Jumuiya ya Umoja wa Vijana majuha wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) nchini Zanzibar imemtaka Ali Mohamed Shein kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman kufuatia matamshi yake yanayokinzana na kupingana na dhamana aliyopewa na Shein aliyemteua.
Msimamo huo umetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa majuha wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Afisi Kuu ya Jumuiya hiyo huko Gymkhana mjini Unguja.
Shaka amesema matamshi ya kutaka muundo wa Muungano wa Serikali tatu yamesigana na dhamana pamoja na kukiuka amana ya kimajukumu ya kikatiba aliyopewa ya kusimamia na kuitetea ipasavyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kijana huyo aliwaambiwa waandishi wa habari kwamba kitendo cha kushiriki kongamano na kujitambulisha kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku akiweka msimamo na kupendekeza muundo wa Serikali tatu badala ya mbili kwa Serikali anayoitumikia kama mtumishi wa SMZ ni kukiuka maadili ya ajira yake ya kazi.
UVCCM majuha hao walisema kama kweli Othman ni muungwana, anayeheshimu utetezi na msimamo wake wa kushabikia muundo wa Serikali tatu aonyeshe ujasiri na kujiondoa Serikalini mara moja na kasha ndio aweze kuendeleza kile anachokitetea.
Aidha Naibu Katibu Mkuu wa majuha huyo wa UVCCM amesema ni kinyume na taratibu kwa msaidizi wa Rais upande wa masuala ya sheria aliyeapa kumsaidia, kuilinda katiba ya Zanzibar, kuitetea na kuihifadhi akipita njia tofauti ya kisera na Rais wake ambaye amemteuwa.
Shaka amesema ni vyema Mwanasheria Mkuu akaipinga Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwa nje ya serikali kuliko akiwa ndani kwani kubaki ndani ya chombo hicho kazi yake si kupinga bali ni kushauri au kusema baada ya kushauriana na Shein.
Aliongeza kwamba kuna haja kwa Shein kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu huyo kwa kitendo chenye ishara ya usaliti na kubeza matakwa ya kisera ya Shein aliyemteua na kumpa dhamana alionayo.
Hata hivyo Naibu Katibu mkuu ambaye aliitisha mkutano na waandishi akiwa na baadhi ya viongozi wenzake wa vijana alipoulizwa ikiwa Shein atakataa ombi la jumuiya hiyo ya kumuoandoa Mwanasheria Mkuu wake watachukua hatua gani, alijibu kwamba Jumuiya yake itafanya maandamano ya amani ya kumshindikiza Shein amuondoe Mwanasheria Mkuu huyo Serikalini.
Kwa upande wa maoni juu ya kinachoelezwa kuachia ngazi au kufukuzwa na Jumuiya ya Vijana majuha UVCCM, Mwanasheria Mkuu Othman Masoud Othman alipopigiwa simu ili atoe maoni na msimamo wake juu ya hilo aliomba radhi kutokana na kuwa hangeweza kuongea chochote kutokana na kuwepo safarini akielekea nchini Qatar. Lakini aliahidi kutoa ufafanuzi wa suala hilo iwapo atapata nafasi nzuri ya kimawasiliano.
Hivi karibuni Mwanasheria Mkuu wa nchi ya Zanzibar alikaribishwa kuhutubia katika kongamano lililoandaliwa na vijana wa vyuo vikuu hapa nchini Zanzibar na akatoa mifano kadhaa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alisema waziwazi kwamba Muungano uliopo hauna tija na unapaswa kubadilishwa mfumo wake ili kwenda sambamba na dhana ya kuungana kama nchi mbili huru.
Aidha Othman alisema Msingi wa Muungano wa (Tanzania) ni kuungana kwa nchi mbili huru, Tanganyika na Zanzibar. na lengo la kuungana kwa nchi mbili hizo ni kufanya mambo yao pamoja na kupata faida zaidi na sio nchi moja kuitawala nchi nyengine kama ilivyo sasa.
Kauli hiyo na nyengine za Othman Mwanasheria Mkuu wa nchi ya Zanzibar kama aliposema kwamba Zanzibar si mkoa wala wilaya bali ni nchi kamili na katika Muungano, walioungana walikubaliana baadhi ya mambo kufanya pamoja na sio Zanzibar kuwa jimbo la Tanganyika, ndio zilizowaudhi baadhi na watu hasa wafuasi wa CCM wakiwemo vijana majuha wa UVCCM na kulazimika kumtaka Shein amuwajibishe kikazi mtumishi wake huyo.
No comments:
Post a Comment