Mheshimiwa Wageni wetu, Wakuu wa Nchi na Serikali na
Mawaziri wa Nchi Rafiki mliohudhuria hapa leo,
Mawaziri wa Nchi Rafiki mliohudhuria hapa leo,
Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dk. Mohamed Gharib Bilal,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad,
Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar;
Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi,
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar;
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar;
Mheshimiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi,
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa,
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dk. Salmin Amour Juma,
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Dk. Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Viongozi Wakuu Wastaafu Mliohudhuria;
Waheshimiwa Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
Mheshimiwa Mama Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
Mheshimiwa Othman Chande Mohamed, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;
Mheshimiwa Abdalla Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi;
Waheshimiwa Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa;
Ndugu Wananchi, Mabibi na Mabwana;
Assalaam Alaykum,
Kwa unyenyekevu mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, kwa kutujaalia uhai na uzima wa afya, tukaweza kukusanyika hapa leo kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ya tarehe 12 Januari, 1964. Namuomba Mola wetu aibariki shughuli yetu hii iwe ya mafanikio.
Kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar, natoa shukrani zangu za dhati kwako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuungana nasi katika sherehe zetu hizi adhimu na muhimu. Vile vile natoa shukrani kwa wageni wetu wote kutoka nje ya nchi yetu akiwemo Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Dk. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Comoro, na Mjumbe Maalum, Waziri wa Makaazi na Maendeleo Miji na Vijiji Mheshimiwa Jiang Weixin anayemwakilisha Rais Xi Jinping wa Jamhuri ya Watu wa China. Kadhalika, natoa shukrani kwa viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, waliopo madarakani na waliostaafu, Mabalozi wa nchi mbali mbali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa dini na vyama vya siasa na wananchi wote kwa kuhudhuria kwa wingi kwenye sherehe hizi.
Kuwepo pamoja nasi wageni wetu mbali mbali kunatupa faraja kubwa sana. Kuja kwenu kunatudhihirishia kuwa Mapinduzi yetu yanaheshimika na yanapewa taadhima kubwa ndani na nje ya nchi yetu. Tuna kila sababu ya kujivunia uhusiano wetu na kuja kwenu ni uthibitisho wa juhudi zetu za pamoja za kuyaenzi Mapinduzi yetu.

Waheshimiwa Viongozi na Ndugu Wananchi,
Leo ni siku muhimu sana katika historia ya wananchi wa Zanzibar, ambapo miaka 50 iliyopita walikata minyororo ya utawala wa Kisultani na ukoloni wa Kiingereza uliodumu kwa miaka 132. Wananchi walikataa kwa vitendo kudharauliwa, kunyanyaswa, kubaguliwa na kutoheshimiwa katika nchi yao.

Ukombozi wa watu wa Zanzibar ulifanywa na Chama cha Afro-Shirazi, ambacho kilianzishwa tarehe 5 Februari, 1957, kwa madhumuni ya kuikomboa Zanzibar kutokana na madhila ya wakoloni, mabwanyenye na mabepari. Madhila haya walitendewa wananchi kwenye mambo yote muhimu katika maisha ya binadamu, kama vile kubaguliwa katika kupata elimu, huduma za matibabu, makaazi, chakula, ubaguzi kwenye kazi, ubaguzi na dhulma kwenye matumizi ya ardhi, ubaguzi katika kupata haki, na kadhalika.
1)unasema kubaguliwa je huu upemba na unguja au wale mahizbu sisi wakulima na wakwezi mbona upo mpaka leo au huu sio ubaguzi...?
2)unasema kubaguliwa katika elimu hapa hapa zanzibar watu wangapi wamefelishwa tu kwa kuwa hakuna jina la kombo,jecha,pandu,kificho,nahodha kama mtu hana jina hilo mwanzo au mwisho munamfelisha je sio ubaguzi huo wa elimu isitoshe hao wakoloni weusi tanganyika washawafelisha dungu zetu wangapi sio ubaguzi huo..?
3)unasema huduma za matibabu ikulu yako iko ubavuni mwa hospitali kubwa hapa zanzibar na unasikia au unasoma kila siku habari kuwa hakuna madawa hakuna vitanda manasi na madaktari wajeuri kupita kiasi kwa wangojwa hakuna hata chumba cha kujifunguwa wanawake wazazi sasa huo ukombozi wenu wakuwapa watu huduma ya matibabu uko wapi..? au kuwa na lili jengo tu ndio matibabu yenu...?
4)unasema makazi kweli kweli wewe kampeni zako zote umefanya vijijini hivi hukuona vibanda vya udongo wanavyo ishi watu toka uingiye madarakani ni miaka mitano inakatika umewajengea nyumba ngapi za kuishi...?
5)unasema chakula muliwandanganya watu mabembe basi mbona mpaka leo mabembe ndio namba moja isitoshe mumewatia wazanzibari ufakiri mpaka wanakula futari ramadhani ugali ugali nchi hii walikuwa watu hawali ugali watu waliokuwa wakila ugali na wanyamwezi na wamakonde na wazaramo wanaokuja kuchuma kaarafu siku za msimu wa karafu ndio watu wanawaona wanakula ugali leo hii zanzibar watu wanafutari ugali ndio maendeleo hayo..?
6)unasema ubaguzi katika kazi nyinyi mpaka leo kama sio mwana maskani hupati kazi je huo sio ubaguzi..? watu wamefukuzwa makazi kisa ni wapemba au wamejiunga na chama cha cuf je sio ubaguzi huo..?
7)unasema ubaguzi na dhulma kwenye matumizi ya ardhi daaah shein weee shein weee nyinyi muliwanyanganya watu mashamba yao 1964 kisha mukayakata heka tatu tatu kuwapa watu sawa sasa kila waziri katika baraza la wawakilishi ana heka karibu 60 kazitowa wapi..? wamewanyanganya hao masikini walio pewa na heka tatu tatu na kujiribikia wao na wake zao na watoto wao mumeuza visiwa vidogo vidogo vyote na fukwe za bahari wewe mwenyewe umeuza nyumba ngapi za shangani kisha ukawambia wazanzibari mtu halaumiwi kuza chake au sio wewe shein..?
8)unasema ubaguzi katika kupata haki, na kadhalika ni wazanzibari wangapi hawapati kitambulisho mpaka sasa..? ni wazanzibari wangapi hawapati paspoti mpaka sasa je sio haki yao..? waznzibari wangapi wamefanyiwa ukiritimbwa wasiende kusoma nje na nafasi wanapewa watoto wa mawaziri nakadhali.
Shein
Kwa research yako uliyoifanya na kujenga hoja maendeleo yaliopatikana kwa miaka 50 iliyopita. Juu ya kuwa kuna counter arguments nyingi za kitaalamu kuhusu uliyoyasema, lakini tu nakuomba ufanye research nyengine ili ututhibitishie kauli yako ifuatayo:
“Hatutokubali kutawaliwa, kudhulumiwa, kubaguliwa na kudharauliwa katika nchi yetu.”
1 Kweli wananchi (Wazanzibari) wanaamini hivyo kuwa hawatawaliwi,kudhulumiwa,kubaguliwa na kudharauliwa katika nchi yao kwa wanamini hayo.....?
2 Ni kweli hatutawaliwi tena...? Maamuzi makubwa ya nchi yetu ya Zanzibar pamoja na kumteua au hata kumfukuza Rais wa nchi yanafanyika wapi pale kisonge au kisiwa nduwi...?
3 Ni kweli hatudhulumiwi tena.....? Hizo KERO ZA MUUNGANO za nini basi......?
4 Ni kweli hatubaguliwi tena......? Huu upemba na Unguja au uarabu na uafrika ni kutukana......?
5 Ni kweli hatudharauliwi tena.....? Mbali ya mifano iliyopo chungu nzima, wa juzi ya kijomba Warioba kakubali kuwa 60% ya Wazanzibari wametaka MUUNGANO WA MKATABA, fikra hizo zimehishimiwa kiasi gani......?

Ikiwa moja kati ya masuala hayo matano yatathibiti kuwa si kweli basi kauli yako “HATUTOKUBALI” tueleze wewe kama ni kiongozi wetu umefanya nini na utafanya nini kutuyakinishia kuwa:
“Hatutokubali kutawaliwa, kudhulumiwa, kubaguliwa na kudharauliwa katika nchi yetu.”? kama si hivyo heshima yako kwa wananchi wako iko hatarini kuvunjika
No comments:
Post a Comment