Saturday, August 31, 2013

MANSOUR YUSSUF HIMID ASEMA HATOENDA MAHAKAMANI


Mansour Yussuf Himid amesema licha ya kufukuzwa Uwanachama katika chama hicho hatoenda Mahakamani kutetea nafasi hiyo kwani kufanya hivyo ni kukaribisha Malumbano ambayo hayana tija.
Amesema kwenda kupinga uamuzi huo Mahakamani ni kuhalalisha
yeye kuwa Mwakilishi wa Mahakama badala ya Wananchi jambo ambalo hapendelei kutokea katika maisha yake.
Mansour ameyasema hayo leo katika Kongamano la Kamati ya Maridhiano lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini nchini Zanzibar.

Amesema amekuwa akiulizwa Maswali mengi na Watu tofauti kuhusu mustakabali wake kisiasa baada ya kufukuzwa uwanachama na kuongeza kuwa hana Pesa za kuchezea kwenda kupinga uamuzi wa Chama cha Mapinduzi Mahakamani.
“Wenzangu wamenipima na wameniona sifai ni haki yao, siendi Mahakamani, sina pesa za kuchezea wala sitaki kuwa Mwakilishi wa Mahakama” Alisema Mansour.
Mansour aliyejiunga CCM mwaka 1987 alienguliwa Uwanachama siku za karibuni kutokana na Kamati kuu ya Chama CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA kuridhika na madai ya kwenda kinyume na misimamo ya Chama pamoja na kushindwa kuitetea Ilani ya Chama cha CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.
Mansour ameongeza kuwa kwenda Mahakamani ni kukaribisha malumbano na kusisitiza kuwa Waungwana hawalumbani hivyo ameamua kukaa pembeni.
Amedai kwamba baada ya kufukuzwa uwanachama wa CCM vyama tofauti nchini vimejitokeza kuzungumza naye ili ajiunge navyo na kudokeza kuwa bado hajaamua ni Chama gani ataenda hadi pale muda utakapofika kufanya hivyo.
Mansour amesisitiza kuwa hata kama Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC itaitisha uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kiembesamaki yeye hatogombea na kwamba anaweza kufanya hivyo ifikapo mwaka 2015.
Ametumia fursa hiyo pia kuwaomba Radhi wana Jimbo la Kiembe Samaki alilokuwa akiliongoza toka 2005 na kuwashukuru Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliomsaidia katika kupindi chake chote cha Uongozi.
Akigusia suala la Muungano Mansour amesema ataendelea na
harakati zake kusimamia maslahi ya Zanzibar ili kuona mchakato wa Katiba Mpya unakuja na Katiba yenye Muundo wa Muungano wa Haki na Usawa baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Awali katika Kongamano hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo alimshukuru Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika kwa ujasiri wa kuleta mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza kuwa Kamati yake itaendelea kudai Muungano wa usawa na haki.
Mzee Moyo amedai kuwa Kamati yake haihitaji kutambuliwa na Watu wengine na kwamba inatosha kujulikana na Wananchi ambao wanafahamu wajibu wa Kamati hiyo.
Itakumbukwa kwamba kabla ya Kongamano hilo Chama cha Mapinduzi kilitoa taarifa kwa Vyombo vya habari kuhusu kutoitambua Kamati hiyo inayoongozwa na Mzee Moyo akisaidiwa na Makamo wake Aboubakar Khamis Bakar.
Katika hatua nyingine Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye alikuwa pia Mwanachama wa Chama cha CCM cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA Eddy Riyami alitangaza kujiengua na Chama hicho na kusema kwa sasa yupo huru bila Chama chochote.
Kabla ya Kongamano hilo Kamati hiyo pia iliwasilisha maoni yake kwa Tume ya Katiba mpya ambapo maoni yake yalijikita katika kuifanya Zanzibar kuwa na Mamlaka yake kamili ndani ya Mfumo wa Muungano.

MARA CHINA MARA UHOLANZI FAIDA GANI WANAYO IPATA RAI WA ZANZIBAR..???

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein, na Ujumbe wake wakiteremka  mlima wakati walipotembelea  Makumbusho ya Kihistoria ya Dr.Sun Yat-sen’s  yaliyopo juu ya Mlima  Nje ya Mji wa Nanjing,katika Jimbo la Jiangsu nchini China,atii wakiwa katika ziara ya Kiserikali yagujuuuu sema kweli umekwenda china kutia raundi tu serekali gani..?

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mwanamwema Shein, wakisalimiana Waongoza Wahusika wa FAya Dr.Sun Yat-sen’walipofika na ujumbe wake kupata historia ya makumbusho hayo huko Nje ya Mji wa Nanjing,katika Jimbi la Jiangsu nchini China.
IMG_2496
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,alipokuwa akiwafuta ujinga kwa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ukioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,katika ziara nchini Uholanzi.
IMG_2524
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,(katikati)na ujumbe wake wakitolewa ujinga  kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,walipofika katika Ofisi za Kituo hicho huko katika Bandari ya Rotterdam,nchini Uholanzi.
IMG_2542
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,(katikati)na Mawaziri pamoja na Balozi Dr.Diadorus B. Kamala wa nchi ya Tanganyika,Mzanzibari jiulizi huyu Balozi wa nchi ya Tanganyika anafanya nini..? na haya ni mafuta ya Wazanzibari yanayojadiliwa hapa(wa pili kulia)wakizungumza na Makamo wa Raisi pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,walipokuwa katika Boti walipoitembelea Bandari ya Rotterdam Nchni Uholanzi.

Balozi wa nchi ya Tanganyika nchini Belgium na Holland Diodorus Kamala akifungua mkutano uliojumuisha Watanganyika wanaoishi nchini Holland kuzungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein hapo  katika hotel ya Hilton iliyopo jijini Den Haag. 

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein akizungumza na Watanganyika wanaoishi nchini Holland Shein yupo huko nchini Holland kwa ziara atii ya kikazi wadanganyeni hao hao CCM.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akisalimiana na  Mkurugenzi wa Kituo cha habari kwa wafugaji wa Ngo’mbe wa maziwa Reimond Van Gent,alipofika kuangalia familia ya ufugaji wa Ngo’mbe wa maziwa na utengenezaaji wa Jibini (Cheese) akiwa huko nchini Uholanzi .

Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,akibadilishana hati ya makubaliano baada ya kutia saini na  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya   Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi AliMohamed Shein je Wazanzibari mushambiwa...??

Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,baada ya kumaliza kutia saini na  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya   Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi  Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akifutwa ujinga kutoka kwa Frank Captein,wakati alipotembelea katika eneo maalum lililohifdhiwa Jibini (cheese) iliyokuwa imehifadhiwa tayari kwa mauzo haya Wazanzibari Shein akirudi tu atawafundisha na nyinyi muanze kutengeza cheese tartibuni tu asije akawatia uchizi badala ya kutengeza cheese.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Frank Captein,wakati alipotembelea ndama wadogo jinsi wanavyolelewa katika famili ya BW.Captein,huko Nchini Uholanzi
IMG_2640
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Mfalme wa Uholanzi Willem Alexander,alipomtembelea katika makazi yake  huko nchini Uholanzi.
IMG_2649
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi

wawakilishi wa Makampuni wakati alipowasilim katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa na

 Famili ya Mfalme pamoja na makampuni nchini Uholanzi.
Ushirikiano katika kuendeleza sekta ya mafuta na gesi.
Makubaliano hayo yametiwa saini juzi tarehe 28 Agosti, 2013 mjini The Hague ambapo Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban alitia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwakilishi wa Kampuni Shell Tanganyika Axel Knospe alitia saini kwa niaba ya  Kampuni hiyo.
Makubaliano hayo yamefikiwa mjini The Hague wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed inayoendelea nchini huko Uholanzi.
Kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo  Shein alifanya mazungumzo na Uongozi wa juu wa kampuni ya Shell  yaliyojielekeza katika kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Zanzibar na Kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo Kampuni ya Shell itaisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujenga uwezo wa kitaalamu, katika hatua za awali za uendelezaji wa sekta hiyo.
Sambamba na hatua hiyo Kampuni ya Shell itasaidia pia shughuli za maendeleo ya vijana katika kuwajengea uwezo kwa kuwapatia elimu na mafunzo mbalimbali yakiwemo ya stadi za ujasiriamali.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban alisema “kutiwa saini kwa makubaliano hayo ni hatua moja kubwa na mwelekeo sahihi katika jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendeleza sekta ya nishati nchini Zanzibar” je Wazanzibari mushambiwa kama mafuta yenu yashatiwa saini huko Uholanzi..??
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Shell Tanganyika Bwana Axel Knospe alieleza kuwa wakati mashauriano yakiendelea kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Tanganyika juu ya kuliondoa suala la mafuta na gesi katika mambo ya muungano, Kampuni hiyo itaendelea na dhamira yake ya ushirikiano na nchi ya Zanzibar hadi hapo muda utakapokuwa tayari kuanza kazi ya shughuli za uchimbaji mafuta na gesi ambapo itaifanya kazi hiyo kwa kuzingatia uwajibikaji kiuchumi, kijamii, kimazingira na  kuifanya sekta hiyo kuwa endelevu
“wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika zikishughulikia kwa pamoja suala la kisheria na kisera kuipatia nchi ya Zanzibar haki pekee ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi nchini Zanzibar, Kampuni ya Shell itaendelea na dhamira yake ya kushirikiana na nchi ya Zanzibar hadi hapo muda muafaka utakapofika kuanza shughuli za uchimbaji wa mafuta na gesi” alieleza bwana Axel Knospe.
Wakati akizungumza na Shein Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Zanzibar nchini Uholanzi juzi Waziri wa Biashara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Uholanzi Bibi Lilianne Ploumen alimueleza Shein kuwa Serikali ya nchi hiyo iko tayari kutumia utaalamu na uzoefu wake katika sekta ya mafuta na gesi kuisaidia nchi ya Zanzibar kuendeleza sekta hiyo.
Bibi Ploumen alieleza kuwa Serikali ya nchi hiyo iko tayari kutoa fursa za mafunzo kwa watumishi wa Serikali ya nchi ya Zanzibar katika sekta ya nishati ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uzoefu katika kusimamia rasilimali hizo,(haya natuone achanguliwe mzanzibari kwenda kusomea yagujuuu)  utunzaji wa mazingira na ushiriki wa wananchi katika matumizi ya rasilimali hiyo kuepusha migogoro.
“Mambo ya msingi ya kupewa kipaumbele ni pamoja na namna ya uendeshaji, usimamizi na matumizi bora ya rasilimali hizo, ushirikishwaji wananchi na utunzaji mazingira”alieleza bibi Ploumen na kusisitiza haja ya nchi ya Zanzibar kujifunza kutoka nchi nyingine kuepuka makosa yaliyofanywa na baadhi ya nchi ikiwemo Uholanzi yenyewe.
Shein anamaliza  ziara yake ya siku tano nchini Uholanzi leo  na anatarajiwa kurejea nyumbani nchini Zanzibar Jumapili.
Katika ziara hiyo Shein amefuatana na Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ramadhani Abdalla Shaaban, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim na Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia.

EDDY RIYAMI AMSHANGA KUMBI SHEIN KUWA WA MWANZO KUPIGANIA MANSOUR AFUKUZWE

MJUMBE wa Kamati ya Maridhiano nchini  Zanzibar, Eddie Riyami, amesikitishwa na hatua ya kuvuliwa uanachama kwa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yussuf Himid. Hata hivyo, mjumbe huyo amemshutumu Ali Mohammed Shein, akisema kuwa ni mmoja kati ya wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kutoka nchini Zanzibar walioshiriki kikao hicho cha kumvua uanachama.
Akihojiwa na Radio ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle), katika kipindi Maalumu cha ‘Meza ya Duara’, Riyami alimtuhumu vikali  Shein, akidai amekosa shukurani kwa Mansour na kumtaka kumuomba radhi. “Shein amesahau kama Mansour ni mmoja kati ya Wazanzibari waliokwenda Dodoma kuhakikisha  Shein anapita kuwania kiti cha urais wa Zanzibar, ili aendeleze maridhiano, namshangaa leo hii, Dk. Shein kuwa wa kwanza kupigania Mansour afukuzwe,” alisema Riyami.

Katika mahojiano hayo, Riyami alimsifu Mansour kuwa ni miongoni mwa vijana shupavu ndani ya CCM waliohakikisha Zanzibar inaingia katika siasa za maridhiano na chama cha upinzani cha CUF na hivyo kuondokana na siasa za chuki na uhasama zilizodumu kwa muda mrefu visiwani humo.
Riyami alisema Mansour hakustahili kufanyiwa aliyofanyiwa, na kusisitiza maoni aliyokuwa akiyatoa akiitaka Zanzibar kuwa na dola yake kamili, yalikuwa ni maoni yake akiwa kama Mzanzibari.
Kauli hiyo ya Riyami imekuja siku chache baada ya Mansour kufukuzwa uanachama wa CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA na kikao cha NEC, kilichokaa wiki hii mjini Giningi Dodoma, akituhumiwa kutamka hadharani misimamo yake inayokinzana na CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

Mansour alituhumiwa na kikao hicho atii kwa kushindwa kusimamia malengo, madhumuni na masharti ya chama pamoja na kukiuka maadili ya kiongozi kwa kukiuka Ilani ya chama hicho ya mwaka 2010.
Hata hivyo, kabla ya hukumu ya Mansour mjini Giningi Dodoma, kulikuwa na hali ya mvutano wa chini uliokuwa ukiendelea kati ya Shein na wajumbe wa Kamati ya Maridhiano, inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Dk Shein aliwatuhumu wajumbe wa kamati hiyo kutoka CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA, akidai inakwenda kinyume na msimamo wa CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA unaotaka serikali mbili.
Shein anawatuhumu wajumbe wa kamati hiyo kutoka CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ambao ni Mzee Moyo, Mansour na Riyami, pamoja na Aboubakar Khamis, Ismail Jussa na Salim Bimani, kwamba Aatii inawapotosha Wazanzibari juu ya muundo wa Muungano.

Katika moja ya mikutano yake ya kisiasa, Shein aliikana kamati hiyo na kusema haitambui na kuwataka wajumbe wake kuacha mara moja kile alichodai kutumia ‘mgongo’ wake katika kufikia malengo yao.
Katika mahojiano na Sauti ya Ujerumani, Riyami alisema kilichofanyika mjini Dodoma ni juhudi zinazoendelezwa na Shein za kutaka kuwaumiza wajumbe wa Kamati ya Maridhiano.
Riyami aliwatuhumu wajumbe wa NEC kutoka nchini Zanzibar akisema, wamepatwa na ‘kihoro’ cha maridhiano yaliyofikiwa kati ya CCM na CUF, baada ya kuundwa kamati nyingi za muafaka ambazo hazikuzaa matunda.
“Hawa ndio wale wahafidhina waliokaa Dodoma kumfukuza Mansour, wamepatwa na kihoro, ziliundwa kamati za muafaka nyingi hazikuzaa matunda, kinachofanyika ni kisingizo cha kuwaumiza wajumbe wa kamati ya maridhiano,” alisema Riyami.
Riyami alisema kitendo alichofanyiwa Mansour hakiwashangazi, akidai vikao vinavyofanyika mjini Gining Dodoma ni sehemu ya ‘machinjio’ ya kuwamaliza Wazanzibari.

Alitaja baadhi ya vikao vya NEC vilivyowahi kufanyika mjini Giningi Dodoma na kuamuru kuwafukuza unachama wa CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA, Maalim Seif Sharrif Hamad, Marehemu Shaban Mloo, Haji Duni, Marehemu Soud Yusuf Mgeni na aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi Zanzibar, Ramadhan Fakih.
Riyami alikumbusha tukio la mwaka 1984, ambako kulifanyika vikao vya NEC na kuamuru kumvua nyadhifa zake zote za urais wa nchi ya Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, akidaiwa kutaka kuusaliti Muungano.

“Haya ya Mansour wala hatuyashangazi…wala si ya ajabu na hili nalisema wazi pasipo na shaka, sitanii, Shein amwite Mansour amuombe radhi hadharani kwa kumdhalilisha mwanasiasa shupavu. Leo wajumbe wa Kamati ya Maridhiano walikutana katika Hoteli ya Bwawani, nchini Zanzibar, kuzungumzia hatima ya kufukuzwa mjumbe mwenzao, Mansour, huku katika kikao hichi kitakachohudhuriwa na Wazanzibari wengi sana, Mansour ametowa dukuduku lake na kutoa yaliyo moyoni mwake juu ya kadhia ya kufukuzwa kwake uanachama wa CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA na kwa kweli Muandishi wetu wa siri wa FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI anasema amakweli Mansoor Yussuf Himid ni MOTO WA KUOTEA MBALI.Pia Mwanaharakati Maarufu Bw Mohamed Riami (Eddy Riami) ametangaza kujiondoa katika Chama Cha Mapinduzi chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

Akizungumza katika Kongamano lililotayarishwa na Kamati ya Maridhiano, hii ilikuwa strong speech ambayo haijawahi kutolewa na Bw Mohammed Eddy Riami amesema yeye sio mwanasiasa, akiwafananisha na Jussa na Mzee Moyo. Bali yeye ni raia kama walivyo raia wengine.

Amewataka Wazanzibar kujitolea kutafuta heshma zao na nchi yao.

Alisema kwamba ni wao ndio waliompigia kura Rais kwani Rais mwenyewe hakupiga kura katika uchaguzi uliopita. Hivyo anajuwa vipi Zanzibar itashinda kabla ya mwaka 2015. Alikuwa akikariri moja ya hotuba ya Mzee Karume alapokuwa anakadiria kuwa Raisi wa  Zanzibar haihitaji uchaguzi
hadi baada ya miaka 50.

Ametaka suala la siasa litolewa katika katiba mpya. Vilevile amewataka viongozi wengine kuachana na siasa badala yake kupigania nchi ya  Zanzibar nje ya siasa. Kwani ni siasa ndio iliyoifikisha hapa nchi yetu ya  Zanzibar.

Friday, August 30, 2013

KAMA KUNA MWANAJESHI WA ZANZIBAR CONGO BASI JITAYERISHENI TENA KUZIKA MWANAKWEREKWE M23 HAWACHEZI KICKBOXING WAO WANAUWA TU


Mashirika. Mpiganaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanganyika, JWT Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na kundi la M23 la nchini congo kwenye Mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano makali.

Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanganyika wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.

Askari wa Tanganyika na wale wa Afrika Kusini wako DRC kwa kazi atii ya kulinda amani. Malawi bado haijapeleka majeshi yake.

Meja Mshindo alikuwemo katika kikosi cha vifaru na alikuwa kwenye Kambi ya 83KJ iliyoko Kiluvya Dar es Salaam.

Kuuawa kwa manajeshi huyo kumekuja ikiwa ni siku 47 tangu kuuawa kwa wanajeshi wanne wa nchi ya Tanganyika na wa wili wa nchi ya Zanzibar  waliokuwa atii wakilinda amani kwenye Mji wa Darfur Sudan na Kikundi cha Janjaweed.
Msemaji wa JWT, Meja Erick Komba alikiri kutokea kifo hicho na kusema: “Jana (juzi) Agosti 28, Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha majeruhi.

“Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.”

Habari zaidi kutoka Congo zinaeleza kuwa mwili wa marehemu Meja Mshindo ulisafirishwa jana kupelekwa Entebbe, Uganda ambako ungefanyiwa matayarisho ya mwisho na tayari kwa kuletwa nchini Tanganyika.

Katika hatua nyingine, wanajeshi wawili wa Umoja wa Mataifa, mmoja akiwa Mtanganyika na mwingine raia wa Afrika Kusini walijeruhiwa kwa bomu eneo la Munigi huko huko Congo.

Bomu hilo lilirushwa na kundi la M23 kuelekezwa kwa askari wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakikagua maeneo mbalimbali karibu na Mji wa Goma.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amelaani mashambulizi na mauaji hayo ya mwanajeshi  huyo wa Tanganyika na kusema: “Ninatoa pole kwa Tanganyika (Watanzania) Zanzibari na familia ya mpiganaji huyu na ninalaani kwa nguvu zote mauaji haya na majeruhi kwa walinzi wa amani.”

Msemaji wa UN, alisema Majeshi ya UN kwa kushirikiana na yale ya Serikali, yalianzisha mapigano makali dhidi ya kundi la M23 kwenye eneo la Kibati Kaskazini mwa Goma, kwenye Mji wa Kivu ya Kaskazini.  Majeshi ya UN na Fardc yalitumia helikopta, vifaru na askari wa miguu kutekeleza mashambulizi hayo yaliyojibiwa na kundi hilo la M23. Kwa mujibu wa msemaji huyo, mapigano bado yanaendelea je hii ndio kueka amani au wamekwenda kuzidisha vita...???

Thursday, August 29, 2013

HAWANA KESI ILA NI KUMTESA TU SHEIKH MPONDA ISSA MPONDA


Nchini Tanganyika Morogoro. Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda jana alisababisha kusimama kwa shughuli za Serikali wilayani Morogoro baada ya ofisi kadhaa ikiwamo ya Mkuu wa Wilaya na baadhi ya mitaa kufungwa ili kupisha kusikilizwa kwa kesi inayomkabili katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro nchini Tanganyika.

Tofauti na Agosti 19, mwaka huu wakati aliposafirishwa kwa helikopta, jana Sheikh Ponda alisafirishwa kwa barabara kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro akiwa chini ya ulinzi.

Mbali ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kufungwa, nyingine ni Hazina Ndogo, Madini, Posta, Vipimo, Ukaguzi na Maktaba ya Mkoa.

Sababu za kufungwa kwa ofisi hizo pamoja na Mtaa wa Stesheni na maeneo ya Posta ni kuwa jirani na Mahakama hiyo. Magari yalizuiwa kutembea katika njia na maeneo ya karibu na ofisi pamoja na Mahakama hiyo huku kukiwa na idadi kubwa ya askari polisi na magereza kwa muda wote wa takriban saa mbili.

Alifikishwa mahakamani hapo saa 4:10 asubuhi akiwa katika basi la Magereza ambalo lilisindikizwa na jingine dogo, huku magari mengine yakisimamishwa kupisha msafara huo. Mahakama hiyo ilifurika umati wa waislamu wanao mjali kiongozi huyo kiasi cha kuwalazimu polisi na wana usalama wengine kuweka utepe kuwazuia wengi wao kufika katika jengo lililokuwa likitumika kuendesha kesi hiyo.
Shughuli katika eneo hilo zilirejea katika hali yake ya kawaida saa 6:25 mchana baada kesi yake kuahirishwa na msafara wa Sheikh Ponda kurejea katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam ambako yuko rumande.

Muda wote tangu kuwasili mpaka kusikilizwa kwa kesi hiyo, wafuasi hao walikuwa kimya hadi pale ilipoahirishwa na hasa baada ya Sheikh Ponda kuwapungia mkono alipokuwa akielekea kwenye basi ambako walisikika wakisema: “Takbriir na kuitikia Allahu Akbar – (Mungu Mkubwa).”

Kesi yenyewe aliyosingiziwa

Katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Benard Kongola alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate kuwa Sheikh Ponda alitenda makosa ya uchochezi Agosti 10, mwaka huu saa 11.45 jioni kwenye maeneo ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro.

Alisema siku hiyo, Sheikh Ponda alialikwa kutoa maelezo machache kwenye Kongamano la Eid lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri Mkoa wa Morogoro (Uwamo) na kwamba akiwa hapo alitamka maneno: “Ndugu Waislamu, msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Baraza la Waislamu Tanganyika (Bakwata), ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao na kujitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, fungeni milango na madirisha ya misikiti yenu na muwapige sana,” huku akijua kutoa maneno hayo ni kosa kisheria.
Alisema kwa kufanya hivyo, Sheikh Ponda anayetetewa na mawakili watatu wanaoongozwa na Juma Nassoro, alivunja masharti ya Mahakama ya kifungo cha nje iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mei 9, mwaka huu iliyokuwa imetamka kuhubiri amani.

Katika shtaka la pili, Sheikh Ponda anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda kosa la jinai kwa kuwaambia: Serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu, lakini haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo waliokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Wakristo.” Shtaka la tatu ni kudaiwa kutamka maneno yaliyoumiza imani ya watu wengine kama yalivyo katika shtaka la pili.
Baada ya kusoma mashtaka hayo, Kongola alisema walikuwa na mashahidi 15 na vielelezo vitatu ambavyo ni DVD mbili na kibali kilichotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro(OCD), Agosti Mosi, 2013 cha kongamano husika na hati ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, Mei 9, 2013.

Baada ya kusomewa, Sheikh Ponda alikana mashtaka yote matatu huku akikubali kuwemo kwenye kongamano hilo. Alikiri kukamatwa na polisi Agosti 11, Dar es Salaam.

Wakili wa utetezi, Nassor aliwasilisha ombi la dhamana kwa mteja akisema mashtaka hayo yote kisheria yana dhamana. Pia aliwasilisha ombi la kupatiwa hati yenye maelezo ya mlalamikaji ambaye ni Jamhuri ya Tanganyika kwani alisema kuwa kutokana na upelelezi upande wa mashtaka kukamilika, wanahitaji maelezo hayo kwa ajili ya kuandaa utetezi.

Hata hivyo, Wakili Kongola aliiomba Mahakama kutompa dhamana mshtakiwa kutokana na cheti kilichotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kupinga dhamana ya mshtakiwa huyo kwa masilahi ya usalama wa nchi. Akitoa mwongozo wa maombi yaliyowasilishwa na pande zote mbili, Hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 11, mwaka huu itakapotajwa tena na kwamba Septemba 17, mwaka huu Mahakama itatoa uamuzi endapo mshtakiwa atapewa dhamana au la wakati itakapoanza kusikilizwa.

Wednesday, August 28, 2013

NCHI YA TANGANYIKA ILIFIKIRI RWANDA NA KENYA NI KAMA NCHI YA ZANZIBAR HEWALA BWANA TANGANYIKA KILA ITAKACHO SEMA.


WABUNGE WA NCHI YA RWANDA WASUSIA KIKAO CHA BUNGE LA EALA

RAIS Paul Kagame wa nchi ya Rwanda, sasa hayupo tayari kukanyaga ardhi ya nchi ya Tanganyika kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Rais Jakaya Kikwete.  wa nchi ya TANGANYIKA Mwandishi wetu wa siri aliyekuwepo mjini Arusha alidokezwa.Wakati hayo yakifikia hapo, kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), linakoketi mjini Arusha nchini TANGANYIKA kilivunjika baada ya Spika wa bunge hilo, Magreth Zziwa, kugongana kauli na Mbunge mmoja wa nchi ya Rwanda jambo lililosababisha wabunge wote wa nchi ya Rwanda kususia kikao na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge shambashi sio wahafidhina wetu wa KIZANZIBARI KILA KITU HEWALA BWANA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

Mwenendo wa hayo yaliyojitokeza jana katika Bunge la Afrika Mashariki hadi kikao kuvunjika, msingi wake ni mgogoro unaowagusa wakuu hao wawili wa dola.
Habari zilizotufikia toka katika vyanzo vyake mbalimbali vilivyo ndani na nje ya mipaka ya Tanganyika, lakini pia katika vikao vya Bunge hilo la Afrika Mashariki vinavyoendelea jijini Arusha nchini TANGANYIKA zinaeleza kuwa, Rais Kagame hata kama ataalikwa kuja nchini leo, hatakuja.
MTANGANYIKA mwandishi wetu wa siri alidokezwa kuwa jambo hilo tayari limethibitishwa na Wabunge wa nchi ya Rwanda wanaohudhuria vikao vya (EALA).

Taarifa toka ndani ya Bunge hilo zilizotufikia sisi Jumatano zinaeleza kuwa, tayari mzimu wa msuguwano huo uliojitokeza baina ya wakuu hao wawili wa dola, umeanza kuwavuruga wabunge hao baada ya jana kikao cha Bunge hilo kuvunjika, kutokana na kuibuliwa kwa hoja ya kutaka vikao vya Bunge hilo kufanyika kwa utaratibu wa kuzunguka kila nchi.
Zinaeleza zaidi kuwa; Ni katika hoja hiyo wabunge wa Kenya na Rwanda walionekana kuungana na kuwa kitu kimoja na hivyo kususia kikao hicho cha jana, jambo ambalo lilimlazimisha Spika wa Bunge hilo, Magreth Zziwa kuvunja kikao.

WAZANZIBARI NYOTE JUMAMOSI MUSIKOSE MANSOOR YUSSUF HIMID NA ISMAIL JUSSA LADHU KUNGURUMA

mansour
HUYU NDIO KIBOKO YA WACHAWI WOTE WILIO NDANI YA CCM CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KILICHO PINDUWA CHAMA CHA A.S.P. NA KUWAPINDUWA WAZANZIBARI.
man
Sasa kuna kila dalili CCM chama cha mkoloni mweusi kimejiandalia Kifo nchini Zanzibari,
Yule Shujaa wa mamlaka kamili ya nchi yetu tunayo ipenda ya zanzibar na anayeweza kuthubutu kusema hapana, huyu hapa mchana huu hana wasiwasi kwa sababu kwake yeye nchi yetu ya Zanzibar ni zaidi ya nafasi ya uwakilishi au kuwa mwananchama wa chama cha mkoloni mweusi Tanganyika
Mambo yote bwaaaa Mambo yote bwaaaa
 Jumamosi ukumbi wa Bwawani asie na mwana abebe jiwe ni Monsour Himid na Ismail Jussa Ladhu Kunguruma
Wahenga walisema sikio la kufa halisikii Dawa maamuzi ya Giningi Dodoma ni msiba kwa CCM chama cha mkoloni mweusi Tanganyika na,wahafidhina wao nchini  Zanzibari

Kwa waliopo nje ya Zanzibar usikose kusikiliza live streaming: http://www.ustream.tv/channel/mazruimedialive

Tuesday, August 27, 2013

MANSOOR YUSSUF HIMID AFUKUZWA NA CCM JE WAZANZIBARI BADO TU HAMJA AMKA KUWA CCM SIO CHAMA CHA WAZNZIBARI BALI NI KABURI LA WAZANZIBARI



GININGI DODOMA.MACHINJIO YA WAZANZIBARI WOTE
1) MZEE KARUME WALIMUWA
2) MZEE JUMBE WAKAMFUKUZA
3) MAALIM SEIF WAKAMFUNGA JELA
4 )MANSOOR YUSSUF HIMID HUYO WASHAMFUKUZA
BARAZA LA WAWAKISHI KUNA WARUGURU WAWILI SHEIN ASHAWAWEKA NGOJENI NA NYINYI WAHAFIDHINA MULIO BAKI PIA MUTAFUKUZWA BARAZA ZIMA LA WAWAKILISHI LITAKUWA LIKIENDESHWA NA MACHOGO KAMA HAMUAMINI NGOJENI.CCM SIO CHAMA CHA WAZANZIBARI NI CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KIMEPINDUWA CHAMA CHA ASP NA KUCHUKUWA MADARAKA YOTE  MPAKA LEO WAZANZIBARI BADO HATUJA AMKA.

MWAKILISHI WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU MANSOUR YUSSUF HIMID AMEFUKUZWA UANACHAMA WA CHAMA HICHO CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA AKIDAIWA KUKISALITI KWA KUUNGA MKONO MUUNGANO WA MKATABA.
TAARIFA KUTOKA MJINI GININGI DODOMA ZINASEMA KUWA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA KILICHOKUTANA KWA SIKU YA TATU CHINI YA MWENYEKITI WAKE RAISI WA NCHI YA TANGANYIKA JAKAYA KIKWETE KIMETOA UAMUZI WA KUFUKUZWA KWA MWANACHAMA HUYO KATIKA CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

KUFUATIA HATUA HIYO CHAMA CHA MAPINDUZI KITATOA TAARIFA KWA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI KUONDOA UDHAMINI WAKE KWA MWANACHAMA HUYO KAMA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WA JIMBO KIEMBESAMAKI.
HATUA HIYO ITAMFANYA SPIKA WA BARAZA HILO KUTANGAZA KITI CHA JIMBO HILO KUWA WAZI NA KUITISHWA UCHAGUZI MDOGO WA KUGOMBEA NAFASI HIYO.
MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA DAUD ISMAIL AMESEMA KUWA KIKAO HICHO KIMEFIKIA UAMUZI HUO BAADA YA KUPOKEA MADAI YA MKOA WA MAGHARIBI KICHAMA KUTAKA MWANACHAMA HUYO AFUKUZWE KWA MADAI YA KUPINGA SERA YA SERIKALI MBILI ZA MUUNGANO INAYOUNGWA MKONO NA CHAMA HICHO CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

KWA MUJIBU WA TARATIBU ZA CCM IWAPO MANSOUR HAKURIDHISHWA NA UAMUZI WA KUFUKUZWA KWAKE ANAWEZA KUKATA RUFAA MAHAKAMA KUU KUPINGA UAMUZI HUO ALA SISI WAZANZIBARI TUNASEMA YA NINI...? NA SOTE SASA TUNAJUWA KUWA CHAMA CHA CCM SIO CHAMA CHA WAZANZIBARI BALI NI CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KWA NINI NIKASEMA HIVYO KUMBUKA MZEE KARUME ALIPOPINGA TU WAKAMUUWA,MZEE JUMBE,MAALIM SEIF,N.K. NA SASA MANSOOR.

Sunday, August 25, 2013

SHEIN YUPO GININGI DODOMA KUMKATAROHO MANSOOR YUSSUF HIMID

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete, Makamo Mwenyekiti Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abrahman Omar Kinana Mjini Dodoma wakisubiri kuanza kikao cha leo ambacho kinatarajia kutoa au kuacha uamuzi wa kumtipia katika chama hicho Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mansoor Yussuf Himid
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete, Makamo Mwenyekiti Zanzibar,  Ali Mohammed Shein na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abrahman Omar Kinana Mjini Giningi Dodoma wakisubiri kuanza kikao cha leo ambacho kinatarajia kutoa au kuacha uamuzi wa kumtimuwa katika chama hicho Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mansoor Yussuf Himid

Baada ya Kamati Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Zanzibar, kudaiwa kumvua uanachama Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansour Yussuf Himid, mwenyewe aimeibuka jana na kusema anasubiri uamuzi wa vikao vya juu vya chama vilivyoanza jana mjini Giningi Dodoma.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo ambazo Mansour amekiri kuzisikia zinaeleza kuwa uamuzi huo umetokana na yeye kudaiwa kupingana na Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2010, ambayo inaunga mkono muundo wa serikali mbili.


Kwa mara ya kwanza, tuhuma za Mansour zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM nchini  Zanzibar, kilichoketi Agosti 16, 2013 katika Ofisi za CCM Kisiwandui ambapo wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumfutaa uanachama mwakilishi huyo.
Uamuzi wa kumvua uanachama Mansour uliwasilishwa katika kikao hicho chini ya Makamu Mwenyekiti wake nchini  Zanzibar, Ali Mohamed Shein.

 Shein ndiye aliyeongoza kikao hicho, huku wajumbe wakiwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mohamed Hija, Mbaruk Rashid Omari na Balozi Mdongo wa Nchi ya Tanganyika, Balozi Seif Ali Idd, huku mapendekezo ya uamuzi huo yakipelekwa mjini Giningi Dodoma kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Mambo mengine ambayo anadaiwa kufanya Mansour ni kuasisi Kikundi cha Kiislamu cha Uamsho!!!! ambacho kinadaiwa kuchochea vurugu visiwani humo. Akizungumza na gazeti hili Mansour alisema, “Mimi sina cha ziada ninachosubiri ni uamuzi wa chama. Baada ya uamuzi wa chama ndiyo nitakuwa na jambo la kuzungumza, tusubiri tu wala tusiwe na haraka.”
Wakati Mansour akieleza hayo mwasisi wa chama hicho, Hassan Nassor Moyo alipinga uamuzi huo, akisisitiza kuwa kama utatekelezwa ni wazi kuwa Mansour atakuwa amenyimwa haki yake ya kikatiba.


Moyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano nchini Zanzibar amesema hata yeye yupo tayari kufukuzwa uanachama kama ikionekana ana msimamo kama wa mwenzake.
Akizungumza wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Radio Deutsche Welle ya Ujerumani jana, Moyo alisema, “Kama wameamua kumfukuza siyo sawasawa, wanasema ametofautiana na msimamo au sera ya CCM ya kuwa na muungano wa serikali mbili, hiyo ni sera ya CCM, lakini serikali ya Tanganyika (Tanzania) Zanzibar kwa kushirikiana na rais wa Zanzibar imetunga sheria ya mchakato wa Katiba Mpya na imeeleza wananchi, vikundi na taasisi.”


“Mansour ni sehemu ya watu hao ana haki ya kutoa maoni yake. Kupanga mikakati ya kumwondoa ndani ya chama ni kumnyima haki yake ya uraia.”
Alipoulizwa swali na mwandishi wa redio hiyo kuwa Mansour siyo raia wa kawaida, kwani mbali na kuwa mwanachama wa CCM aliyeshika nafasi nyingi ndani ya chama hicho na serikali pia ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi hivyo maoni yake yanaweza kukiathiri chama alijibu, “Pamoja na kuwa ameshika nafasi za juu za CCM, lakini kubwa ni kwamba Mansour ni raia, raia ana haki yake ya kutoa maoni tena kisheria kabisa.”

Thursday, August 22, 2013

MAMA WA AFRICA NI MISRI NA LEO ANALIA NA KUMWAGWA DAMU KAMA HIVI


GAMAL ABDEL NASSER WAKATI WA UHAI WAKE ALIYEKUWA RAISI WA MISRI

YALIYOJIRI Misri tangu Jumatano iliyopita ni maafa makubwa. Ni maafa kwa Misri. Ni maafa kwa Afrika. Ni maafa kwa nchi zote zenye kuulea mfumo wa demokrasia uliomchanga katika nchi hizo. Michirizi ya damu imeonekana na itaendelea kuonekana katika sehemu mbalimbali za jiji hilo. Damu hiyo ni ya Wamisri na walioimwaga na wataoendelea kuimwaga ni Wamisri wenyewe. Wamekuwa wakitwangana risasi wenyewe kwa wenyewe usiku kwa mchana.
Wengi wetu barani Afrika tumeshika tama; twaililia Misri iliyomzaa Gamal Abdel Nasser, mmoja wa wana majumui wa Kiafrika aliyekuwa adhimu.
Wakati nchi nyingi za Kiafrika zilipokuwa zikitawaliwa na wakoloni, Nasser alikuwa pekee miongoni mwa viongozi wa nchi za Kiafrika aliyeufanya mji mkuu wa nchi yake uwe makao ya vyama vya ukombozi vya Kiafrika.
Vyama vingi vya Kiafrika vilivyokuwa vikiwania uhuru wa nchi zao vilikuwa na ofisi jijini Cairo. Kutoka kanda ya Afrika ya Mashariki kulikuwa ofisi za vyama vya Eritrea na Somalia. Kulikuwako pia ofisi za vyama vya Kenya African National Union (KANU), Uganda Peoples’ Congress (UPC) na Zanzibar Nationalist Party (ZNP).
Ingawaje, vyama vya Afro-Shirazi Party (ASP) na Tanganyika African National Union (TANU) havikuwa na ofisi Cairo. Mwanzoni Julius Nyerere, kiongozi wa TANU,hakuwa akimchangamkia Nasser. Alikuwa na wasiwasi kuhusu ushawishi wake Visiwani Zanzibar, hasa usuhuba wake na Ali Muhsin Barwani, kiongozi wa ZNP. Pia alikuwa na shaka kuhusu umaarufu wake miongoni mwa Waarabu waAfrika ya Mashariki.
Misri nayo kwa upande wake, ikiungwa mkono na wawakilishi wa vyama vingi vya ukombozi, mwanzoni ilikuwa haikupendezewa na sera za awali za Nyerere hasa baada ya Tanganyika kupata uhuru. Ikihisi kuwa sera hizo za Nyerere hazikuwa za kimapinduzi vya kutosha na zikipingana na wito wa Kwame Nkrumah wa Ghana wa kutaka bara la Afrika liungane.
Mahusiano kati ya Nasser na Nyerere yalitengenea baadaye Tanganyika ilipopata uhuru na zaidi baada ya kutolewa Azimio la Arusha.
Nasser na serikali yake waliviunga mkono kwa hali na mali hata vile vyama vilivyoamua kuchukua silaha na kupigana na wakoloni ili nchi zao ziwe huru. Kwa hivyo vyama hivyo navyo pia vilikuwa na ofisi zao Cairo.
Baadhi ya nchi zilikuwa na zaidi ya chama kimoja.Lengo la kwanza la chama chochote kipya lilikuwa ni kuelekea Cairo ili kiweze kuwapatia msaada watoto waweze kusoma bure Misri, kikubaliwe kuleta watu nchini humo kwa mafunzo ya kijeshi na kipatiwe nafasi ya kuwa na matangazo ya redio yatayorushwa hewani na Sauti ya Afrika kutoka Cairo.
Ofisi za vyama vyote hivyo, ambavyo wakati mmoja havikupungua 22, zilikuwa katika jengo moja la Rabta Afriqiyya (Jumuiya ya Kiafrika) lililokuwa katika njia ya Ahmed Hishmat Street katika mtaa wa Zamalek huko Cairo.
Katika jengo hilo uliwakuta watu kama akina Odhiambo Okello, aliyekuwa katibu wa Oginga Odinga wa KANU, Suleiman Malik mwakilishi wa chama cha ZNP, Amilcar Cabral kiongozi wa PAIGC cha Guinea-Bissau na Cape Verde, Agostinho Neto kiongozi wa chama cha MPLA cha Angola, John Kaley wa UPC, Felix Moumie, kiongozi wa chama cha UPC cha Cameroon, Sam Nujoma wa Swapo cha Namibia, Alfred Nzowa ANC cha Afrika Kusini au Joshua Nkomo wa ZAPU cha iliyokuwa Rhodesia ya Kusini.
Kadhalika, mji wa Cairo ndio uliokuwa makao makuu ya Sauti ya Afrika kutoka Cairo, ile stesheni ni ya redio niliyokwisha itaja ya kupigania uhuru na ukombozi wa Afrika. Stesheni hiyo ya redio ilikuwa ikitangaza kwa lugha 30 za Kiafrika, Kiswahili ikiwa mojawao.
Baada ya Patrice Lumumba wa Congo-Kinshasa kuuawa na Wabelgiji wakishirikiana na Waingereza pamoja na CIA, shirika la ujasusi la Marekani, Nasser aliagiza kwamba wana balozi wa Misri nchini Congo wafanye kila njia za kumkimbiza mjane wake Lumumba na wanawe hadi Cairo ambako waliishi.
Kwa hivyo Cairo, uliibuka kuwa mji mkuu wa kwanza duniani, kuipaza sauti yake kwa niaba ya Afrika nzima dhidi ya ukoloni.
Hivyo ndivyo ulivyokuwa mji wa Cairo katika miaka ya 1950 na 1960. Cairo pamoja na miji mingine nchini humo ili kuwa ni miji iliyojivunia uvumilivu na ustaarabu wao.
Sio leo ambapo miji hiyo inawashuhudia Wamisri wakiuana kinyama wenyewe kwa wenyewe kwa sababu za kisiasa.
Hakuna aliyetarajia hali kama hiyo kuwa itatokea nchini humo kama tusivyoitarajia kutokea nchini mwetu. Na Mungu atuvue salama, atupishe mbali na hayo.
Pande zote mbili zilizoingia vitani nchini Misri zina makosa. Mohamed Morsi, Rais aliyepinduliwa, na vuguvugu lake la Moslem Brotherhood wamefanya makosa kadhaa.
Kosa moja ni kudhani kwamba wanaweza kufanya watakalo kwa vile wameshinda uchaguzi. Julai 2, Morsi alilihutubia taifa bila ya kujua kwamba hiyo ilikuwa mara yake ya mwisho kufanya hivyo kwani alipinduliwa siku mbili baadaye.
Katika hotuba hiyo Morsi alikariri mara chungu nzima kwamba yeye amechaguliwa na watu na hivyo ana uhalali wa kutawala. Yeye na wafuasi wake walisahau kwamba ushindi wao haukuwa wa kishindo na kwamba nchi iligawika takriban nusu nusu.
Kwa hakika mahasimu wake walimshambulia kwa namna alivyokuwa akishikilia kuwa uchaguzi ndio pekee wenye kumpa uhalali wa kutawala.
Lakini hawa pia wamekosea kwa kufikiri kuwa nguvu zao za kijeshi na mtindo wao wa kutawala kimabavu utawawezesha kuendelea kutawala nchini humo na kuyapindua mapinduzi yaliyompindua Rais wa zamani Hosni Mubarak.
Majeshi ya Misri yanaweza yakaendelea kuwaua wananchi wa kawaida wenye kuwaunga mkono akina Morsi na yanaweza yakaendelea kuwaminya na kuwakandamiza wananchi hao lakini iko siku — na siku hiyo haiko mbali — ambapo majeshi hayo yatashindwa na nguvu za umma.
Kila wananchi wanapodhalilishwa ndipo wanapozidi kusimama kidete kupamba na wanaowadhalilisha. Historia mara kwa mara imetufunza kwamba hayo yakijirudia ni majeshi huwa ndio yanayoshindwa.
Iwapo kuna majeshi kwingineko Afrika yanayotamani kuyaiga yanayotendwa sasa na majeshi ya Misri basi na yafikirie tena. Badali ya kutuletea kheri na ufanisi ukatili huo wa majeshi daima huleta nakama na huyarudisha nyuma maendeleo.