Friday, August 9, 2013

HUTUBA YA SHEIN YA SIKU YA EID EL FITRI BAADA YA KUWONA MWEZI WA BAKWATA


SHEIN AKIHUTUBIA SIKU YA EID BAADA YA KUWONA MWEZI WAO WA BAKWATA

WAKOMBOZI WA NCHI YA ZANZIBAR WALA IDDI EL FITRI JELA

WANAO FUATA MWEZI WA BAKWATA

HUYU ATI NDIO MUFTI ALIYE KATA KUFUATA MWEZI WA WASAUDI NA WAPEMBA LAKINI ANAFUATA WA BAKWATA

TUNATAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR SHENGESHA LENU BAADAYE

WANAO FUATA MWEZI WA BAKWATA

WAZANZIBARI JIULIZENI MBONA WAKE ZENU WANAO KULA MASHELISHELI NA MIHOGO KILA SIKU HAWANGARI KAMA HIVI..? KISHA MUNAMBIWA ZANZIBAR NCHI MASIKINI.

HAKUNA KITU KIBAYA KAMA NJAAA NCHI IKIWA NA VIONGOZI WADILIFU HIZI KEKI SIO LOLOTE LEO HAPA MUNAZIONA IDDI MPAKA IDDI TENA MPAKA UALIKWE IKULU DUUUUH!!!

HAKUNA KITU KIBAYA KAMA NJAAA NCHI IKIWA NA VIONGOZI WADILIFU HIZI KEKI SIO LOLOTE LEO HAPA MUNAZIONA IDDI MPAKA IDDI TENA MPAKA UALIKWE IKULU DUUUUH!!!

SHEIN AHUTUBIA BARAZA LA IDD NA KUSEMANA KUWATAKA WANANCHI WAIMARISHE AMANI NA UTULIVU YA UWONGO  NCHINI

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameonya kuwa Serikali haitawavumilia wale wote wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa amani nchini na kuahidi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha kuwa inawatia mbaroni na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika kuwamwagia tindikali vijana wawili raia wa Uingereza hivi karibuni.

Ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa akizungumza kwenye Baraza la Idd El Fitri lililofanyika kwenye ukumbi wa Salama katika Hoteli ya Bwawani nchini Zanzibar. 

Akionyesha kukerwa na kitendo hicho pamoja na kile cha baadhi ya viongozi wa dini ambao katika mahubiri yao wakati wa mwezi Mtukufu wa wa Ramadhani baadhi ya hoja zao anavyo fikiri yeye zilikuwa za kuleta uchochezi Shein alieleza kuwa yeye binafsi na Serikali anayoiongoza imesikitishwa sana na vitendo hivyo. 

“Tukio la tarehe 7 Agosti, 2013 la kuwamwagia tindikali vijana wadogo wanawake raia wa Uingereza wasio na hatia limenihuzunisha sana mimi na Serikali ninayoiongoza”alisema Shein na kuonesha hisia kali za kuchukizwa na kitendo hicho.

Aliongeza kuwa ni jambo ambalo Serikali halitarajia kusikia kitendo cha kikatili kama hicho walichofanyiwa vijana hao ambao walikuwa nchini kwa huduma za kujitolea ikiwa ni pamoja na kusomesha vijana wa Zanzibar.

“Kitendo hiki kimeleta dhahma ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu. Si uungwana, si uislamu, ni ukatili kuwamwagia tindikali vijana wale bila ya sababu yeyote” na kusisitiza kuwa Serikali “haitawatia hatiani wasiohusika hata siku moja, hatutawadhulumu wasio na hatia lakini waliohusika hatutawasamehe, sheria itafuata mkondo wake”alisisitiza.

Aliwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kuonyesha utulivu na kutumia busara kwa kuwa baadhi ya matamko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya viongozi wa dini katika mwezi Mtukufu wa Ramdhani yalikuwa yakichochea machafuko na kuvuruga amani.

“katika mwezi wa Ramdhani kuliibuka hoja za kuleta uchochezi na kama si utulivu na busara za wananchi kungeibuka machafuko kutokana na lugha kali za kuwachochea kwa kisingizio cha siasa kwenye dini” Shein alifafanua.

Shein alibainisha kuwa vitendo vya uchochezi vimekuwa vikifanyika katika mwezi wa Ramdhani kwa mwaka wa pili mfululizo sasa hivyo kuchafua sikuu ya Eid ambayo ni ibada kwa waislamu duniani kote.

“vitendo vya aina hii vimekuwa vikifanyika mwaka wa pili mfululizo katika mwezi wa Ramadhani na kuondoa utulivu wakati wa sherehe za Eid El Fitri ambayo ni ibada kwetu sisi waislamu waja wote duniani”alieleza.

Wakati huo huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu imeazimia kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo vitendo vya ubakaji hasa kwa watoto na kuwataka wananchi waelewe kuwa jukumu la kupambana na uovu huo si la serikali peke yake.

Akizungumza kwenye Baraza la Idd El Fitri Shein nchi  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein amesema kuwa ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba silka, ustaarabu na mila za Kizanzibari zinapotea kwa nguvu kutokana na mtindo unaoendelea kushamiri wa vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia.

Akinukuu taarifa ya hivi karibuni ya Waziri wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Shein alisema kuwa jumla ya watoto wa kike 480 Unguja na Pemba wamebakwa katika kipindi cha mwezi Julai 2012 na Aprili mwaka huu.

Alifafanua zaidi kuwa taarifa hiyo ya Waziri zilibainisha kuwa watoto 53 wameharibiwa na wanawake 273 wamekashifiwa na kusisitiza kuwa wakati umefika kuchukua hatua zinazofaa kuthibiti vitendo hivyo.

“Hatuwezi kuona watoto wetu na wananchi wanadhalilishwa, kuiachia hali hii iendelee ni kuwanyima haki watoto, vijana na wanawake.Tukubali kwamba vitendo hivi vimekuwa ni tatizo kubwa katika nchi yetu na kwa hivyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu ashiriki katika mapambano dhidi ya vitendo hivi”alisema Shein.

Shein aliikumbusha jamii kutimiza wajibu wao wa kusimamia na kuendeleza maadili mema kwa ajili ya malezi bora ya watoto na vijana ili waje kuwa raia bora na waumini wa dhati.

Hivyo alitoa wito kwa wazazi, wazee, walezi na viongozi mbali mbali kuungana na kushirikiana kwa karibu katika kutoa malezi na maadili mema katika jamii ili inusurike na maovu.

Sambamba wito huo kwa jamii,Shein aliwahakikishia wananchi kuwa nchi iko salama na itaendelea kuwa salama kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihada ya Serikali zote mbili.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuimarisha umoja, utulivu na mshikamano ambayo ni mambo muhimu ambayo lazima Wazanzibari wayajali na kuyapa umuhimu unostahiki.

Alieleza kuwa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama vipo imara huku akieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2013/2014 uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia saba, hatua ambayo ni maendeleo makubwa.

Alisisitiza kuwa kutokana na kuimarika kwake, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 imechukua hatua ya kuziimarisha huduma mbali mbali zikiwemo za kijamii, afya, elimu, maji safi na salama, miundombinu, kilimo na nyenginezo.

Aidha, Shein aliwataka wananchi kuitumia fursa ya sikukuu kwa kuwajaalia furaha wagonjwa, wanyonge, watu wasiojiweza na waislamu kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuwapa vyakula vizuri na nguo kwani ni miongoni mwa mambo ya furaha.

Katika hotuba yake hiyo, Shein alitoa wito kwa wananchi na viongozi wote kuendelea kupendana bila ya kuchukiana au kubaguana sambamba na kuendeleza amani, umoja, mshikamano na kuvumiliana kwa manufaa yao na nchi kwa ujumla.

Hata hivyo, aliwaomba viongozi wa dini waendelee bila ya kuchoka kukemea maovu na kuamrishana mambo mema pamoja na kuendelea kufanya ibada bila ya kuzozana, kulaumiana na kugombana na pale zinapotokea khitlafu basi ni wajibu kuwa na subira na kufuata misingi inayoongoza dini.

Viongozi mbali mbali wa dini, vyama vya siasa na serikali walihudhuria katika hafla hiyo akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad,Balozi Mdogo wa nchi ya Tanganyika  Balozi Seif Ali Idd,Ati Mufti Mkuu wa Zanzibar anaye fuata Mwezi wa Bakwata, Sheikh Saleh Kabih, Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji na Mabalozi wadogo wanaofanya kazi zao hapa nchini Zanzibar.

Mapema asubuhi, Shein alihudhuria Sala ya Idd huko katika uwanja wa Maisara nchini Zanzibar na baadae alielekea Ikulu kwa ajili ya kusalimiana na Masheikh na viongozi mbali mbali na baada ya hapo alitoa mkono wa Idd kwa watoto na wananchi mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu nchini  Zanzibar.

No comments:

Post a Comment