Thursday, January 9, 2014

ABDALLA KASSIM HANGA MZANZIBARI ALIYE KUWA MSTARI WA MBELE NA KUMRISHA MAUWAJI YA WAZANZIBARI WENZAKE KWA UCHU WAKUTAKA MADARAKA


Abdalla Kassim Hanga
Kuwa Hanga ndiye aliyekuwa kinara wa (Mapinduzi) Mauwaji ya Wazanzibari hili si jambo lenye utata tena katika miaka hii japo kuwa yalikuwa yamefichwa haya na serekali ya Zanzibar yasijulikana unyama na mauwaji yao hao wanaojita Mapinduzi walivyo wafanya Waznzibari wenzao wakishirikiana na mkoloni mweusi Tanganyika kuwachinja na kuwanajisi wanawake wa nchi yao ya Zanzibar. Ikiwa hivyo ndivyo Hanga hatoweza kuutua mzigo wa roho zilizopotea katika (mapinduzi) Mauwaji ya Wazanzibari hao. Ikiwa Hanga atalaumiwa kwa vifo vya maelfu ya Wazanzibari nani alaumiwe kwa umauti uliomfika Hanga tena kwa kuuliwa kishenzi kwani hapana neno zaidi ya hilo linaloweza kutosheleza kuelezea jinsi Hanga alivyouliwa. Kichekesho kikubwa ni kuwa wale waliopoteza roho kwa hiyo kutangulia mbele ya haki, yao yalikuwa yamekwisha. Lakini kwa wale wajane na mayatima waliobakia nyuma wakihangaika, kifo cha Hanga na wenzake katika wale waliofanikisha Mauwaji ya Wazanzibari (mapinduzi) kuuliwa kwao kulikuwa miujiza ya aina yake, Maana wao ndio waliopanga Mauwaji ya Wazanzibari (mapinduzi) kisha yalipo kamilika tu na wao wakaanza kuliwa. uchawi usioelezeka nani fundi wake. Ilikuwa vigumu kueleza. Ingeeleweka vyema endapo kisasi cha kuitoa roho ya Hanga kingetimizwa kutoka katika mikono ya wanao itwa maadui zake waliopinduliwa. Haikuwa hivyo.
Wale wajane na mayatima walililipiziwa kisasi na watu waliokuwa maadui wakubwa wa waume na baba zao waliopinduliwa. Vipi Hanga kiongozi mkuu wa Mauwaji ya Waznzibari (mapinduzi) aje kuwa adui wa mapinduzi yenyewe kiasi cha kuwa hukumu ya kumtosheleza haikuwa isipokuwa kifo tu...? nasio kifo tu cha kawaida bali kifo cha kishenzi. Fikra ya Hanga ilikuwaje alipokuwa peke yake ndani ya selo Ukonga Prison nchini Tanganyika…usiku ukimpita bila ya hata lepe la usingizi akiwaza yanayomkabili. Nini kilikuwa kikipitika katika ubongo wake wakati wauaji wake walipomtoa katika selo yake na yeye akawakabili ilhali aikijua kuwa walikuwa wamekuja kuitoa roho yake....? Fikra yake ilikwenda wapi...?? Ilikwenda kwa Sultan Jamshid bin Abdullah aliyempindua na kwa Masultani wengi waliopita ambao wameiaga dunia mikono yao ikiwa haina damu au kwa Abeid Amani Karume aliyeingia madarakani kwa mapanga ya Wamakonde kutoka nchini Tanganyika...????, wakata mkonge kutoka nchi ya Tanganyika wakifanya kazi mashamba ya Sakura na Kipumbwi....?? Fikra ya Hanga ilielekea wapi.....? Kwa Nyerere aliyemsaliti......?
Hakika ni wazi hakutegemea Mauwaji ya Waznzibari (mapinduzi) aliyoyaasisi yangemgeukia na kuwa sababu ya yeye kutolewa roho kwa kuuliwa kishenzi. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi pale alipokamatwa na kuwekwa jela Ukonga nchini Tanganyika na kufikishwa mbele ya mkutano wa hadhara na kuadhiriwa na Julius Nyerere tayari alikuwa keshapoteza kila kitu achilia mbali dira ya Mauwaji ya Wazanzibari (mapinduzi) aliyokusudia ingeongoza nchi ya Zanzibar Baada ya kuwauwa Wazanzibari. Hanga hakuwa kamwe na uwezo wa kumfanya Karume lolote kwani Karume tayari alikuwa chini ya mbawa za Nyerere ngome ambayo Hanga asingeweza kuitikisa achalia mbali kuibomoa. Muungano feki baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa hirizi tosha ya kumkinga Karume kwa mbinu au marifa yoyote ambayo Hanga alikuwa nayo kichwani mwake kutaka kumuondowa karume na yeye ndiye awe raisi au kiongozi wa nchi ya Zanzibar kama alivyokuwa kiongozi wa kuongoza Mauwaji ya Waznzibari (mapinduzi.)
Katika mkasa wa kuuliwa kwa Hanga ndipo msemaji mmoja akasema, “Maiti toka makaburini mwao walionyesha ujuzi wa kufanya miujiza na uchawi wao kwani laiti kifo cha Hanga kingesababishwa na wale waliopinduliwa kisasi chake kingekuwa cha kutisha. Ilibidi Hanga kwa miujiza ya maiti zile auliwe na wale wale aliowaweka madarakani watu ambao hapakuwepo na sababu ya wao kumuona adui au kumuuwa maana yeye Hanga ndio aliyewaweka madarakani sasa vipi wamuuwe. Halikudondoka chozi kwa kifo cha Hanga. Kila aliyepata mnong’ono wa kuuliwa kwake alikuwa kimya kama vile ile taarifa ile ya kifo haimuhusu na mpaka leo kaburi la Hanga  halijulikani lilipo.

No comments:

Post a Comment