UKIALIKWA IKULU YA NCHI YA ZANZIBAR USICHUKUWE SIMU YAKO,WALETE YAKO YA PESA WALA USIVUWE SUTI YAKO NA VIATU VYAKO MIGUUNI VIANGALIYE KILA UKIPIGA TOGE NYAMA VIANGALIYE AU UKINYWA MAJI ILI UJUWE KAMA BADO VIPO MIGUNI MWAKO AU USHAVULIWA BILA YA KUJUWA
SHEREHE za maadhimisho ya miaka 50 ya Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi), zimekuwa chungu na kujuta kwa nini amekubali kuja katika hafla hiyo kwa balozi mmoja wa nchi za kigeni (jina kapuni) nchini hapa Zanzibar, baada ya kuibiwa simu yake ya mkononi yenye thamani ya zaidi ya sh milioni moja.
Habari ambazo Muandishi wetu wa FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA aliyekuwa ndani ya IKULU NCHINI ZANZIBAR alishuhudia balozi huyo akihaha kuitafuta simu hiyo bila ya mafanikio ndipo alipo juwa kuwa simu hiyo itakuwa imeibiwa kiswahili cha mtaa imekwenda na maji katika mazingira ya kutatanisha wakati wa dhifa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Ikulu ya nchi ya Zanzibar, na Ali Mohammed Shein.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya dhifa hiyo iliyohudhuriwa na watu maalumu, akiwemo Rais Jakaya Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika, balozi huyo alijikuta simu yake imekwenda na maji-imeibiwa baada ya kuangali simu hiyo aliyokuwa ameweka kando ya meza aliyoketi na maofisa wa Ikulu na wageni wengine waalikwa kuwa haipo tena.
Hadi sasa haijulikani nani aliondoka na simu hiyo, lakini habari zaidi kutoka kwenye dhifa hiyo zinasema kuwa huenda simu hiyo ilichukuliwa na watu wa Idara ya Usalama kwa ajili ya mambo ya usalama....!!!! je ni nani hao Idara ya Usalama kama sio Tanganyika na kwa nini waichukuwe simu ya Balozi huyu tu....?
Mmoja wa maofisa wa Ikulu ya nchi ya Zanzibar ambaye aliomba jina lake lisitajwe, alikiri kumuambiya Muandishi wetu kuwa hakuna lolote hiyo simu ya balozi ni kweli aliibiwa simu yake na hadi anaondoka kwenye dhifa hiyo hakuweza kuipata simu yake tena pia alisema umeona Mitanganyika iliyo jaa hapa kweli kutakuwa na salama kama sio wizi.alihoji
“Ni tukio la aibu sana tena sana kwa nchi yetu ya Zanzibar, lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba simu hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama,” alisema mtoa habari moja kujaribu kuficha aibu hii.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadamu Khamis Mkadamu, alisema kuwa hana taarifa za tukio hilo.
Alisema yeye alikuwa mtu wa mwisho kutoka kwenye hafla hiyo, hivyo hakukuwa na tukio hilo.
Alipobanwa zaidi, kamanda huyo alisema kama tukio hilo lipo, kuna uwezekano mkubwa wa simu hiyo kudondoka kwa bahati mbaya, lakini haiwezekani na si sahihi kusema imeibwa.
“Ile ilikuwa hafla maalumu, kwa watu maalumu, na walioalikwa ni watu wenye hadhi na heshima zao katika taifa hili. Hakuna mtu wa mtaani aliyeingia.(haya ndio matusi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadamu Khamis Mkadamu kuwa watu wote wa mtaani ndio wezi sio wewe kabla ya kuwa Kamanda ulikuwa umezaliwa ikulu ya marekani..?
Wewe pia umezaliwa mtaani kama sisi..? kama ni mtaani kama sisi basi mkadamu wewe pia ni mwizi na si hasha wewe ndio uleye ibaa hiyo simu ndio maana ukatoka mwisho.) Katika kundi lile sioni mtu wa kuiba simu, wote ni watu wazima, wenye heshima na nyadhifa kubwa ndani na nje ya nchi. aliendelea kusema Mkadamu. (Mkadamu mtaani hakuna watu wazima..? wenye hishim..? na busara ni ikulu tu....?)
“Mimi mwenyewe juzi niliangusha kadi yangu, niliitafuta sana lakini siku moja dereva wangu wakati anafanya usafi wa gari aliiona. Kwa hiyo simu hiyo haiwezi kuibwa, ila anaweza kuwa ameidondosha au ameiweka sehemu ambayo hakuweza kuiona kwa wakati ule,” alisema kamanda huyo.
No comments:
Post a Comment