi cha 11, Kambi ya Bark-Lanet  kilichoasi na kuteka silaha nyingi usiku, 
kilipigwa vilivyo na kunyang’anywa silaha; hali ikawa shwari.
Ndiyo kusema kwamba, kutoka Jumamosi hiyo, jukumu la ulinzi wa nchi za Afrika Mashariki 
Kenya, Uganda na Tanganyika lilikuwa mikononi mwa majeshi ya Uingereza. 
Swali kuu ni:  Ilikuwaje maasi yakazikumba nchi tatu za Afrika Mashariki wakati ule ule 
na wiki moja tu kufuatia Mapinduzi ya Zanzibar..?  Je, kulikuwa na mkono wa mtu – wanasiasa..?
Tukianzia na mshukiwa nambari wani, Oscar Kambona, ambaye ujasiri wake ulisaidia kutuliza 
hali, hana hatia, kama tulivyohoji na kujibu hapo mwanzo.  Na kuhusu “Field Marshal” 
John Okello aliyekuwa Ikulu dakika chache kabla ya maasi kutokea, naye hana tuhuma, 
kwani kwa kipindi chote tangu Mapinduzi ya Zanzibar, alikuwa kwenye harakati za kulinda 
madaraka yake dhidi ya mahasimu wake (Karume na kikundi) ambao alidai hawakushiriki 
katika Mapinduzi. Sababu za kuasi kwa majeshi ya nchi za Afrika Mashariki ni kwamba, 
yalitokana na jeshi la wakoloni wa Kiingereza yakiwa na muundo na utawala unaofanana; 
na kwamba mazingira, matatizo na malalamiko yao yalifanana kuwafanya wadai haki kwa njia 
na kwa mtindo unaofanana. Lakini ni dhahiri waasi walitiwa moyo na mafanikio ya wananchi 
wa Zanzibar.Maafisa wa jeshi wa Kiingereza walitupiwa lawama kwa kutoiarifu 
Serikali mapema juu ya malalamiko hayo.  Kwa mujibu wa Rashidi Kawawa baadaye, 
“Maasi yangeepukika kama tu Mkuu wa Majeshi angewahi kutuambia ukweli, 
hatukuwa na utaratibu mzuri wa kuambiwa mawazo ya wanajeshi wetu wenyewe”.
Pamoja na hayo,Oscar Kambona analaumiwa kwa uzembe, na, kwa maelezo ya aliyekuwa 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (1962-63), Abbas Sykes kwa mwandishi wa makala haya 
siku za nyuma, “Kambona alipelekewa malalamiko mengi; lakini kwa uzembe wake yakawa 
yanajazana tu kwenye trei lake la kuingia; na kila wakati unamwona ana maharakati ya 
kwenda huku na huko ….. ikatuletea kitimtim kidogo, wanajeshi wakaasi”.
Kila ovu lina baraka zake na ubaya wake
Baada ya maasi ya wanajeshi hao, waliojiita “Jeshi la Wapigania Uhuru wa Usiku”, 
Mwalimu alikifuta kikosi chote cha kwanza na kuwafukuza kazi askari 100 wa kikosi cha pili 
walioasi Tabora. Alifukuza pia asilimia 10 ya polisi 5,000 kwa kushindwa kudhibiti maasi.  
Nalo Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TFL) lilifutwa, badala yake ukaundwa 
Muungano wa Wafanyakazi nchini – “National Union of Tanganyika Workers” (NUTA) kama 
Jumuiya ya Chama tawala, TANU.Mwanzoni mwa Aprili, 1964, majeshi ya Uingereza yaliondoka 
na nafasi yake kuchukuliwa na kikosi cha tatu cha jeshi la Nigeria, chini ya Luteni James Pam, 
na  Mwalimu akamteua Kapteni Mirisho Sarakikya, kuwa Mkuu mpya wa Jeshi kwa cheo cha 
Bregedia.Watu zaidi ya 400, wakiwamo viongozi wa vyama vya wafanyakazi, 
walikamatwa na kuhojiwa, na wengine 500 kutiwa nguvuni chini ya sheria ya kuzuia hali ya 
hatari, lakini wengi waliachiwa.  Sajini Ilogi alipatikana na hatia na kufungwa miaka 15 pamoja 
na washirika wake wakuu 13, waliofungwa kati ya miaka mitano na 10.
Maasi hayo, kwa kufufua zoezi la Afrikanaizesheni, japo kwa kasi ndogo  kuliko mwanzo, 
yaliipa sekta ya Utumishi serikalini watendaji dhaifu, hohe hahe kwa misingi ya siasa, 
wasiojua lolote kuhusu usimamizi wa Serikali na hivyo kuharibu kabisa taswira ya utumishi 
makini, tija, ufanisi, maadili na uadilifu kazini, hali ambayo imeendelea hadi leo.
“Tulikuwa tumeingia katika shughuli ambazo tulikuwa hatuzijui, nasi tukakubali tu mradi 
bora liende lakini tuko huru”, anakiri Balozi Abbas Sykes.Ni ukweli usiopingika kwamba, 
bila kuongozwa kwa misingi ya maadili ya kiutumishi na uadilifu chini ya sekta imara ya 
utumishi wa umma, Serikali itapwaya kama inavyopwaya sasa, na hivyo nchi kuongozwa 
kisiasa na kwa wanasiasa walafi kushika hatamu za utendaji.Lakini kila ovu lina baraka zake:  
Serikali ilinywea na kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa wanajeshi, 
kutoka 105/= hadi 240/= kwa mwezi. Lakini muhimu kuliko yote ni kwamba, 
maasi hayo yalitusaidia kujihoji juu ya aina ya jeshi lililotakiwa kwa nchi kama yetu; 
tukaweza kulijenga upya, tukapata “Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania”
JWTZ na kwa ajili ya Watanzania. Septemba 1964, vijana wa “TANU Youth League” TYL, 
waliokuwa wakichukua mafunzo ya kijeshi, walifuzu na kuunda vikosi vya kwanza vya JWTZ 
na kuhitimisha safari ya jeshi letu kutoka KAR, TR hadi JWTZ.





No comments:

Post a Comment