VIONGOZI WOTE WA ZANZIBAR HAYA NDIO YAWE MAKAZI YENU MILELE
Kumekuwa na mjadala mkubwa nchini Zanzibar kuhusu bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Miundo Mbinu, hususan katika utendaji mbovu wa wizara hiyo, ubadhirifu wa mali ya umma, rushwa na wizi wa jumla wa mali ya umma. Wawakilishi waliiweka ‘inbox’ wizara hii na hasa ujenzi wa Uwanja ‘mpya’ wa ndege wa Zanzibar. Pesa nyingi zimeliwa, na kazi yote iliyofanyika ni mbovu sana, sasa badala ya kujenga uwanja, SMZ inziba viraka vya run-way hahahaha nacheka kwanza toka 1964 SMZ ilipo ingia madaraka mpaka leo viongozi wezi wakubwa hata haya wala vibaya hawaoni.
Yalipoibuka haya kwa wizara hii, na wizara nyengine zote takriban zimetajwa kwa njia moja au nyengine na hali kama hii; ila mambo kuzidiana ila wote ni WIZI TU.
Ambacho hakikunishangaza sana, ni kumuona Makamo wa Pili wa Rais, ambaye ni mtendaji mkuu wa serikali katika baraza la wawakilishi na ndio Jambazi Kuu, Balozi Seif Ali Iddi akiwakingia kifua watendaji wabovu na wizara kama hii, inayonuka uoza.
Alichokisema Makamo wa Pili wa Rais ni kuwa ‘SMZ itayafuatilia na kuyafanyia kazi mapendekezo yote, malalamiko yote ya wajumbe wa BLW…..’ Hii ni kauli ya kila siku inakuwa hivi na huku watu wanaficha siri na kuzidisha uoza, “wanafagia na kuweka taka chini ya Zulia”…….!!!!!!!
Je, kuna scandal kama iliyoiukumba shirika la Umeme, na ushahidi upo wazi wazi je, serikali imechukua hatua gani...???
Je, kuna uoza kuliko unaofanywa na ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kuanzia udokozi/wizi, hali nepotism(upendeleo) katika ajira, lazima uwe jamaa wa Fulani na Fulani ndio uajiriwe hapo, hata kama huna sifa za kitaaluma, lakini ‘sifa kuu ni unatoka wapi, na umezaliwa wapi, na wazee wako nani). Nafasi za masomo hapo kadhalika zinatolewa kwa misingi hiyo – mtu na mumewe, na mkwe, na mjomba wote wanafnya kazi ofisi moja, desk moja!!!!!! kisha SMZ inasema sio wabaguzi huu ni nini...???
Je, kuna scandal kuliko ya baraza la mji Zanzibar – ushahidi kamili, na Waziri Mwinyihaji Makame Mwadini,(CCM) amekiri lakini kuondoka hataki, na serikali ya Shein haiwezi kumuondosha, na anajulikana kuwa ni ‘worn out’ na hafai hata kupuga decki pala baraza la mji wachiliambali kuwa kiongozi.
Kuna scandal kama ya wizara ya elimu, inajulikana na kila mtu kuhusu mishahara hewa na wafanyakazi hewa (ghost workers).Imekuwa NINI....???
Kuna zaidi kuliko rushwa inayotembea mahakamani au haki ya kupat cheti cha kuzaliwa/kufa – hiyo ni wizara ya abubakar khamis bakari (CUF) – huwezi kupata haki Zanzibar kama hujatoa rushwa — na majaji — watoto wetu, ndugu zetu na jamaa zetu wanayafanya haya ‘mchana’ bila kuogopa — iwe Ramadhan au mwezi wa kula mchana au makka au madina – ngoma draw. Wao ni pesa mbele kwa mbele.
Kuna scandal kubwa sana wizara ya afya — wizara ya Juma Duni (CUF), wameleta dawa fake za kisukari, kinyume cha makubaliano na wafadhili wao ‘Danish government’. Kuna dawa za wagonjwa wa kili, ambayo chini ya makamo wa rais wa kwanza – bei yake ni kama 8-14 million, lakini hesabu inasema milioni 80/ — mpaka leo akina Juma Duni na Fatma Fereji wapo juu ya kiti cha raha na uwaziri WAKIENDELE KUIBA.
Ukiachilia scandals hizi na nyengine — utendaji mbovu nao umejaa, mawaziri wengi na watendaji wao hawaendi kazini – si huyo Nyanga tu kwa sababu ni mgonjwa bali hata hao waliokuwa wazima na afya zao imara. UTORO umekuwa tatizo kwa nchi yetu ya Zanzibar.hii ni kuonyesha wazi viongozi hawa walipokuwa mashuleni walikuwa hawasomi wakitoroka tu basi sasa wamepata uwongozi bado wanakumbuka zama zao za utoro mashuleni. Je, hali kama hii kweli itaifanya nchi ya Zanzibar kusogea mbele kimaendeleo..??? je viongozi kama hawa kweli watasimama kidete kudai mamlaka kamili ya nchi yetu ya Zanzibar..??? YAGUJUUUUUU Uongozi mbovu wa Shein na wasaidizi wake unazidi kuifisidi nchi ya Zanzibar.
Nchi yeyote au jamii yeyote haiwezi kwenda mbele kama public discipline haipo, Zanzibar imekumbwa na tatizo hilo – public discipline ime – collapse, matokeo yake SMZ haina njia nyengine za kupata mapato ila kuwakamua wafanya biashara hata anayeuza pipi, matokeo yake makubwa zaidi, ni ukali wa maisha na gharama za maisha kwa watumiaji ambao ndio sisi wananchi wa kawaida tunaoishi Kengeja, Tundauwa, Kitope, Kiboje, Kangani Gae la Mtungi,Vitongoji, Darajani, Mkokotoni n.k ni mifano tu hiyo –kama hakuna uanzilishwaji, utatumia nini...???
Dr. Kumbi Shein ‘hebu kama kweli wewe ni Kiongozi kama unavyojinata mwenyewe basi wapige sindano watendaji wako’ tunataka tuone tiba halisi mara tu baada ya Eid, badilisha cabinet, inject new blood, na tuone matokeo yake – kuendelea kuwangangania akina Mwinyihaji, Duni, Shamhuna, Gavu, Haji Omar Kheri, Rashid Seif, Fereji, Nyanga, n.k hatufiki pahala.laa kama wewe mwenyewe upo upo tu kutafuta tonge na wake zako na watoto wako basi sawa endelea kuwangangania akina Mwinyihaji, Duni, Shamhuna, Gavu, Haji Omar Kheri, Rashid Seif, Fereji, Nyanga, n.k mpaka miaka yako mitano imelizike kisha muendelea na sera zenu za uwarabu na wanyamwezi basi ndilo munalojuwa maendeleo ni kwa wake zenu na watoto wenu tu rai waache wafe au sio.
MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment