JUMUIYA YA ULAYA (EU) KUPUNGUZA MCHANGO WAKE WA JUMLA YA EURO MILLIONI 800 KATIKA BAJETI YA NCHI YA TANGANYIKA ((TANZANIA)) MWAKA HUU SMZ KUPUNGUZA WAFANYAKAZI. NA KUFUTA MIKATABA YA WALIONGEZEWA MUDA BAADA YA KUFIKIA UMRI WA KUSTAAFU
Baada ya kusuasua kwa uchumi wa nchi ya Tanganyika ((Tanzania)) na kupanda kwa kiwango wa ubadilishajiwa fedha za kigeni, bajeti ya nchi ya Tanganyika ((Tanzania) na hususan ya nchi ya Zanzibar itaathika kwa kiasi kikubwa na hasa baada ya wahisani kuondoka msaada wa kibajeti. Habari kutoka ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zinasema serikali imeanza kufikiria njia mbadala kukabiliana na mikosi hii ni pamoja na kupunguza wafanyakazi wa serikali wa kada mbali mbali na ikiwa ni pamoja na kufuta mikataba ya wale waliongezewa hali ya kuwa walishafika umri wa kustaafu hususan maafisa wa ngazi ya juu serikalini, imeelezwa makatibu wakuu wengi wameshafikia umri wa kustaafu lakini serikali imewaongezea muda wa miaka miwili na kuigharimu serikali mamilioni kila mwaka wakila pesa za bure na kuzui nafasi hizo kuchukuliwa na vijana guvu kazi mizee ikiwa bado ipo ipo tu. Pamoja na serikali kuazimia kupunguza wafanyakazi wakati huo huo inakabiliwa na kikwazo chengine, haina fedha za kuwalipa wale ambao wataondolewa kazini bila ya kufikia umri wa kustaafu ambapo mafao yao hayatalipwa hadi wafikie umri wa kustaafu, hivyo SMZ italazimika kuwafidia na haina fedha hizo.
Njia nyengine ilioelezwa ni kwa Shein kuzungumza na CUF kuona ni jinsi gani wataweza kushiriki katika serikali shirikishi na hivyo kubadili msimamo wa wafadhili wa kibajeti jambo ambalo pia lina utata kufikia makubaliano baada ya serikali kuendesha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi 2016 na baraza la wawakilishi kuapishwa. Karata ya mwisho kwa SMZ na Shein yeye kujiuzulu na kuvunja baraza la wawakilishi ambalo hali uhalali wowote wala faida yoyote halina hata mwezi ili kuitisha uchaguzi mpya, lakini pia katika hili serikali inakabiliwa na mtihani mwengine haina fedha za kugharamia uchaguzi upya kuanzia uandikishaji wapiga kura hadi kupiga kura ila suali linakuja walizipata wapi pesa za kufanyia uchaguzi wao wa pili wa kiwizi wizi.....?? Baadhi ya nchi wafadhili wameonyesha nia ya kugharamia uchaguzi mpya lakini kwa masharti maalum ikiwa ni pamoja na Tume huru kusimamia uchaguzi huo itakayoshirika wawakilishi wa nchi wahisani na mashirika ya kimataifa, aidha uchaguzi uwe wa wazi na shirikishi, na katika hali hiyo CCM itakuwa na nafasi ndogo sana ya kushinda uchaguzi hasa baada ya kukimbiwa na wapiga kura wengi vijana na hata wazee walio kata tama kabisa baada ya miaka 50 na ushaeya kuna hakuna liwalo zaidi ya kudanganywa mwaka hadi mwaka, na CCM haiwezi kushinda kwa idadi ya wanachama wake pekee inahitaji wapiga kura wasio na mrengu ambayo wengi ni vijana ambao hawana ajira.
No comments:
Post a Comment