HII NDIO AMANI ANAYO IMBWA SIKU ZOTE NA VIONGOZI AMANI AMANI MUNAIYONA
Wakili Nassor Jumaa anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam
nchini Tanganyika, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa
na kesi mpya ati ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya
Tanganyika amezungumzia kitendo cha kumhamisha mteja wake kutoka
hositalini hadi jela ya Segerea.Leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanganyika amesema
kuwa amesikitishwa na hatua ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda
aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na
Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha
kumhamishia katika gereza la Segerea.Wakili Jumaa amesema amesikitishwa na
kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali
Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili,
Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya
ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.Jumaa akaongeza kuwa
ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na
kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena
mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo
upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.“Kwa kweli kitendo hicho kime
nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria
tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa. Kwa upande wao familia ya
Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo kilichofanywa na serikali cha
kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa anaendelea kupata matibabu.
Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na hali hiyo kama
familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi
za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa
salama. “Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya
serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui
kwanini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzoni
tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa tunaachia hili
walizungumzie wao.”alisema Is-haq.
Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa viongozi wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu walikuwa katika kikao kizito cha kujadili hatua hiyo ya
kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu
No comments:
Post a Comment