Friday, January 24, 2014

NCHI YA ZANZIBAR HAITAMBULIKI KATIKA UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI EAC IMO NDANI YA TUMBO LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.


SERIKALI ya Wauwaji (Mapinduzi) ya Zanzibar imesema kuwa msimamo wake katika suala la uwanachama wa  Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni ule ule uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakoloni weusi Tanganyika.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt Mwinyihaji Makame Mwadini aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kilichoanza jana huko Chukwani nje kidogo na Mjini Magharib wa nchi ya  Zanzibar.
Akijibu suali la mwakilishi wa nafasi za wanawake (CCM) Mgeni Hassan Juma, Waziri huyo alisema kuwa nchi ya  Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Mungano na nchi ya Tanganyika msimamo wake katika suala hilo ni ule ule wa Tanganyika  uliotolewa na Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika.
“Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika tayari imeshatowa msimamo wake kuhusu mambo yaliyojitokeza hivi karibuni juu ya uwanachama wake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, msimamo ambao ulitolewa na Rais Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika katika hotuba yake aliyoitowa katika bunge la nchi yao mjini Dodoma Nchini Tanganyika ((Giningi ya kuuliwa na kufukuzwa viongozi wa nchi ya Zanzabar wasio tii amri ya MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA)) Novemba 7 mwaka jana hivyo sisi nchi ya Zanzibar hatuwezi kwenda kinyume chake”, alisema Waziri.((Wazanzibari mnasiki kama sio ukoloni ni nini..?))
Alisema kuwa katika msimamo huo Rais Jakaya Raisi wa nchi ya Tanganyika alisisitiza kuwa Jamhuri ya Tanganyika haijajitowa na wala haina lengo na kujitowa katika mtangamano wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo mambo yaliojitokeza yatamalizwa kwa njia ya kidiplomasia.
Mwakilishi huyo alitaka kujua Wazanzibari na nchi yao ya Zanzibar wanaelezwa nini kuhusiana na suala zima la Afrika Mashariki ambapo hivi karibuni kumekuwepo na hisia kuwa uwanachama wa nchi ya Tanganyika katika Jumuiya hiyo unayumba na kuwa kumeshakuwa na mikutano mbali mbali inayohusisha wanachama wake wa EAC ikiendelea wakati nchi ya Tanganyika haihusishwi  na kwa kuwa nchi ya Zanzibar inaingia katika Jumuiya hiyo  chini ya kivuli cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.
Aidha alitaka kujuwa iwapo nchi ya Tanganyika itajitowa  kwenye Umoja huo nchi Zanzibar itakuwa na nafasi gani katika kutoa ushauri na katika kuendeleza malengo na dhamira ya umoja huo wakati nchi ya Zanzibar haitambuliki katima umoja huwo imefichwa ndani ya tumbo la MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

No comments:

Post a Comment