Makamo wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad, akimfariji Muhafidhina Naibu Katibu Mkuu wa CCM nchini Zanzibar Vuai Ali Vuai alipofika katika kijiji cha pongwe kuhudhuria maziko hayo pembeni ni Abu Jahal Borafya Jahal la Kizanzibari.
UKIFUNGUA wavuti ya google.co.tz kwenye intaneti na kuandika “Vuai Ali Vuai,” halafu ukabonyeza kitufe cha kutafuta, zitakuja taarifa zinazomhusu mtu mwenye jina hilo.
Vuai Ali Vuai ni mwanasiasa wa miaka ya kati ambaye kwa sasa anashika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha (Mapinduzi) Wauwaji wa Wazanzibari (CCM) upande wa Zanzibar.
Lakini ukishafungua na ukaangalia eneo lenye picha zake huyu mwenye asili ya kijiji cha Pongwe, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, picha ya pili utakayoiona, baada ya ile aliyopigwa akiwa amevalia shati ya rangi kijani, ya CCM, inamuonesha Vuai akisalimiana kwa kupeana mikono na Maalim Seif Shariff Hamad kama unavyo iona hapo juu.
Picha hii imepigwa kijijini kwao tarehe 5 Novemba mwaka 2013, siku ya maziko ya baba yake mzazi, Mzee Ali Vuai. Hiyo ina maana Maalim Seif, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), na Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, alikuwa mmoja wa viongozi wa kitaifa waliohudhuria maziko ya baba yake Vuai, kijijini Pongwe Pwani.
Katika picha hii, unamuona Vuai anaitika mkono wa salamu kwa Maalim Seif kwa moyo mkunjufu kabisa, roho tulivu (roho kwatu), na usoni kwake akijenga sura yenye tabasamu kubwa. Pamoja na ukweli kwamba ile kwake ilikuwa siku ya msiba mkubwa, kwa kuondokewa na mmoja wa wazazi wake, Vuai anaonesha kama vile ni mtu aliyekutana na mtu anayemheshimu sana.
Katika hali ya kawaida, huwezi kusema kama Vuai atakuwa na shaka katika kiwango cha kumheshimu Maalim Seif. Hampati kwa umri. Hampati kwa ujuzi, uzoefu na ufundi katika siasa. Hampati hata kwa umbo. Maalim ni mrefu kwa kimo na mng’avu kwa rangi kuliko alivyo Vuai.
Vuai kwa Maalim Seif kwa mambo mengi ni kama unapozungumzia kichuguu na mlima Kilimanjaro. Vitu viwili tofauti. Vuai ni wa daraja dogo mno kwa hali hizo akilinganishwa na Maalim Seif.
Lakini amekuwa akijitokeza kama mtu anayejua sana kila jambo mbele ya Maalim Seif. Ukunjufu wa moyo aliouonesha alipokuwa akishikana mkono na Maalim Seif siku ya msiba wa baba yake kijijini Pongwe Pwani, huwezi kuupata kamwe unapomkuta akimtaja Maalim Seif kwenye medani ya siasa.
Nathubutu kusema Vuai anamuona Maalim Seif adui mkubwa. Kwa hali hiyo, pengine Vuai wala hakutarajia kuwa anayesalimiana naye mazikoni ni, Maalim Seif, angethubutu kufika Pongwe Pwani kwa lengo la kuhudhuria maziko ya baba yake.
Isitoshe, picha ya Vuai na Maalim Seif iliyopigwa kutoka kwenye uwanja wa maziko siku hiyo, kwenye mtandao huo wa google, imetangulia picha aliyopiga Vuai siku hiyohiyo na kiongozi mkubwa wa chama chake – CCM, Ali Mohamed Shein.
Hii inawezekana isiwe na maana yoyote kwani bila ya shaka kihadhi katika jamii, Shein ni raisi wa Kisonge na Maalim Seif ni Makamu wa Raisi wa nchi ya Zanzibar.
Kama kuhusu hadhi nyengine, poo simo; wewe msomaji utaamua mwenyewe.
Uadui aliouweka Vuai dhidi ya Maalim Seif si wa kutafuta kwa tochi. Ukimsikia Vuai akizungumza mchana kweupe, hafichi chuki yake kwa kiongozi huyo msikivu na ambaye Wazanzibari wamempa imani kubwa.
Nataka kuamini kuwa kwa Vuai, ni haramu kukamilisha hutuba yake popote anapokuwa katika medani ya siasa, bila ya kumtaja Maalim Seif. Hata pasiwe na sababu, ataitafuta tu, almuradi ataje jina la Seif Shariff Hamad.
Kwa kuwa hata waandishi wanaomtii Vuai wanalijua hili, hata asipomtaja kwa jina kamili, vikaragosi wake watalitaja tu.
Mwenendo huu inawezekana umewaambukiza viongozi wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UV-CCM), ambao nao ni kama vile wameapa kuishi na jina la Maalim Seif, iwe usiku iwe mchana, iwe jua iwe mvua.
Ni nani hajawahi kusikia viongozi wa UV-CCM kama Shaka Hamdu Shaka na Sadifa Juma wakimsema ovyo Maalim Seif majukwaani..? Tena mara kadhaa maneno ya vituku na vilembwe wa CCM hawa wanapomtaja Maalim Seif huwa ni makali yanayochoma moyo na kuumiza mapafu kwa anayeyasikia lakini nathani wao wanaumiya zaidi kwa kumuona Maalim Seif ndio maana hurupoka ili kupunguza maumivu walio nayo kumbe hawajuwi ndio wanazidisha maumivu ndani ya mili yao.
Wazanzibari wameyazoea sana maneno ya wajuku na vilimbwe wa CCM dhidi ya Maalim Seif. Wamekuwa wakiyachukulia kama upuuzi mtupu kwa sababu huwa mara nyingi yamekosa heshima na haya malengo wala faida yoyote kwa nchi ya Zanzibar na hata kwa Wazanzibari wenyewe pia.
Ni maneno yasiyo na maana. Ni kama yamesemwa na mtu aliyeuchapa ulevi usiku kuchaa kisha siku ya pili akakurupuka na kuhubiria watu nini unatarajia katika hutaba hiyoo..? jibu nalo wewe msomaji.
Lakini wakati sina uthibitisho kama viongozi hao wa UV-CCM huwa wanalewa kabla ya kupanda jukwaani na kuanza kumtusi Maalim Seif, inajulikana wanatema maneno yanayoashiria matusi ya nguoni kama mashangingi au majimama yanayo imbaa nyimbo za mipasho.
Vuai yeye hamtukani Maalim Seif. Sijawahi hata mara moja kusikia akimtukana. Hatoi matusi kwa maana ile ya wanavyofanya wasaidizi wake hao wa UV-CCM. Lakini kauli zake naye zinaonesha sura yake halisi Vuai kisiasa na kiumantiki.
Mwanasiasa anayechoka na asiyejitambua.
Wakati kauli za wenzake huashiria matusi ya nguoni, Vuai zake ni za kebehi na upotoshaji wa mambo. Kauli za Vuai wakati mwingine zinawataka wananchi kuamini jambo lisilokuwepo, ingawa kwake labda huwa ndio jitihada za kumbomoa Maalim Seif.
Tatizo hapa, Vuai hajajua namna ya kumbomoa kisiasa Maalim Seif. Hajapata maneno ya kutumia kumbomoa kiongozi huyu. Badala yake, anapodhani anambomoa, kwa hakika huwa anamjenga au anazindi kumjengea taswira nzuri kwa rai au wananchi wa Zanzibar.
Wiki kadhaa nyuma, Vuai aliwahi kusema Maalim Seif ni msaliti wa Wazanzibari kwa kuwashawishi wavunje Muungano wa nchi ya Tanganyika na nchi yetu ya Zanzibar.
Kwamba Vuai anasema, Maalim Seif amewalaghai Wazanzibari kuwa chini ya mfumo wa Muungano wa Serikali Tatu ndio watapata mamlaka.
Kama ninakosea, ingia ujikumbushe utakapofungua mtandao ule wa jina la Vuai Ali Vuai, ukute habari inayoeleza dhana hii.
Wakati fulani Vuai aliwahi kumtuhumu Maalim Seif kuunga mkono viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI).
Kauli yake ilikuwa inajenga imani watu kwamba Maalim Seif anapalilia au kushadidia vurugu zilizokuwa zikitokea Zanzibar na CCM kutuhumu kuwa zikifanywa na Uamsho.
Vuai alikuwa anasema isingekuwa hivyo, Maalim Seif angekuwa amekanusha na kukemea viongozi wa Uamsho ambao yeye na wakubwa zake yumkini humshutumu kuwa anawasaidia katika harakati zao za kutetea haki za Wazanzibari, ambazo wao kina Vuai, wanasema ni kuvunja amani.
Vuai anamaanisha kuwa Maalim Seif akiwapa nguvu Uamsho wafanye vurugu. Vuai anajua fika kwamba hakuna hata mara moja viongozi wa Uamsho wamethibitishwa kuhusika na vurugu.
Hakuna mpaka leo hii. Wanachoendelea kukiamini kina Vuai ni propaganda yao ya kuwachafua viongozi wa Uamsho ambao wanaamini kwa kazi waliyoifanya, wamefanikiwa kuwaamsha Wazanzibari kwa kiwango cha kupigiwa mfano katika kuhimiza kutambua na kudai haki zao.
Sasa safari hii, Vuai, akiwa jukwaani tena kupokea walichoita wenyewe matembezi ya vijana wa CCM, anasema kwa njia ya kuwakampeni Wazanzibari, wasimchague Maalim Seif. Anasema hachaguliki.
Vuai anajua wazi hakuna uchaguzi kwa sasa. Kwa Zanzibar, hakuna kabisa uchaguzi ambao unahusisha ushiriki wa Maalim Seif. Kilichopo ni kampeni za uchaguzi mdogo wa kuwania kiti cha ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, jimbo la Kiembesamaki, Wilaya ya Mjini Unguja nchini Zanzibar.
Kiti hicho kimekuwa wazi tangu mwakilishi wake, Mansour Yussuf Himid alipokosa sifa za kuwa mwakilishi katika chama cha CCM na baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM kutokana na tuhuma za kusaliti chama kama wanavyosema wenyewe CCM.
Kwa nchi ya Tanganyika, kuna uchaguzi wa serikali za mitaa. Kama ni ushiriki, basi Maalim Seif atakuwa anashiriki kupigia kampeni wale walioomba kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo kupitia CUF.
Sasa kama sote tunakubaliana kwamba kwa sasa hakuna uchaguzi wowote unaomhusisha mwanasiasa anayeitwa Maalim Seif Shariff Hamad, Vuai anataka watu wasimchague kwa uchaguzi upi...? Kuna kinyang’anyiro gani kinachofanyika na ambacho ameingia kugombea..?
Hakuna uchaguzi. Hakuna uwaniaji wowote kwa sasa. Lakini Vuai si mpumbavu. Ana akili. Tena, anajua anachokifanya. Na hicho anachokifanya, anajua kuwa ni cha haramu na dhulma kwa Maalim Seif. Kumchafua.
Anafanya hivyo kwasababu ya ukweli kwamba Vuai ni mwanasiasa anayechoka kwa kasi wakati Maalim Seif anazidi kung’ara na kuaminiwa. Vuai hataki kufikiri kwa akili yake. Kama anaitumia akili, basi anafikiri vibaya.
Vuai kampeni za uchaguzi hazijafika bado. Angeacha kufikiri vibaya na akatuliza akili yake na kutafuta namna vya kukiokoa chama chake na hatari ya kuanguka kibudu.
Vuai achangamke kunusuru chama chake, kwa sababu akifanya hivyo atakuwa pia anajinusuru yeye na anguko la kisiasa vilevile. Uanasiasa wake unahatarishwa na vile anavyokataa kukubali haki ilipo.
Vuai anaamini siasa za kulazimisha mambo. Siasa hizi ajuwe hazina nafasi tena zama hizi. Anaamini siasa za ulaghai, hazina nafasi. Anaamini siasa za upotoshaji, hazina nafasi na hazifai leo, siasa za chuki na kuwabaguwa watu hazina nafasi tena, siasa za kudanganya watu huku watu wakirudi majumbani wanakula mihogo yeye anachakaza pilau na biriani hazina nafasi.
Nionavyo kwa hatua hii, Vuai anachokifanya kingine ni kuinua sauti za wahafidhina wenzake wanaoshikilia mfumo wa serikali mbili uendelee. Hapa ndipo Vuai anapomchukulia Maalim Seif kama adui kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kuutilia shindo mfumo wa serikali tatu kama sera ya CUF tangu kilipoundwa mwaka 1992.
Bali Maalim Seif ameutaka mfumo huu kwa kuja na kitu kipya alichokiita “Muungano wa Mkataba,” akitaka washirika wawili wa Muungano, Zanzibar na Tanganyika wakae na kukubaliana upya maeneo ya ushirikiano na kuyaandikia mkataba.
Vuai na wenzake wanaamini mfumo wa serikali mbili bado unanguvu. Ni sawa yaweza kuwa hivo, lakini, kweli unauimarisha muungano kwa maana ya kuukomaza kwa wananchi kwamba unawaletea maendeleo au unazidisha kero ambazo zimekuwepo kwa miaka yote 50 ya Muungano....? yako vuai yanakuende wanao wanasoma vizuri nyumba nzuri magari pesa za kubadili mchuzi kama kawa huku mtaani watu bado wanakula ngumu wewe bado unawapa bla bla bla ungelikuwa wewe ungekubali vuai...?
Vuai anasema Maalim Seif anawashawishi Wazanzibari wavunje Muungano. Anajua hata mara moja Maalim Seif hajasema muungano uvunjwe au labda angependa kuona muungano unavunjika, isipokuwa ndio kile ninachosema, Vuai hataki mdomo wake ukauke kulitaja jina la Seif Shariff Hamad.
No comments:
Post a Comment